Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015

Punguzeni ushabiki na mahaba kwa maslahi ya taifa!watu wengi wakiwemo waandishi wa habari hawajui ukweli kuhusu Lowassa!

Ahsante sana Dkt slaa nimekuelewa vyema sana
 
Tatizo waandishi wetu wa Habari hawaulizagi maswali magumu, Nilitegemea Dr Slaa aulizwe ana maoni gani/anamzunguziaje Mgombea wa CCM Dr Magufuli......ili tu-connect dots
 
Halaf kumbe lowassa aliletwa na gwajima na yeye, kwanini analia lia? Ina maana lowassa angehamia chadema na kuwa mwanachama wa kawaida tu, Dr slaa angejiuzulu. Au ni hasira ya lowassa kupewa nafasi ya kugombea?
 
Assert aliyokuja nayo inatosha .Cha kushangaza anawaita waliohamia kwamba si lolote . ana lake jambo na hashairiki . Mboe Aliona mbali inhetokea akawa raisi ilikuwa ni vigumu kumshauri.
 
wengine ni kama waliandika maswali in advance na hawakuwa wanasikiliza chochote....inasikitisha...kama walitumwa kaulize hili...na hawakujua kesha lizungumzia....wanapoteza nafasi za wenye maswali makini (kama walikuwepo)
 
ngoja niongezee popcorn.. movie ndio kwanzaaaa linaanza kunoga naona kama starring anataka kuuwawa but mara nyingi katika movie starring huwa ana maliza movie...????
 
Siku Zote MFALME Wa NYIKA Simba AKIUNGURUMA Lazima Mbuga Yote ITAZIZIMA. Dr. Slaa KAHAMISHA RASMI UPEPO Wa KISIASA NCHINI Tanzania Na Sasa Naiona NJIA Ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli NYEUPE IKULU. Hakika ALICHOWAFANYIA LEO CHADEMA Na UKAWA Ni Kuwavua Nguo Kabisa Na Kwa UADILIFU ULIOTUKUKA Wa Dr. Slaa NINA UHAKIKA Tena Wa Zaidi Ya 100% Kuwa KILICHOSEMWA CHOTE Na Dr. Slaa Ni UKWELI MTUPU Na Ili Kukuhakikishia Kuwa Jamaa Hana Masihara Na Hajapata PhD Yake Kwa Kuungaunga Na Anajiamini Amekuambia Kuwa Kama Kuna Yoyote Ktk Hao Aliowatuhumu au Kuwataja Na Kuyasema AJITOKEZE Hadharani ILI Awazidishie Watanzania USHAHIDI Mwingine Kwani Leo Hajatoa SILAHA Zote.

mtahangaika sana lakini mabadiliko yako palepale. mknd yenu!
 
Natafakari sijaelewa mfano wa Dr slaa.."Ukichukua kinyesi chooni na kukihamishia chumbani, chumba kitageuka kuwa choo na hakifai kuishi mana kina harufu kali."..Je kwa mawazo ya Dr ni bora tuhamie kuishi chooni ambako ndo sehemu maalum ya kinyesi na kitaendelea kushushwa kule kila siku au tutafute njia ya kuzuia hii harufu ya chumbani na tuendelee kuishi huku chumbani??...maana hapa options ni mbili tu..
 
Kama kweli Slaa yuko serious, kwanini aliomba orodha ya mtaji wa Lowasa wakati akijua Lowasa ni mchafu?

There you are GT anatufanya watu mazombie ukweli ni kuwa mzee alikuwa anaamini urais kwa upinzani ni yeye tu mpaka afe! sasa EL kampruvu wrong kaniacha hoi anadai hoo nimeona hata kwenye magazeti wanasema watu wanapelekwa na mabasi na malori kwenye mikutano ya cdm! halafu anawaambia waandishi wa habari mara kwa mara hawafanyi utafiti mi nilikuwepo jangwani for sure hakuna walioletwa na mabasi wala malori. Dhambi hii ya kushuhudia uwongo itamtafuna sana Dr. Slaa. Hata kama ana chuki na EL Sumaye asipindishe ukweli!
 
Mzee mi Sina imani naye maana hata yeye Aliweka ahadi ya useja na usafi wa moyo lkn alishindwa kuyaishi ahadi zake na akaacha kwa sababu za tamaa za kidunia na mali ya dunia Leo anakuja nakujidai kwamba yeye msafi kama angekuwa msafi. Angeyaishi ahadi zake alizoweka mbele ya Mungu na kanisa
 
ndicho kitu ambacho wengi walikuwa wanashabikia mageuzi na mabadiliko ya kweli hayaletwi kwa ulaghai kama wanaofanya lowasa,sumaye na timu yake sasa sumaye ameambiwa hawez kwenda kuomba kura mvomero kwanini wa sababu anajua ni kitu gani amewafanyia wananchi wa kule ,lowasa alimega ardhi ya karatu kuipeleka monduli na pia ana hisa kwenye makmpuni ambayo hajaorodhesha kwenye tume ya maadili kwa kifupi wamekuja kuua mageuzi inabidi tuanze upya
 
Mi Hata Moja Halikuniingia Kichwani Sanasana Kaniacha Na Mashaka Makubwa Juu Yake, Mfano, Anasema Ya Ni Mwadilifu Na Msema Ukweli, Huo Ukweli Ameuanza Lini? Huyu Si Alikuwa Padri? Kwanini Aliusaliti Upadri Na Kukimbilia Ndoa? Je Huyu Baada Ya Kukimbilia Ndoa Si Ndo Huyu Huyu Akamsaliti Mkewe? Mbaya Zaidi Akakimbilia Kuishi Na Mke Wa Mtu, Sasa Huo Uadilifu Kipindi Hicho Hakuwa Nao? Haya Leo Anasema Hakuwa Akilipwa Mshahara Milion Saba, Je Kama Kweli Yeye Ni Mkweli Na Mwadilifu Kwanini Hakukanusha Tangu Kipindi Kilekile Pale Chadema Ilipotangaza Kuwa Analipwa Milioni Saba? Kwa Kunyamaza Kwake Alishiri Kuunga Mkono Uongo! Sasa Tutamwaminije Kwa Haya Aliyozungumza Ikiwa Tayari Yeye Mwenyewe Siyo Msafi Ingawa Anataka Tumwamini Kuwa Ni Mwadilifu?
Maswali yako yooooote Dr. kayajibu ktk maelezo yake, sijui ni nini hukuelewa??
Ila nafikiri ----- alioumwaga unawasha sana, watu mnatafuta mlango wa kutokea! Na bado, kama mlivyomsikia, yeyote anayebisha kuitwa fisadi ajitokeze, yuko na artillery + plus gun ship.
 
Back
Top Bottom