Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015

Hakuna siku ktk maisha yangu nimeumia kama leo, moyo umesinyaa, nafsi imedhoofika, mwili umepauka, dhamira imenyauka.

Nimetambua ukweli ni mchungu, ukakasi wake unapenya mpk mifupani.

Huyu ndiye kiongozi pekee niliyeamini/ninayeamini ndiye atatusuuza mioyo yetu.

Slaa utadumu kwenye moyo wangu, siwezi kamwe kupuuza kitokachp kinywani mwangu. Nitakua mnafiki wa kwanza kunyanyua ulimi wangu na kukutusi.

Naumia zaidi waTZ tunaingia miaka mingine mi5 ya maumivu.

Mungu atuoneshe chaguo sahihi, Mungu atupe nguvu.

Mbowe na genge lako, mlaaniwe hata kizazi cha 7.

Matusi yote mliokuwa mnampa, leo amekuwa mungu wenu. Mabadiliko mbele kwa mbele. Wananchi wameshaamua
 
Ni haki yake kuzungumza na waandishi wa habari kama raia yeyote wa Tanzania. Lakini kwa upande Wangu amechelewa sana maana swala la Lowassa halikwwpeki kama atalizungumza maana Lowassa anapendwa tu alivyo hata kama anatuhuma lukuki. Binafsi nampenda tu hata hukuniambia kashfa ganiii mi kesho unakuta anampenda tu. Niko alergic kuhusu Lowassa anampenda tu alivyo.
Dr anatumia nafasi yake ipasavyo kwani amekuwa kimya sana hata Mimi nilikuwa najiuliza nakosa majibu. Kama mtanzania mwenzangu nilikuwa najisikia kutakuwa na amani. Mwenzangu yukwapi? Kuna hata mwanasiasa mmoja aliwahi andikwa kwenye twitter Dr. Slaa rafiki yangu uko wapi?
Pia kipindi kingine Dr usikae kimya namna hiyo kwani kama mtanzania mwenzetu unatuweka njia panda maana mengi yanazungumzwa kwa kipindi hicho.
Asante kwa kututoa hofu mheshimiwa. Chadema kwa sasa wako yanaendelea na kampeni na zimeshika kasi sana kwani nchi ni kubwa sana. Karibu tujumuike pamoja Dr. Umekaa kimya sana. Tunakuhitaji.
Karibuni tusonge mbele Dr. Slaa.
 
magufuli - lowasa hafai kuwa rais
uhuru - lowasa visadi
mzalendo - slaa aingamiza ukawa
daily news - slaa on corrupt leaders
tbc fm - upinzani kwisha hata ccm ispo piga kampeni
tbc tv - ???????????????????? ukawa
 
Mi Hata Moja Halikuniingia Kichwani Sanasana Kaniacha Na Mashaka Makubwa Juu Yake, Mfano, Anasema Ya Ni Mwadilifu Na Msema Ukweli, Huo Ukweli Ameuanza Lini? Huyu Si Alikuwa Padri? Kwanini Aliusaliti Upadri Na Kukimbilia Ndoa? Je Huyu Baada Ya Kukimbilia Ndoa Si Ndo Huyu Huyu Akamsaliti Mkewe? Mbaya Zaidi Akakimbilia Kuishi Na Mke Wa Mtu, Sasa Huo Uadilifu Kipindi Hicho Hakuwa Nao? Haya Leo Anasema Hakuwa Akilipwa Mshahara Milion Saba, Je Kama Kweli Yeye Ni Mkweli Na Mwadilifu Kwanini Hakukanusha Tangu Kipindi Kilekile Pale Chadema Ilipotangaza Kuwa Analipwa Milioni Saba? Kwa Kunyamaza Kwake Alishiri Kuunga Mkono Uongo! Sasa Tutamwaminije Kwa Haya Aliyozungumza Ikiwa Tayari Yeye Mwenyewe Siyo Msafi Ingawa Anataka Tumwamini Kuwa Ni Mwadilifu?

Ukwel wa madai hayo ungekuwepo serena ukamuuliza hayo maswal ndo maana alitoa muda wa maswal..Alichoongea kaz n kwako kupembua kma n pumba ama Michele.
 
Namsikitikia sana dr.Namshauri aende kijijini akakae na familia yake! umejichafua sana na umejishushia heshima sana!
 
Wana JF,

Kuishi kwingi kuona mengi, zimwi likujualo alikuli likakwisha, sijutii uamuzi wangu kuipigia kura ukawa kwani malengo yangu ni mabadiliko ya kuondoa chama kikongwe kiwe cha upinzani ili kuleta mizani iliyo sahihi katika kuiwajibisha serikali , ili wananchi tupate maendeleo yaliyobora, sio kuendekeza maendeleo kwa watu bora.

Nguvu zangu nilizozikusanya kuiondoa ccm na makandokando yake, siwezi kurudi nyuma kwa sababu nimemsikiliza mshawishi yoyote aliyeamua kwa chuki yake au kwa kutotimiza malengo yake, anishawishi niache kuondoa mzimu na mibuyu yake ili wanangu waje wanishukru kuona hata nasi tumeingia kwenye orodha ya kudhaminiwa.

Rais ajaye kama atatoka ccm , hakuna mabadiliko, kitendo cha Rais kuwa na kofia mbili ni cha ki-utawala ambao hausahahihishi wala kushauriwa, kwani Urais na Wenyekiti unawezwa kufanywa kuwa taasisi ya familia ya rais, hivyo tutaishi kwa uoga daima kama ilivyo sasa.

namaliza kwa kusema hivi yote tutayasikia lakini lengo kuu ni kuiondoa ccm tu.

Ndio lengo kuu
 
Jamani napendekeza tambwe hiza apewe mikoba ya ukatibu mkuu wa chadema kutokana na umahiri na mapenzi yake kwa chama
 
Kufuatia mkutano uliofanyika leo. Nawashauri UKAWA, ili wasiyumbishwe na wasiyape umaarufu aliyoyasema Dr. Slaa, dawa ni kukaa kimya, na waendelee na Kampeni kama vile hawajasikia alichosema. Na wawataarifu Wagombea wa Ubunge woote wafanye hivyo hivyo. Wananchi tunataka Sera, tunataka Maendeleo. Hatutafuti malaika kuja kuongoza nchi yetu.

#Ila Daaaah, kukosa Uraisi Kunauma saaaaana jamani, kunaweza sababisha mtu akakubali kudharaulika kwenye jamii#
 
Yaani hana jingine la kufanya kumalizia siasa yake. Kilichobakia ni kurusha makombora kwa Lowasa.

Lakini angewashutumu wananchi kwa kupenda mabadiliko.

Lakini kama tulivyokupenda kipindi kile , sasa amekuja mwingine tunampenda tutavuka naye kwenye haya mabadiliko.

Pole Dr. muda wako na wewe umekwisha, angalau umeambulia kiinua mgongo toka CCM, kale salama na shuntama.
 
Back
Top Bottom