Zanzibar 2020 Hotuba ya Dkt. Hussein Mwinyi kisiwani Pemba (Julai 19, 2020): Yajayo yanafurahisha

Mzanzibari

New Member
Nov 6, 2008
2
0
Mapokezi yalianzia Uwanja wa Ndege wa Karume, mkoa wa Kusini Pemba na kupita barabara kuu kuelekea viwanja vya Tibirinzi akiwa katika gari la wazi, akisindikizwa na umati wa watu wenye sare za CCM na wengine wakipunga kando ya barabara.

Katika viwanja vya Tibirinzi, Chakechake, Kusini Pemba, vilifurika hadi mamia ya wananchi wakiwa wamekosa nafasi na kubaki nje ya viwanja hivyo.

AAD9B493-3E3D-4E58-86E5-E0A58543273F.jpeg

C48E512E-180D-4E95-813B-5A5112AB4639.jpeg

CDFD556E-D773-46E5-9978-7CF36A6085D4.jpeg


======

HOTUBA YA MGOMBEA WA URAIS WA CCM VISIANI ZANZIBAR, DKT. HUSSEIN ALI HASSAN MWINYI - KISIWANI PEMBA

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezimungu, mwingi wa rehma kwa kutuwezesha kukutana hapa hii leo. Kuwashukuru wananchi wa Pemba kwa mapokezi makubwa sana. Napata faraja kazi yetu sasa itakamilika mapema sana.

Nashukuru chama kwa kumaliza uteuzi wake kwa kwa haki, na sasa sote tumekuwa wamoja, hakuna timu Mwinyi wala timu Mbarawa, na lengo letu sasa ni moja kushika dola.

Kabla ya yote tuwaombee wale waliopata maafa Mwenyezi Mungu awarehemu, na wengine waliopata ajali ya kuezuliwa mapaa nyumba zao Mungu awafariji.

Sitosema mengi.

Muwe na hakika nitaenzi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Nitadumisha Muungano wetu ni wa aina yake, na unatiliwa mfano duniani kote.

Kuna suala kubwa, nalo ni suala la amani na ndio maana tunapata maendeleo. Nchi nyingi za jirani zetu hakuna amani. Namshukuru sana

Mheshimiwa Rais Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuongoza nchi kwa amani.

Jukumu langu ni kuhakikisha amani inadumu. Lazima tudumishe umoja wetu. Kusiwe na Upemba na Uunguja, kusiwe na ukusini na Ukaskazini.

Sote ni Wazanzibari. Suala la ajira tutalishughulikia hasa kwa vijana.

Niwapongeze hasa Rais Dkt. Shein na viongozi wote wa serikali na chama.

Nihakikishe alipoachia yeye nitaendeleza. Nitaendeleza miundombinu, huduma za jamii, ustawi wa watu, maendeleo ya jamii, afya, elimu, na yote yanayogusa watu. Nitahakikisha Mzazibari anakua na maisha bora.

Ukitaka kuyafanya hayo, lazima uwajibike. Huwezi kuwa na program kukawa na wala rushwa, wabadhirifu, Wazembe. Sitokuwa na huruma kwa wenye tabia hizo. Serikali itafanya kazi kwa maslahi ya Wazanzibari wote.

Wapo wanaosema Mwinyi ni mpole. Mimi Nasema wataniewa.

Nasema haya kwa sababu pengine hamjanisikia nikiongea sana kwenye vyombo vya habari. Sababu kubwa ni kwamba Wizara ya Ulinzi huko mambo yetu ni ya siri hatufanyi hadharani. Siwezi kusema ila kwa wale wabadhirifu, wala rushwa, wazembe, wasiowajibika, hao watawajibika.

Nitasimamia maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya za Kimataifa.

Nikwambieni nimeamua nigombee na ili nitakaposhinda dhamira yangu ni moja kuwatumikia Wazanzibari wote.

Tukishika dola, tutakuja na miradi ya kusaidia Wazanzibari ikiwemo ajira kwa wote bila ubaguzi.

Panapo dhamira njema Mwenyezi Mungu atatupa neema.

Mwaka huu, tunataka tupate ushindi wa kishindo usiwe mwembemba tukapata malalamiko. Na niliyoyaona Unguja na hapa Pemba kwa sasa sina shaka ushindi ni mkubwa. Sina shaka ushindi utakua ni mkubwa.

Nasema tena kwamba ‘Yajayo yanafurahisha.’ Ni ahadi naichukua mbele ya Mungu na mbele yenu. Nitahakikisha nawahudumia wananchi.

Sasa na wakati huu nina hakika tunafanya mambo mazuri kwa maisha yetu yawe mazuri. Kazi iliyobakia ni kwenda kushika dola na si vyenginevyo. Kwa sasa lililobakia ni umoja mshikamano na ushirikiano ndani ya CCM.

Katika risala ya mikoa miwili ya Pemba ya Kusini na Kaskazini salamu nimezipokea na kuondoka Pemba nikiwa na faraja kubwa hivyo hayo yanaonekana ni mapenzi ya dhati ninaahidi kuitumikia Zanzibar kwa moyo wangu wote. Ihsani hulipwa kwa Ihsani.

Maneno yanayosemwa na wagombea kama wametumwa na Hussein, nataka kuwaambia hapa leo, sijamtuma mtu, kila mtu apambane na hali yake, maana wengine wanasema eti wachaguliwe ili nitakapounda Baraza la Mawaziri, niwateuwe, nawaambia sijamtuma mtu.

Nataka kurudia maneno aliyosema Kama Makamu Mwenyekitu wetu Rais Dkt. Shein kuwa tutumie uchaguzi huu ndani ya Chama kupata wagombea bora.

Baada ya kusema hayo sasa naomba nimalizie kwa kuwashukuru wana CCM na wananchi wote waliojitokeza katika mapokezi yetu na hapa uwanjani.
 

ZENJIBARIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
561
1,000
Na mie niseme Tu. kwa wanzibari wote ccm act Chadema na Wa vyama vyengine vyote hawahitaji maendeleo kama wanavohitaji heshma ya zanzibar, akili za wazanzibari zimekwamishwa na hazitaweza kuleta au kushukuru maendeleo yeyote bila ya hadhi ya zanzibari kurudi Kwanza.
The mind of the people is under psychological arrest,the only key to release it is dignity , help the weak if you’re strong
 

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
536
1,000
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Ametowa Poingezi Kwa WanaCCM Pemba na Wananchi Kisiuwani Pemba Kwa Mapokezi Makubwa Mgombea Urais wa Zanzibar Kwa Tiketi ya CCM Dkt. Mwinyi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia, Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ametoa pongezi kwa wanaCCM na wananchi kisiwani Pemba kwa mapokezi makubwa waliyomfanyia mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi.

Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hafla ya kumtambulisha Mgombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa wanaCCM na wananchi wa mikoa miwili ya Pemba, hafla iliyofanyika katika uwanja wa kufurahishia watoto Tibirinzi Chake chake Mkoa wa kusini Pemba.

Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanaCCM na wananchi pamoja na kuzipongeza Kamati zote za maandalizi kwa kuandaa mapokezi hayo ambayo yametia fora kisiwani humo pamoja na yale yaliyofanyika hivi karibuni kisiwani Unguja.

Aidha, Rais Dk Shein alisisitiza kuwa ushindi kwa CCM ni lazima kama inavyoeleza Katiba ya chama hicho kifungu cha Tano kuwa ushindi ni lazima kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM aliwataka viongozi katika Majimbo kwenye uchaguzi unaotarajiwa kuanza kesho kuwachagua viongozi makini, wenye uwezo na bila ya kufanya upendeleo.

Aliwataka viongozi hao kutowachagua wababaishaji wenye tamaa na badala yake wawachague viongozi watakaokiimarisha chama hicho.

Alieleza kuwa CCM ni chama kikubwa sana kina viongozi mbali mbali wenye sifa hivyo wasing’ang’aniwe viongozi waliokuwa hawana sifa hao kwa hao kila siku na kusisitiza kuwa ni vyema wakawachagua viongozi wenye sifa ambao wakisimama wanasikilizwa na wanamvuto kwa wapiga kura.

Alisema kuwa viongozi wanaotakiwa wawe na sifa nzuri ambazo wataweza kufanya kazi na Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi “Wajadilini kama tulivyowajadili wale 31 waliogombania nafasi ya Urais kupitia chama chetu, wajadilini nje ndani ndani nje”, alisisitiza Makamo huyo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Alieleza kuwa CCM ina sifa kumi na mbili ambazo mtu ama mgombea hutakiwa kuwa nazo, ambapo kwa mgombea wa urais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi ni miongoni mwa viongozi wenye sifa zote hizo.

Makamo Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar alimuelezea mgombea huyo kuwa ana heshima kubwa kwenye Serikali pamoja na ndani ya CCM.

Nae Mgombea wa Nafasi hiyo ameahidi kusimamia maslahi ya Zanzibar katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na kusimaamia maslahi ya Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya za Kimataifa kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Mgombea huyo alisisitiza haja ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa mwaka huu na kueleza kuwa ushindi wa mwaka uwe ushindi mkubwa na usiwe ushindi mwembamba ambao utaleta malalamiko na kueleza kwamba kutokana na mapokezi hayo hana wasi wasi kuwa ushindi utakuwa wa kishindo.

Alisema kuwa ushindi huo utapelekea kuunda Serikali itakayokuwa na maslahi kwa wananchi wote huku akiwahakikishia kuwa Serikali atakayoiunda itawatumikia wananchi wote.

“Yajayo yanafurahisha naahidi kwamba tutaboresha maisha ya Wazanzibari....hisani hulipwa kwa hisani na hivyo na mimi naahidi hisani ya kuwatumikia wananchi ”,alisema Dk. Hussein Mwinyi.

Aidha, alipongeza risala na kusema kuwa salamu amezipokea huku akitoa shukurani na pongezi kwa mapokezi aliyoyapata kisiwani humo.

Alisisitiza haja ya kuwachagua viongozi bora katika chaguzi za chama hicho zinazoanza kesho zikiwemo nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani ili iwe rahisi kuyatekeleza yale yanayoahidiwa na Chama hicho.

Dk. Hussein Mwinyi aliwathibitishia wananchi kwamba yeye hajamtuma mtu hata mmoja ili agombee katika chama hicho kwa azma ya kuja kumteuwa kuwa Waziri na kusisitiza kwamba kila mmoja apambane na hali yake.


Katika hatua nyingine, Mgombe huyo wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, alisema kama atapata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar, atafanyakazi kwa maslahi ya watu wote na kamwe hatowavumilia wala rushwa, wazembe na wasiowajibika.

Alisema kama wapo watendaji wa aina hiyo na hawamjui yeye utendaji wake, basi watamjua muda mfupi tu baada ya kuwa rais wa Zanzibar, baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

“Nitafanya kazi kwa maslahi ya watu wote, nitahakikisha watu wote wanafanya kazi ipasavyo, kwa dhamira ya kuwatumikia Wazanzibari wote na sio vyenginevyo tena bila ya ubaguzi”, alisema.

Akizungumzia suala la amani na utulivu wa nchi, Dk. Mwinyi alisema kuwa atahakikisha amani iliyopo Zanzibar itaendelea kudumu hivyo, aliwataka wananchi kudumisha umoja huku akiamini kuwa ndio silaha pekee ya kuwaletea maendeleo.

“Umoja wetu tutauenzi, tutaudumisha na hata katika masuala ya ajira nitahakikisha kwamba hakutakuwa na ubaguzi…..,”alisema.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Mabodi alieleza hatua zilizochukuliwa na chama hicho kuwapata wagombea Urais na hatimae kumpata kinara wa kupeperusha bendera kwa tiketi ya CCM huku akiwapongeza wanaCCM na wananchi wa Pemba kwa mapokezi makubwa.

Nao wanaCCM, waliokuwa wagombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM na kuingia tano bora walitoa maneno yao ya shukurani huku wakimuahidi Dk. Hussein Mwinyi kuwa watakuwa nae bega kwa bega na kuwataka wanaCCM na wananchi kuendelea kumuunga mkono pamoja na kukiunga mkono chama hicho.

Katika salamu za WanaCCM wa Mikoa miwili ya Pemba kwa mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi walieleza kuwa chama hicho kimepata nahodha mweliedi, mahiri, mzoefu, mchapa kazi na asiyechoka wala kuogopa anaeelewa mazingira ya pepo zote za bahari asiyechoka wala kukata tamaa.

Waliongeza kuwa wanaamini kuwa mgombea huyo atawavusha salama kwa malezi aliyolelewa yeye ni mtoto mwema na atawapeleka wanakotaka kwenye maendeleo endelevu ya nchi.

“Karibu Pemba kwa WanaCCM wenzako tunakukubali, tunakupenda, tunakuthamini, tunakutaka, tumekuchagua na tunakuahidi tutakupa kura za kutosha ili uiongoze nchi yetu, Mhe. Mgombea ondoa hofu Pemba ya jana sio ya leo” walieleza wana CCM hao.

Aidha, walitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli na Makamo Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuongoza vyema mchakato wa kumpata mgombea Urais wa Tanzania na Rais wa Zanzibar.

Nao waliokuwa wanachama wa vyama vya upinzani waliojiunga na CCM, walieleza azma yao ya kumuunga mkono Dk. Mwinyi pamoja na kuiunga mkono CCM ili ishinde uchaguzi ujao kwa kishindo.

Mapema ndege ya Shirika la ndege la “Pression Air” ilituwa katika kiwanja cha ndege cha Pemba, mnamo majira ya saa 4:11 asubuhi ambayo ilimchukua mgombea huyo ambaye alipokelewa kwa vifijo na nderemo kutoka kwa Wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi mbali mbali waliokuwa na shauku kubwa ya kumpokea Mgombea wao wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Mamia ya wanaCCM walifurika katika kiwanja hicho kwa ajili ya kumpokea Mgombea huyo akitokea Unguja , huku rangi na kijani kibichi na njano kavu ikitawala ambayo ni sare ya Chama hicho kiwanjani hapo.

Bendi ya Chipukizi pamoja na ngoma nyengine za kienyeji zilitowa burudani ya muruwa katika Kiwanja hicho, ikiwa ni ishara ya furaha ya mapokezi ya mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Mwinyi.

Pamoja na mapokezi hayo, katika kiwanja cha Ndege cha Karume Pemba wananchi wakiwemo wanachama , wapenzi wa Chama hicho walipata fursa ya kujipanga kando kando ya bara bara kwa ajili ya kumpokea mgombea huyo baada ya kufika Kisiwani Pemba kwa utambulisho.

Wananchi na WanaCCM hao walijipanga barabarani kutoka kiwanja cha ndege hadi Kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi nje kidogo ya mji wa Chake Chake Pemba.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
IMG-20200719-WA0048.jpg
IMG-20200719-WA0049.jpg
IMG-20200719-WA0041.jpg
IMG-20200719-WA0043.jpg
IMG-20200719-WA0047.jpg
IMG-20200719-WA0045.jpg
IMG-20200719-WA0025.jpg
IMG-20200719-WA0039.jpg
IMG-20200719-WA0030.jpg
IMG-20200719-WA0028.jpg
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
13,932
2,000
Sijasoma hata ndefu sana nimepitia pitia hizo picha tuu nikapita zangu
wa stendi,
Hii pia ndefu:

SIASA ZA PEMBA NA MUUJIZA UNAOJITOKEZA NA KUPOTEA

"Binadamu tunapenda muujiza kwa kuwa inarahishisha kufikiri.

Kwanza nataka kukutoa hofu juu yangu ili nikufahamishe kuwa mimi hupenda kuukubali ukweli unapodhihiri na hii ndiyo sifa inayomnyanyua binadamu yeyote yule akathaminika achilia mbali wale wanojiita wasomi.

Ukisikiliza kile ukipendacho ukaukataa ukweli heshima ya usomi wako itakwenda chini.

Nimeangalia ‘’clip’’ ya mapokezi makubwa aliyopata Dr. Hussein Mwinyi Pemba.

Niliyoyaona kwenye clip ni tofauti ya hali ya Pemba kama tunavyosikia.

Hali ya Pemba hivi sasa ni kuwa tunaelezwa na wananchi wa Pemba wenywe kuwa wananyimwa vitambulisho ili wasipige kura.

Nani anawanyima Wapemba vitambulisho na kwa sababu gani?

Ipo clip hapa ya tatizo hili mimi kwa kurahisisha utambulisho nimeipa jina "Ngoma za Vita Zinapashwa Moto Huu ni wakati wa Masheikh wa Zanzibar Kuzungumza."

Ukisikiliza ‘’clip’’ hii moyo utaingia hofu ya hayo yanayoweza kutokea.

Haya yanafahamika hayahitaji maelezo zaidi.

Miezi michache iliyopita tumeona CUF ilivyokufa Zanzibar kwa dakika moja au ukipenda nukta moja katika "Shusha Tanga Pandisha Tanga Safari Iendelee..."

Wimbi hili nimetafuta mfano wake pengine duniani sijaona.

Maalim kahama na wanachama wote na ofisi zao mitaani kwa dakika moja na kuzigeuza ofisi zote kuwa zambarau.

Wanachama, ofisi zao na bendera ndiyo "symbols" za nguvu ya chama.

Chama kikiwa hakina vitu hivi kama viaashiria basi jua hapo hakuna chama.

Katika hali kama hii sijaona juhudi za CCM kukijenga chama chao Pemba au hata Unguja au kusikia hotuba za kuwavutia wale waliokuwa wanawapinga kuvutika kuwaunga mkono, ila nilichosoma ni taarifa kuwa Dr. Mwinyi apokelewe na yaorodheshwe majina ya watakaotoka kumpokea.

Huu ni ujumbe kutoka serikalini.

Hiki ni kichekesho.

Haiwezekani kujenga chama chochote kwa namna hii au kuhamasisha wanachama kwa mtindo huu.

Chama hakijengeki kwa vitisho vya "roll call," chama kinajengwa kwa mapenzi na ari ya wanachama wenyewe.

Lakini hapa ndipo ulipo muujiza wenyewe.

Dr. Hussein Mwinyi kapata mapokezi makubwa Pemba kama ‘’clip’’ inavyoonyesha.

Binadamu tunapenda miujiza kwa kuwa huhitaji kufikiri sana kujua kwa nini kishowezekana kimewezekana.

Nayasema haya nikitazama historia ya TANU vipi watu masikini na wasio na elimu walivyounda TANU kikawa chama kikubwa cha kupigiwa mfano Afrika nzima.

Chini ya mwaka mmoja TANU na Nyerere wakawa wanafahamika Tanganyika nzima na wananchi wanakiunga mkono chama.

Wanachama wakitoa nyumba zao kufanya ofisi za TANU.

Walifanya haya kwa ari na mapenzi sio kwa vitisho.

Hebu tuangalia hali ya leo mapokezi ya Dr. Hussein Mwinyi.

Muujiza gani umefanyika kuwaleta wananchi wa Pemba ngome ya ACT Wazalendo kujitokeza kwa wingi kiasi hiki?

Ni hii hofu ya jina kutoonekama katika daftari la mahudhurio au ni mapenzi ya dhati kwa Rais ‘’Mtarajiwa?’’

Au ni silka ya binadamu ile "cunning, wily people," watu walio na uwezo mkubwa wa ghilba na kulaghai.

Nasema haya kwa sababu CCM Pemba haijaweza kupata kiti hata kimoja katika miaka yote ya uchaguzi kutokea 1995.

Sasa cha kujiuliza ni hao washangiliaji wametokea wapi?

Kuna kitabu "The Ugly American," ni ‘’novel’’ na ‘’movie’’ kuhusu watu wa Mashariki ya Mbali katika tabia zao za ujanja wa kujifanya wajinga na wewe ukaamini kuwa ni wajinga kumbe ile ni mtego wao wanatega wanapokutana na adui.

Yawezekana tuliyoshuhudia ni katika sura mbili za Pemba?

Ikiwa yapo yaliyofanywa na CCM Pemba kupata wanachama na kuungwa mkono mimi yamenipita ningependa sana kujifunza kutoka kwenu kwani miujiza haifanyiki tena siku hizi.

Kila cha kustaajabisha lazima tukieleze kisayansi."
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom