Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015

kwahiyo CDM inateketea si ndio vizuri kwa CCM sasa mbona kama mnakua na mashaka tena? Harafu kwenu Lipumba poa eeeh? Hizi siasa za mahamnazo
 
Hebu tujikumbushe Dr. Slaa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuachana na lichama libovu linalomilikiwa na wapiga dili la CHADEMA.

Link hii hapa chini: -

 
Bado tutauliza na bado tutasisitiza waliohamia CHADEMA ni ASSETS AU LIABILITIES???
Na waliohama CHADEMA kwenda CCM ni ASSETS AMA LIABILITIES?
 
Nani aligharimia conference ya Dr Slaa wakati huo?.Nani alimpeleka Canada?Nani aliikomboa nyumba yake ilipopigwa mnada ili kulipia madeni?.Ukinijibu nitakuonyesha aliye nyuma ya Dr Slaa tangu kipindi kile hadi leo
 
Nani aligharimia conference ya Dr Slaa wakati huo?.Nani alimpeleka Canada?Nani aliikomboa nyumba yake ilipopigwa mnada ili kulipia madeni?.Ukinijibu nitakuonyesha aliye nyuma ya Dr Slaa tangu kipindi kile hadi leo

Unataka kujua.

Nenda NMB uliza akiba aliyokuwa nayo.
Nenda NBC uliza Mapato yake..............

Uliza safari zote za Ulaya alizofanya Dr Slaa chadema walichangia kiasi gani....alafu ujijibu aliyempeleka Canada na kukomboa nyumba.

Mwisho jiulize Dr alifanya kazi kwa kuuwa mawasiliano au kujenga mawasiliano.....

Nyumbu ukimaliza rudisha hapa na proof.
 
Bado uchambuzi wa safari ya Kisiasa ya Dr. Willibrod Slaa unaendelea.

Tumepelekwa moja kwa moja kutoka Hoteli ya Serena, JamiiForums imetuma mwakilishi wake.

Mtangulizi wa shuguli ambaye anatoka kwenye kampuni ya mahusiano ya umma anamtambulisha Dr. Willibrod Slaa.

Anasema kuwa kwa muda mrefu Slaa amekuwa alama ya harakati za ukombozi dhidi ya makucha ya mkoloni mweusi.

anaongeza kuwa Dr. ataongea kwa muda kisha kuruhusu maswali kutoka kwa waandishi, anamkaribisha!

-------------------



MAELEZO YA NYONGEZA

Dr. Slaa Anasema ukweli na upotoshwaji lazima usemwe, utamkwe na yanayoaminiwa yasemwe.

Sina tabia ya kuyumbishwa, nasimamia ninachokiamini. Mengi yamesemwa mitandaoni, magazeti na hata na viongozi wenzangu. Sina ugomvi, chuki wala hasira na mtu yeyote.

Lakini katika nchi kuna misingi inayoongoza taifa.Hakuna siasa safi inayokwenda kwa propaganda. Matokeo ya propaganda ni vita.

Anasema
1. Sikuwa likizo
2. Sina barua yyte kwamba naenda likizo

Kilichotokea ni hiki - Niliamua kuachana na siasa na kimsingi kazi hiyo ilitokea tarehe 28 July usiku baada ya kuona yale yaliyofanyika ndani ya chama changu sikufurahishwa pia.

2. Kusema dr. Slaa alikuwepo tangu mwanzo kumleta Edward Lowassa kwenye chama ni uongo.

Kwa kifupi sana baada ya tarehe 11- 08 baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma, mshenga wake Lowassa mch. Gwajima alinipigia simu kuwa nini kinafuata.

Nilimwambia tumsikie Mwenyekiti anasemaje, nikamwambia tukutane ofsini.Nilichoshiriki ni kutaka kujua kama atahama CCM au la na pili anapoenda kutangaza ajisafishe na kashfa ya ufisadi wa Richmond.Cha ajabu tangu ahame CCM hajatangaza wala kujisafisha

Mambo mawili;
1. Anayekuja kwako ni ASSET au LIABILITY

Binafsi sijatoka CHADEMA kwa sababu ya urais. Dr anataka mgombea mwenye sifa, mwenye uwezo na anayeweza kuivusha CHADEMA kuchukua nchi. Hata mwaka 2010 sikugombea ila niliombwa.

- Tulitaka kujua anakuja na nani, na wenzake, viongozi serious au na vijana wa mitaani.
- Tuliambiwa anakuja na wabunge wasiopungua 50, wenyeviti wa mikoa 20 na wenyeviti wa wilaya 100.
- Niliomba majina hayo lakini sikuyapewa. kama katibu mkuu makini nisingekubali kupokea mtu bila kupima kama asset au liability.

Tangu 2004 sijawahi kutofautiana na mwenyekiti wangu Mbowe lakini kwa mara ya kwanza tumetofautiana naye katika hili.
kabla ya kamati kuu tulikaa watu wanne Mbowe,mimi,Lissu na Gwajima.

Nilivyoona hivi niliandika barua ya kujiuzulu pale pale lakini ikachanwa na prof. Safari. Nikaandika nyingine kwa makamu Zanzibar akaniambia haya mambo yamepangwa unajisumbua bure.

2. Propaganda ni nyingi mara Dr. Slaa amefungiwa nyumbani, mara atakuja ofsini kuongea na media.

- Sijawahi kuzuiwa na Josephine kufanya jambo lolote, lakini kumbeni amewahi kumwaga damu kwa ajili ya ukombozi wa nchi hii, amezunguka nchi hii kila kona.
-Silipwi milioni saba kama inavyodaiwa.Tunakula mihogo kama watz wengine,tunakula maharage kama watz wengine.

Cha muhimu
Jina la chama tulichokijenga kwa muda mrefu lisiharibiwe.
Jina la uadilifu la mwanasiasa ulilolijenga kwa muda mrefu lisiharibiwe.
Hapa tunaangalia credibility.

Jambo lingine
Asset ni jambo linalopimika,hakuna asset tuliyopata kwa Lowassa. Ni uongo mtupu.Kina Mahanga walioshindwa huko,Sumaye ambaye ni mzigo kabisa ana uchafu wa kutosha, amechukua shamba la magereza huko Kibaigwa.Huyu huyu Sumaye aliyesema atajiuzulu.Sumaye ni kapi,Lowassa ni kapi, tumekula matapishi yetu.

Msindai ni mzigo, namjua tangu tukiwa bungeni.Mgeja simjui siwezi kumsemea.

Guninita ni mzigo hata kuandika report hawezi, ni mzigo tangu akiwa UVCCM.

Wengine wanasema ni muhimu tuiondoe CCM hata kwa kumtumia shetani.Si kweli unaiondoa CCM kwa program serious, kwa mpango makini.Leo Lowasa anatufunga mdomo hata haijaisha mmwezi mmoja.

Suala lingine nani hana madhambi,si sahihi.
CCM kinalea matatizo, kimemlea Lowassa hadi hapo alipofikia.
Ukimuona mtu anahamisha choo kutoka kilipo na kuukihamishia chumbani anakolala utasemaje? Hawa wamehamishia choo chumbani.

Tuhuma dhidi ya Lowassa
1. Tulimwambia atoke hadharani atueleze ukweli wa RICHMOND.
Msingi wa kwanza wa RICHMOND lazima urudi kwenye taarifa ya Mwakyembe.Nawashukuru Sitta na Mwakyembe kwa kutoka hadharani kusema hayo, watoke zaidi ya hapo tuwanyamazishe hawa. nihongwa mil 500 nikakataa.

Mwanzo wa RICHMOND ni lazima urudi kwenye taarifa ya baraza la mawaziri ya kabla ya taarifa ya RICHMOND.
RICHMOND ilianzia kwa Mkapa sio Kikwete.

2006 wakati maamuzi ya RICHMOND yanafanyika waziri mkuu alikuwa Lowassa.

Dr. Slaa anaelezea mchakato mchafu wa upatikanaji na upewaji wa zabuni wa kampuni ya RICHMOND uliosimamiwa na Lowassa akiwa waziri mkuu.

Dr. Slaa anaelezea mchakato mchafu wa upatikanaji na upewaji wa zabuni wa kampuni ya RICHMOND uliosimamiwa na lowasa akiwa waziri mkuu.

Kwa mengine, fuatilia akaunti yetu ya Twitter, www.twitter.com/JamiiForums


Miaka kadhaa imepita
 
Back
Top Bottom