Hotuba ya Bajeti ya msemaji Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni katika Wizara ya fedha na mipango, mheshimiwa Halima Mdee 2020|2021

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,987
144,319
Nimejaribu kupita mitandaoni, hasa Twitter kujaribu kuona reaction ya wadau hasa wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wasomi mbalimbali juu ya Bajeti ya Serikali iliyosomwa jana ila cha ajabu wanajadili au kuongelea maswala mengine tofauti huku Bajeti ya nchi wakiipa kisogo kama vile haipo, wakati kwa kawaida Bajeti inaposomwa tu watu mara moja huanza uchambuzi na mijadala jambo ambalo tangu jana mpaka asubuhi ya leo silioni mitandaoni zaidi ya hapa JF ingawa na penyewe mjadala wake umekosa mashiko kabisa.

Binafsi naona hii ni dalili ya watu kukatishwa tamaa na mwenendo wa Bajeti hizi za serikali kiasi kwamba wanaona mambo ni yale yale hivyo wanaona bora tu. waendelee na agenda zingine.

Anyway, ngoja tuone labda kuanzia leo watu wataanza kujijadili hiyo Bajeti.

Tusubiri hii ya leo ya upinzani labda inaweza kuipiga jeki bajeti ya serikali kwa kuiongezea hamasa japo kidogo.

1591949142512.png

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA HALIMA JAMES MDEE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU HALI YA UCHUMI WA TAIFA, MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021

Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016

_______________



A. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
kabla sijatoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu hali ya uchumi wa Taifa, Mpango wa Taifa wa Maendeleo na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2020/2021; napenda kutumia fursa hii kumpa pole Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (Mb) kwa tukio la shambulio dhidi yake ambalo lilimjeruhi na kupelekea kuvunjika mguu wake wa kulia. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inalaani kitendo hicho; na inaitaka Serikali kupitia vyombo vyake vya dola, kufanya uchunguzi wa haraka na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuhusika na uhalifu huo.

Mheshimiwa Spika, ninapohitimisha kipindi changu cha tatu cha miaka mitano mfululizo cha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na ninapohitimisha kipindi cha miaka mitano cha kuwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Fedha na Mipango; nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo nililotenda au nililotendewa katika kuitumikia nafasi yangu. Hii ni kwa sababu ninaamini kuwa; yote yalifanyika kwa mpango wake; na ni katika mpango wake huohuo, nimefanya yale niliyoweza kufanya na sikufanya yale ambayo sikuweza kufanya.

Mheshimiwa Spika, safari yangu hiyo ya utumishi na uwakilishi wa wananchi haikuwa rahisi; ilikuwa na vikwazo na changamoto nyingi. Lakini nanaendelea kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuvishinda vikwazo na changamoto zilizonikabili na hatimaye kuyaweza yote katika yeye anitiaye nguvu. Ninapenda kutumia nafasi hii kipekee kuwakumbuka wale wote tulioanza nao safari pamoja lakini leo hawapo nasi kwa kuwa wametangulia mbele ya haki. Mungu awape pumziko la milele. Haina maana kwamba sisi ambao Mungu ametuacha hai mpaka sasa ni wema kuliko hao waliotangulia; la hasha! bali ametupa muda zaidi ili tuyatimize mapenzi yake kupitia wajibu wetu; na zaidi sana ametupa nafasi ya upendeleo ili tujirekebishe kwa kutubu na kutenda mema ili tustahili kuurithi ufalme wa mbinguni. Ni namna gani tunautumia muda huo wa upendeleo ili kutimiza malengo hayo; kila mmoja atajibu kwa muda wake na kwa kadiri ya wajibu na nafasi yake.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa uhai wa Bunge hili la 11 unaelekea ukingoni na kwa maana hiyo kuifanya hotuba hii kuwa hotuba yangu ya mwisho kwa Bunge hili kama Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Fedha na Mipango; nitajielekeza zaidi kwenye kutoa tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano sambamba na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali katika kuutekeleza Mpango huo kwa kipindi cha mhula wa miaka mitano wa Serikali hii ya awamu ya tano.Aidha, nitazungumzia kwa kifupi sana majanga yanayolikabili taifa kwa sasa, na namna majanga hayo yalivyoathiri uchumi kwa ujumla na hususan makisio na upangaji wa Bajeti ya 2020/2021.



B. TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA TAIFA WA MAENDELEO WA MIKA MITANO 2016/17 – 2020/21
Mheshimiwa Spika,
hii ni bajeti ya tano na ya mwisho kwa Serikali hii ya awamu ya tano inayotarajiwa kuondoka madarakani mapema mwezi Oktoba mwaka 2020 baada ya kumaliza mhula wake wa miaka mitano ya uongozi. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeona ni wakati muafaka kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka mitano ili kuona ni kwa kiwango gani Serikali hii ya CCM imeweza kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika,
katika kufanya tathmini hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni itaonyesha hali ilivyokuwa mwaka 2015 wakati Mpango unaandaliwa; malengo yaliyokusudiwa kufikiwa hadi kufikia mwaka 2021 na hali halisi iliyofikiwa kwa utekelezaji hadi kufikia mwaka 2019. Hata hivyo, tathmini hii itahusu baadhi ya maeneo ya kipaumbele ambayo kimsingi yanabeba uwakilishi mkubwa wa Mpango mzima. Vyanzo vya Taarifa katika tathmini hii ni Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21; Taarifa ya Hali ya Uchumi 2018 na Hotuba za Bajeti Kuu za Serikali kwa miaka ya fedha 2016/17; 2017/18; 2018/19 na 2019/2020.

i. Wastani wa Ukuaji wa Uchumi
Mheshimiwa Spika,
Wakati Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano unamaliza muda wake mwaka 2015, wastani wa ukuaji wa uchumi ulikuwa ni asilimia 7. Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitanoambao ndio huu tulio nao sasa hivi ukaweka malengo ya ukuaji wa uchumi kwa wastani wa asilimia 10. Mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wasatani wa ukuaji wa uchumi ukashuka kwa asilimia 0.2 hadi kufikia ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017. Miaka miwili iliyofuata, yaani 2018 na 2019; ukuaji wa uchumi ulirejea kwenye wastani wa kawaida wa asilimia 7 lakini haukuweza kuvuka hapo!

Mheshimiwa Spika, tafsiri ya uchambuzi huo mdogo ni kwamba Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano umeshindwa kabisa (0%) kufikia lengo la wastani wa asilimia 10 la ukuaji wa uchumi. Kwa hiyo; Serikali ijue, inaposema uchumi wetu ni miongoni mwa chumi zinazokuwa kwa kasi katika Afrika ya Mashariki na Kati; ikumbuke pia kwamba imeshindwa kusogeza ukuaji wa uchumi wetu hata kwa nukta moja (0.1%) kwa kipindi chote cha miaka mitano iliyokaa madarakani na badala yake iliushusha ukuaji huo kwa nukta mbili (0.2%) katika mwaka wake wa kwanza wa kuwa madarakani.



ii. Pato la Wastani kwa Kila Mtu

Mheshimiwa Spika,
Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (huu unaotekelezwa sasa hivi) ulikusudia kupandisha pato la wastani kwa kila mtu kutoka Dola za Kimarekni 1,043 sawa na Shilingi za Kitanzania 2,412,459 mwaka

2015 hadi kufikia Dola za Kimarekani 1,500 sawa na shilingi za Kitanzania 3,469,500 itakapofika mwaka 2021.

Mheshimiwa Spika, Kinyume na matarajio hayo; mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Mpango huo; yaani mwaka 2017; Pato la Wastani kwa Kila Mtu liliweza kuongezeka kwa Dola Moja tu ya Kimarekani sawa na Shilingi 2,313 kwa kiwango cha ubadilishaji fedha (exchange rate) cha sasa na kufanya Pato jumla la Wastani kwa kila mtu kufikia Dola za Kimarekani 1,044 kutoka Dola 1,043 zilizokuwepo.

Mheshimiwa Spika, mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango, yaani 2018; Pato la Wastani kwa Kila Mtu liliongezeka kwa Dola za Kimarekani46 sawa na shilingi za Kitanzania 60,398 (kwa kiwango cha ubadilishaji fedha cha sasa cha dola moja kwa shilingi 2,313) na kufikia Dolar za Kimarekani 1,090 kutoka Dolar 1,044 zilizorekodiwa mwaka 2017.Hata hivyo, mpaka naandaa hotuba hii, hakukuwa na taarifa za ukuaji wa Pato la Wastani kwa Kila Mtu kwa mwaka 2019 na 2020.

Mheshimiwa Spika, ukitazama mwenendo wa ukuaji wa Pato la Wastani kwa kila mtu kwa miaka hiyo miwili ambayo taarifa zake zipo; utagundua kwamba hakukuwa na ongezeko la maana la Pato la Wastani kwa Kila Mtu ambalo Serikali hii inaweza kujivunia kwamba ilipiga hatua. Kwa mfano, tukichukulia kwamba ongezeko kubwa la Dola za Kimarekani 46 lililotokea mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango – yaani 2018 ndilo ongezeko litakalotokea kila mwaka; ina maana kwamba ili kufikia lengo la Mpango la kuwa na Pato la Dola za Kimarekani 1,500 kutoka Dola 1,043 zilizorekodiwa mwaka 2015; itatakiwa kuwe na ongezeko la Wastani wa Pato la Kila mtu la jumla ya Dola za Kimarekani 457 kwa kipindi chote cha miaka mitano ya utekelezaji wa Mpango. Hii ina maana kwamba, itachukua miaka takriba tisa (9) ili kufikia lengo hilo (kwa maana ya kugawanya Dola 457 dhidi ya ongezeko la kila mwaka la Dola 46).

Mheshimiwa Spika, ikizingatiwa kwamba huu ndio mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa mpango; na kuna nakisi kubwa namna hiyo ya kufikia lengo; Kambi Rasmi ya Upinzani inashawishika kuamini kwamba ama uandaaji wa Mpango huo ulikosewa (miscalculated) kwa kuweka makisio makubwa kuliko uwezo wa utekelezaji au Serikali imeshindwa kabisa kujiendesha kwa kushindwa kutekeleza Mipango yake (Failed State).



iii. Kiwango cha Umaskini
Mheshimiwa Spika,
Kiwango cha Umaskini kilichorekodiwa katika mwaka wa fedha 2011/12 kilikuwa ni asilimia 28.2. Hata hivyo, Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 - 2020/21) ulikusudia kupunguza kiwango hicho hadi kufikia asilimia 16.7 ifikapo 2021. Ili kufikia lengo la kupunguza kiwango cha umaskini hadi kufikia asilimia 16.7 kutoka asilimia 28.2 ilitakiwa umaskini upungue kwa asilimia 11.5 ndani ya kipindi chote cha miaka mitano ya utekelezaji wa Mpango. Hii ina maana kwamba kila mwaka ilitakiwa tuweze kupunguza umaskini kwa asilimia 2.3.

Mheshimiwa Spika, kinyume na matarajio hayo, kiwango cha umaskini kilipungua hadi kufikia asilimia 26.4 mwaka 2018 ikiwa ni sawa na punguzo la asilimia 1.8 na hii ikiwa ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango. Ikiwa punguzo la asilimia 11.5 ndio kiwango cha asilimia 100 cha kufikia lengo la kupunguza kiwango cha umasikini, ina maana kwamba punguzo la asilimia 1.8 ni sawa na kiwango cha asilimia 15.6 tu cha utekelezaji wa Mpango katika kufikia lengo la kupunguza kiwango cha umaskini hadi kufikia asilimia 16.7. Kwa maneno mengine Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano umeshindwa kwa asilimia 84.4 kufikia lengo lake la kupunguza kiwango cha umaskini kutoka asilimia 28.2 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 16.7 ifikapo 2021.



iv. Uwekezaji wa Mitaji Kutoka Nje
Mheshimiwa Spika,
mwaka 2014, uwekezaji wa mitaji kutoka nje hapa nchini ulikuwa ni wa jumla ya Dola za Kimarekani bilioni 2.4 sawa na Shilingi za Kitanzania takriban trilioni 5.5. Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo uliweka malengo ya kuongeza uwekezaji huo hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 9 sawa na shilingi trilioni 20.8 (kwa kiwango cha ubadilishaji fedha (exchange rate) cha shilingi 2,313 kwa Dola moja ya Kimarekani).

Mheshimiwa Spika, ili kufikia lengo hilo ilitakiwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ambacho Serikali hii ya awamu ya tano imekaa madarakani uwekezaji wa mitaji ya nje uwe umeongezeka kwa jumla ya Dola za Kimarekani bilioni 6.6 sawa na shilingi trilioni 14.8 (kwa maana ya kutoka Dola bilioni 2.4 hadi Dola bilioni 9 kama mpango ulivyokusudia).

Mheshimiwa Spika, tofauti na malengo hayo ya Mpango, uwekezaji wa Mitaji kutoka nje ulifikia Dola za Kimarekani bilioni 4.634 mwaka 2016, ikiwa ni ongezeko la Dola bilioni 2.234 kutoka dola bilioni 2.4 zilizorekodiwa mwaka 2014. Mwaka 2018 uwekezaji ulifikia Dola za Kimarekani bilioni 5.393, ikiwa ni ongezeko la Dola milioni 759 kutoka dola bilioni 4.634 zilizorekodiwa mwaka 2016.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hakuna taarifa za uwekezaji wa mitaji kutoka nje kwa mwaka 2019 na 2020; Kambi Rasmi ya Upinzani inachukulia kwamba kwa kipindi chote cha miaka mitano cha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, uwekezaji wa mitaji kutoka nje uliongezeka kwa wastani wa Dola za Kimarekani bilioni 1.4965 kutoka dollar bilioni 2.4 zilizorekodiwa mwaka 2914 na kutoka dola bilioni 4.634 zilizorekodiwa mwaka 2016.

Mheshimiwa Spika,
Ongezeko hilo la uwekezaji wa mitaji toka nje la wastani wa Dolla bilioni 1.4965 ni sawa na asilimia 16.6 tu ya malengo ya Mpango ya kufikia uwekezaji wa mitaji kutoka nje wa Dolla za Kimarekani bilioni 9 ifikapo 2021. Hii ina maana kwamba, Serikali imeshindwa kwa kiwango cha asilimia 84.4 kuutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano. Na kwa kuwa kuna janga la Corona ambalo bado haijulikani litakwisha lini; upo uwezekano mkubwa wa kuendelea kuporomoka kwa uwekezaji wa mitaji kutoka nje.

v. Uzalishaji wa Umeme
Mheshimwa Spika,
Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka mitano ulikusudia kupandisha kiwango cha uzalishaji wa umeke kutoka MW 1,501 zilizokuwepo mwaka 2015 hadi kufikia MW 4,915 ifikapo 2020. Hata hivyo, hadi kufikia mwaka 2020; ikiwa

ni mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa Mpango, Serikali imeweza kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme hadi kufikia MW 1,603.38. Kiwango hiki ni sawa na ongezeko la MW 102.38 kutoka MW 1,501 zilizorekodiwa mwaka 2015.

Mheshimiwa Spika, ilikufikia lengo la kuzalisha MW 4,915, ilitakiwa katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Mpango kuwe na uzalishaji wa MW 3,414. Kwa hiyo, uzalishaji wa MW 102.38 uliofanywa ni sawa na asilimia 2.9 tu ya lengo. Hii maana yake ni kwamba Mpango umeshindwa kufikia lengo la uzalishaji wa MW 4,915 kwa asilimia 97.1

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa sana na utekelezaji duni kiasi hiki wa Mpango katika kipengele cha uzalishaji wa umeme hasa ukizingatia kwamba Serikali hii imekuwa ikiwaaminisha wananchi kuwa uzalishaji wa umeme unaridhisha na kwamba Serikali ina mpango wa kuanza kuuza umeme kwa nchi jirani kutokana na utoshelevu wa umeme nchini. vi. Vifo vya Mama Wajawazito wakati wa Kujifungua

Mheshimiwa Spika,
Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulikusudia kupunguza vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua hadi kufikia vifo 250 kati ya mama wajawazito 100,000 wanaojifungua kutoka vifo 432 kati ya mama wajawazito 100,000 wanajifungua vilivyorekodiwa mwaka 2014/15.

Mheshimiwa Spika, badala ya vifo vya mama wajawazito wanaojifungua kupungua kadiri ya malengo ya Mpango; vifo hivyo vimekuwa vikiongezeka kila mwaka. Kwa mujibu wa Shirika

la Afya Duniani (WHO); vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua vilifikia 556/100,000 mwaka 2016/17; 524/100,000 mwaka 2017 na 578/100,000 mwaka 2018. Takwimu hizi zinaonyesha kwamba; kumekuwa na ongezeko la vifo 124, 92 na 146 kati ya akina mama 100,000 wanaojifungua kwa mtiririko wa miaka tajwa ikilinganishwa na vifo 432 vilivyorekodiwa mwaka 2014/15.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatafsiri ongezeko hili la vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua kama taswira halisi ya Serikali hii ya CCM kupuuzia na kutolichukulia kwa uzito stahili suala la afya ya mama na mtoto. Kwakuwa katika eneo hili la kupunguza vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua Serikali imeshindwa kupunguza kifo hata kimoja kutoka vifo 432/1000 vilivyorekodiwa mwaka 2014/15 na hivyo kupata alama chini ya asilimia sifuri katika utekelezaji wa mpango kuhusu jambo hilo; Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kujibu maswali yafuatayo; Je, hakukuwa na bajeti ya kutosha kutekeleza mpango wa kupunguza vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua ndio maana vifo vimeongezeka au vifo hivyo vilitokana na uzembe wa watendani katika Wizara ya Afya na Ofisi ya Rasi (TAMISEMI). Kwa majibu yoyote yale; Serikali imechukua hatua gani kuhakikisha kuwa vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua vinapungua? vii. Huduma ya Maji Safi na Salama Vijijini

Mheshimiwa Spika,
hili ni eneo muhimu sana kwa maisha ya wananchi kwa kuwa maji ni mojawapo ya mahitaji msingi ya binadamu ili aweze kuishi. Kutokanana umuhimu wa maji katika maisha ya wananchi; na kwa kutambua changamoto nyingi zinazowakabili wananchi waishio vijijini ikiwemo ya upungufu wa huduma za maji, Mpango ulikusudia kuongeza kiwango cha huduma ya maji safi na salama vijijini hadi kufikia zaidi ya asilimia 80 ifikapo 2021 kutoka asilimia 72 iliyorekodiwa mwaka 2014/15.

Mheshimiwa Spika, kinyume na malengo hayo ya Mpango; kiwango cha huduma ya maji safi na salama vijijini kilipungua hadi kufikia asilimia 64.8 kutoka asilimia 72 iliyorekodiwa mwaka 2014/15 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 7.2



Mheshimiwa Spika, kushindwa kufikiwa kwa malengo ya

Mpango kunatokana na mapungufu yafuatayo:-

i. Kukosekana kwa Sheria ya Kusimamia Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo:-
Mheshimiwa Spika,
tangu wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011/12-2015/16); na kwa miaka yote minne ya utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleleo 2016/17 – 2020/2021; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikiisisitiza Serikali kuleta Muswada wa Sheria Bungeni ili kukidhi matakwa ya ibara ya 63(3) (c) ya Katiba ya Nchi ya kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa Mpango wowote unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano.

Mheshimiwa Spika, hili halikuwa pendekezo la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na wala halikuwa ombi; bali ni sharti la kikatiba; na kazi ya Upinzani ilikuwa ni kuikumbusha Serikali kutimiza wajibu huo wa kikatiba. Na lengo la kufanya hivyo lilikuwa ni kuisaidia Serikali kuweka utaratibu mzuri wa kisheria wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ili kudhibiti vikwazo vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wa mipango hiyo na hivyo kuifanya Serikali iweze kufikia malengo iliyokusudia kuyafikia katika mipango hiyo.

Mheshimiwa Spika,
pamoja na nia hiyo njema ya

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Serikali, Serikali hii ya CCM haijawahi hata mara moja kutekeleza wajibu huo wa kikatiba; ikiwa tunaingia mwaka wa kumi wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Kumi na Mitano, uliogawanywa katika vipindi vitatu vya miaka mitano mitano (yaani mpango wa kwanza 2011/12 -2015/16; mpango wa pili 2016/17 – 2020/21 na mpango wa tatu 2021/22 – 2025/26.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilieleza jinsi Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) ulivyoshindwa kufikia malengo yake kwa takriban asilimia 50, kutokana na kukosekana kwa sheria ya kusimamia utekelezaji wake ambapo mambo yalikuwa yakifanyika kiholela.

Mheshimiwa Spika, hatari ya kushindwa kufikia malengo ya Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano (2016/17 – 2020/21) imekuwa kubwa zaidi kwa kuwa Serikali hii ya awamu ya tano imeacha utamaduni wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, na badala yake utashi na maelekezo ya viongozi; na hasa kiongozi mmoja; ndiyo yanachukuliwa kama dira ya kuiongoza Nchi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inathubutu kusema kwamba; Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo umefeli kwa kuwa tuko kwenye mwaka wa mwisho wa utekelezaji wake ikiwa malengo yake makubwa hayajafikiwa kwa hata robo. Lengo kuu la Mpango wa Pili lilikuwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania inaingia katika uchumi wa kipato cha kati. Serikali iwaambie wananchi, ni viashiria gani vya uchumi wa kipato cha kati vimeanza kuonekana ikiwa ajira na fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara na wakulima zimebanwa na vipato kwa wananchi vimeporomoka? Na hali imekuwa mbaya zadi hasa kwa kipindi hiki ambacho taifa linakumbwa na janga la Corona!

Mheshimiwa Spika, lengo jingine la Mpango wa Pili lilikuwa kuziimarisha Serikali za Mitaa katika kupanga na kutekeleza mipango yao. Serikali ijipime imefikia lengo hilo kwa kiwango gani ikiwa imezifilisi mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzinyang’anya vyanzo vya mapato na kuzifanya kuwa ombaomba kwa Serikali Kuu? Lengo jingine lilikuwa ni kuboresha viwango vya maisha ya watu. Serikali ijipime imefikia lengo hilo kwa kiwango gani ikiwa kila mwananchi analia ukata na ugumu wa maisha kiasi cha kushindwa kumudu gharama za milo mitatu kwa siku. Bado wapo wananchi wanaoishi chini ya dola moja kwa siku!! Je, hayo ndiyo maisha bora kwa watanzania?

Mheshimiwa Spika, si nia yangu kufanya tathmini ya kila lengo, isipokuwa nataka kusisitiza kwamba tunashindwa kufikia malengo hayo kwa kuwa utekelezaji wa malengo hayo hauna mwongozo wa kisheria; na pia watekelezaji wanajua kwamba hata wasipofikia hayo malengo hawawajibiki kisheria. Ndio maana bado Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza kwamba; kama Serikali itaendelea kupuuzia matakwa ya Katiba ya Nchi ya kutaka kuwe na sheria ya kusimamia utekelezaji wa Mipango yetu ya Maendeleo; tutakuwa tukipanga mipango ambayo haitekelezeki na hivyo kuendelea kutumia vibaya fedha za umma kutekeleza mipango ambayo haifikii malengo yake.



ii. Kutotekeleza Bajeti ya Miradi ya Maendeleo

Kikamilifu
Mheshimiwa Spika,
hoja nyingine ya msingi ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika utekelezaji bora wa Mipango ya Maendeleo hapa nchini ni tabia sugu ya Serikali ya kutotekeleza Bajeti ya Miradi ya Maendeleo kama ilivyopitishwa na Bunge. Hii ni hoja ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikiipigia kelele tangu wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo mpaka kipindi hiki cha utekelezaji wa Mpango wa Pili.

Mheshimiwa Spika, si jambo la kubishaniwa kwamba; ili Mpango wowote uweze kutekelezwa unahitaji bajeti (kwa maana ya fedha za kuutekeleza mpango huo). Hata hivyo, pamoja na ukweli na uhalisia huo; Serikali yetu kwa muda mrefu, imekuwa ikitoa fedha pungufu ya zile zilizoidhinishwa na Bunge kutekeleza miradi ya maendeleo inayokuwa imepangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha husika. Mbaya zaidi, fedha hizo hutolewa kwa kuchelewa na hivyo kushindwa kutelekeleza kazi zilizokuwa zimepangwa kwa wakati au muda husika.

Mheshimiwa Spika, ili kuthibitisha hoja hii ni kwamba

Katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 Mpango wa Taifa wa Maendeleo ulitengewa shilingi trilioni 12.25 sawa na 37 ya bajeti nzima ya Serikali. Hata hivyo, Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali Uchumi iliyosomwa hapa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango jana tarehe 11 Juni, 2020; fedha iliyopelekwa ni shilingi trilioni 7.63 tu sawa na asilimia 62.04 ya fedha iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge.



Mheshimiwa Spika, Upungufu huo wa utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo kwa ujumla wake umeathiri pia utekelezaji wa bajeti za maendeleo katika sekta mbalimbali. Si nia yangu kutoa mifano mingi ya namna Serikali inavyofanya utekelezaji duni wa bajeti ya maendeleo; lakini kwa ajili ya kuipa nguvu hoja hii nitatoa mifano ya sekta kadhaa hususan zile zinazogusa maisha ya wananchi wengi moja kwa moja:-

(a) Sekta ya Kilimo
Mheshimiwa Spika,
ukichukua sekta ya Kilimo ambayo inakadiriwa kuajiri takriban asilimia 80 ya watanzania, bajeti ya maendeleo imetekelezwa kwa wastan wa asilimia 17.55 kwa miaka yote minne ya utawala wa Serikali hii. Hii ni kwa mujibu wa Randama za Wizara ya Kilimo ambapo, mwaka 2016/17 bajeti ya maendeleo kwenye Kilimo ilitekelezwa kwa asilimia 2.22; mwaka 2017/18 asilimia 11, mwaka 2018/19 asilimia 42, na mwaka 2019/2020 asilimia 15.

Mheshimiwa Spika, ikiwa Serikali imetekeleza bajeti ya maendeleo kwenye kilimo kwa wastani wa asilimia 17.55; hii ina maana kwamba, asilimia 82.45 ya bajeti ya maendeleo kwenye Sekta ya Kilimo haikutekelezwa! Kwa maneno mengine, asilimia 82.45 ya miradi ya maendeleo ya Kilimo haikutekelezwa! Hapa utajua ni kiasi gani cha ajira kwa wananchi wanaotegemea kilimo zilipotea. Aidha, unaweza pia kufanya hesabu ni kiasi gani cha hasara kilichopatikana kutokana na kutotekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia mnyororo wa thamani ya mazao ya Kilimo (Value chain in Agro Economy)

Mheshimiwa Spika, licha ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, kuitambua Sekta ya Kilimo kama eneo muhimu ambapo mpango- mkakati wa kiuchumi

utatekelezwa ili kuchangia kujenga msingi imara wa uchumi wenye ushidani na wenye nguvu; na licha ya Mpango Mkakati kuweka malengo ya kubadilisha kilimo kutoka kwenye uzalishaji mdogo kwenda kwenye uzalishaji mkubwa na hivyo kuchangia ukuaji wa viwanda; Ukaguzi wa Ufanisi uliofanywa na CAG umebaini kwamba Serikali imeshindwa kubadili kilimo na kukifanya kuwa cha kisasa ili kichangie katika ukuaji wa uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Spika, miongoni mwa changamoto zilizobainika katika sekta ya Kilimo tofauti na utekelezaji duni wa bajeti ya maendeleo katika sekta hiyo ni pamoja na hizi zifuatazo:-

K atika kipindi cha miaka mine iliyopita, ni wastani wa 39% tu ya ugavi wa pembejeo za kilimo uliofanyika ikiwa ni pamoja na mbegu,mbolea na viuatilifu.

U sambazaji wa pembejeo zisizo na ubora

kutokana na udhibiti dhaifu

U wepo wa wauzaji na mawakala wa pembejeo za kilimo ambao hawakusajiliwa pamoja na pembejeo za kilimo zisizosajiliwa katika soko. iv.

Ukaguzi ulibaini 33% ya mawakala wa Kilimo hawakusajiliwa kuuza mbegu na Mbolea kwenye soko.

U kaguzi ulibaini kwamba hadi kufikia mwaka 2018 Wizara ya kilimo ilishindwa kufanya utafiti wa msingi ili kujua mahitaji halisi ya pembejeo kwa wakulima walioko nchini kwa kuzingatia ikolojia na idadi ya wakulima. Wizara ya kilimo inatumia makadirio tu ili kuweza kupata mahitaji ya wakulima. Maelezo ya Wizara ni kwamba kufanya utafiti wa msingi kwenye pembejeo za

kilimo ni gharama!! Kwa sasa Mbolea inayosambazwa nchini haizingatii hali ya uhitaji wa udongo katika maeneo mbalimbali nchini. Ukaguzi ulibaini kutoshirikishwa kwa wakulima wakati wa mchakato wa kutambua mahitaji ya pembejeo nchini hivyo kupelekea mahitaji kutojumuisha aina ya pembejeo zinazokidhi mahitaji ya kanda mbalimbali za kilimo.

A silimia 90 ya viuatilifu vinavyotumika nchini vinaingizwa toka nje ya nchi. Na hakuna utafiti wa msingi uliofanywa na wizara ya Kilimo ili kuweza kusaidia uingizaji wa viuatilifu nchini.

T athmini ya ujuzi na ufahamu wa pembejea za Kilimo ilionyesha kuwa wakulima hawakuwa na ujuzi wa matumizi mazuri ya mbegu , viuatilifu na mbolea. Maafisa ugani hawakuwa na ujuzi wa utoaji wa huduma za utaalam wa kilimo kwa wakulima ambazo ni pamoja na matumizi sahihi ya mbegu,viuwatilifu na mbolea.

U kaguzi ulibaini kwamba ni 3% tu ya miradi ya umwagiliaji ndiyo ilifanyiwa upembuzi yakinifu kati ya miradi iliyopangwa kufanyiwa , kinyume na sheria ya umwagiliaji . Kati ya pembuzi yakinifu 360 zilizopangwa kufanywa, zilizotekelezwa ni 11

tu.

U kaguzi ulibaini kuwepo kwa utegemezi wa fedha za wafadhili zilizofikia 90% ya fedha zote zilizotolewa kwa ajili ya kugharamia miradi ya umwagiliaji kuanzia mwaka 2014/15 hadi 2017/18.

U kaguzi ulibaini maafisa UGANI hawakuwezeshwa na nyenzo na maarifa ya kisasa kuhusu utoaji wa huduma za ugani ili kuwapa ujuzi wa mbinu mpya.

U kaguzi ulibaini udhaifu katika mchakato wa bajeti. Shughuli za ugani zilitengewa kiasi kidogo cha fedha na baadhi ya fedha zilizotengwa zilitumika kwenye shughuli nyingine. Utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji wa kilimo kwa sababu ina uwezo wa kubadilisha changamoto zingine zote ili kuboresha maisha na ustawiwa wananchi. Huduma za ugani, utafiti na mafunzo zina umuhimu katika kuunganisha wakulima kupata teknolojia mpya, taarifa na ujuzi ambao ni muhimu katika kuimarisha uzalishaji wa Kilimo.

I libainika pia kwamba ni asilimia 1 tu ya wakukima ndio walipewa mafunzo ya mbinu bora za kilimo.

I libainika kuwa maafisa ugani hawakuwa wanapatiwa mafunzo vizuri, wengi walikuwa wanategemea elimu walizopata vyuoni.

U kaguzi ulibaini kwambani 9% tu ya wajasiriamali wakiwemo wasindikaji wa mazao ya kilimo na wenye viwanda vidogo waliosajiliwa na shirika la maendeleo la viwanda vidogo walipatiwa mafunzo huku 37% hawakupata Mikopo licha ya kukidhi vigezo.

K wenye Mbegu na Mbolea imebainika kwamba kutosambazwa kwa wakati kwa pembejeo husababishwa na uwezo mdogo wa wazalishaji wa ndani kuzalisha pembejeo za Kilimo hapa nchini. Uzalishaji wa ndani husaidia upatikanaji kwa wakati wa pembejeo ikilinganishwa na uingizaji wa pembejeo kuoka nje ambao huchukua muda mrefu kwa sababu inajumuisha mchakato wa manunuzi,usafirishaji na usambazaji mikoani kutokea kwenye mipaka iingayo nchini. xvi. U zalishaji mdogo wa Mbegu bora wa wakala wa Mbegu ni matokeo ya kukosekana kwa mashamba ya Mbegu yenye tija. Ilibainika kwamba ni shamba 1 tu la Mbegu kati ya mashamba 9 yanayozalisha mbegu ndio lina uwezo wa kuzalisha mbegu katika kipindi cha mwaka mmoja. Shamba hilo pekee ndio limewekewa mifumo ya umwagiliaji wakati mashamba mengine 8 yanategemea mvua kuzalisha mbegu.

K wa kipindi cha mwaka 2015-18 , wakala wa Mbegu uliweza kuzalisha kwa kiwango cha juu cha msimu ambacho ulizalisha asilimia 2.2 ya malengo waliojiwekea wa kuzalisha tani 36,000.

B

ei za pembejeo ziko juu sana, hali iliyosababishwa na serikali kushindwa kutekeleza makubaliano ya utoaji ruzuku kwa wakulima . Ilibainika makubaliano yalikuwa ni kulipia asilimia 50 ya gharama za pembejeo (sh.200,000) kama ruzuku. Hata hivyo ilibainika kwamba serikali ilitoa kiasi cha shilingi 78,500 kama mchango wake ambao ni sawa na 39% ya gharama za pembejeo. Hivyo wakulima kutakiwa kuchangia 61% badala ya 50% ya Bei ya soko. Gharama za kununua pembejeo zilikuwa zikikaribiana na kipato ambacho Mkulima hukipata baada ya kuuza mazao yako.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kulieleza Bunge hili itawezaje kufikia malengo yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati kupitia mageuzi ya viwanda ikiwa imeshindwa kuihudumia Sekta ya Kilimo ambayo ndiyo mzalishaji mkubwa wa malighafi za viwanda? Aidha, Serikali ilieleze Bunge, ni kwa namna gani Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa ikiwa bajeti yake ya maendeleo na hususan Kilimo cha Umwagiliaji ni tegemezi kwa fedha za nje kwa asilimia 90?



(b) S ekta ya Afya
Mheshimiwa Spika,
ukienda kwenye Sekta ya Afya – ambayo ndiyo sekta inayoshikilia sekta nyingine kwa maana kutoa hakikisho la nguvu kazi yenye afya (healthy labourforce); hali ni mbaya zaidi. Kwa mfano, Bajeti nzima ya Afya ilipungua kutoka shilingi trilioni 1.07 mwaka 2017/18 mpaka kufikia shilingi billion 866.233 mwaka 2018/19 ikiwa ni anguko la shilingi bilioni 211.468 sawa na asilimia 19.622.

Mheshimiwa Spika, ukiachilia mbali kuporomoka kwabajeti ya afya; bado utekelezaji wa bajeti ya maendeleo kwenye sekta ya afya umekuwa kizungumkuti! Kwa mujibu wa Taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Sekta ya Afya ni kwamba kwa mwaka wa fedha 2018/2019 fedha za miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya zilizokuwa zimetolewa hadi kufikia Machi, 2019 zilikuwa ni asilimia 16 tu! Hii ni sawa na kusema kwamba bajeti ya maendeleo katika sekta ya afya haikutekelezwa kwa asilimia 84 kwa mwaka husika.

Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2019/20 wizara ya Afya ilitengewa jumla ya shilingi bilioni 544.137; lakini hadi kufikia mwezi Machi, 2020 kiasi cha fedha kilichokuwa kimetolewa ni shilingi bilioni 83.066 sawa na asilimia 15.3 tu ya bajeti ya maendeleo. Aidha kati ya fedha zilizotolewa, fedha za ndani ni asilimia 9.2 na za nje ni asilimia 21.

Mheshimiwa Spika, sambamba na utekelezaji duni wa bajeti ya afya, bado lipo tatizo la muda mrefu la Serikali mosi, kutopeleka kikamilifu fedha za MSD ziliyoidhinishwa na Bunge na pili kutolipa madeni ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) jambo ambalo limekuwa na athari kubwa katika ufanisi wa Bohari hiyo. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali ya 2018/19 deni la Serikali limeongezeka kwa kiasi cha shilingi bilioni 16.18 kutoka shilingi bilioni 37.45 za mwaka uliopita na hivyo kufanya jumla ya deni kuwa shilingi bilioni 53.63. Hali hii imesababisha ukwasi wa Bohari Kuu ya Dawa kuzidi kudidimia hali inayoweza kuathiri utekelezaji wa mipango mbalimbali ikiwamo usambazaji wa dawa na vifaatiba kwa jamii pamoja na utekelezaji wa mipango yake mbalimbali. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaungana na CAG kuitaka Serikali ilipe madeni yake kwa Bohari Kuu ya Dawa kikamilifu na kwa wakati, ili kuleta tija katika utendaji na kuongeza wigo wa usambazaji wa dawa na vifaatiba kwa jamii na hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID - 19.

(c) S

ekta ya Viwanda na Biashara
51. Mheshimiwa Spika,
mgawo wa fedha za maedeleo katika Sekta ya Viwanda na Biashara kwa miaka mitatu iliyopita ilikuwa kama ifuatavyao. Mwaka 2016/17 fedha iliyotolewa ilikuwa ni asilimia 44; 2017/18 asilimia 9.51; na 2018/19 asilimia 6.5. Ukitafuta wastani wa utekelezaji wa bajeti katika sekta hii kwa miaka tajwa utagundua kwamba bajeti ya maendeleo katika sekta ya viwanda na biashara imetekelezwa kwa kwa asilimia 20 tu kwa miaka yote minne ya utekelezaji.

(d) Sekta ya Maji
Mheshimiwa Spika,
kwenye sekta ya maji mgawo wa bajeti ya maendeleo ulikuwa kama ifuatavyo. Mwaka2016/17 asilimia 25; mwaka 2017/18 asilimia 22, mwaka 2018/19 asilimia 15 na 2019/2020 asilimia 61.9

Mheshimiwa Spika, mbali na utekelezaji duni wa bajeti ya maendeleo katika sekta ya maji; ukaguzi wa ufanisi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika mwaka wa fedha 2018/19 ulibaini kuwa sekta ya maji inakabiliwa na changamoto zifuatazo:-

z aidi ya 30% ya skimu za maji vijijini hazikufanya kazi vizuri (uk.5 ripoti)

9

% ya idadi ya watu nchini ndio wamefikiwa na maji taka. Kati ya 72% ya watu wanaopata maji mijini 9% wako kwenye mfumo wa maji taka. 91% wanategemea magari au maji ya vyoo kuririka mtaani

N i asilimia 58.7 tu ya watu wanaoishi vijijini wanapata maji safi na salama

M iundombinu ya maji ilijengwa bila ya kuwa na vyanzo vya uhakika

K ati ya sampuli 6615. Sampuli 709 (10%) hazikuwa na viwango vya kutumiwa na binadamu (Sampuli hizo zilibainika kuwa na chuma, madini ya manganizi, fluoride,nitrate,vimelea vya magonjwa nk) vi.

Kulikuwa na Makandarasi wasiokuwa na sifa na uwezo wa kutekeleza miradi ya maji na pia hakukuwa na uhakiki wala tathmini ya uwezo wa makandarasi.

T amisemi na Wizara ya Maji haina mikakati endelevu ya kutenga Bajeti kwa ajili ya miradi ya Maji. Aidha,Wizara ya Maji inapokea chini ya 41%

(wastani kwa Mwaka) wa bajeti ya maendeleo

K utokukamilika kwa miradi ya maji iliyoanzishwa nan na pia kuongezeka kwa riba kutokana na kucheleweshwa kwa malipo kwa wakandrasi.

S erikali bado haijafikia malengo ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na huduma bora za usafi wa mazingira ili kuboresha maisha yao

K wa miaka mitatu mfululizo (2010/11-2013/14. Miradi ya maji iligharibu 27% ya Bajeti ya manunuzi ya nchi. Takribani trillion 2.8 zilitumika kwenye miradi ya Maji. Hata hivyo 46% ya miradi iliyotekelezwa haikufanya kazi kama ilivyokusudiwa.



54. Mheshimiwa Spika,
Hizi ni Wizara kama mfano. Lakini ukifanya tathmini ya utoaji wa fedha za maendeleo kwa wizara nyingine hali ni hiyo hiyo. Hakuna wizara inayopata fedha zote za maendeleo kwa asilimia 100. Kwa mwenendo huo, hakuna muujiza wowote unaweza kutendeka ili Mipango yetu ya Maendeleo iweze kutekelezwa kwa ufanisi, ikiwa Serikali haitoi fedha zote za maendeleo kama zilivyoidhinishwa na Bunge na kwa wakati.



xix. Matumizi ya Fedha nje ya Mpango wa Bajeti (Budget Reallocation):-
Mheshimiwa Spika,
kama nilivyosema hapo awali, ili mpango wowote wa maendeleo uweze kutekelezwa unahitaji bajeti; lakini hilo halitoshi; inahitajika pia nidhamu ya matumizi ya bajeti hiyo. Kama mpango umeanisha mambo kumi ya kutekeleza na ikatengwa bajeti ya kutosha kutekeleza mambo hayo kumi; kutumia fedha yoyote katika bajeti hiyo kwa ajili ya kutekeleza mambo mengine ambayo hayakuwa yameainishwa katika Mpango husika; huko ni kuuvuruga Mpango; na huko ni kukosa nidhamu ya matumizi ya bajeti iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya kuutekeleza mpango husika.

Mheshimiwa Spika, hali kama hiyo inapotokea; inakuwa vigumu sana kufikia malengo ya Mpango uliokusudiwa kwa kuwa unakuwa umeshavurugwa tayari kwa kuingiza mambo mengine ambayo hayakuwepo awali.



xx. Kukosekana kwa Uwajibikaji katika Masuala ya Fedha
Mheshimiwa Spika,
pamoja na mambo mengine yote, uwajibikaji ni sifa ya msingi kabisa inayopelekea ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wowote wa Maendeleo. Wanazuoni wa mausala ya utawala bora wanasema kwamba; naomba kunukuu “Accountability is the obligation of power holders to take responsibility for their actions”. Hii maana yake ni kwamba, uwajibikaji ni ile hali ya wenye madaraka kutambua kwamba wamekosea na kuchukua hatua ya kuwajibika kwa makosa waliyoyafanya.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani imekuwa ikipigia sana kelele suala hili la uwajibikaji katika masuala ya fedha kutokana na kitendo cha Serikali kuonekana dhahiri ikikwepa kuwajibika katika mchakato mzima wa usimamizi wa Mipango ya Maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kwa miaka yote mitano ya utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Mandaleo na kwa miaka yote minne ya utekelezaji wa Mpango wa Pili; Kambi Rasmi ya Upinzani ilionyesha jinsi Serikali inavyokwepa uwajibikaji katika kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo; Mosi, kwa kushindwa kuleta Muswada Bungeni kwa ajili ya Kutunga Sheria ya kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama Ibara ya 63(3)(c) ya Katiba inavyoelekeza; lakini pili, kwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Bajeti ili kuondoa vipengele vilivyokuwa vinaibana Serikali kuwajibika katika masuala ya fedha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani ilieleza kwamba; kitendo cha Serikali kuifanyia marekebisho sheria ya bajeti ambayo inatoa mwongozo wa uwajibikaji wa kifedha/kibajeti (financial accountability) katika kutekeleza miradi ya maendeleo ni uthibitisho tosha wa Serikali kukwepa uwajibikaji.

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kwamba, mwaka

2018, Serikali ilileta mapendekezo ya kuvifanyia marekebisho vifungu vya 41, 53, 56, 57 na 63 vya sheria ya bajeti ya 2017 kwa kuondoa wajibu wa Serikali wa kuwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Bungeni ripoti ya matumizi ya fedha kwa kila robo mwaka ya mzunguko wa bajeti (yaani kila baada ya miezi mitatu) ambapo sasa ripoti hiyo itakuwa ya nusu mwaka wa mzunguko wa bajeti (yaani kila baada ya miezi sita).

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani ilieleza kwamba; athari za marekebisho hayo ya sheria ya bajeti ilikuwa ni kudumaza ufuatiliaji thabiti (tight follow-up) wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali; na jambo hilo linaweza kupelekea utekelezaji mbovu wa bajeti kutokana na matumizi yasiyofaa au hata ubadhirifu wa fedha za umma. Sababu ya kueleza hivyo ilitokana na ukweli kwamba; ikiwa ripoti ya matumizi ya Serikali itatolewa kwa kila nusu mwaka wa utekelezaji wa bajeti, maana yake ni kwamba, ripoti hiyo itatoka wakati mchakato wa maandalizi ya mpango wa maendeleo na bajeti ya mwaka wa fedha unaofuata ukiwa umeshaanza. Kwa hiyo, ripoti hiyo inakuwa haisaidii katika kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika mwaka wa fedha unaoendelea (current financial year) ili hatimaye kuweza kufanya makisio na maoteo ya bajeti inayofuata.

Mheshimiwa Spika,Kwa minajili ya kuwa na tija katika Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo; Kambi Rasmi ya Upinzani ilishauri na kupendekeza kwamba; Serikali ilete muswada wa marekebisho ya sheria ya bajeti ili kurejesha vile vifungu vilivyokuwa vinaelekeza ripoti za matumizi ya fedha ziwe zinaletwa kila baada ya miezi mitatu (robo mwaka). Kwa kufanya hivyo, kwanza kutakuwa na ufuatiliaji madhubuti wa matumizi ya Serikali, lakini pia ripoti za robo mwaka, zitawezesha kufanya tathmini ya mwenendo wa utekelezaji wa bajeti na hivyo kuisadia Serikali kujipanga vizuri zaidi kwa bajeti zinazofuata”.



C. SERIKALI IFANYE MAPITIO YA MAKISIO YA BAJETI DHIDI YA

VYANZO HALISI VYA MAPATO NA UWEZO WA MAKUSANYO YA MAPATO
Mheshimiwa Spika,
kwa miaka minne mfululizo; Serikali imekuwa ikifanya makisio makubwa ya bajetibila kuoanisha makisio hayo na vyanzo halisi vya mapato na pia uwezo wake wa kukusanya mapato; jambo ambalo limesababisha Serikali kushindwa kufikia lengo la makusanyo kwa miaka yote.

Mheshimiwa Spika,ukifanya tathmini ya miaka minne iliyopita, utaona kwamba kuna tatizo kubwa kwenye ukusanyaji wa mapato. Kwa mfano, katika mwaka wa fedha 2016/17 Serikali ilipanga kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 29.54[SUP][1][/SUP] lakini iliweza kukusanya mapato kutoka vyanzo vyote yaliyofikia shilingi trilioni 20.7[SUP][2][/SUP] sawa na asilimia 70.1 ya lengo. Hii ina maana kwamba, asilimia takriban 30 iliyobaki (sawa na shilingi trilioni 8.83) ilikuwa ni nakisi ya bajeti husika na kwa maana hiyo bajeti ya mwaka husika haikutekelezwa kwa asilimia 30. Aidha, katika mwaka wa fedha 2017/18 Serikali ilipanga kukusanya jumla ya shilingi trilioni 31.71[SUP][3][/SUP] lakini iliweza kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 21.89[SUP][4][/SUP] sawa na asilimia 69

ya lengo. Hii ina maana kwamba, asilimia 31 iliyobaki (sawa na shilingi trilioni 9.82) ilikuwa ni nakisi ya bajeti na kwa maana hiyo, bajeti ya mwaka husika haikutekelezwa kwa asilimia 31.



[TD valign="top"]
66.
[/TD]

Mheshimiwa Spika, katika muktadha huohuo, katika mwaka wa Fedha 2018/19 Serikali ilipanga kukusanya shilingi trilioni 32.47 hata hivyo iliweza kukusanya shilingi trilioni 28.8 sawa na asilimia 79.1 ya lengo. Hivyo kiasi cha shillingi trilioni

6.65 hakikukusanywa ikiwa ni sawa na asilimia 20.1 ya

Mheshimiwa Spika,ukiachilia mbali tatizo la kufanya makisio makubwa kuliko vyanzo halisi vya mapato; uwezo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nao umekuwa ni changamoto. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uwezo wa TRA kukusanya mapato ya kodi umekuwa na mserereko wa kushuka. Mathalani kwa mwaka fedha 2018/19, Mamlaka ya Mapato ilikadiria kukusanya mapato ya kodi jumla ya shilingi trilioni 18.297 lakini iliweza kukusanya shilingi trilioni 15.744 tu ikiwa ni pungufu ya shilingi trilioni 2.552 ambazo ni sawa na asilimia 14 ya malengo.



Mheshimiwa Spika, kwa mwaka uliotangulia 2017/18; hali ilikuwa hivyohivyo. Kwa mwaka huo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikusanya jumla ya shilingi trilioni

15.386
ikiwa ni pungufu ya shilingi trilioni 1.929 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 17.315. Upungufu huo ni sawa na asmilimia 11 ya lengo[SUP][5][/SUP].



Mheshimiwa Spika, taarifa ya CAG ya mwaka 2017/18 inaonyesha kwamba; idara zote tatu za mapato zilishindwa kufikia malengo kwa mwaka wa fedha 2017/18. Taarifa hiyo inaonesha kwamba Idara ya walipa kodi wakubwa ilikusanya asilimia 41 ya makusanyo yote ambayo ndiyo sehemu kubwa kuliko idara zote; ikifuatiwa na Idara ya Forodha yenye asilimia 40 na idara ya kodi za ndani yenye asilimia 19 ambayo ndiyo ya mwisho kwa mwaka wa fedha 2017/2018, makusanyo haya hayahusishi vocha ya misamaha ya kodi kutoka Hazina.



Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa, taarifa ya CAG ya mwaka 2018/19 imeendelea kuonyesha udhaifu huo wa idara kushindwa kufikia malengo yake ya makusanyo. Taarifa hiyo inaonyesha kwamba, kwa mwaka wa fedha 2018/19 Idara ya Forodha na Ushuru wa bidhaa iliongoza kwa kukusanya asilimia 40.2 ya mapato yote; ikifuatiwa na Idara ya Walipakodi wakubwa iliyokusanya asilimia 39.8 na Idara ya Kodi za Ndani iliyokusanya asilimia 20. Makusanyo haya hayahusishi vocha za misamaha ya kodi kutoka Hazina.



Mheshimiwa Spika, Kutokana na mchanganuo huo, ni dhahiri kuwa mchango wa makusanyo kutoka Idara ya Mapato ya Ndani umekuwa nyuma ikilinganishwa na idara nyingine. Aidha, taarifa hiyo inaonyesha kuwa mwelekeo wa makusanyo ya mapato kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa wastani, ulikuwa chini ya makadirio yaliyoidhinishwa, isipokuwa kwa mwaka wa fedha 2015/16 wakati wa Serikali ya awamu ya nne ndipo makusanyo halisi yalikuwa juu ya makadirio kwa asilimia 0.13.Kwa hiyo, Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa hiyo ya CAG, ni dhahiri kwamba Serikali ya awamu ya tano imeshindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato kadiri ya mpango iliyojiwekea jambo linalotoa picha kwamba Mpango wa Taifa wa Maendeleo haujatekelezwa kikamilifu kutokana na upungufu wa fedha unaotokana na makusanyo kidogo.



Mheshimiwa Spika, uwezo mdogo wa TRA kukusanya kodi unafahamika pia kimataifa. Ripoti ya CAG inasema kwamba; Mchanganuo linganifu wa ufanisi wa kodi kwa nchi za Afrika Mashariki unaonesha kwamba, Tanzania ilishika nafasi ya mwisho katika ukusanyaji mapato kwa mwaka wa fedha 2017/18. Kambi Rasmi ya Upinzani inaionya Serikali kuacha kujitapa kuwa ina uwezo mkubwa wa kukusanya mapato wakati tafiti zimeonyesha kuwa ina uwezo mdogo na badala yake ijielekeze kutekeleza mapendekezo ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tuliyoyatoa siku nyingi.



Mheshimiwa Spika, mapendekezo hayo ni pamoja na kuongeza wigo wa vyanzo vya kodi, kudhibiti mianya ya upotevu wa kodi na kuwapa motisha walipa kodi, ili kuongeza ulipaji kodi kwa hiari.



D. MAREKEBISHO YA MPANGO WA BAJETI KUKABILIANA NA MADHARA YA JANGA LA CORONA (BUDGET ADJUSTMENT TO MITIGATE THE EFFECTS OF COVID 19 PANDEMIC)
Mheshimiwa Spika,
ni ukweli usiopingika kwamba; wakati Serikali inapanga bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021; kulikuwa hakuna janga la Corona hapa nchini; na kwa sababu hiyo, bajeti hii haikuzingatia kwa mapana yake, madhara ya Corona katika uchumi jumla wa Taifa na uchumi wa kila mwananchi. Hata hivyo, baada ya Corona kubisha hodi hapa nchini; hakuna ubishi tena kuwa janga hilo limeathiri kwa kiwango kikubwa uchumi wa nchi yetu na maisha ya mwananchi mmoja mmoja. Hii ni kwa sababu ya kupungua kwa mapato ya Serikali kutokana na kupungua au kusimama kwa biashara nyingi hususan katika sekta ya utalii, usafiri wa anga na uwekezaji wa mitaji kutoka nje. Mtikisiko huo wa kiuchumi umesababisha pia kupungua kwa ajira za moja kwa moja na zile ambazo si za moja kwa moja na hivyo kuathiri kipato cha mtu mmoja mmoja (per capita income)

Mheshimiwa Spika, katika mazingira kama hayo ambapo uchumi umetikisika na katika mazingira ambayo taifa halikuwa na maandalizi ya mtikisiko huo; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri na kupendekeza kwamba; Serikali ifanye marekebisho ya bajeti (adjustment) ili iendane na mazingira ya sasa ya janga la corona ambapo mapato ya Serikali yameshuka na yanategemewa kuendelea kushuka ikiwa gonjwa hili litaendelea. Kwa mujibu wa Hotuba ya Waziri wa fedha wakati anasoma taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ni kwamba ukuaji wa Pato la Taifa unatarajiwa kupungua kidogo kutoka maoteo ya awali ya asilimia 6.9 hadi 5.5.

Mheshimiwa Spika, Ili Serikali iweze kuendelea kugharamia huduma za kijamii kwa kiwango cha kuridhisha na wakati huohuo kuweza kupambana na gonjwa la corona; Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba; miradi yote ya maendeleo ambayo haina masharti ya mkataba ana ambayo kutotekelezwa kwake kwa mwaka wa fedha 2020/21 hakutakuwa na madhara yoyote ya kiuchumi au kijamii isimame kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuelekeza nguvu kwenye sekta za huduma za jamii ambazo zimeathiriwa na janga la corona na ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na maisha ya wananchi ya kila siku. Aidha, Serikali ifanye mapitio ya Bajeti ya Matumizi Mengineyo katika idara na vitengo mbalimbali vya Serikali ili kupunguza fedha katika matumizi ambayo si ya lazima ili fedha hizo zielekezwe kwenye sekta ya huduma za jamii ambazo zimetikiswa na COVID – 19.



E. HATUA ZA ZIADA ZA KUCHUKUA KUNUSURU KUPOROMOKA KWA UCHUMI KUFUATIA ATHARI ZA JANGA LA CORONA
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua na inaheshimu hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu kupunguza Kiwango cha Kisheria cha Hifadhi ya Fedha katika mabenki kutoka asilimia 7 mpaka 6 ili kuongeza uwepo wa fedha katika benki; kushusha punguzo la riba kutoka asilimia 7 mpaka 5 ili kutoa unafuu kwa mabenki ya biashara kukopa Benki Kuu kwa gharama nafuu na kwa sababu hiyo mabenki hayo kukopesha kwa riba nafuu zaidi kwa wateja wao; Kushusha viwango vya amana za Serikali kupitia hati fungani ili uwezo wa mabenki kukopesha uongezeke, na pia kuzielekeza taasisi za fedha kufanya marekebisho ya mifumo ya utoaji mikopo, riba na urejeshaji wa mikopo ili kuendana na mazingira ya sasa ambapo COVID 19 imeathiri shughuli nyingi za kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, hatua hizo ni njema kwa kuwa zinalenga kunusuru mabenki kuanguka na pia kuzipa uwezo zaidi kukopesha. Hatua hizo zimelenga zaidi kunusuru taasisi za fedha zisishindwe kujiendesha; lakini kwa upande wa wajasiriamali wadogo, wafanya biashara na mwananchi mmoja mmoja hatua hizo zinaweza zisiwe na tija sana. Hii ni kwa sababu baada ya mtikisiko wa uchumi, wengi wa wajasiriamali na wafanyabiashara wanaogopa kwenda kukopa benki kwa kuwa biashara hazitabiriki na hivyo kuna hofu ya kushindwa kufanya marejesho na amana zao kuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika, kutokana na tishio la Virusi vya Corona katika uchumi; nchi nyingi Duniani zimechukua hatua madhubuti kuzuia chumi zao zisianguke. Mathalan Nchi Jirani ya Rwanda Katika kukabiliana na hali hiyo, mamlaka ya nchi hiyo imetangaza hatua kadhaa kukabiliana na kupanda kwa bei kiholela. Kwa mujibu wa tovuti ya Rfi[SUP][6][/SUP] Benki Kuu ya Rwanda imetangaza kupunguza masharti ya ulipaji wa mikopo ya benki kwa kampuni na watu walioathirika na ugonjwa wa Covid-19. Ili kufanikisha mpango huo, Karibu Euro milioni 50 zimetolewakwa benki za biashara, ambazo zitahitaji ukwasi zaidi. Aidha, Ili kuzuia maambukizi ya virusi kupitia biashara ya fedha (kutoa na kupokea fedha), mamlaka pia imesitisha ada ambayo ilikuwa ikitozwa kwa kutoa fedha kupitia mfumo wa kidijitali ili kuwavutia watu wengi zaidi kutumia mifumo ya kielekroniki zaidi katika miamala ya kifedha kuliko fedha taslimu. Hatua hizo zinalenga kupunguza athari za Covid-19 kwenye uchumi wa Rwanda. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato ya Rwanda, sekta ya utalii imeathiriwa zaidi na mlipuko wa COVID 19, ambapo matukio takriban 20 ya kitalii yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mwezi Machi na Aprili, 2020 yamesogezwa mbele, na hivyo kusababisha nchi hiyo kupoteza Euro milioni 7.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Kenya nayo imetangaza hatua za kunusuru uchumi kipindi hiki cha janga la Corona. Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Kenyatta kwa wananchi wa Kenya ni kwamba, ili kulinda ajira kwa wananchi na kuwapa waajiri uhakika wa kutopata hasara; Serikali ya Kenya imetoa nafuu ya kodi ya mapato kwa asilimia 100 kwa wafanyakazi wote wenye pato ghafi lisilozidi shilingi za Kenya 24,000/= kwa mwezi (kwa hapa kwetu ingekuwa takribani shilingi za kitanzania 524,000/=. Hii imekwenda sambamba na kupunguza kodi ya mapato (Kulingana na mtu anavyopata – Pay As You Earn-PAYE) kutoka ukomo wa kiwango cha juu cha asilimia 30 hadi asilimia 25 na kodi nyingine za mapato.

Mheshimiwa Spika, hatua nyingine kubwa iliyochukuliwa na Serikali ya Kenya ni kupunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kutoka asilimia 16 hadi asilimia 14 kuanzia mwezi Aprili, 2020. Hatua hii imekwenda sambamba na Mamlaka ya Mapato ya Nchi hiyo (KRA) kutakiwa kuharakisha kulipa kiasi kilichohakikiwa cha shilingi za Kenya Bilioni 10 za madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refund claims) kwa wafanyabiashara ili kuhakikisha kwamba kuna mzunguko wa fedha wa kutosha katika biashara.

Mheshimiwa Spika,
pamoja na hatua nyingine nyingi za kiuchumi ambazo Kenya imechukua kukabiliana na janga la Corona, Rais Kenyatta amependekeza punguzo la mishahara kwa hiari kwa viongozi wakuu wa Serikali kama ifuatavyo:- Rais na Makamu wa Rais asilimia 80, Mawaziri asilimia 30 na Makatibu Wakuu wa Wizara asilimia 20.

Mheshimiwa Spika, si nia yangu kuishawishi Serikali yetu kuiga hatua walizochukua wenzetu, lakini ni Wajibu wa Serikali kulihakikishia Taifa usalama wa uchumi hasa kipindi cha janga hili. Serikali inatakiwa kuwa na ‘interest’ kwenye jambo hili zaidi kuliko hata jumuiya ya wafanyabiashara; kwa kuwa endapo kutatokea anguko la kiuchumi, Serikali ndiyo itakayokuwa ya kwanza kushindwa kuendesha nchi.

Mheshimiwa Spika, katika mazingira kama hayo; Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza hatua za ziada kuchukuliwa ili kunusuru biashara na mitaji ya wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na kipato cha wafanyakazi kwenye taasisi za umma na binafsi visiyumbe na kuhakikisha kwamba kunakuwa na ukwasi wa kutosha katika mzunguko wa fedha.

i. S erikali Irejeshe Madai ya Kodi kwa

Wafanyabiashara (Tax Refunds)
Mheshimiwa Spika,
kumekuwepo na malalamiko mengi sana kutoka kwa jamii ya wafanyabiashara kuhusiana na kutorejeshewa fedha zao za kodi na hususan ongezeko la asilimia 15 ya ushuru wa forodha ambao hulipwa kabla, kwa ajili ya kuagiza sukari ya viwandani toka nje ya nchi. Utafiti uliofanywa na Shirikisho la wamiliki wa Viwanda CTI kwa viwanda na makampuni mbalimbali ya biashara ulibaini uwepo wa tatizo kubwa la uhaba wa fedha unaovikabili viwanda na makampuni mengi ya biashara kutokana na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na pia uuzaji wa bidhaa nje ya nchi kutokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA kutorejesha madai ya kodi hiyo kwa viwanda na makampuni yanayofanya biashara ya kimataifa.

Meshimiwa Spika, biashara nyingi ambazo zilikuwa zimeathirika ni zile ambazo zimesajiliwa katika mfumo wa kodi ya ongezeko la thamani-VAT, kama vile sekta ya madini, ujenzi, kilimo na kampuni nyingineza biashara zinazomilikwa na wazawa na zile zinazotoka nje lakini zikifanya shughuli zake hapa nchini. Utafiti ulilenga kuangalia madhara ya kutokurejeshwa kwa kodi ya Ongezeko la Thamani –VAT, Ushuru wa Forodha - Import duty, na madai mengine ya marejesho ya kodi kwa mfano asilimia 15 ya nyongeza ya Ushuru wa Forodha. Aidha, utafiti ulilenga kuanisha athari za kiuchumi za ucheleweshaji wa marejesho hayo ya kodi sambamba na kuangalia kiasi halisi kinachodaiwa na viwanda na wafanyabiashara mbalimbali ambao ni wanachama wa CTI.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya utafiti huo yalionesha kuwa viwanda na biashara kampuni nyingine za biashara hazikuwa zimerejeshewa fedha za kodi kwa kipindi cha miaka miwili hadi mitatu iliyopita; na sekta zilizoongoza kwa madai ni sekta za ujenzi, madini, biashara ya huduma na bidhaa, na makampuni ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa za viwandani nje ya nchi pamoja na sekta ya Kilimo.

Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo inaonesha kuwa marejesho ya kodi yaliyofanyika kwa kipindi cha miaka minne ya fedha yalikuwa ni shilingi trilioni 1.52 wakati madai halisi ambayo yalikuwa hayajalipwa (outstanding refunds) yalikuwa ni shilingi trilioni 2.3. Hii maana yake ni kwamba kiasi kikubwa cha madai ya kodi kilikuwa hakijalipwa kwa wafanyabiashara. Utafiti huo ulibaini pia kwamba, kiasi hicho cha madai ya kodi hakikuingizwa kwenye bajeti ya mwaka mwaka wa fedha 2018/19 ili kilipwe jambo ambalo linaashiria kwamba deni hilo lipo na litaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Spika, utafiti wa CTI, ulibaini pia kwamba ulipaji wa madai ya marejesho ya kodi una mwelekeo wa kushuka na pia fedha zinazotengwa kwa ajili kulipa marejesho ya kodi zimekuwa zikipungua kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita. Mwenendo huu wa kupungua kwa ulipaji wa marejesho ya kodi sambamba na kutotenga fedha za kutosha kulipa marejesho hayo umetajwa kama sababu mojawapo ya kuendelea kuongezeka kwa malimbikizo ya madai ya marejesho ya kodi ambayo yalifikia kiwango cha asilimia 7.2 ya bajeti yote ya mwaka wa fedha 2018/19[SUP][7][/SUP].

Mheshimiwa Spika, ucheleweshaji wa malipo ya madai ya kodi ya Ongezeko la Thamani – VAT pamoja na madai ya asilimia 15 ya ushuru wa forodha unaolipwa kabla kwa ajili ya uagizaji wa sukari ya viwandani umekuwa na athari kubwa sana kwa wazalishaji wa viwandani na kwenye uchumi kwa jumla. Athari hizo ni pamoja na kama vile kuongezeka kwa madeni ya viwanda na uzalishaji, kuongezeka kwa riba, kutokana na mikopo toka kwenye mabenki kwani viwanda vinalazimika kukopa tena ili kulipa kodi ambazo zinatakiwa kulipwa. Matokeo yake ni kwamba viwanda vingi vinashindwa kufanya uwekezaji katika uzalishaji, jambo ambalo linasababisha kupunguza wafanyakazi, uzalishaji unashuka na hivyo badala ya uchumi kushamiri unaanza kusinyaa.

Mheshimiwa Spika, ni kutokana na sababu hizo ambapo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaishauri Serikali kuchukua na kutekeleza mapendekezo ya CTI,ili kunusuru anguko la viwanda vya uzalishaji na makampuni ya uuzaji na uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi. Mapendekezo hayo ni kama ifuatavyo:-

Serikali ilipe malimbikizo madai ya kodi (VAT na asilimia 15 ya ushuru wa forodha unaolipwa kabla) pamoja na riba kama iliyoelekezwa kwenye mwongozo wa marejesho ya madai hayo.

Serikali ifute mara moja mfumo wa kulipa kabla asilimia 15 ya ushuru wa forodha kwa uagizaji wa sukari ya viwandani. Licha ya mfumo huo kuwa kikwazo kwa uzalishaji wa viwandani na kandamizi kwa makampuni yanayoagiza sukari ya viwandani kutoka nje; mfumo huo hauna uhalali wa kisheria

kwa kuwa haujatajwa popote katika sheria za Tanzania na kwa maana hiyo unakiuka taratibu na kanuni za kiforodha za Afrika Mashariki na pia unaongeza gharama za uzalishaji na kufanya mazingira ya biashara nchini kuwa magumu.

Serikali ifungue Akaunti Maalum ya Akiba kwa ajili ya Kuweka Fedha za Kulipa madai ya Kodi kwa wafanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina mtazamo kwamba; Serikali ikirejesha kwa wafanyabiashara kiasi cha shilingi trilioni 2.3 ambacho ni madai ya kodi; uzalishaji wa viwandani utaongezeka; biashara zitaimarika hasa katika kipindi hiki ambacho biashara nyingi zimefungwa na wafanyakazi wamesimamishwa kazi kutokana na madhara Corona. Hivyo basi badala ya kutoa fedha taslimu kwa ajili ya kusaidia sekta ya viwanda na biashara (STIMULUS PACKAGE) Serikali iwarejeshee wafanyabiashara fedha zao za madai ya kodi ili wazitumie kuimarisha biashara zao na hivyo kuurudisha uchumi katika hali yake ya kawaida.

ii. Serikali ilipe Madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili Wastaafu waweze kulipwa Mafao yao na pia Kuiwezesha Mifuko ya Hifadhi Kujiendesha
Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya 2018/19 kuhusu Utendaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kwamba Mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) haujafanya tathmini ya hali ya mali na madeni (actuarial valuation); na pia kumekuwepo madai ya muda mrefu ya shilingi bilioni 171.91 ya michango katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa Fidia kwa

Wafanyakazi (WCF), na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Mheshimiwa Spika, ukaguzi wa CAG ulibaini kuwa kuna hatari ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma kutolipwa kiasi cha shilingi bilioni 111.8 kilichowekezwa katika Benki ya Uwekezaji Tanzania kutokana na matatizo ya ukwasi yanayoikabili Benki hiyo.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa miaka mingi sasa imekuwa ikiitaka Serikali kulipa madeni ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili mosi, mifuko hiyo iweze kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati lakini pia ili iweze kujiendesha. Serikali kuendelea kutolipa madeni hayo ni kuwahujumu wastaafu na pia ni kuihujumu mifuko ya hifadhi ya jamii.

iii. Serikali ilipe Fao la Kukosa Ajira kwa Wafanyakazi wote ambao wamekidhi vigezo vya kisheria. Tangu kuingia kwa janga la Corona nchini taasisi binafsi, zikiwemo shule binafsi zilisimamisha ajira.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chama cha

Walimu wa Shule Binafsi (Tanzania Private Schools Teachers’ Union); ni kwamba janga la Corona limesababisha walimu 89,475/- kusimamishwa kazi na hivyo hawalipwi mishaharaw. Kwa hiyo, Serikali itumie Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi kuwalipa watumishi wote waliokosa ajirana ambao wamekidhi vigezo vya kisheria fao la kukosa ajira ili waweze kumudu maisha yao.



F. MFUKO MKUU WA HAZINA YA SERIKALI
Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa ibara ya 135 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, makusanyo yote ya Serikali yanatakiwa kuwekwa katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali. Hata hivyo, licha ya maelekezo hayo ya kikatiba; imebainika kuwa utaratibu huo haufuatwi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2018/19 kati ya shilingi bilioni 659 ambazo ni makusanyo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ni shilingi bilioni 105 tu ndizo zilithibitika kupokelewa na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, Sambamba na hilo, kati ya shilingi trilioni 3.4 ambazo ni makusanyo yote ya mikopo ya nje ni shilingi trilioni 2.17 tu ambazo ziliripotiwa na Mfuko Mkuu wa

Hazina. Hii ina maana kwamba, kiasi ambacho hakikuripotiwa hakijulikani kilikwenda wapi na kwa kazi gani jambo ambalo linatoa taswira kwamba kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa ubadhirifu na ufisadi unaofanyika kwa kutopeleka makusanyo yote katika Mfuko Mkuu wa Hazina kama Katiba ya Nchi inavyoelekeza. Na hii inadhihirishwa na uhalisia kwamba, Jumla ya fedha

zilizoripotiwa katika Mfuko mkuu wa Hazina ni shilingi trilioni 24.2 lakini jumla ya fedha zilizotumika ni shilingi trilioni 26.6, na hivyo kuwa na nyongeza ya matumizi ya shilingi trilioni 2.3 ambayo hayakupita katika Mfuko Mkuu wa Hazina.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa maelezo mbele ya Bunge hili, ni kwanini haipeleki makusanyo yote kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina na ni kwanini inafanya matumizi ya fedha ambazo hazijapita katika Mfuko Mkuu wa Hazina.



G. DENI LA TAIFA NA HATMA YA UCHUMI WA NCHI F1. Deni la Serikali
Mheshimiwa Spika,
Deni la Taifa, limeendelea kuwa kubwa kila mwaka jambo ambalo limekuwa na athari kubwa katika bajeti ya Serikali na hivyo kuathiri uchumi wetu na maisha ya wananchi kwa jumla.

Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2018/19; ni kwamba hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2019, deni la Serikali lilikuwa limefikia Shilingi trilioni 53.1. Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 14.9 zilikuwa ni deni la ndani na shilingi trilioni 38.2 zilikuwa ni deni la nje. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, deni la Serikali limeongezeka kwa shilingi trilioni 2.2 sawa na asilimia 4.3 ikilinganishwa na deni la Shilingi trilioni 50.9 lililoripotiwa tarehe 30 Juni, 2018.

Mheshimiwa Spika,
sababu zilizotolewa na CAG kuhusu ongezeko hili la deni la Serikali, ni mikopo kwa ajili ya kulipa mitaji na riba ya dhamana za Serikali za muda mfupi pamoja na mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, jedwali Na. 1 hapo chini linaonyesha mwenendo wa ukuaji wa deni kwa miaka minne iliyopita:-



Jedwali Na. 1. Mwenendo wa Ukuaji wa Deni la

Serikali kwa miaka minne iliyopita


[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"] 2 0 1 5 / 1 6 [/TD][TD valign="top"] 2 0 1 6 / 1 7 [/TD][TD valign="top"] 2017/18 [/TD][TD valign="top"] 2 0 1 8 / 2 0 1 9 [/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
S h i l i n g i B i l i o n i
[/TD]

[TD valign="top"] Jumla ya Deni [/TD][TD valign="top"] 4 1 , 0 3 9 [/TD][TD valign="top"] 4 6 , 0 8 1 [/TD][TD valign="top"] 5 0 , 9 2 7 [/TD]
[TD valign="top"]
5 3 , 1 0 5
[/TD]

[TD valign="top"] Deni la Nje [/TD][TD valign="top"] 2 9 , 8 4 6 [/TD][TD valign="top"] 3 2 , 7 4 6 [/TD][TD valign="top"] 3 6 , 1 9 4 [/TD]
[TD valign="top"]
3 8 , 2 4 1
[/TD]

[TD valign="top"] Deni la Ndani [/TD][TD valign="top"] 1 1 , 1 9 3 [/TD][TD valign="top"] 1 3 , 3 3 5 [/TD][TD valign="top"] 14,732.45 [/TD]
[TD valign="top"]
1 4 , 8 6 3
[/TD]
Chanzo: CAG 2017/18 ; 2018/19


Mheshimiwa Spika,
ukiangalia mwenendo huo wa ukuaji wa deni utaona kwamba Serikali hii ya awamu ya tano inayojigamba kwamba haikopi nje, na kwamba inatumia fedha zake za ndani kuendesha miradi yake ya maendeleo, ilikuta deni la Serikali likiwa shilingi trilioni 41.039 ilipoingia madarakani; ikaongeza deni hilo kwa shilingi trilioni 5 hadi kufikia shilingi trilioni 46.081 kwa mwaka wake wa kwanza tu madarakani. Aidha, katika mwaka wake wa

pili madarakani, Serikali hii imeliongeza deni kwa shilingi kwa takribani shilingi trilioni 5 nyingine hadi kufikia shilingi trilioni 50.927.

Mheshimiwa Spika,
kana kwamba kuwa na madeni mengi ni sifa; Serikali hii, licha ya kuonywa na kupewa maangalizo mengi juu ya athari za kukopa kwingi kuliko uwezo wa kulipa; bado imeendelea kuongeza deni kwa takriban shilingi trilioni 2 zaidi na sasa limefikia shilingi trilioni 53 .105.

Mheshimiwa Spika,
deni la shilingi trilioni 53.105 ni sawa na asilimia 38.9 ya Pato la Taifa ambalo kwa sasa ni Dola za Kimarekani bilioni 59[SUP][8][/SUP] ambazo ni sawa na shilingi trilioni 136.504 kwa kiwango cha ubadilishaji fedha cha dola moja kwa shilingi 2,313.63[SUP][9][/SUP]cha tarehe 14 Mei, 2020. Kiwango hiki cha deni ni kikubwa mno na kina mwelekeo wa kuiweka nchi rehani kwa kuwa kinakaribia kufikia nusu ya pato letu.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameshaeleza kuwa sababu kubwa ya deni la taifa kuongezeka kwa kasi ni kuongezeka kwa mikopo ya ndani na nje – ambapo mikopo peke yake inachangia ukuaji wa deni kwa asilimia 77; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inarejea tena ushauri wake ambao imekuwa ikiutoa miaka yote kuwa; mikopo yote ya Serikali iwe inaidhinishwa na Bunge kabla ya kukopa.

F2. Deni la Sekta Binafsi
Mheshimiwa Spika,
kwa muda mrefu sasa, Serikali imekuwa ikikwepa kuonyesha takwimu za deni la Taifa kwa ujumla wake kwa maana ya Deni la Serikali na Deni la Sekta Binafsi ambalo hudhaminiwa na Serikali. Badala yake, Serikali imekuwa ikitoa takwimu za deni la Serikali pekee na kuuaminisha umma kuwa deni hilo ni himilivu.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwezi Aprili, 2020, jumla ya deni la nje kwa maana ya Deni la Serikali na Deni la Sekta Binafsi, lilifikia Dola za Kimarekani milioni 22,386.7 kwa rekodi ya mwezi Machi,

2020. Kiasi hicho ni sawa na shilingi

51,825,210,500,000/=
(kwa kiwango cha kubadilsha fedha cha shilingi 2,315, kwa dola moja ya kimarekani) kama kilivyorekodiwa tarehe 10 Juni, 2020. Ukiondoa deni la Serikali la nje ambalo kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa

Hesabu za Serikali ni shilingi trilioni 38.241; deni la sekta binafsi la nje (ambalo ndilo lenye dhamana ya Serikali) litabaki kuwa shilingi 13,584,210,500,000/=

Mheshimiwa Spika,
ili kupata takwimu halisi za deni la Taifa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imechukua jumla ya deni la Serikali (la nje na ndani) ambalo kwa sasa ni shilingi trilioni 53.105 na kujumlisha na deni la sekta binafsi ambalo limefikia shilingi trilioni 13.584 na kupata jumla ya Deni la Taifa kuwa shilingi trilioni 66.689

F3. Uhimilivu wa Deni la Taifa
Mheshimiwa Spika,
ukifanya tathmini ya wastani wa makusanyo halisi ya mapato kwa miaka minne iliyopita na fedha inayotengwa kila mwaka kulipa deni la Taifa na mishahara ya wafanyakazi, utagundua kuwa deni la Taifa si himilivu tena! Hii ni kwa sababu wastani wa makusanyo kwa miaka minne iliyopita ni shilingi trilioni 15[SUP][10][/SUP]; ilihali fedha inayokwenda kulipa deni la taifa ni wastani wa trilioni 9 kila mwaka na fedha ya mishahara ni wastani wa trilioni 7 kila mwaka.

Mheshimiwa Spika, tafsiri ya takwimu hizo ni kwamba nchi inaendeshwa kwa mikopo ni sio mapato ya ndani jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu.



H. MASLAHI YA WAFANYAKAZI NA HIFADHI YA JAMII
Mheshimiwa Spika,
Serikali hii ya CCM ya awamu ya tano inamaliza mhula wake wa uongozi, ikiwa haijaongeza mishahara ya wafanyakazi kwa muda wote wa miaka mitano iliyokaa madarakani. Licha ya kutotekeleza wajibu huo wa kisheria; imekwenda mbali zaidi na kuingilia mafao ya wafanyakazi kwa lengo la kuyapunguza ili wafanyakazi waishi maisha ya dhiki baada ya kustaafu utumishi wao

Serikalini.

Mheshimiwa Spika,
hakuna asiyefahamu sakata la marekebisho ya kikokotoo cha mafao ya wastaafu baada ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuunganishwa. Kimsingi sheria

ile ya kikokotoo bado hijafanyiwa marekebisho. Alichokifanya Mheshimiwa Rais, ni kuahirisha matumizi ya sheria hiyo kwa kuisogeza mbele hadi mwaka 2023 ndipo kikokotoo kipya kianze kufanya kazi. Kambi Rasmi ya Upinzani inatafsiri kitendo hicho kama hadaa na danganya toto kwa wafanyakazi ili waichague Serikali ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020, lakini baada ya hapo tatizo liko palepale.

Mheshimiwa Spika,
athari za kutofanya marekebisho ya kikokotoo cha mafao ya wastaafu katika sheria kimekuwa na athari kubwa katika utumishi wa umma. Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali watumishi wengi wanaomba kustaafu mapema kabla ya

umri wa kisheria wa miaka 60 ili wanufaike na kikokotoo cha zamani cha mafao yao, ambacho kinatumika sasa kwenye kipindi cha mpito; kabla kikokotoo kipya kinacholalamikiwa hakijaanza kutumika mwaka 2023.

Mheshimiwa Spika,
sambamba na kutopandisha mishahara na kuminya haki ya wafanyakazi kupata mafao mazuri wanapostaafu ajira; Serikali imefumbia macho utekelezaji wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wanaokosa ajira kwa sababu mbalimbali tofauti na kufukuzwa isipokuwa kuacha kazi kwa hiari (resignation).

Msheshimiwa Spika, kifungu cha 35 cha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ya mwaka 2018 (Pulic Service Social Security Fund Act, 2018) kinaeleza kama ifuatavyo; naomba kunukuu:-

35.-(1) A member of a pension scheme who ceases to be employed shall, subject to the provisions of subsection (2), be entitled to unemployment benefit.

(2) Unemployment benefit shall not be paid unless the applicant-

has been a contributing member for a period not less than eighteen months;

is terminated or ceased to be employed in the circumstances other than resignation;

is a citizen of the United Republic of Tanzania; (d) is not qualified for pension, gratuity or any other long-term benefits payable under this Act. (e) proves to the Director General that he has not secured another employment;

(f) is below fifty five year old.

(3) Unemployment benefit shall be payable in a manner and at the rate to be prescribed in the regulations.


Msheshimiwa Spika,
kifungu hiki kinatoa ulinzi kwa wafanyakazi watakaokosa ajira kutokana na sababu mbalimbali isipokuwa kufukuzwa kazi au kuachishwa kazi kwa sababu nyingine tofauti na kuacha kazi kwa hiari, ilimradi wawe wamechangia katika mfuko wa hifadhi ya jamii kwa muda wa usiopungua miezi 18; wawe ni raia wa Jamhuri ya Muungano; hawana mafao mengine chini ya sheria hii; wamethibitisha kwa Mkurugenzi Mkuu kuwa hawajapata ajira nyingine; na wako chini ya umri wa miaka 55 ya kuzaliwa.

Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilitarajia kwamba kipindi hiki cha janga la Corona ambapo taasisi nyingi zikiwemo hoteli, shule na vyuo vya elimu, viwanda na makampuni mbalimbali ya biashara zimepunguza wafanya kazi; sheria hii ingetumika ili wafanyakazi ambao wanakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria hii walipwe stahili zao kama ambavyo imeanishwa kwenye kanuni za utekelezaji wa sheria hii.



I. SURA YA BAJETI NA SEKTA ZA KIPAUMBELE
Mheshimiwa Spika,
bajeti mbadala ya mwaka 2020/21 imejikita katika uhalisia wa uchumi wa ndani na pia katika uchumi wa Dunia. Kwa muktadha huo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imefanya rejea ya makusanyo halisi ya mapato ya ndani na kufanya tathmini ya utekelezaji halisi wa bajeti za Serikali kwa miaka minne iliyopita na kufikia uamuzi wa kupanga bajeti mbadala kwa kuzingatia uhalisia huo.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imezingatia pia madhara ya janga la Corona ambalo limetikisha uchumi wa dunia; na hivyo kufikia uamuzi kushusha makisio yake ya bajeti kwa kuwa janga hili limefanya mwelekeo wa uchumi kuwa na mserereko wa kushuka badala ya kupanda. Mbali na mlipuko wa ugonjwa wa Corona kulitokea pia mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu katika kipindi cha mvua za masika, jambo ambalo limesababisha maafa na athari kubwa katika sekta mbalimbali za uchumi hususani sekta ya kilimo, na uchukuzi (kutokana na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara na reli). Matukio yote hayo kwa vyovyote vile yameathiri upangaji wa bajeti ya Serikali kwa kuwa yalitokea bajeti hiyo ikiwa imeshapangwa.

Mheshimiwa Spika,
kwa kuwa wastani wa makusanyo halisi ya mapato kwa miaka minne iliyopita ni shilingi trilioni 26.273; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepunguza kiasi hicho kwa asilimi 10 na kufikia kiwango cha bajeti ya shilingi trilioni 23.646 ili kuzingatia madhara ya COVID -19.

Mheshimiwa Spika, kwa muktadha huo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inarejea ushauri wake kuwa Serikali kufanya marekebisho ya bajeti yake ili iendane na uhalisia huo. Vinginevyo utekelezaji wa bajeti utakuwa mgumu kwa kuwa msingi wake hauna uhalisia kama ilivyoelezwa katika hotuba hii.



Jedwali Na. 1: Sura ya Bajeti Mbadala kwa mwaka wa Fedha 2020/21
11


[TD valign="top"]
M A E L E Z O
[/TD]
[TD valign="top"]
M A P A T
[/TD]
[TD valign="top"]
O
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
(
[/TD]
[TD valign="top"]
T
[/TD]
[TD valign="top"]
Z
[/TD]
[TD valign="top"]
S
[/TD]
[TD valign="top"] ) [/TD]
[TD valign="top"] JUMLA YA MAPATO YA KODI12
[/TD]
[TD valign="top"]
15,125,250,000,000.00
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"] MAPATO YASIYO YA KODI [/TD]
[TD valign="top"]
1,774,683,333,333.33
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
MAPATO YA HALMASHAURI13
[/TD]
[TD valign="top"]
517,798,229,763.60
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]


Taarifa ya CAG Serikali Kuu- Utekelezaji halisi wa bajeti- 2016/17, 2017/18,2018/19

Taarifa ya CAG Serikali Kuu-Makusanyo halisi ya kodi kwa miaka ya 2016/17, 2017/18,2018/19

Taarifa ya CAG Serikali za mitaa- Makusanyo halisi kwa miaka 2016/17, 2017/18 na 2018/19


[TD valign="top"]
JUMLA YA MAKUSANYO YA NDANI
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
17,417,731,563,096.90
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
MISAADA YA KIBAJETI TOKANJE
[/TD]
[TD valign="top"]
935,622,133,119.6 0
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
Mikopo ya ndani na nje
[/TD]
[TD valign="top"]
5,292,913,303,783.5 0
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"] J U M L A Y A M A P A T O [/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
23,646,267,000,000
[/TD]

[TD valign="top"] MATUMIZI YA KAWAIDA [/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
D e n i l a T a i f a
[/TD]
[TD valign="top"]
7,004,480,000,000.00
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
Mishahara ni 25% ya bajeti mbadala
[/TD]
[TD valign="top"]
5,911,566,750,000.00
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
Matumizi mengineyo 15% ya bajeti Mbadala
[/TD]
[TD valign="top"]
3,546,940,050,000 .00
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
JUMLA YA MATUMIZI YA KAWAIDA
[/TD]
[TD valign="top"]
16,462,986,800,000.00
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"] MATUMIZI YA MAENDELEO [/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
F e dh a z a n d a n i + N j e
[/TD]
[TD valign="top"]
7,183,280,200,000.00
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]

[TD valign="top"]
JUMLA YA FEDHA ZA MATUMIZI
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
23,646,267,000,000
[/TD]




Jedwali Na. 2 :Mgawanyo wa Fedha katika Sekta za Kipaumbele



[TD valign="top"]
N
[/TD]
[TD valign="top"]
a .
[/TD]
[TD valign="top"]
S e k t a
[/TD]
[TD valign="top"]
K i a s i ( T s h s . )
[/TD]
[TD valign="top"]
Asilimia (%)
[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
1.
[/TD]
[TD valign="top"]
E l i m u
[/TD]
[TD valign="top"]
4,729,253,400,000
[/TD]
[TD valign="top"]
20
[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
2.
[/TD]
[TD valign="top"]
K i l i m o
[/TD]
[TD valign="top"]
3,546,940,050,000
[/TD]
[TD valign="top"]
15
[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
3.
[/TD]
[TD valign="top"] V i w a n d a [/TD]
[TD valign="top"]
3,546,940,050,000
[/TD]
[TD valign="top"]
15
[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
4.
[/TD]
[TD valign="top"]
M a j i
[/TD]
[TD valign="top"]
2,364,626,700,000
[/TD]
[TD valign="top"]
10
[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
5.
[/TD]
[TD valign="top"]
A f y a
[/TD]
[TD valign="top"]
4,729,253,400,000
[/TD]
[TD valign="top"]
2 0
[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
6.
[/TD]
[TD valign="top"]
Nyinginezo
[/TD]
[TD valign="top"]
4,729,253,400,000
[/TD]
[TD valign="top"]
2 0
[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
7.
[/TD]
[TD valign="top"] J U M L A [/TD]
[TD valign="top"]
23,646,267,000,000
[/TD]
[TD valign="top"]
100
[/TD]


J. HITIMISHO
Mheshimiwa Spika,
pamoja na Serikali kusisitiza kuwa Ugonjwa wa COVID 19 umepungua nchini, lakini kiuhalisia ugonjwa bado upo duniani na kwa maana hiyo milango ya shughuli za kiuchumi duniani bado imefungwa na inaendelea kuwa na athari kwa uchumi wetu. Kwa sababu hiyo,Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021 inatakiwa kuelekeza nguvu zake kwenye kunusuru kuanguka kwa uchumi ambao umeathiriwa na janga la mlipuko wa ungonjwa wa COVID – 19 kama ambavyo pia imeainishwa na Ripoti ya Benki Kuu ya Tanznaia ya Aprili, 2020 na kama ambavyo Waziri wa Fedha amekiri katika hotuba yake ya Hali ya Uchumi. Ili kuweza kufikia lengo hilo, ni lazima Serikali ihakikishe kuwa kuna mzunguko wa kutosha wa fedha katika sekta mbalimbali za uchumi ili kuwapa wananchi nguvu ya kununua (purchasing power)

Mheshimiwa Spika, uhakika wa mzunguko wa fedha utakuwepo tu pale ambapo Serikali itapunguza kodi katika biashara mbalimbli ili kuhamasisha uzalishaji kwa gharama nafuu na kukuza soko la ndani; kulipa madeni ya kodi (tax refunds) ili kuwezesha viwanda kuendelea kuzalisha bila vikwazo na pia kuyawezesha makampuni ya biashara kuendelea na biashara za manunuzi na mauzo nje ya nchi bila vikwazo vya uhaba wa fedha.

Mheshimiwa Spika,
tatizo kubwa ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imelibaini katika upangaji wa bajeti ya Seirikali kwa miaka yote, ni kwamba Serikali imekuwa ikifanya makisio makubwa ya bajeti bila kuzingatia vyanzo halisi vya mapato na uwezo wa ukusanyaji mapato. Matokeo yake kila mwaka wa bajeti Serikali imekuwa ikishindwa kufikia malengo ya makusanyo kwa wastani wa takribani asilimia 20 mpaka 30.Kutofikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kumesababisha Serikali kushindwa kutekeleza Mpango wa Taifa wa Maendeleo na pia kulazimika kukopa kwa masharti ya kibiashara ili kuziba pengo la nakisi ya bajeti jambo ambalo limepelekea deni la taifa kuwa kubwa.

Mheshimiwa Spika, napenda kumalizia hotuba yangu kwa kwa kurejea tena ushauri ambao Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeutoa kwa miaka yote mitano ya Serikali hii ya awamu ya tano kwamba; Serikali ipange makisio ya bajeti kwa kuzingatia vyanzo vya mapato vilivyopo na uwezo wa kukusanya; pili iwe na utaratibu wa kutunga sheria ya kusimamamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo, na mikopo yote ya Serikali iwe inaidhinishwa na Bunge ili kudhibiti ukopaji usio na tija.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuwasilisha.

Halima James Mdee

WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI

YA UPINZANI BUNGENI, KATIKA WIZARA YAFEDHA NA MIPANGO

12 Juni, 2020




[1] Rejea Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Seriakali kwa Mwaka wa Fedha 2016/17
[2] Ibid.
[3] Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango akiwashilisha Bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18
[4] Ibid.
[5] Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18
[6] http://www.rfi.fr/sw/afya-mazingira...zakiuchumi-kukabiliana-na-ugonjwa-wa-covid-19


[7] EXECUTIVE SUMMARY OF DRAFT REPORT STUDY ON DELAYS IN TAX REFUNDS:

[8] Pato la Taifa kwa mwaka 2019 kama lilivyorekodiwa kwenye tovuti Tanzania GDP | 1988-2019 Data | 2020-2022 Forecast | Historical | Chart | News iliyosomwa tarehe 14 Mei, 2020.
[9] Hicho ni kiwango cha ubadilishaji fedha (exchange rate) cha dola moja ya marekani kwa shilingi ya Tanzania kwa tarehe 14 Mei, 2020 kama kilivyorekodiwa kwenye tovuti:
XE: Convert USD/TZS. United States Dollar to Tanzania Shilling
[10] Vitabu vya makusanya ya Mapato ( Revenue Books – Volume I) kwa miaka ya fedha 2016/17; 2017/18; 2018/19 na 2018/2020
 

Attachments

  • HOTUBA MBADALA BAJETI KUU YA SERIKALI 2020.pdf
    365.3 KB · Views: 11
Nimejaribu kupita mitandaoni, hasa Twitter kujaribu kuona reaction ya wadau hasa wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wasomi mbalimbali juu ya Bajeti ya Serikali iliyosomwa jana ila cha ajabu wanajadili au kuongelea maswala mengine tofauti huku Bajeti ya nchi wakiipa kisogo kama vile haipo, wakati kwa kawaida Bajeti inaposomwa tu watu mara moja huanza uchambuzi na mijadala jambo ambalo tangu jana mpaka asubuhi ya leo silioni mitandaoni zaidi ya hapa JF ingawa na penyewe mjadala wake umekosa mashiko kabisa.

Binafsi naona hii ni dalili ya watu kukatishwa tamaa na mwenendo wa Bajeti hizi za serikali kiasi kwamba wanaona mambo ni yale yale hivyo wanaona bora tu. waendelee na agenda zingine.

Anyway, ngoja tuone labda kuanzia leo watu wataanza kujijadili hiyo Bajeti.
Bado tupo na MAVUVUZELA yaliyokuwa yanasema yatamlazimisha MAGUFULI ABADILI KATIBA, eti hakuna mtu anayeweza ziba nafasi yake, hawa MAVUVUELA wanamkufuru MUNGU na Mungu hana iana, Mungu ana wivu, any time anaweza kujitwalia utukufu "kwa kumpenda sana huyo mtu" yani akampenda akamuita kwake! endeleeni tu
 
Bado tupo na MAVUVUZELA yaliyokuwa yanasema yatamlazimisha MAGUFULI ABADILI KATIBA, eti hakuna mtu anayeweza ziba nafasi yake, hawa MAVUVUELA wanamkufuru MUNGU na Mungu hana iana, Mungu ana wivu, any time anaweza kujitwalia utukufu "kwa kumpenda sana huyo mtu" yani akampenda akamuita kwake! endeleeni tu

Sio raisi wa kwanza kuongezewa mda, na hatakua raisi wa mwisho!
 
Bado tupo na MAVUVUZELA yaliyokuwa yanasema yatamlazimisha MAGUFULI ABADILI KATIBA, eti hakuna mtu anayeweza ziba nafasi yake, hawa MAVUVUELA wanamkufuru MUNGU na Mungu hana iana, Mungu ana wivu, any time anaweza kujitwalia utukufu "kwa kumpenda sana huyo mtu" yani akampenda akamuita kwake! endeleeni tu

Halafu sio yeye anabadili katiba, bunge lina mamlaka ya kubadili katiba! na yeye lazima afuate katiba inasema nn, kama inasema aongoze miaka 60 hana budi kuifuata.
 
Ukiona Mwalimu anawauliza wanafunzi wake, Je kuna swali? Kwa kile alichokifundisha halafu asitokee hata mmoja wa kuinua mkono kutaka kuuliza, maana yake, somo limewaingia na wameelewa!
 
Nimejaribu kupita mitandaoni, hasa Twitter kujaribu kuona reaction ya wadau hasa wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wasomi mbalimbali juu ya Bajeti ya Serikali iliyosomwa jana ila cha ajabu wanajadili au kuongelea maswala mengine tofauti huku Bajeti ya nchi wakiipa kisogo kama vile haipo, wakati kwa kawaida Bajeti inaposomwa tu watu mara moja huanza uchambuzi na mijadala jambo ambalo tangu jana mpaka asubuhi ya leo silioni mitandaoni zaidi ya hapa JF ingawa na penyewe mjadala wake umekosa mashiko kabisa.

Binafsi naona hii ni dalili ya watu kukatishwa tamaa na mwenendo wa Bajeti hizi za serikali kiasi kwamba wanaona mambo ni yale yale hivyo wanaona bora tu. waendelee na agenda zingine.

Anyway, ngoja tuone labda kuanzia leo watu wataanza kujijadili hiyo Bajeti.
Mkuu, watu waseme nini wakati hotuba ya bajeti ni kama hotuba kwenye campaign rally?

Mtu serious atoe comment ipi mathalani Mpango anaposema "moja ya mafanikio ya sera za viwanda kati ya 2015 na 2019 ni ongezeko maradufu katika uzalishaji wa ndani wa cement" ilihali huku mtaani tumekuwa tukishuhudia bei ya cement ikipaa kila uchwao tangu awamu ya 5 iingie madarakani?

does it add up kweli?
 
MATAGA wanaona huyu JIWE ndio Mungu wao

Angalia tu usikufuru ndugu, dhambi ya kukufuru imeandikwa haitasamehewa! as long watu wanaenda kanisan na wanasali na yeye mwenyewe anatoa credits kwa Mungu, chunga tu maneno yako.
 
mkuu, watu waseme nini wakati hotuba ya bajeti ni kama hotuba kwenye campaign rally?

mtu serious atoe comment ipi mathalani Mpango anaposema "moja ya mafanikio ya sera za viwanda kati ya 2015 na 2019 ni ongezeko maradufu katika uzalishaji wa ndani wa cement" ilihali huku mtaani tumekuwa tukishuhudia bei ya cement ikipaa kila uchwao tangu awamu ya 5 iingie madarakani?
Bora kuipotezea tu kama haipo.
 
Kimya kina sababu zake za msingi, Kwa kuwa sisi wavuta bangi hatutambuliki kwenye bajeti, tumeamua kuisusia sijui makundi mengine yana sababu gani
 
Nimejaribu kupita mitandaoni, hasa Twitter kujaribu kuona reaction ya wadau hasa wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wasomi mbalimbali juu ya Bajeti ya Serikali iliyosomwa jana ila cha ajabu wanajadili au kuongelea maswala mengine tofauti huku Bajeti ya nchi wakiipa kisogo kama vile haipo, wakati kwa kawaida Bajeti inaposomwa tu watu mara moja huanza uchambuzi na mijadala jambo ambalo tangu jana mpaka asubuhi ya leo silioni mitandaoni zaidi ya hapa JF ingawa na penyewe mjadala wake umekosa mashiko kabisa.

Binafsi naona hii ni dalili ya watu kukatishwa tamaa na mwenendo wa Bajeti hizi za serikali kiasi kwamba wanaona mambo ni yale yale hivyo wanaona bora tu. waendelee na agenda zingine.

Anyway, ngoja tuone labda kuanzia leo watu wataanza kujijadili hiyo Bajeti.
Sijawahi kuona bajeti iliyodharauliwa kama hii
 
Angalia tu usikufuru ndugu, dhambi ya kukufuru imeandikwa haitasamehewa! as long watu wanaenda kanisan na wanasali na yeye mwenyewe anatoa credits kwa Mungu, chunga tu maneno yako.
Hata Idd Amin alikuwa anaenda msikitini kuswali... Hitler pia alikuwa hachezi mbali na kumhusisha Mungu kwenye mambo yake.... oh nikitaka kumsahau Nkurunziza
 
Nimejaribu kupita mitandaoni, hasa Twitter kujaribu kuona reaction ya wadau hasa wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wasomi mbalimbali juu ya Bajeti ya Serikali iliyosomwa jana ila cha ajabu wanajadili au kuongelea maswala mengine tofauti huku Bajeti ya nchi wakiipa kisogo kama vile haipo, wakati kwa kawaida Bajeti inaposomwa tu watu mara moja huanza uchambuzi na mijadala jambo ambalo tangu jana mpaka asubuhi ya leo silioni mitandaoni zaidi ya hapa JF ingawa na penyewe mjadala wake umekosa mashiko kabisa.

Binafsi naona hii ni dalili ya watu kukatishwa tamaa na mwenendo wa Bajeti hizi za serikali kiasi kwamba wanaona mambo ni yale yale hivyo wanaona bora tu. waendelee na agenda zingine.

Anyway, ngoja tuone labda kuanzia leo watu wataanza kujijadili hiyo Bajeti.
Nimemuona Cecilia Pareso akiichambua bajeti bungeni!
 
Hata Idd Amin alikuwa anaenda msikitini kuswali... Hitler pia alikuwa hachezi mbali na kumhusisha Mungu kwenye mambo yake.... oh nikitaka kumsahau Nkurunziza

nakukumbusha tu, angalia dhambi ya kukufuru haisameheki, mambo ya dunia yaishie hapa hapa
 
Back
Top Bottom