Hotuba Wizara ya Elimu: Tozo ya 6% kwenye mikopo ya Elimu kuondolewa Julai 1. Pia Serikali itaondoa tozo ya 10% kwa wanaochelewa kulipa mikopo yao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,479
9,234
Serikali itaondoa tozo ya asilimia sita ya kulinda thamani ya fedha katika urejeshaji wa mkopo kuanzia 1 Julai 2021, iliyokuwa inatozwa kwa wanufaika wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ikiwa ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan

Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichakob ameeleza bungeni kuwa Serikali inaiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuondoa pia tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo hiyo

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), hadi kufikia Machi 2021, imekusanya Sh.139.2 bilioni ya lengo la Sh.194.1 bilioni kwa mwaka 2020/21. Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), imetoa mikopo kwa wanafunzi 149,398. Kati yao 55,337 wa mwaka wa kwanza na 94,061 wanaoendelea na masomo.

Mwaka 2021/22, Serikali itapitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 kwa lengo la kuhakikisha kuwa inakidhi mahitaji ya sasa. Pia, itafanya mapitio ya Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 ili kuhakikisha inaendana na mazingira ya sasa ya utoaji wa elimu nchini

=====

HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA MHESHIMIWA PROF. JOYCE LAZARO NDALICHAKO (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2021/22

UTANGULIZI​

Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii iliyochambua makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia naomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako Tukufu, likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2020/21. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema, kuniwezesha kuendelea kutimiza majukumu yangu na kusimama tena mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha 2020/21 umekuwa ni mwaka wenye majonzi makubwa katika nchi yetu. Tumeondokewa na mpendwa wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyefariki tarehe 17 Machi, 2021; Pia tumeondokewa na Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyefariki tarehe 24 Julai, 2020; Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyefariki tarehe 17 Februari, 2021; na Balozi John William Herbert Kijazi aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi aliyefariki tarehe 17 Februari, 2021.

Mheshimiwa Spika, Vile vile Bunge lako Tukufu limewapoteza Waheshimiwa Wabunge wawili: Mheshimiwa Martha Jachi Umbulla aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM – Mkoa wa Manyara aliyefariki

tarehe 21 Januari, 2021; na Mheshimiwa Atashasta Justus Nditiye Mbunge wa Jimbo la Muhambwe aliyefariki tarehe 12 Februari, 2021. Nitumie fursa hii kutoa pole kwa ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa kuondokewa na Viongozi wetu; tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

Mheshimiwa Spika, nampongeza kwa dhati Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa na kuwa Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa Mwanamke wa Kwanza kuwa Rais wa nchi yetu. Nampongeza pia kwa Hotuba aliyoitoa tarehe 22 Aprili, 2021 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imetoa dira na mwelekeo wa Serikali yake. Vilevile, natoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kuniteua kuendelea kusimamia Sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Naahidi kuwa nitatekeleza majukumu yangu kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu. Naomba Mwenyezi Mungu anisaidie niweze kukidhi matarajio ya Mheshimiwa Rais na Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Phillip Isdor Mpango kwa kuteuliwa na kuthibitishwa na Bunge lako Tukufu kwa kura zote kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, nimpongeze Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kwa uongozi wake makini. Nampongeza pia kwa miongozo anayoitoa na ufuatiliaji anaofanya katika kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Hussein Ally Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Nampongeza kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya. Vile vile nampongeza Mheshimiwa Othman Masoud

Othman kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mheshimiwa Hemedy Suleiman Abdullah kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, naomba nikupongeze kwa dhati wewe mwenyewe Mheshimiwa Job Yustino Ndugai na Naibu Spika Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kwa kuchaguliwa kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu nyingine. Kuchaguliwa kwenu ni matokeo ya umahiri mliouonesha katika kutekeleza majukumu yenu katika Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo (Mb), Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Aloyce John Kamamba (Mb), na Wajumbe wote wa Kamati kwa kuchambua na kuishauri Wizara kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka 2021/22. Kamati hii ni makini sana na imekuwa ikitoa maoni na ushauri wenye lengo la kuhakikisha tunaendelea kuboresha elimu ili kutoa wahitimu wenye ujuzi unaokidhi mahiataji ya sasa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwapongeza Mawaziri na Manaibu Mawaziri wote walioteuliwa kuongoza Wizara mbalimbali. Nawaahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika kuhakikisha tunatoa huduma na kuleta maendeleo kwa taifa letu hasa katika Sekta ya Elimu hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hii ni Hotuba yangu ya kwanza kwenye Bunge hili la 12 napenda pia kuwapongeza waheshimiwa Wabunge wote kwa kuchaguliwa na kuteuliwa kwao kuwa Wabunge wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hongereni sana na naomba ushirikiano wenu katika kuiendeleza Sekta hii muhimu ya Elimu.

Mheshimiwa Spika, naishukuru kwa dhati familia yangu kwa kuendelea kunipa ushirikiano na kuniwezesha kutekeleza majukumu ya ujenzi wa Taifa kupitia Sekta ya Elimu.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi sasa naomba nitoe taarifa ya utelekezaji wa majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2020/21 na Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/22.

UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2020/21​

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21 Bunge lako Tukufu liliidhinisha kiasi cha Shilingi 1,348,563,375,000.00 kwa ajili ya Fungu 46 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo Shilingi 491,049,151,000.00 zilikuwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 857,514,224,000.00 zilikuwa ni kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Aidha, kupitia Tume ya Taifa ya UNESCO - Fungu 18 Bunge liliidhinisha kiasi cha Shilingi 2,239,181,000.00 ambapo Shilingi 1,532,293,000.00 zilikuwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 706,888,000.00 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Tume.

Ukusanyaji wa Maduhuli​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Wizara kupitia Fungu 46 ilitarajia kukusanya maduhuli yenye thamani ya Shilingi 555,651,650,346.52 ambapo kiasi cha Shilingi 15,459,750,000.00 kilipangwa kukusanywa na Idara na Vitengo na Shilingi 540,191,900,346.52 zilipangwa kukusanywa na Taasisi zilizo chini ya Wizara. Vyanzo vya maduhuli haya ni kutokana na ada, ushauri elekezi, ukaguzi wa shule na utoaji wa huduma mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2021, Wizara ilikuwa imekusanya Shilingi 339,128,992,104.16 sawa na asilimia 61 ya makadirio ambapo Shilingi 6,050,266,699.80 zimekusanywa na Idara na Vitengo na Shilingi 333,078,725,404.36 zimekusanywa na Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Matumizi ya Kawaida​

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2021, Wizara ilikuwa imepokea Jumla ya Shilingi 434,737,497,950.09 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida, kupitia Fungu 46, ambazo ni sawa na asilimia 88.5 ya fedha za Matumizi ya Kawaida zilizoidhinishwa. Aidha, kupitia Tume ya UNESCO – Fungu 18 Wizara ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi 1,515,856,166.60 sawa na asilimia 68 ya fedha iliyoidhinishwa na Bunge lako Tukufu.

Miradi ya Maendeleo​

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya maendeleo hadi kufikia Aprili 2021, Wizara ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi 634,622,139,494.67 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambazo ni sawa na asilimia 74 ya bajeti iliyotengwa. Kati ya Fedha hizo Shilingi 397,496,012,792.52 ni fedha za ndani na Shilingi 237,126,126,702.15 ni fedha za nje.

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA​

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nitoe taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa Fungu 46 na Fungu 18 katika mwaka wa fedha 2020/21.

Uendelezaji wa Elimumsingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu​

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha Elimu ya Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu ambapo katika mwaka wa fedha 2020/21 imetekeleza yafuatayo:
imewezesha mafunzo kwa walimu 174 wa shule za sekondari yaliyohusu utoaji wa ushauri na unasihi kwa wanafunzi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuimarisha stadi za utoaji wa huduma za malezi na unasihi shuleni;
imekamilisha Mwongozo wa Malezi, Unasihi na Ulinzi wa Mtoto kwa Shule na Vyuo vya Ualimu.

Mwongozo huo utawasaidia walimu wanasihi kuwa na fasili sahihi ya huduma katika Shule na Vyuo na kukuza stadi za kutoa huduma, kuzipima na kuzitathmini. Mwongozo huo unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; na
imeandaa Mwongozo wa Utoaji wa Huduma ya Chakula na Lishe Shuleni. Mwongozo huo utawezesha utolewaji wa huduma ya chakula shuleni katika viwango stahiki na hatimaye kuboresha mahudhurio ya wanafunzi.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mradi wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shuleni (School Water, Sanitation and Hygiene – SWASH), katika mwaka wa fedha 2020/21 imetekeleza yafuatayo:
imeendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa matundu ya vyoo, miundombinu ya maji na vifaa vya kunawia mikono katika Shule za Msingi 602 ambapo shule 380 zimekamilisha ujenzi na shule 222 zipo

katika hatua mbalimbali za ukamilishaji wa miundombinu hiyo; na

imewezesha ununuzi wa gari moja kwa ajili ya kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mradi.


Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari – SEQUIP katika mwaka wa fedha 2020/21, imetekeleza yafuatayo:
imeandaa Nyaraka ya uendeshaji wa mradi (Programme Operation Manual) na Andiko la Tathmini ya Mradi (Project Appraisal Document) pamoja na andiko la Makubaliano ya Kifedha (Financial Agreement) ambapo nyaraka hizo zitatoa mwongozo wa utekelezaji wa mradi; na imedurusu mihtasari na moduli za Elimu Nje ya Mfumo Rasmi kwa hatua ya kwanza kwa Kidato cha I na II na hatua ya pili kwa Kidato cha III na IV kwa masomo saba (7) ya English, Kiswahili, Geography, History, Civics, Biology na Mathematics. Mihtasari hiyo itawezesha utoaji Elimu kwa Njia Mbadala (Alternative Education Pathway - AEP) na kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Programu ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) - Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Elimu ya Awali na Msingi (GPE - LANES II), katika mwaka wa fedha 2020/21 imetekeleza yafuatayo:
imekamilisha uchapaji wa vitabu 46,830 vya uchambuzi wa matokeo ya upimaji wa darasa la pili 2019 (PIRA -STNA). Aidha, inaendelea na uchapaji wa vitabu 304,897 vya uchambuzi wa matokeo ya upimaji wa darasa la nne, 2020 (PIRA - SFNA) na vitabu 249,020 vya uchambuzi wa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi 2020 (PIRA - PSLE);
imechapa na kusambaza vitabu vya kiada 4,905,586, Kiongozi cha

Mwalimu 268,000 na mihtasari 365,368 kwa masomo yote ya Darasa la VI na VII. Aidha, inaendelea na uchapaji wa vitabu vya kiada 14,650,531;
imeandaa moduli 10 za mafunzo endelevu kazini kwa walimu wa Shule za Msingi (Darasa V - VII), wawezeshaji wa MEMKWA, na walimu wa Elimu Maalum ikijumuisha moduli tatu (3) kwa kila kundi ambazo ni: Moduli ya Ufundishaji na Ujifunzaji; Upimaji na Tathmini; na Stadi za Maisha pamoja na moduli moja (1) ya mbinu za mawasiliano kwa Lugha ya Kiingereza;

imewezesha ukamilishaji wa vitini vya Miongozo ya Mafunzo ya Uthibiti Ubora wa Shule wa Ndani na kutoa mafunzo kwa wawezeshaji (TOT) 445 ikijumuisha Maafisa Taaluma wa Wilaya 184, Viongozi 20 kutoka Makao Makuu ya WyEST na OR - TAMISEMI, Maafisa 70 kutoka ADEM na Wathibiti Ubora wa Shule 183. Wawezeshaji hawa walitoa mafunzo kwa Walimu Wakuu 8,091 sawa na asilimia 99.74 ya Walimu Wakuu 8,112 waliokuwa kwenye mpango wa mafunzo awamu ya kwanza;

imewezesha Wathibiti Ubora wa Shule kufanya Tathmini ya Jumla kwa Shule za Awali na Msingi 2,755 ambazo ni sawa na asilimia 101 ya Shule 2,726 zilizolengwa kufanyiwa tathmini ya ubora wa elimu nchini katika mwaka wa fedha 2020/21;
imefanya ufuatiliaji na tathmini katika Vituo vya Walimu (TRCs) 269 sawa na asilimia 87 ya vituo 308 vilivyokuwa katika mpango. Ufuatiliaji ulibaini kuwa asilimia 54 ya vituo vilikuwa vinafanya kazi ya kuendesha mafunzo kwa walimu katika kipindi cha miaka mitatu ya nyuma.

Aidha, vituo hivyo vilionekana kuwa na mahitaji makubwa ya miundombinu pamoja na vitendea kazi ikiwemo mifumo ya TEHAMA ili kusaidia vituo hivyo kuwa sehemu sahihi kwa walimu kujiendeleza kitaaluma na kitaalam; na

imeandaa rasimu ya Mwongozo wa Uendeshaji wa Vituo vya Walimu (Teachers Resources Centers – TRCs) kwa ajili ya Waratibu wa Vituo ili kuendana na Mpango wa Kitaifa wa Mafunzo Endelevu kazini.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Sekta ya Elimu - EP4R) imeendelea kuboresha miundombinu ya shule, Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule na Vyuo vya Ualimu kama ifuatavyo:
imejenga Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule 55 kwa lengo la kusogeza huduma kwa wateja na kuimarisha mazingira ya utendaji kazi ambapo ujenzi upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji;

imewezesha ujenzi wa hosteli, bwalo la chakula na mifumo ya maji katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji;
inaendelea na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano Dodoma ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilika mwezi Februari, 2022. Kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kutawezesha ufundishaji na ujifunzaji fanisi kutokana na kuwepo kwa mahitaji muhimu na hivyo kuhamasisha shule nyingine na jamii kujifunza umuhimu wa utoshelevu wa mahitaji katika kujifunza;

imewezesha ujenzi wa shule mpya 19 (Msingi 11 na Sekondari 8) kwa awamu ya kwanza na shule 25 (Msingi 9 na Sekondari 16) kwa awamu ya pili kwa lengo la kuongeza fursa za upatikanaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari na kupunguza msongamo wa wanafunzi unaotokana na utekelezaji wa Sera ya Elimu Bila Malipo;
imewezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa 3,283, matundu ya vyoo 5,383, mabweni 112, nyumba za watumishi 32 (2 in 1), mabwalo sita (6), majengo ya utawala matano (5) na maabara 12

katika shule 1,714 (Msingi 998 na Sekondari 716) zilizopo katika Halmashauri 184 kwa lengo la kuimarisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji; na
imekarabati Vyuo vya Ualimu tisa (9) vya Monduli, Mamire, Singachini, Bustani, Bunda, Mtwara (U), Mtwara (K), Katoke na Vikindu ambapo ukarabati upo katika hatua mbalimbali. Aidha, imewezesha ujenzi wa Vyuo vya Ualimu vitatu (3) vya Dakawa, Mhonda na Sumbawanga pamoja na ukarabati wa nyumba za wakufunzi katika Vyuo vya Ualimu 18. Kukamilika kwa ujenzi na ukarabati kutaimarisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Ithibati na Usajili wa Shule na Vyuo vya Ualimu​

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu la upatikanaji wa fursa ya Elimu na Mafunzo, Serikali imetekeleza kazi zifuatazo:
imefuatilia na kutathmini shule 213 zilizosajiliwa kwa masharti na kubaini kuwa shule hizo zimefuata sheria, kanuni na taratibu za usajili wa shule ikiwa ni pamoja na kuongeza miundombinu ya vyumba vya madarasa, ofisi na matundu ya vyoo vya watumishi na wanafunzi;

imesajili shule 433 zilizoomba na kukidhi vigezo vya usajili kwa lengo la kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa katika Shule za msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu;
imechapa na kutoa jumla ya vyeti vya usajili wa shule 86 kwa lengo la kuwezesha shule kutambulika rasmi na kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu;
imekamilisha uandaaji wa mfumo wa kieletroniki wa Usajili wa Shule za Awali na Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu ambao utawezesha usajili kufanyika kwa ufanisi zaidi; na
imehuisha Mwongozo wa Uanzishaji na Usajili wa Shule za Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu ili kukidhi mahitaji ya sasa ya

jamii.

Usimamizi na Uendelezaji wa Elimu Maalum​

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuendelea kuimarisha utekelezaji wa afua zenye kuhakikisha elimu yetu inakuwa jumuishi, Serikali imeendelea kutoa mafunzo yanayolenga kuboresha utoaji wa Elimu Maalum na Jumuishi kama ifuatavyo:
imetoa mafunzo kazini kwa walimu 1,076 wa shule za msingi na sekondari wanaofundisha wanafunzi viziwi, wasioona, wenye ulemavu wa akili na wenye usonji kuhusu matumizi ya Lugha ya Alama ya Tanzania, mbinu za ufundishaji na ujifunzaji, huduma ya utengamao na matumizi ya vifaa vya kuchapia maandishi ya Nukta Nundu (Braille) kwa wanafunzi wasioona;

imehamasisha jamii kuhusu utambuzi wa mapema, uandikishaji na utoaji wa huduma za kielimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika ngazi zote za elimu. Lengo ni kuongeza ushiriki wa wazazi, walezi, jamii na wadau wa elimu katika kutoa elimu kwa usawa kwa watoto wenye mahitaji maalum nchini; na

imehamasisha Walimu, Maafisa Elimu Maalum, Maafisa Afya na Ustawi 314 kuhusu namna bora ya kuwabaini watoto wenye mahitaji maalum wenye umri wa kuandikishwa shule.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum, Serikali imetekeleza yafuatayo:
imenunua vishikwambi 402 kwa lengo la kuimarisha ujifunzaji wa Lugha ya Alama ya Tanzania katika Shule 38 (Msingi 15 na Sekondari 23). Vilevile, imenunua vitimwendo 536 kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo waliopo shule ya msingi na sekondari ili

kurahisisha ujifunzaji wa wanafunzi hao; na

imesambaza jumla ya vifaa vya kielimu na saidizi 33,458 kwa ajili ya Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum katika shule 1,305 (msingi 1,260 na sekondari 45) kwa lengo la kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji.

Kuimarisha Mafunzo ya Elimu ya Ualimu​

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa walimu bora wanaandaliwa na wanakidhi mahitaji nchini Serikali imeendelea kuimarisha Elimu ya Ualimu na kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu nchini ambapo katika mwaka wa fedha 2020/21 imetekeleza yafuatayo:
imedahili jumla ya wanachuo 7,046 (Wanawake: 3,529 Wanaume: 3,517) wa mwaka wa kwanza katika mafunzo ya Ualimu. Udahili wa wanachuo hao utaongeza idadi ya walimu tarajali kwa lengo la kukidhi mahitaji ya walimu nchini;

imeandaa miongozo ya Umahiri wa Walimu na Wakufunzi, Mafunzo ya Ualimu kwa Vitendo na Mwongozo wa Elimu ya Kujitegemea katika Vyuo vya Ualimu kwa lengo la kuboresha uendeshaji wa Mafunzo ya Ualimu nchini; na

imegharamia Mafunzo ya Ualimu kwa Vitendo (BTP) kwa wanachuo 15,576 wa Astashahada na Stashahada ili kuwawezesha kufanya mazoezi ya kufundisha na hivyo kuimarisha ubora wa walimu.


Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mradi wa Kuimarisha Mafunzo ya Elimu ya Ualimu (Teacher Education Support Program – TESP) imetekeleza yafuatayo:
imewezesha ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali 35 kwa uwiano wa Shilingi 25,000 kwa mwanachuo kwa lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na

ujifunzaji;

inatekeleza Mkakati wa Usawa wa Kijinsia wa Elimu ya Ualimu ili kuimarisha usimamizi wa masuala ya jinsia katika ufundishaji na ujifunzaji katika Vyuo vya Ualimu;
imewezesha mafunzo ya Lugha ya Alama kwa walimu wa sekondari
269 kutoka shule 24 zinazopokea wanafunzi viziwi kwa lengo la kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule za sekondari na Vyuo vya Ualimu; na imewezesha mafunzo ya TEHAMA awamu ya pili kwa wakufunzi 366 katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali 35 ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.


Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Mradi wa Ukarabati wa Vyuo vya Ualimu (Upgrading Teachers’ Colleges - UTC) imetekeleza kazi zifuatazo:
inaendelea kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika Chuo cha Ualimu Shinyanga (Lot 1) unaohusisha: Ujenzi wa Bweni la ghorofa moja (1); Jengo la ghorofa moja (1) kwa ajili ya nyumba za wafanyakazi na ukuta kuzunguka eneo la Chuo. Aidha, imekarabati nyumba mbili (2) za wafanyakazi na nyumba ya Mkuu wa Chuo;
imekamilisha ujenzi wa Bwalo katika Chuo cha Ualimu Mpuguso (Lot 2). Aidha, inaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu mingine ikiwemo jengo la ghorofa lenye madarasa 16, maktaba, jengo la mihadhara na jengo la mikutano;
imekamilisha ukarabati wa mabweni, vyoo vya wanachuo na nyumba za watumishi katika Chuo cha Ualimu Ndala (Lot 2).

Aidha, inaendelea na ujenzi (Lot 1) wa Mabweni mawili (2) ya ghorofa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 304, ghorofa lenye vyumba 16 vya madarasa, jengo la mihadhara, jengo la maktaba na jengo la maabara; na

inaendelea kukamilisha ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Ualimu Kitangali (Lot 2) ambapo ujenzi huo unahusisha jengo la ghorofa lenye madarasa 16, maktaba, jengo la mihadhara na majengo mawili (2) ya ghorofa kwa ajili ya mabweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 304.

Kusimamia Ubora wa Elimu katika Shule na Vyuo vya Ualimu​

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa taasisi zilizopata Ithibati na Usajili zinatoa elimu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Kutokana na azma hiyo, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali imetekeleza yafuatayo:
imefanya tathmini ya jumla katika asasi 5,057 kati ya 6,020 (sawa na asilimia 84) zikiwemo shule za Awali na Msingi 4,286 kati ya lengo la 4,700, Sekondari 718 kati ya 1200 na Vyuo vya Ualimu 53 kati ya 120 ambapo shule zilizobainika kuwa na mapungufu zilipewa ushauri wa kitaalam na kitaaluma kwa ajili ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji;
imefanya ufuatiliaji wa ushauri uliotolewa katika asasi 569 zikiwemo: Shule za Awali na Msingi 490, Sekondari 74 na Vyuo vya Ualimu vitano
(5) kati ya 870 zilizobainika kuwa na kiwango dhaifu na kisichoridhisha kutokana na matokeo ya tathmini ya jumla ya mwaka 2018/19 na 2019/20 kwa lengo la kutathmini hali ya utekelezaji wa ushauri na mapendekezo yaliyotolewa;
imesimamia ujenzi wa ofisi mpya 55 na ukarabati wa ofisi 31 za Uthibiti Ubora wa Shule zilizojengwa na kukarabatiwa kupitia Mradi EP4R; na
imefanya mafunzo ya usimamizi na uwajibikaji kwa Wathibiti Wakuu Ubora wa Shule 368 wakiwemo Wathibiti Wakuu Ubora wa Shule Kanda 11, Wathibiti Wakuu Ubora wa Shule Wilaya 173, Naibu Wathibiti Wakuu Kanda 11 na Naibu Wathibiti Wakuu Wilaya 173 kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi.

Usimamizi na Uendelezaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi​


Mheshimiwa Spika, katika kusimamia na kuendeleza Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 imetekeleza kazi zifuatazo:
imewezesha upatikanaji wa hati miliki katika Vyuo nane (8) vya Maendeleo ya Wananchi. Aidha, taratibu za upimaji na upatikanaji wa hati miliki unaendelea kwa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 46; na

inaendelea na uanzishwaji wa vituo vinne (4) vya umahiri katika nyanja za TEHAMA, mazao ya Ngozi, usafiri wa ang ana nishati jadidifu katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam katika Kampasi Kuu ya Dar es Salaam na Kampasi ya Mwanza, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji na Chuo cha Ufundi Arusha mtawalia kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi Afrika Mashariki (EASTRIP) kwa lengo la kuviongezea vyuo hivyo uwezo wa kutoa mafunzo kwa vitendo yanayoendana na mpango wa nchi na soko la ajira.

Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha uwezo wa kutoa mafunzo kwa vitendo katika taasisi nchini, Serikali kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi Afrika Mashariki - East Africa for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP) katika mwaka wa fedha 2020/21, imetekeleza kazi zifuatazo:

imeandaa mitaala mipya 54 inayohusu mafunzo kwa vitendo kwa lengo la kukidhi mahitaji ya soko la ajira na tayari imeanza kutumika katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Kampasi Kuu ya Dar es Salaam na Kampasi ya Mwanza, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji na Chuo cha Ufundi Arusha; na
imenunua magari nane (8) na mabasi mawili (2) katika taasisi ya

Teknolojia Dar es Salaam Kampasi ya Dar es Salaam na Mwanza, Chuo cha Usafirishaji na Chuo cha Ufundi Arusha kwa lengo la kuwezesha utendaji kazi.

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ujuzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 imeendelea kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali kama ifuatavyo:

imewezesha mafunzo ya muda mrefu ya Ufundi Stadi kwa wanachuo 9,565 katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 54 ili kuwapa ujuzi unaohitajika katika soko la ajira;
imetoa mafunzo ya muda mfupi ya fani mbalimbali kwa Washiriki 10,449 (Wanawake: 6,224 Wanaume: 4,225) katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 54 ili kuwaongezea uwezo wa kutekeleza miradi ya maendeleo na shughuli katika maeneo wanayoishi; na
imewezesha mafunzo kwa wakufunzi 412 wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 54 ili kuboresha ufundishaji kwa masafa na kwa kutumia mitaala inayoendana na soko la ajira.

Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha utoaji wa huduma za Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini, Serikali kupitia Mradi wa Elimu na Kukuza Stadi za Kazi na Ujuzi (Education and Skills for Productive Jobs – ESPJ) katika mwaka wa fedha 2020/21 imetekeleza kazi zifuatazo:

imetoa mafunzo kwa watumishi 1,177 (Wanawake: 591, Wanaume:
586) kulingana na maeneo ya ubobezi na aina ya kazi wanazosimamia ili kuimarisha utendaji;

imeendelea na ujenzi wa Vyuo vya VETA vya Wilaya 29 ambavyo ni; Kongwa, Kasulu, Ruangwa, Nyasa, Igunga, Bahi, Lushoto, Masasi, Iringa, Mbarali, Uvinza, Buhigwe, Kishapu, Longido, Mafia, Butiama, Ulanga, Korogwe, Mkinga, Chemba, Kilindi, Kwimba, Ukerewe,

Ikungi, Monduli, Chunya, Uyui, Pangani na Rufiji ambapo ujenzi upo katika hatua mbalimbali;
imewezesha uanzishwaji wa programu za mafunzo 80 ambazo zinaendana na vipaumbele vya Mkakati wa Kitaifa wa Kuendeleza Ujuzi ambavyo ni Kilimo-Biashara, Utalii na Ukarimu, Ujenzi, Uchukuzi, Nishati na TEHAMA. Aidha, vijana 29,047 wamenufaika na programu hizo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF);
imewezesha mafunzo kwa vitendo (uanagenzi) kwa wahandisi wahitimu 500 (Wanawake: 130, Wanaume: 370) katika miradi mikubwa ya ujenzi ya kitaifa ikiwemo Standard Gauge Railway (SGR) na Mwalimu Julius Nyerere Hydropower Project (MJNHP) na Ubungo Interchange Bridge kwa usimamizi wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wahitimu kuajiriwa na kujiajiri na hivyo kufikia lengo la Serikali la kukuza uchumi nchini;

imeendelea na ukarabati wa maktaba za Mikoa saba (7) ambazo ni; Tabora, Morogoro, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Rukwa na Iringa. Ukarabati huo umekamilika katika Mikoa ya Kagera, Iringa na Rukwa na Mikoa mingine ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji;
imewezesha ujenzi wa Shule Maalumu ya Viziwi ya Lukuledi Masasi ili kuongeza fursa ya upatikanaji wa Elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini ambapo ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji; na imeendelea na ujenzi wa ofisi za NACTE katika Kanda tano (5) za Kaskazini, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Magharibi ili kusogeza huduma karibu na wananchi ambapo ujenzi umefikia asilimia 55.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaandaa miongozo mbalimbali itakayotumika katika taasisi zinazotoa elimu ya ufundi ukiwemo Mwongozo wa ulinganifu wa Kitaaluma wa Kitaifa (National Qualification Framework); “TVET Curricula Development Manual”; “CBET Training Manual on CBET Curricula Development/Review, Delivery and Assessment”; na “Occupational Standards for EASTRIP TVET Priority Sectors (Energy, Leather Processing, Transport and ICT)”. Miongozo hiyo ipo katika hatua mbalimbali za kupata maoni kutoka kwa wadau kwa lengo la kuboresha maudhui yatakayokidhi mahitaji ya soko la ajira.

Usimamizi na Uendelezaji wa Elimu ya Juu​

Mheshimiwa Spika, katika usimamizi na uendelezaji wa Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetekeleza kazi zifuatazo:
imeratibu ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 134 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Morocco wanafunzi 26 (Wanawake 6), Hangaria
27 (Wanawake 6), Jumuiya ya Madola wanafunzi watano (5) (Shahada ya Umahiri watatu (3) na Uzamivu wawili (2) na China 76 (Wanawake 23) kuanzia ngazi ya Shahada ya Kwanza hadi Shahada ya Uzamivu;

imeratibu vikao vinne (4) vya Uongozi na Usimamizi (National Steering Committee) wa Vituo vya Umahiri vya Africa (African Centre of Excellence ACE II) katika Taasisi za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa lengo la kujadili utendaji wa pamoja na kuweka mikakati itakayowezesha vituo hivyo kuwa endelevu;

imeendelea kuratibu ufadhili wa masomo kwa wanataaluma 68 katika ngazi ya Shahada ya Umahiri wanne 4 (wanaume) na Shahada ya Uzamivu 64 (Wanawake 17) kutoka katika Vyuo Vikuu

vya Umma katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Usanifu majengo, Hisabati na ICT; na

imefanya ufuatiliaji wa mahitaji ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu katika Vyuo Vikuu vya Umma na uchambuzi wa maombi unaendelea ili kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa saidizi kwa wanafunzi hao.


Usimamizi na Uendelezaji wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
Mheshimiwa Spika,
katika kuratibu na kusimamia uendelezaji wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu nchini, Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21 kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetekeleza kazi zifuatazo:
imeendelea na kazi ya kuwaendeleza wabunifu 130 waliopatikana katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) ya mwaka 2019 na 2020 kwa kuboresha ubunifu wao ili ufikie hatua ya ubiasharishaji na kuwa fursa ya kiuchumi kwa wabunifu wenyewe na jamii kwa ujumla. Aidha, bunifu 26 kati ya
130 zinazoendelezwa na Serikali zipo katika hatua ya kubiasharishwa na hivyo kutumika kutatua changamoto mbalimbali katika sekta za kilimo, maji, nishati, madini, afya na elimu;

imeratibu maandalizi ya Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2021 kwa lengo la kuibua, kutambua na kuendeleza wabunifu na wavumbuzi wachanga nchini. Jumla ya wabunifu 714 wamejitokeza kushiriki mashindano ya mwaka 2020/21 ambapo wabunifu mahiri takribani 70 wamepatikana na watashiriki kilele cha mashindano kitakachofanyika tarehe 6 – 11 Mei, 2021 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Wabunifu watatu kwa kila kundi watapewa tuzo mbalimbali;

imetambua na kuhakiki teknolojia mpya 79 na kufanya jumla ya

teknolojia zilizozalishwa nchini na kutambuliwa hadi sasa kufikia
310. Lengo la utambuzi huo ni kuwa na kanzidata ya kitaifa itakayorahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kuhusu teknolojia na bunifu nchini;

imefanya mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Mkoa kwa Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kuibua, kutambua na kuendeleza wabunifu na wavumbuzi wachanga nchini;

imetambua matokeo ya tafiti na vifaa ya kufanyia utafiti katika Taasisi 154 za Utafiti na Maendeleo na Elimu ya Juu za umma kwa lengo la kuanisha matokeo ya utafiti hususan yale yenye manufaa ya moja kwa moja kwa jamii, pamoja na kubaini uwezo wa vifaa na wataalam katika Taasisi hizo;

imefanya ufuatiliaji na tathmini ya miradi (10) ya utafiti inayofadhiliwa na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) na kuratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania katika Sekta za Maji, Afya, Kilimo na Mifugo na kubaini kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unafanyika kulingana na makubaliano; na

imeshiriki Mkutano Mkuu wa 64 wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) uliofanyika Vienna, Austria mwezi Septemba, 2020 ambapo ushiriki huo uliwezesha miradi mitatu ya utafiti katika sekta za afya, kilimo (food irradiator) na elimu (research reactor) kupata ufadhili.

Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Wizara​

Mheshimiwa Spika, katika kusimamia na kuendeleza Rasilimaliwatu kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetekeleza kazi zifuatazo:
imeandaa Muundo na Mgawanyo wa Majukumu ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu pamoja na Miundo na Mgawanyo wa Majukumu ya Vyuo Vikuu na kuwasilisha Ofisi ya Rais Utumishi (OR – UTUMISHI);

imekamilisha Muundo wa Uthibiti Ubora wa Shule ili kurahisisha usimamizi na uendelezaji wa watumishi kwa lengo la kuongeza ufanisi na uwajibikaji;

imeandaa, kuchambua na kutoa vibali vya ajira za kigeni kwa waombaji 184 waliokidhi vigezo kati ya maombi 185 yaliyowasilishwa kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma; na

imefanya ukaguzi wa Ufanisi (Performamce Audit) katika Taasisi 13 zilizo chini ya Wizara kwa lengo la kubainisha hali halisi ya utendaji na utekelezaji wa kazi mbalimbali za taasisi ikilinganishwa na Sheria ya uanzishwaji wa Taasisi husika.

SHUGHULI ZILIZOFANYWA NA TAASISI, MAMLAKA NA WAKALA ZILIZO CHINI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21​

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu majukumu ya Taasisi, Mamlaka na Wakala zilizo chini yake ili kuhakikisha nchi inazalisha rasilimaliwatu yenye weledi kwa kuzingatia mahitaji ya Mipango ya ndani ya nchi, Soko la Kitaifa, Kikanda na Kimataifa. Kazi zilizofanyika kwa kila taasisi ni kama ifuatavyo:

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili jumla ya wanafunzi 42,745 (Wanawake 19,633 Wanaume 23,112);

imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 60 (Shahada za Awali 50 na Umahiri 10) ambapo asilimia 50 ya wanufaika ni wanafunzi wa kike. Kati ya wanufaika hao asilimia 90 ni wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi;

imefadhili wanafunzi watatu (3) wa shahada ya umahiri katika lugha ya kiswahili kutoka nchi za; Ghana, Rwanda na Uganda;

imefadhili wanataaluma 38 (Shahada za Uzamivu 21 na Shahada za Umahiri 17) kwa lengo la kuongeza idadi ya wahadhiri wenye sifa stahiki;

imeongeza miradi mipya ya utafiti 66 na hivyo kuwezesha chuo kuwa na jumla ya miradi 239 kutoka 173 ya awali. Miradi hiyo inahusisha: Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, TEHAMA na Maendeleo ya Viwanda; Elimu, Kilimo, Usalama wa Chakula na Afya; Utawala Bora, Sera za Viwanda na Uzalishaji na Matumizi Endelevu; Jinsia, Ukuzaji wa

Utaalamu, Uandaaji na Utekelezaji wa Sera; Historia, Utamaduni, lugha, Urithi na Utalii Endelevu; na Maliasili, Mazingira na Teknolojia; na Sheria na Maendeleo Jumuishi ya Taifa; na

imeongeza idadi ya machapisho ya chuo katika majarida ya kitaifa na kimataifa kutoka machapisho 1,048 hadi kufikia 1,172.


Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 Serikali imetekeleza kazi zifuatazo:
imekamilisha usanifu na inaendelea na hatua za manunuzi ya kumpata mkandarasi atakayefanya upanuzi wa bweni la Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa ghorofa mbili zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,280 na hivyo kufanya bweni kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 5,120;
imekamilisha utiaji saini mkataba na kukabidhi eneo la ujenzi kwa mkandarasi ili kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa Jengo la Shule Kuu ya Uchumi katika kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere. Jengo litakuwa na ukubwa wa ghorofa sita (6) zenye ofisi 50 za wafanyakazi, ofisi za kukaa wanafunzi 60 wa masomo ya uzamili, kumbi za mihadhara sita (6) zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 800, ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 80; na sehemu ya huduma ya chakula yenye uwezo wa kuchukua watu 120;

inaendelea na mradi wa kituo cha wanafunzi ambacho tayari ujenzi wa ghorofa saba (7) umekamilika na kazi zilizobaki ni ujenzi wa paa, nguzo za mapambo (decorative columns) na kuanza awamu ya umaliziaji na kufunga samani. Jengo hili litakapokamilika litatoa huduma za sehemu za kujisomea, huduma za kibenki, maduka, saluni za kike na kiume, sehemu za vinywaji, ukumbi wa burudani na wa kutumbuiza na ofisi ya Mlezi wa Wanafunzi; na

imekarabati hosteli za wanafunzi, kumbi za mihadhara, kituo cha polisi, nyumba za wahadhiri, miundombinu ya maji safi na majitaka, umeme, barabara na kuta za kuzuia udongo.


Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili jumla ya wanafunzi wapya 5,499 kati ya hao Astashahada wanafunzi 38 (Wanawake: 12, Wanaume: 26), Stashahada wanafunzi 249 (Wanawake: 106, Wanaume: 143) na Shahada za Awali 4,964 (Wanawake: 1,864 Wanaume: 3,100) na Shahada za Uzamili (Umahiri na Uzamivu) wanafunzi 248 (Wanawake: 97 Wanaume: 151);
imeanza kutoa mafunzo katika Kampasi mpya ya Mizengo Pinda - Katavi kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada katika nyanja za Kilimo, Utalii, Mifugo na Misitu ambapo wanafunzi 105 (Wanawake: 32, Wanaume: 73) wamesajiliwa;
imeendelea kuviongezea uwezo vitengo vya uzalishaji ikiwa ni pamoja na: Kitengo cha kuzalisha mikate; Kitengo cha daharia kilichopo katika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (Institute of Continuing Education - ICE); Kitengo cha Msitu wa Mafunzo Olmotonyi; na Kitengo cha Ng’ombe wa Maziwa na shamba la Katani lililopo katika shamba la chuo na Maabara ya Udongo; na

imepima jumla ya sampuli 2,500 za udongo kutoka kwa wakulima kupitia Maabara ya Udongo kwa lengo la kuleta tija katika kuzalisha mazao ya kilimo na kuweza kupunguza umaskini. Sampuli hizo ni kama ifuatavyo: udongo (1,678); maji (252); mbolea za viwandani (151); samadi (6); na mimea (413).

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo iliandaa na kushiriki katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Morogoro na maonesho ya kilimo ya kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi - Mkoani Simiyu. Maonesho hayo yalilenga kutoa elimu kuhusu kilimo na ufugaji na yaliwafikia zaidi ya wadau 10,000. Katika maonesho ya kilimo ya kitaifa Simiyu, SUA ilishinda kombe na cheti cha mshindi wa kwanza katika kundi la Vyuo Vikuu na katika maonesho ya ukanda wa mashariki Morogoro, SUA ilipata cheti cha mshindi wa tatu katika kitengo cha mashirika ya umma.

Mheshimiwa Spika, katika kutoa elimu na kuendeleza Sekta ya Kilimo nchini, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo imetekeleza kazi zifuatazo:
imeendelea kutoa elimu na ushauri kwa washiriki 1,280 kupitia Vituo Atamizi vya Mafunzo ya Kilimo-Biashara, mashamba darasa na semina katika maeneo ya Manispaa ya Morogoro, Bahi, Kongwa, Mlali na Simiyu. Utoaji wa elimu na ushauri ulilenga kuongeza tija katika uzalishaji na hatimaye kupunguza umaskini miongoni mwa washiriki; na
imeendesha semina kupitia washirika wa maendeleo kwa lengo la kuwashirikisha wadau wa ndani na nje ya chuo kutoa maoni kuhusu uundaji wa sera itakayotumika kuinua kilimo na mifugo nchini.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga na kukarabati miundombinu kama ifuatavyo:
imejenga jengo la Maabara Mtambuka ambalo lina maabara nane (8) na madarasa nane (8) na lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,200 kwa wakati mmoja. Jengo hilo litajumuisha ofisi saba (7) zitakazo

tumika na wafanyakazi 38, vyumba vya maandalizi 11 na stoo saba
(7) za kuhifadhia kemikali;

imekarabati miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa, karakana, maabara, majengo ya Ndaki ya Tiba ya Wanyama ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Wanyama, Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Sokoine, mabweni ya wanafunzi na nyumba za wafanyakazi kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia;
imekarabati majengo katika kampasi mpya ya Mizengo Pinda - Katavi ambapo ukarabati huo uliwezesha udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2020/21; na
imeboresha sehemu ya Makumbusho ya Mazao (Crop Museum) kwa kudumisha mazao yaliyopo na kupanda mazao mapya.

Mheshimiwa Spika, ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira, Serikali imeongeza programu mpya za masomo 20 katika ngazi tofauti kama ifuatavyo: Shahada za Uzamili (12); Shahada za Awali (6); Stashahada (1); na Astashahada (1) ambapo baadhi ya programu hizo zimeanza kutolewa kwa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2020/21.

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) imetekeleza kazi zifuatazo:
imeongeza udahili wa wanafunzi kutoka 4,051 kwa mwaka wa masomo 2019/20 hadi kufikia 4,200 kwa mwaka 2020/21 (Stashahada 373, Shahada ya kwanza 2,695 na Shahada ya Uzamili 1,132); na
imesajili jumla ya kozi 172 katika mfumo wa TEHAMA na kati ya kozi hizo kozi 81 zimetumika katika mwaka wa masomo wa 2020/21.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa na ubora unaokidhi viwango na mahitaji ya soko la ajira Kitaifa, Kikanda na Kimataifa, Serikali kupitia MUHAS imetekeleza yafuatayo:
imeandaa jumla ya maandiko dhana ya tafiti 21 na kuwasilisha katika taasisi mbalimbali zinazoweza kufadhili tafiti hizo ambapo maandiko 16 kati ya hayo yalipata ufadhili kwa ajili ya kutekeleza tafiti husika; na
imepata Mshauri Elekezi (Consultant) kwa ajili ya kutengeneza Andiko la Mpango wa Biashara la Kuanzisha Kliniki ya Uporoto (Uporoto Polyclinic) na yupo katika hatua za uandishi wa andiko hilo kwa kushirikiana na wataalamu wa MUHAS.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga na kukarabati miundombinu kama ifuatavyo:
inaendelea na ujenzi wa kituo cha umahiri wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (Center of Excellence in Cardiovascular Sciences) katika kampasi ya Mloganzila ambapo ujenzi umekamilika kwa asilimia 75;
imekarabati chumba cha kutolea huduma binafsi katika shule ya meno na taratibu za ununuzi wa vifaa vya meno zinaendelea; na
imekarabati hosteli za wanafunzi zilizopo barabara ya Chole - Dar es Salaam zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 550.

Chuo Kikuu Ardhi (ARU)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu Ardhi imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili jumla ya wanafunzi 4,920 wakiwemo wa ngazi ya Shahada ya Kwanza 4,619 (Wanawake: 1,965 Wanaume: 2,654), Shahada ya

Umahiri 226 (Wanawake: 68 Wanaume: 158) na Shahada ya Uzamivu 75 (Wanawake: 10 Wanaume: 65);
imechapisha jumla ya machapisho 59 katika majarida mbalimbali (peer reviewed journals) kwa lengo la kuongeza maarifa kwa jamii kuhusu usimamizi wa ardhi na mazingira, uboreshaji wa mazingira na usanifu majengo;
imetoa mafunzo kwa wakazi wa kata ya Goba, Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu ujenzi bora wa makazi ili kujikinga na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi ambapo wananchi walielimishwa kuhusu viwango na kanuni za mipango miji na matumizi bora ya ardhi;
imepata mradi wa kujenga uwezo katika elimu, utafiti, ubunifu na huduma kwa jamii kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Hasselt cha Ubeligiji. Mradi unalenga kukuza mazingira jengwa (Built Environment) jumuishi na endelevu katika miji inayokua haraka (SDG 11 in Dar es Salaam) na utatekelezwa katika mkoa wa Dar es Salaam. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la VLIR - OUS la Ubeligiji kwa kiasi cha fedha Euro 300,000 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 10;

imeendelea kufanya utafiti wa kubuni modeli ya urasimishaji makazi holela katika miji inayoibukia katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambapo takribani viwanja 70,000 vitapimwa. Mradi unalenga kutatua changamoto ya makazi holela na utapima kila kipande cha ardhi ya jumla (general land). Aidha, utekelezaji wa mradi huo utawezesha Serikali kupata mapato kutokana na ada za umilikishaji ardhi, tozo ya thamani ya ardhi wakati wa umilikishaji na kodi ya pango la ardhi; na
imeendelea kusimamia miradi ya tafiti 53 zinazolenga kutatua changamoto za kijamii hususan katika maeneo ya matumizi bora ya ardhi, utunzaji wa mazingira, kujikinga na maafa, usimamizi bora wa ardhi, makazi na ujenzi.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Chuo Kikuu Ardhi imetoa ushauri wa kitaalamu kwa jamii kwenye miradi ya: Ujenzi wa kituo cha mabasi cha Kimataifa cha Magufuli Dar es Salaam; Shule ya mfano ya sekondari ya Dodoma (Dodoma Model Secondary School); na Ukabarati wa vyuo vya ualimu nchini (Kleruu, Mpwapwa, Kitangali, Mpuguso, Shinyanga na Ndala). Vilevile, imetoa ushauri wa kusanifu michoro ya jengo la maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) linalotarajiwa kujengwa jijini Dodoma; kusanifu michoro na kusimamia ujenzi wa majengo ya Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Butiama, majengo ya hospitali za rufaa za Mwalimu Nyerere - Mara, Simiyu, Mtwara na Njombe; pamoja na majengo ya maabara za Tume ya Taifa ya Nguvu za Atomiki (TAEC) zinazotarijiwa kujengwa Dodoma, Mwanza na Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, Serikali imetekeleza kazi zifuatazo:
imekamilisha ujenzi wa Jengo la Ardhi (Land Building) ‘wing B’ lenye ofisi 42 zenye uwezo wa kuchukua wafanyakazi 84 na vyumba vinne
(4) vya madarasa vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 32 wa Shahada ya Uzamivu pamoja na vyumba vitatu (3) vya mikutano vyenye uwezo wa kuchukua watu 36 kwa kila chumba. Pia, inaendelea na ujenzi wa bweni la wanafunzi lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 592 ambapo hadi sasa sehemu ya jengo hilo lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 352 imekamilika pamoja na uwekaji wa samani. Vilevile, imefanya ukarabati wa mabweni ya wanafunzi, maabara, madarasa, ofisi za wafanyakazi, miundombinu ya TEHAMA, maji safi na majitaka pamoja na kuweka taa za barabarani.
Mheshimiwa Spika, ili kujenga uwezo wa chuo katika kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa huduma kwa jamii, Serikali imeendelea kutoa

mafunzo ya muda mrefu kwa wafanyakazi wapatao 35; wakiwemo wa ngazi ya shahada ya Uzamivu 17 (Wanawake: 2 Wanaume: 15), ngazi ya Umahiri
15 (Wanawake: 6 Wanaume: 9) ngazi ya Shahada ya Awali mmoja (mwanaume) na wa ngazi ya Stashahada wawili (mwanamke na mwanaume).

Chuo Kikuu Mzumbe​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Mzumbe imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili wanafunzi wapya 4,754 (Astashahada 455, Stashahada 379, Shahada ya Awali 3,304, Shahada ya Umahiri 603 na Shahada ya Uzamivu 13);
imefadhili masomo kwa watumishi 69 kwa ngazi ya Uzamili (Shahada ya Uzamivu 59 na Shahada ya Umahiri 10);
imechapisha jumla ya machapisho 51 ya kitaaluma kwa lengo la kuwezesha jamii kupata maarifa;
imeendelea kutekeleza miradi ya utafiti 29 katika maeneo ya utawala, uongozi na ujasiriamali; na
imekamilisha ujenzi wa majengo mapya manne (4) ya hosteli zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,024 katika Kampasi Kuu na taratibu za ununuzi wa samani unaendelea. Vilevile, imekamilisha ujenzi wa jengo jipya la madarasa na kumbi za mihadhara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000.


Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Dodoma imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili jumla ya wanafunzi 9,713 ambapo Shahada ya Awali 9,033 na Shahada za Uzamili 680 (Uzamivu 114, Umahiri 545 na Stashahada

ya Uzamili 21);

imeanzisha progamu mpya tano (5) ambapo Shahada ya Awali moja (1), Shahada za Umahiri mbili (2) na katika Shahada ya Uzamivu mbili
(2) ili kuwezesha chuo kuzalisha wahitimu wanaoendana na soko la ajira;
imechapisha jumla ya machapisho 282 ambayo yalichapishwa katika majarida mbalimbali. Aidha, imeanzisha majarida manne (4) ya ndani kwa ajili ya tafiti;
imefadhili mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 141 na mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 296 kuanzia ngazi ya Astashahada hadi Shahada ya uzamili. Aidha, imewezesha mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi 73 wa ngazi mbalimbali za uongozi; na
imeboresha mfumo wa usajili wa wanafunzi ambapo wanafunzi wote walisajiliwa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki (Online Registration). Mfumo huu umepunguza gharama za usajili na kurahisisha zoezi la usajili na kuwawezesha wanafunzi kusajili popote walipo.


Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kununua vitabu 828, vifaa vya maabara, TEHAMA na kufunga Kamera za Uoni (CCTV Camera) kwa ajili ya maeneo muhimu ya chuo kwa lengo la kuimarisha usalama. Aidha, imefunga viti vipya 600 katika ukumbi wa Chimwaga na kukarabati mabweni 20 Ndaki ya Elimu.


Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi imetekeleza yafuatayo:
imedahili wanafunzi wapya 5,025 katika ngazi mbalimbali ambapo

Astashahada ni wanafunzi 1,796 (Wanawake: 949 Wanaume: 847),
Stashahada 1,070 (Wanawake: 559 Wanaume: 471), Shahada za
Awali 2,052 (Wanawake: 948 Wanaume: 1,104) na Shahada za
Uzamili 147 (Wanawake: 48 Wanaume: 99);

imewezesha watumishi 69 (Wanataaluma 58 na Waendeshaji 11) kuhudhuria mafunzo katika ngazi mbalimbali kama ifuatavyo: Shahada ya Uzamivu (43); Shahada za Umahiri (20); Stashahada za Uzamili (2); Shahada za Awali (3); na Stashahada (1);
imeandaa programu tano (5) za mafunzo ili kuongeza wigo wa udahili wa wanafunzi hususan katika fani za ushirika na biashara, huduma za kibenki, usimamizi wa fedha pamoja na ushirika wa mazao na masoko;
imechapisha jumla ya machapisho 70 ya kitaaluma kwa lengo la kueneza matokeo ya tafiti kwa jamii; na
imeandaa mpango kazi wa tafiti tatu (3) za kimkakati kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini kwa lengo la kusaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya ushirika.


Mheshimiwa Spika, ili kuwajengea uwezo wahadhiri na wanafunzi katika masuala ya kutatua matatizo ya kijamii kupitia TEHAMA pamoja na kuwawezesha wanafunzi kubaini fursa mbalimbali za ajira, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi imetekeleza yafuatayo:
imeratibu upatikanaji wa miradi miwili ambayo ni “Sustainable Business and Employability through Active Pedagogy in HEI (SUSIE) Research Project” na “Social Innovations in GEO-ICT Education at Tanzanian HEIs for Improved Employability (GeoICT4e)”; na
imeendelea na utekelezaji wa mradi wa kutoa mafunzo ya Kilimo- Biashara na Ujasiriamali (Skills Development Fund) kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana 181 wa mwaka wa pili na wa

tatu wa Shahada ya Awali ya uchumi wa biashara.


Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Elimu ya Ushirika inawafikia wadau mbalimbali nchini, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi imetekeleza yafuatayo:
imeratibu mafunzo kuhusu elimu ya ushirika kupitia ofisi za Chuo za mikoani ambapo wanachama, viongozi na watendaji wa vyama mbalimbali vya ushirika 7,296 wamepatiwa mafunzo. Mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kuongeza ufanisi wa usimamizi wa vyama vya ushirika;
imetoa huduma za kijamii na ushauri kwa wanachama 3,130 katika vyama vya ushirika na vikundi mbalimbali vya maendeleo ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa vyama vya ushirika; na
imeandaa na kurusha vipindi vya redio kuhusu masuala ya ushirika ambapo jumla ya vipindi vya redio 36 vimerushwa kupitia TBC – Taifa na vipindi 15 kupitia redio za kijamii.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi imekarabati kumbi nne (4) pamoja na vyumba 10 vya mihadhara vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,308 kwa wakati mmoja pamoja na maabara ya kompyuta moja na nyumba 10 za makazi. Aidha, inaendelea na ujenzi wa ukumbi mmoja wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kwa wakati mmoja.

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili wanafunzi 12,929 (Astashahada 3,831, Stashahada 2,596, Shahada ya Awali 3,895, Stashahada ya Uzamili 518, Shahada ya

Umahiri 1,982, na Shahada ya Uzamivu 107);

imeandaa kongamano lililowezesha uandaaji wa maandiko yatakayochapishwa katika toleo maalum la Jarida la Huria. Kongamano hilo lilifanyika kwa njia ya “Zoom” na lilivutia washiriki 22 kutoka katika taasisi zifuatazo; Saint Mary’s University of Minnesota - USA (4); Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (3); na wafanyakazi na wanafunzi wa shahada za uzamivu kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (15);
imeandaa Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Wanafunzi wa Shahada za Uzamili “Postgradute Management Information System” (PGMIS) unaopatikana kupitia tovuti ya chuo . Mfumo huo utawezesha wanafunzi kuwasilisha mapendekezo yao, kupokea maelekezo, ushauri wa wasimamizi na ufuatiliaji; na
imerekodi mihadhara ya video 204 kwa kozi 61 inayopatikana kwa njia ya mtandao (youtube) kwa jina la “ODL TV”.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga vituo vitano (5) katika mikoa ya Geita, Manyara, Lindi, Simiyu na Kigoma ambapo ujenzi upo katika hatua mbalimbali. Aidha, imekarabati Mfumo wa Umeme katika Kituo cha Mkoa wa Mwanza pamoja na kukarabati vyoo katika Kituo cha Mbeya.

Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kimetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili wanafunzi 2,104 wa mwaka wa kwanza ambapo Shahada ya Awali ni 2,039 (Wanawake: 1,061 Wanaume: 978) na Shahada za Uzamili ni 65 (Wanawake: 30 na Wanaume: 35);
imeandaa mitaala miwili (2) ya Stashahada ya Uzamili ya Ushauri na

Unasihi na Shahada ya Elimu Jamii katika Lugha ya Kitaalamu kwa lengo la kuongeza idadi ya wataalamu wa kada ya ushauri na unasihi;
imewezesha mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 36 (Wanataaluma 29 na Waendeshaji 7) na mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 80 kwa lengo la kuleta ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu yao; na
imefanya tafiti 21 zikiwemo tafiti mpya 19 kwa lengo la kupata maarifa yatakayosaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, Serikali kupitia Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam imetekeleza Awamu ya Pili ya upanuzi wa jengo la Utawala ambapo nafasi
136 za ofisi zimepatikana. Vilevile, imekarabati vyumba vya madarasa, hosteli za wanafunzi na ofisi na kuweka samani zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 216 katika hosteli za wanafunzi (NSSF Mtoni Kijichi).

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kinatoa elimu bora na kwa usawa, Serikali imetekeleza yafuatayo:
imenunua kompyuta 20 pamoja na vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia vya wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwezesha utoaji wa elimu jumuishi na kutimiza azma ya Serikali ya kutoa elimu bora kwa wote; na
imenunua kompyuta 100 kwa ajili ya wanafunzi na watumishi na kuongeza ujazo wa intaneti kutoka Mbps 50 hadi Mbps 60 na hivyo kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya intaneti chuoni pamoja na kuwezesha chuo kutumia TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa imetekeleza yafuatayo:
imedahili jumla ya wanafunzi 6,399 ambapo kati yao Shahada ya Awali 6,378 na Shahada za Umahiri 21;
imeanzisha programu moja (1) isiyo ya kielimu (B.Sc. Chemistry) ikiwa ni asilimia 17 ya lengo la programu sita (6). Aidha, programu tano (5) zipo katika hatua za uidhinishaji;
imetoa machapisho 34 katika Nyanja za Insia na Sayansi za Jamii, Elimu na Sayansi;
imeratibu semina moja (1) ya kitaaluma na kutekeleza miradi 21 ya utafiti na ushauri ili kuongeza wingi na ubora wa kazi za kitafiti na kiugunduzi;
imeratibu kongamano moja (1) la Kimataifa la Sayansi na Teknolojia kwa Maendeleo Endelevu. Kongamano hili liliwakusanya watafiti ambao waliwasilisha mada mbalimbali, lengo likiwa ni kutafuta majawabu ya changamoto za jamii na kubadilishana uzoefu na kuongeza wigo wa mashirikiano katika utafiti na maendeleo;
iliendesha mafunzo kwa walimu 40 kutoka katika Wilaya za Mpwapwa, Kilosa na Iramba kwa lengo la kuwaongezea uwezo hivyo kuboresha elimu ya awali kwa watoto wa kitanzania; na
imewezesha watumishi 88 kupata mafunzo ya muda mrefu katika ngazi za Shahada ya Kwanza na Uzamili ili kuongeza weledi na ufanisi katika utendaji kazi.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, Serikali kupitia Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa imenunua vitabu 449, vifaa vya maabara, kompyuta na vifaa vya TEHAMA. Aidha, imekarabati miundombinu ya Chuo pamoja na kujenga jengo la maabara ya Kemia.

Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo cha Ufundi Arusha imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili jumla ya wanafunzi 2,814 ambapo ngazi ya Stashahada (NTA Level 4) 1,350, Shahada (NTA Level 7) 311 na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET) 1,153;
imetoa mafunzo kwa vitendo (industrial practical training) kwa wanafunzi 2,050; na
imeanzisha mifumo saba (7) ya ndani ya uthibiti ubora ambayo itawezesha mwanafunzi kufuatilia maendeleo yake na chuo kufuatilia utaratibu unaotumika katika kutoa mafunzo na upimaji.


Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kufanya utafiti wa matumizi bora ya maji katika kilimo cha mpunga kwa kushirikiana na Japan International Research Centre for Agricultural Sciences (JIRCAS) katika maeneo ya miradi ya Skimu za Mahande (Mto wa Mbu) na Lower Moshi (Kilimanjaro). Utafiti huo utawezesha kufanya kilimo cha mpunga hata katika maeneo yenye mvua chache na uhaba wa maji.

Mheshimiwa Spika, ili kutoa ushauri wa kitaalamu katika miradi ya maendeleo, Serikali kupitia Chuo cha Ufundi Arusha imetekeleza yafuatayo:
imesanifu na kusimamia miradi ya ujenzi katika: Vyuo vya VETA (Kasulu, Ruangwa, Kongwa na Nyasa); Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 31; Vyuo vya Ualimu 16; na Mradi wa stendi kuu ya mabasi ya Kahumo – Wilaya ya Chato - Geita;
imepima udongo katika miradi ya: Upanuzi wa maji safi na majitaka katika Jiji la Arusha; Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Arusha; Ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai; Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya

ya Babati na Ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji Kivingo – Lushoto, Tanga;
imepima lami katika miradi ya ukarabati wa barabara Bariadi – Slama A, Lamadi – Wigelekelo na Bariadi – Kisesa pamoja na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Arusha; na
imetekeleza miradi midogo kama vile usanifu na ufungaji wa taa za kuongozea magari barabarani, upimaji wa udongo kwa makampuni ya ujenzi na ujenzi wa nyumba za watu binafsi kwa wananchi wa kawaida katika Mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Chuo cha Ufundi Arusha imeendelea kuboresha miundombinu kwa kutekeleza kazi zifuatazo:
imejenga jengo la ghorofa tatu (3) kwa ajili ya madarasa, maabara na ofisi za walimu ambapo kukamilika kwa ujenzi huo kutaongeza udahili na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia;
imejenga tenki la kuhifadhia maji safi lenye uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo 1,125,000 ambalo litapunguza changamoto ya upatikanaji wa maji safi kwa wanafunzi;
imenunua vifaa vya kufundishia mazoezi kwa vitendo katika idara nane (8) za kitaaluma ili kujenga weledi kwa wanafunzi wa fani za ufundi na uhandisi ambazo zinahitaji zaidi mazoezi kwa vitendo; na
imefanya usanifu na uandaaji wa michoro na makadirio, upimaji wa udongo (geotechnical investigations) kwa ajili ya ujenzi wa kliniki ya kisasa ya kutolea huduma za afya. Kliniki hiyo itahudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa maeneo ya jirani.

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imetekeleza kazi zifuatazo:-

imeongeza udahili wa wanafunzi ambapo hadi mwezi Machi, 2021 jumla ya waliodahiliwa ni 11,790 kati ya lengo la wanafunzi 9,389 kwa mwaka 2020/21. Ongezeko la wanafunzi 2,401 limechangiwa na kuboreshwa kwa mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kufunguliwa kwa Tawi jipya la Pemba na kuanzishwa kwa programu mpya ya shahada ya uzamili katika masomo ya Utawala na Rasilimaliwatu;
imefanya tafiti 17 katika masuala ya Maendeleo ya Uchumi, Jamii, Jinsia, Elimu na Maadili ambazo zimechapishwa katika majarida mbalimbali ya kitaaluma ya ndani na nje ya nchi;
imegharamia mafunzo ya shahada ya uzamivu kwa watumishi 24 ili kuongeza umahiri wa Wahadhiri Waandamizi;
imeanza taratibu za ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Kampasi ya Karume Zanzibar ambapo Mshauri Elekezi na Mkandarasi wamepatikana kwa ajili ya ujenzi wa mradi;
imehuisha mitaala 29 ya chuo ili iendane na mahitaji ya soko na mingine ipo katika hatua za mapitio kwa ajili ya kupatiwa ithibati; na
imetoa mafunzo kwa wakutubi watatu (3) kuhusu kuingiza taarifa (vitabu na majarida) katika mfumo wa kielektroniki (KOHA) uliopo maktaba za Kampasi ya Kivukoni, Karume na Pemba.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)​

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili jumla ya wanafunzi 357,850 (Wanawake: 145,251 Wanaume: 212,599) sawa na asilimia 97 ya lengo la mwaka wa masomo 2020/21 la kudahili wanafunzi 370,000 ikiwa ni pamoja na wanafunzi 807 wenye ulemavu na wanafunzi 1,368 kutoka katika mazingira magumu;

imefanya maandalizi ya kuanzisha Kituo cha Uchapaji katika Chuo cha
Mafunzo ya Ufundi Stadi Chang’ombe - Dar es Salaam;

imekamilisha andiko la mfumo wa kuwezesha kutoa taarifa za soko la ajira kupitia mtandao; na
imetekeleza mpango wa kukuza ujuzi viwandani katika viwanda vidogo 26 vya kusindika mbegu za alizeti katika Manispaa ya Singida chini ya uratibu wa Jumuiya ya SIMUSOPA. Mpango huo unatarajiwa kuwanufaisha wananchi 100 wanaojishughulisha na usindikaji wa mbegu za Alizeti katika Manispaa ya Singida.


Mheshimiwa Spika, katika kutoa mafunzo kazini na kuwajengea uwezo watumishi pamoja na kukuza ujuzi nchini, Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, imetekeleza yafuatayo:
imewezesha masomo ya muda mrefu kwa watumishi 51 ili kuongeza ufanisi wa kazi;
imetoa mafunzo ya Elimu Masafa (ODL) kwa wakufunzi 25 na walimu 60 kutoka vyuo vya Ufundi Stadi na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi ikiwa ni majaribio ya awali ya mafunzo ya ualimu kwa njia ya Elimu Masafa;

imetoa mafunzo kwa wajasiriamali 282 wa Sekta Isiyo Rasmi kupitia programu ya Intergrated Training for Enterpreneurship Promotion (INTEP) kwa lengo la kuboresha uwezo wao wa kuendesha shughuli za uzalishaji na kuboresha hali zao kiuchumi; na
imeendelea kuelimisha umma kuhusu shughuli za Mamlaka kupitia vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo kipindi cha Ujuzi ni Maisha kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) pamoja na makala mbalimbali kupitia redio na mitandao ya kijamii, programu za kuhabarisha jamii, ushiriki katika maonesho na kufanikisha

mawasiliano ya kidigitali.


Mheshimiwa Spika, ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Ufundi Stadi, Serikali imeendelea na ujenzi wa chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha mkoa wa Kagera. Aidha, Serikali imekamilisha ujenzi wa karakana nne (4) katika maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
karakana ya kisasa ya zana za kilimo (modern agro-mechanics workshop) katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Arusha (Oljoro);
karakana ya teknolojia ya ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo katika Mkoa wa Lindi;
karakana ya ufundi wa majokofu na viyoyozi, ufundi bomba, uchomeleaji na vyuma, na uashi katika Chuo cha VETA cha Mkoa wa Lindi; na
karakana ya matengenezo ya breki za magari (side slip and brake tester) katika Chuo cha VETA cha Mkoa wa Lindi.


Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW)​

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ili kuhakikisha kuwa vijana na watu wazima wengi wanapata stadi, ujuzi na maarifa stahiki. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imetekeleza yafuatayo:
imedahili jumla ya wanafunzi wapya 4,766 (Astashahada 165, Stashahada 4,510 na Shahada 91) kwa mwaka wa masomo 2020/21;
imesajili jumla ya wanafunzi 9,939 wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Shule yaani Integrated Programme for Out of School Adolescents (IPOSA) kwa ajili ya kuanza mafunzo na wanafunzi 3,440 wamesajiliwa ili kuwawezesha kufanya mitihani ya hatua ya I na II katika vituo vya mradi wa IPOSA;

imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma yaani National Adult Literacy and Mass Education Rolling Strategy (NALMERS) ambao ulizinduliwa Septemba, 2020; na umetafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili; na
imekusanya takwimu za hali ya kisomo kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara ikiwa ni hatua ya mwanzo ya utafiti wa hali ya kisomo na elimu kwa umma nchini.


Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza elimu ya watu wazima nchini, Serikali kupitia Taasisi imetekeleza kazi zifuatazo:
imetoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi ambapo jumla ya vijana na watu wazima 13,050 (Wanawake: 7,050 na Wanaume: 6,000) wamepatiwa elimu hiyo;
imetoa mafunzo ya ualimu na usimamizi wa elimu ya watu wazima kwa vijana na watu wazima 6,607 kupitia utoaji wa programu za elimu masafa mikoani na kuendesha programu 13 katika kampasi za Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza;
imewezesha programu sita (6) za elimu masafa katika vituo mbalimbali ambapo uwezeshaji wa ana kwa ana ulifanyika katika vituo 50 vya utoaji wa elimu kwa njia huria na masafa nchini; na
imetekeleza programu na miradi mbalimbali ya elimu ya watu wazima, ikiwemo mradi wa kuwawezesha wasichana kwa njia ya elimu, mradi wa sekondari kwa wasichana na Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Shule (IPOSA) kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.


Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imeanza kutumia mitaala mipya kwa mwaka wa masomo 2020/2021 iliyopitiwa na kuidhinishwa na NACTE ambapo mitaala hiyo ni: Elimu ya

Watu Wazima na Maendeleo ya Jamii (Adult Education and Community Development NTA level 4 - 8); na Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu (Adult and Continuing Education NTA level 4 - 8). Aidha, maboresho ya mitaala mingine ya Usimamizi wa Elimu Masafa (Management of Distance Education NTA level 7 - 8 ODL) na Stashahada ya Elimu Masafa (Ordinary Diploma in Distance Education NTA level 4, 5 and 6 ODL) yapo katika hatua ya kuidhinishwa.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi inayotolewa inakidhi vigezo vya kuwezesha wahitimu kuendana na mahitaji ya soko la ajira, Serikali kupitia Taasisi ya Watu Wazima imetekeleza kazi zifuatazo:
imefanya ufuatiliaji wa mradi wa utoaji elimu ya sekondari kwa wasichana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu yaani Secondary Education for Out of School Adolescent Girls (SEOSAG) unaoendeshwa kwa kushirikiana na shirika la BRAC Maendeleo katika mkoa wa Tanga katika vituo 35 vya wilaya mbili (Tanga Mjini vituo 23 na Korogwe vituo 12);
imetathmini maendeleo ya wanafunzi 98 waliohitimu Mafunzo ya Kuongeza Thamani ya Mazao ya Samaki, na wanaendelea na mafunzo kwa vitendo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (Skills Development Fund – SDF) kwa lengo la kubaini manufaa yanayotokana na mradi huo;

imehakiki vituo 151 vinavyomilikiwa na TEWW na vituo vipya 82 vinavyotarajiwa kutekeleza Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa Njia Mbadala (Alternative Education Pathway - AEP);
imefanya tathmini ya utolewaji wa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi katika mikoa mitano (5) ambayo ni: Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Mwanza na Iringa; na

imefanya ufuatiliaji wa wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi kwa kuandaa na kusimamia mtihani wa Utimilifu kwa wanafunzi 5,383.


Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imeboresha huduma za maktaba kwa kuongeza nakala za vitabu 1,140 pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji huduma ya maktaba kwa njia ya Kidigitali.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili wanafunzi 142 katika programu za masomo ya Ualimu wa Ufundi (Shahada ya Ualimu wa Ufundi 134, Stashahada ya Ualimu wa Ufundi 7 na Stashahada ya Uzamili ya Ualimu wa Ufundi 1);

imesajili wanafunzi 6,817 ambapo ngazi ya Astashahada 87, Stashahada 3,228, Shahada 3,468, Stashahada ya Uzamili 1, Shahada ya Umahiri 26, na wanafunzi 7 katika Shahada za Uzamivu;

inaendelea na ubunifu na utafiti wa kutengeneza kitanda cha kuinulia wagonjwa hospitalini;

imeshiriki maonesho na mashindano ya MAKISATU ambapo tafiti nne
(4) zilifanya vizuri na kuwezesha chuo kupata ufadhili wa Shilingi 69,000,000 zitakazotumika kuendeleza tafiti hizo;

imeshirikiana na MATI Uyole, Hanze University of Applied Science (Netherlands) na kufanikiwa kupata mradi wenye thamani ya Euro 398,052.65 unaolenga kufanya tafiti katika kilimo cha kisasa cha viazi ambacho kitaleta tija katika uzalishaji na kutengeneza ajira; na

imekamilisha ujenzi wa maktaba kwa awamu ya kwanza. Aidha, inaendelea na ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 ambapo kukamilika kwa hosteli hiyo kutatatua changamoto ya uhaba wa malazi chuoni.


Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha ujenzi wa maktaba kwa awamu ya kwanza na kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi ambapo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja. Aidha, inaendelea na ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 ambapo ujenzi umekamilika kwa asilimia 40. Kukamilika kwa hosteli hiyo kutatatua changamoto ya uhaba wa malazi chuoni. Vilevile, imeendelea na ukarabati wa karakana na mabweni katika Kampasi ya chuo Rukwa.

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam imetekeleza kazi zifuatazo:
imedahili jumla ya wanafunzi 6,219 wakiwemo Stashahada 3,533 (Wanawake: 1,005 Wanaume: 2,528), Shahada ya Awali 2,622 (Wanawake: 457 Wanaume: 2,165) na Shahada ya Umahiri 64 (Wanawake: 9 Wanaume: 55);

imekamilisha utafiti wa mfumo wa kielektroniki wa malipo na usimamizi wa hospitali “Electronic Hospital Management System’” na kuusimika katika Hospitali ya Amana; na

imepitia mitaala 15 katika ngazi za Stashahada, Shahada ya Awali na Shahada ya Umahiri. Katika fani mbalimbali ambazo ni pamoja na TEHAMA, uhandisi mitambo, uhandisi ujenzi, uhandisi umeme, uhandisi vifaatiba, uhandisi teknolojia ya nishati jadidifu, teknolojia ya sayansi ya usindikaji wa chakula, sayansi na Teknolojia ya

maabara.


Mheshimiwa Spika katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, Serikali kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam inaendelea na taratibu za kumpata Mshauri Elekezi kwa ajili ya kusanifu mabweni mawili
(2) yenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 500 na jengo la kituo cha umahiri wa TEHAMA katika kampasi ya Dar es Salaam. Aidha, inaendelea na taratibu za kumpata Mshauri Elekezi kwa ajili ya kusanifu mabweni mawili
(2) yenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 600 na jengo la kituo cha umahiri wa teknolojia ya utengezaji wa bidhaa za ngozi katika Kampasi ya Mwanza.

Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza teknolojia na ubunifu nchini, Serikali kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam imeendelea kukamilisha utafiti wa teknolojia kama ifuatavyo:
imesanifu modal ya mfumo wa mawasiliano yasiyotumia nyaya katika magari yasiyo na dereva na kwa sasa taasisi ipo katika hatua ya utengenezaji wa “Prototype”;
imeanza kusanifu modal mbalimbali kwa ajili ya kufanya majaribio ya mifumo itakayosaidia katika uchakataji wa kahawa;
imeunda injini ya kutumia mafuta ya petroli na kwa sasa maboresho yanafanyika kwa ajili ya kuongeza mfumo wa kutumia gesi asilia;
imeanzisha kituo cha atamizi ya teknolojia ili kuwajengea uwezo wahandisi na wanasayansi wa kutatua matatizo mbalimbali ya vifaa tiba. Kwa sasa kituo kinahudumia washiriki zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi;
imefanya utafiti wa utengenezaji wa teknolojia za bei nafuu za kupimia hali ya hewa;
imeboresha mfumo wa kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa wakulima kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (FARMSMS). Mfumo huu

una lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na utabiri wa siku 10, utabiri wa msimu na taarifa za hali ya majanga; na
imeendelea kutekeleza mradi wa tiba mtandao (telemedicine) wenye lengo la kufikisha huduma za afya kwa urahisi kwa wananchi. Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro zimeunganishwa katika mfumo huo.


Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia imetoa mafunzo ya mfumo wa kuhifadhi, kusambaza, kuchakata na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za bioanwai hapa nchini kwa wafanyakazi wa baadhi ya taasisi zinazohusika na masuala ya bioanwai zikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na Makumbusho ya Taifa. Aidha, imeanza ukusanyaji wa taarifa za awali za bioanwai kwa taasisi za Elimu ya Juu na taasisi za utafiti zinazohusika na maswala ya bioanwai zinaendelea kukusanywa.

Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela (NM-AIST)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela imetekeleza yafuatayo:
imedahili wanafunzi wapya 120 (Uzamili 92, Uzamivu 28) na hivyo kufikisha jumla ya wanafunzi 591 ambapo Umahiri ni 212 (Wanawake: 59 Wanaume: 153) na uzamivu ni 379 (Wanawake 132: Wanaume 247);

imezalisha bunifu mbili (2) za Mfumo wa Kurahisisha Uratibu wa Usafiri na Ugunduzi wa Jiko la Gesi Asilia;

inaendelea na tafiti 21 ambapo hadi kufikia kipindi cha nusu mwaka kiasi cha Shilingi 3,280,800,293.11 kilikuwa kimepokelewa kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa ni sawa na 126% ya lengo la shilingi 3,025,000,000. Fedha hizo ni kwa ajili ya kulipia ufadhili wa wanafunzi na gharama za utafiti kwa wanafunzi na wanataaluma; na

imeongeza wadau wa kimataifa kutoka 36 hadi 38, Afrika Mashariki kutoka 37 hadi 39 na wadau wa ndani wameongezeka kutoka 21 hadi 23.


Mheshimiwa Spika, ili kukuza ushirikiano katika ufanyaji wa tafiti zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali, Serikali kupitia Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela imeongeza wadau wa kimataifa kutoka 36 hadi 38, Afrika Mashariki kutoka 37 hadi 39 na wadau wa ndani wameongezeka kutoka 21 hadi 23.

Tathmini ya Utoaji wa Elimu na Mafunzo​

Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha elimu yetu inaendana na mahitaji ya mipango ya nchi pamoja na soko la ajira la ndani, kikanda na kimataifa, Serikali imeendelea kuziwezesha taasisi zetu zenye majukumu ya kutathmini ubora na utoaji wa elimu kama ifuatavyo:

Baraza la Mitihani la Tanzania - NECTA​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania imetekeleza kazi zifuatazo:
imeendesha Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2020 kwa watahiniwa 1,008,307;
imeendesha Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA) 2020 kwa watahiniwa 1,704,404;

imeendesha Upimaji wa Kidato cha Pili (FTNA) 2020 kwa watahiniwa 601,948;
imeendesha Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2020 kwa watahiniwa 475,981 wa Kidato cha Nne (CSEE) 2020 na watahiniwa 8,056 wa Maarifa (QT) 2020;
imesajili watahiniwa wa Kidato cha Sita 90,280 wanaotarajiwa kufanya Mitihani kuanzia tarehe 3 hadi 22 Mei, 2021;
imesajili watahiniwa 6,742 wa Mitihani ya Ualimu wanaotarajiwa kufanya mitihani kuanzia tarehe 3 hadi 22 Mei, 2021; na
imeendelea kufanya maandalizi ya zana za upimaji wa Kusoma, Kuandika na kuhesabu – KKK unaotarajiwa kufanyika 2021.


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)​

Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa elimu itolewayo inawawezesha wahitimu kukidhi vigezo vya mahitaji ya soko la ajira Kitaifa, Kikanda na Kimataifa, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021, Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu imeendelea kutekeleza yafuatayo:
imekagua Vyuo Vikuu 19 kwa lengo la kuhakiki ubora wake ikiwa ni sawa na asilimia 76 ya lengo la kukagua vyuo 25 kwa mwaka; na

imepokea na kuhakiki maombi manne (4) ya uanzishwaji wa vyuo vikuu vipya na maombi mengine manne (4) ya utoaji na uhuishaji wa ithibati kwa vyuo vilivyopo (Accreditation and Re-accreditation). Matokeo ya uhakiki wa maombi ya uanzishwaji wa vyuo vipya yamebainisha kuwa kati ya vyuo vinne (4) vilivyoomba kuanzishwa, chuo kimoja kimekidhi vigezo na hivyo kupewa ithibati. Vyuo ambavyo havikukidhi vigezo vilipewa ushauri na maelekezo ya kuzingatia ili kutimiza masharti na vigezo vya uanzishaji wa chuo kikuu hapa nchini. Aidha, vyuo vilivyoomba kupewa ithibati au

kuhuisha ithibati vyote vilikidhi vigezo na hivyo kupewa ithibati na/au kuhuishwa ithibati zao.


Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa mitaala inayotolewa na Vyuo Vikuu nchini inakidhi vigezo na kuendana na mahitaji ya soko la ajira, Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imefanya tathmini na kutoa ithibati ya Mitaala 153 iliyowasilishwa na Vyuo Vikuu nchini ikiwa ni sawa na asilimia
76.5 ya lengo la kutathmini mitaala 200 kwa mwaka.


Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaodahiliwa wanakidhi vigezo vya udahili na wanadahiliwa katika vyuo na programu zinazotambulika, katika mwaka wa masomo 2020/21 Serikali kupitia Tume imeendelea kuratibu udahili wa wanafunzi wanojiunga na Elimu ya Juu nchini kwa ngazi ya Shahada ya Awali kwa kufanya yafuatayo:
imeratibu maombi 101,354 ya wanafunzi walioomba kujiunga na Elimu ya Juu kwa ngazi ya Shahada ya Awali katika vyuo 74 nchini kwa mwaka wa masomo 2020/21. Kati ya maombi hayo, jumla ya waombaji 87,371 wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali nchini kati ya wadahiliwa hao wanawake ni 37,748 (43.2%) na wanaume ni 49,623 (56.8%);
imeandaa Mwongozo wa Udahili kwa mwaka wa masomo 2020/21 kwa ngazi ya Shahada ya Awali na kusambaza nakala laini katika tovuti ya Tume na mitandao ya kijamii.

Vilevile, nakala ngumu 800 zilisambazwa kwa wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanafunzi na wananchi wanapata taarifa ya vyuo vinavyotambulika na vigezo vya udahili ili kuwawezesha kutuma maombi yao kwa usahihi; na
imeratibu programu mbalimbali za kuwajengea uelewa wanaotaka kujiunga na Elimu ya Juu nchini kupitia vyombo vya habari ikiwemo Tovuti ya Tume na machapisho. Vilevile, Tume ilishiriki katika juma la

Elimu ya Juu Zanzibar ambapo iliweza kutoa elimu kuhusu Elimu ya Juu kwa wanafunzi na wananchi. Aidha, kupitia kambi 17 za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), elimu kuhusu udahili ilitolewa kwa vijana 20,500 ambao ni wahitimu wa Kidato cha Sita.

Mheshimiwa Spika, katika kutambua sifa za kitaaluma za wahitimu wa Elimu ya Juu iliyotolewa na vyuo vya nje ya nchi, Serikali kupitia Tume imetathmini na kutambua tuzo 4,311 kati ya 5,179 zilizowasilishwa kwa utambuzi na wahitimu waliotunukiwa na Vyuo Vikuu vya nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imeendelea kuboresha mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini pamoja na wadau wengine na kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wakati kwa ajili ya maamuzi ya kisera, mipango na kiutendaji. Aidha, imeendelea kufanya maboresho ya mifumo mitatu (3) ya kielektroniki ambayo ni: Programme Management System (PMS); University Information Management System (UIMS); na Foreign Award Assessment System (FAAS). Mifumo hiyo inatumika katika ithibati za mitaala, ukusanyaji wa taarifa na uratibu wa udahili pamoja na uchakataji wa tuzo za nje kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi.

Mheshimiwa Spika, ili kujenga uelewa kwa jamii kuhusu kazi zinazotekelezwa na Taasisi za Elimu ya Juu, Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imetekeleza yafuatayo:
imeratibu utoaji wa mafunzo na semina za kubadilishana uzoefu kwa Maafisa Uthibiti Ubora, Maafisa Udahili, Maafisa TEHAMA, Wasimamizi wa kanzidata, Wahadhiri na Viongozi wa Vyuo vya Elimu ya Juu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi. Jumla ya washiriki 218 wa Vyuo vya Elimu ya Juu walinufaika na mafunzo hayo;

imeendelea kuratibu semina na makongamano ya kubadilishana ujuzi na uzoefu kwa Wanataaluma na Viongozi wa Vyuo Vikuu kuhusu masuala ya ubora wa Elimu ya Juu, uandaaji wa mitaala inayokidhi na kuzingatia mahitaji ya soko la ajira, uongozi na uendeshaji wa vyuo vikuu. Jumla ya Viongozi 312 wa Vyuo Vikuu wamenufaika na mafunzo hayo;
imeandaa maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambapo taasisi 67 za ndani ya nchi zilishiriki na zaidi ya wananchi 60,000 wakiwemo wanafunzi walihudhuria maonesho hayo na kupata uelewa wa huduma zinazotolewa na taasisi za Elimu ya Juu;
imeshiriki makongamano na mikutano inayohusu uimarishaji na Uthibiti wa Ubora wa Elimu ya Juu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kimataifa kwa lengo la kuongeza ujuzi na weledi katika kuthibiti ubora wa Elimu ya Juu nchini; na
imeandaa mkutano na kufanya majadiliano na wamiliki wa Vyuo Vikuu vinavyomilikiwa na taasisi binafsi kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja kuhusiana na taratibu, miongozo na kanuni za uendeshaji wa Vyuo Vikuu pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo na namna ya kukabiliana nazo. Jumla ya washikiri 32 kutoka vyuo binafsi 18 walihudhuria.

Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa kuna wataalamu wa kutosha wa kuhakiki Mitaala na kufanya ukaguzi wa ubora wa Vyuo Vikuu hapa nchini, Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imeandaa kanzidata ya Wataalamu wa Kuhakiki Mitaala (Curricula Peer Reviewers) kutoka katika programu mbalimbali za masomo na Wakaguzi wa Vyuo Vikuu (Institutional Audit Experts) kutoka katika vyuo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kurahisisha na kuongeza kasi ya utoaji wa ithibati ya Mitaala na Vyuo. Aidha, imetoa mafunzo kwa Wataalamu wa Kuhakiki Mitaala na Wakaguzi wa Vyuo ili kuwajengea uwezo na umahiri wa kutekeleza majukumu yao. Jumla ya

Wanataaluma 134 kutoka Vyuo Vikuu vya umma na binafsi wamenufaika na mafunzo haya.

Mheshimiwa Spika, ili kulinda haki na maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla, Watanzania wanaokwenda kusoma nje ya nchi kupitia kwa Mawakala, Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imeendelea kukagua Asasi/Kampuni zinazojishughulisha na uratibu wa wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi kwa lengo la kuzitambua na kuzisajili. Kwa mwaka 2020/21, Serikali imepokea na kutathmini maombi ya taasisi tano (5) za mawakala wanaotaka kupata leseni ya kuwatafutia wanafunzi Vyuo Vikuu nje ya nchi. Lengo ni kuhakikisha watanzania wanaokwenda nje ya nchi wanasoma katika vyuo vinavyotambulika kitaifa na kimataifa. Taasisi hizo ni: Tebeth Mentors and Information Centre; Sangeni International; Edukwanza Consultancy Ltd; Sultan Academics; na Cognita Consultancy Ltd.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)​

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi wa Elimu ya Ufundi katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi imetekeleza yafuatayo:
imehakiki udahili wa wanafunzi 157,420, (Wanawake 75,194: Wanaume: 82,226) katika ngazi ya Astashahada ya Awali, Astashahada na Stashahada;
imesajili vyuo 22 katika bodi za masomo zifuatazo: Afya na Sayansi Shirikishi 11; Biashara, Utalii na Mipango 6; na Sayansi na Teknolojia Shirikishi 5. Usajili huo umewezesha udhibiti wa uanzishwaji na uendeshaji wa mafunzo kiholela;
imetoa ithibati kwa vyuo 26 katika bodi za masomo zifuatazo: Afya na Sayansi Shirikishi 10; Biashara, Utalii na Mipango 8; na Sayansi na Teknolojia Shirikishi 8. Utoaji wa ithibati umesaidia vyuo kukua na

kukidhi viwango vya utoaji wa elimu bora;

imeidhinisha uanzishwaji na utambuzi wa programu 20 katika vyuo kwa mchanganuo ufuatao: Afya na Sayansi Shirikishi 8; Biashara, Utalii na Mipango 6; na programu za Sayansi na Teknolojia Shirikishi 6;
imetoa mafunzo ya namna ya upimaji na ufundishaji wa mitaala inayozingatia umahiri (CBET) kwa wakufunzi 806 wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi. Mafunzo hayo yatasaidia wahitimu kuwa mahiri katika ujuzi uliokusudiwa; na
imefanya ufuatiliaji na tathmini ya ubora wa elimu katika vyuo 138 vya elimu ya ufundi sawa na asilimia 69 ya lengo. Katika ukaguzi huo vyuo ambavyo havikukidhi vigezo vilichukuliwa hatua stahiki ambapo vyuo vitano (5) vilifutiwa usajili na vyuo 13 vilisimamishwa kudahili wanafunzi ili kuvipa nafasi ya kurekebisha upungufu uliobainika. Vyuo vyote vilipatiwa ushauri wa kuboresha utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo.


Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa na kuhakikisha inawawezesha wahitimu kujiajiri na kuajiriwa, Serikali kupitia Baraza imetekeleza kazi zifuatazo:
imetoa namba ya uhakiki wa tuzo (AVN) 17,234 ambazo zimewezesha kuepuka udanganyifu wa wahitimu wanaoendelea na Elimu ya Juu;
imefanya ulinganifu wa Tuzo 1,028 ili kuthibiti viwango vya Elimu ya Ufundi nchini; na
imehakiki Mitaala 118 iliyoandaliwa na Vyuo vya Ufundi ili kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanakidhi mahitaji ya soko la ajira.


Mheshimiwa Spika, ili kusogeza huduma kwa wananchi, Serikali kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi imenunua kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa

ofisi katika kanda ya Magharibi (Tabora) na hivyo Baraza kuwa na jumla ya viwanja sita (6) katika Mikoa ya Dodoma, Arusha, Tabora, Mtwara, Mwanza na Mbeya.

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)​

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania imeendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kutekeleza yafuatayo:
imeandaa vitabu vya kiada kwa masomo nane (8) vya Darasa la VII pamoja na viongozi vya mwalimu ili kuwezesha uwepo wa vitabu vinavyoendana na mtaala ulioboreshwa;
imeandaa vitabu vya masomo 14 vya maandishi yaliyokuzwa kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu wa Darasa la VI na VII kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanapata elimu sawa na wanafunzi wengine;
imeandaa vitabu vya masomo 14 vya maandishi ya Breli kwa ajili ya wanafunzi wasioona wa Darasa la VI na VII kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanapata elimu sawa na wanafunzi wengine;
imetafsiri vitabu vya kiada vya masomo matano (5) vya Darasa la VII pamoja na Viongozi vya Mwalimu kwa ajili ya matumizi ya shule zinazotumia Lugha ya Kiingereza;
imeandaa maudhui ya aina 31 ya Vitabu vya Kiada Ngazi ya Sekondari Kidato cha I hadi cha IV ili kukidhi mahitaji ya mtaala na kuwezesha uwepo wa vitabu hivyo;
imeandaa mitaala minne (4) na mihtasari 36 ya Elimu ya Ualimu ngazi ya Stashahada ili kukidhi mahitaji ya sasa; na
imeandaa moduli ya Kielektroniki (Cartoon Based Lessons) kwa Ngazi ya Elimu ya Awali ili kumuwezesha mtoto kujenga umahiri muhimu utakaomsaidia kujifunza na kujitawala.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuhakikisha vitabu vinapatikana shuleni ambapo katika mwaka wa fedha 2020/21 imechapa na kusambaza vitabu na miongozo mbalimbali ikiwemo:
nakala 4,443,586 za vitabu vya kiada kwa wanafunzi na nakala 253,408 za Kiongozi cha Mwalimu Darasa la VII katika Halmashauri zote nchini;
nakala 322,000 za vitabu vya Kiada Darasa la VI, nakala 154,000 na nakala 560 za vitabu na Kiongozi cha Mwalimu Darasa la VII kwa shule zinazotumia Lugha ya Kiingereza kufundishia katika Halmashauri zote nchini;
nakala 43,671 na 305,697 za mtaala wa Darasa la I - VII na mihtasari ya Darasa la III - VII kwa shule zinazotumia Lugha ya Kiswahili na Kiingereza kufundishia na kujifunzia katika Halmashauri zote nchini;
nakala 2,000 za Mwongozo wa Utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Sekondari Kidato cha I - IV kwa Wanafunzi Viziwi na wenye Bakaa ya Usikivu Tanzania Bara na Visiwani; na
nakala 4,100 za vitabu vya kiada vya Breli vya sekondari vya Wanafunzi Wasiona Tanzania Bara na Visiwani.


Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania imeandaa mwongozo wa utekelezaji wa mtaala wa elimu ya Sekondari kwa Wanafunzi Viziwi Kidato cha I - IV ili kusaidia ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi viziwi na kuinua kiwango cha ufaulu. Aidha, imeandaa Kamusi ya Kidigitali ya Lugha ya Alama Tanzania (LAT) kwa ajili ya kuboresha ufundishaji wa wanafunzi viziwi nchini.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuwajengea uwezo watumishi kazini ambapo katika mwaka wa fedha 2020/21 imetekeleza yafuatayo:
imetoa mafunzo kwa walimu 72 wa shule 26 zenye wanafunzi viziwi nchini ili kuwawezesha kutumia Kamusi ya Lugha ya Alama ya

Tanzania na mwongozo wa utekelezaji wa mtaala wa elimu ya sekondari Kidato cha I - IV; na
imetoa mafunzo kazini kwa washiriki 5,598 (Wakufunzi 1,206 kutoka Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali; Walimu 3,957 kutoka Shule za Msingi na Sekondari za Serikali na zisizo za Serikali; Maafisa Elimu Kata 226; Wathibiti Ubora 48; Walimu wa Elimu ya Awali 105; Maafisa Elimu Sekondari na Msingi 56). Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha watekelezaji wa mtaala kutekeleza mtaala kwa usahihi.

Mheshimiwa Spika, katika kushughulikia agizo la Hayati John Pombe Joseph Magufu, Rais wa Awamu ta Tano, kuhusu kufundishwa kwa somo la Historia ya Tanzania kwa wanafunzi wote, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania imetekeleza yafuatayo:
imekamilisha uandaaji wa mihtasari ya Somo la Historia ya Tanzania kuanzia Ngazi ya Elimu ya Awali hadi Sekondari (Kidato cha I - VI; na
inaendelea na uandaaji wa Vitabu vya Kiada 14 vya Somo la Historia ya Tanzania kuanzia Ngazi ya Elimu ya Awali hadi Sekondari Kidato cha VI. Aidha, inaendelea na maandalizi ya mafunzo kwa walimu kwa lengo la kuwezesha kufundisha somo hilo.


Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)​

Mheshimiwa Spika, ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania katika mwaka wa fedha 2020/21, imetekeleza kazi zifuatazo:
imewezesha ujenzi wa madarasa 180 (madarasa 3 kwa kila shule) katika shule 45 za msingi na 15 za sekondari ambapo ujenzi unaendelea kwa kutumia utaratibu wa Force Account;
imewezesha ujenzi wa nyumba 100 za walimu katika shule 15 za

sekondari na 10 za msingi zilizopo katika maeneo yenye mazingira magumu kwa lengo la kuimarisha makazi ya walimu na kuongeza ufanisi;
imewezesha ujenzi wa matundu ya vyoo 360 katika shule tisa (9) za msingi na sita (6) sekondari zenye upungufu ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia;
imeboresha miundombinu kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu katika shule za msingi nane (8);
imeboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika Chuo cha Karume cha Sayansi na Teknolojia kilichopo Zanzibar; na
inaendelea kuwezesha ujenzi wa mabweni 15 katika shule 15 za sekondari zenye mazingira magumu.

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)​

Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi kazini, Serikali kupitia Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu katika mwaka wa fedha 2020/21 imetekeleza kazi zifuatazo:
imetoa mafunzo ya Astashahada, Stashahada katika Uongozi na Usimamizi wa Elimu (DEMA) pamoja na Stashahada ya Uthibiti Ubora wa Shule kwa walimu 1,985 kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa elimu ngazi ya Shule, Kata, Halmashauri na Mkoa;
imetoa mafunzo ya Uthibiti Ubora wa Shule wa Ndani kwa Maafisa Elimu Taaluma Msingi 184, Wathibiti Ubora wa Shule wa Wilaya 183 na Wakuu wa Shule za Msingi 8,800 kutoka Halmashauri zote za Tanzania Bara;
imetoa mafunzo ya muda mfupi ya Uandaaji wa Mpango Mkakati, Masuala ya Manunuzi na Fedha, Uongozi na Usimamizi wa Elimu kwa Timu za Menejimenti ya Vyuo vya Ualimu ambapo wajumbe 315 walishiriki;

inagharamia watumishi watano (5) katika Shahada ya Uzamivu; na

imefanya ufuatiliaji kwa Wakuu wa Shule za Sekondari na wadau mbalimbali waliopewa mafunzo na ADEM hususan wahitimu wa Programu ya DEMA kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ilikubaini hali ya utendaji kazi wao. Tathmini ya ufuatiliaji inaendelea.


Mheshimiwa Spika, ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, Serikali kupitia Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu imekarabati nyumba tatu (3) za watumishi katika Kampasi ya Bagamoyo zenye uwezo wa kuchukua familia sita (6). Aidha, imewezesha upatikanaji wa hati ya kiwanja na kukamilisha michoro ya Mpango Kabambe wa Matumizi ya Ardhi (Master Plan) ya eneo itakapojengwa Kampasi ya Mbeya.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetekeleza kazi zifuatazo:
imetoa mikopo kwa wanafunzi 149,398 (Wanafunzi wa mwaka wa kwanza 55,337 na wanaoendelea na masomo 94,061);
imekusanya kiasi cha Shilingi 139,244,569,882.91 hadi kufikia Machi, 2021 ikiwa ni asilimia 72 ya lengo la kukusanya Shilingi 194,100,000,000 ya mikopo iliyoiva;
imebainisha wanufaika wapya 14,807 na kupewa ankara zao ili kurejesha mkopo. Aidha, ukaguzi umefanyika kwa waajiri 3,979 na taarifa za mkopo zimehuishwa kwa wanufaika 321,629 kupitia kwa waajiri wao;
imefanya mapitio ya makato na tozo za mikopo ya elimu ya juu ambazo zimekuwa zikitumika kwa takribani miaka 10 ili maoni ya wadau mbalimbali yenye tija ikiwemo kutunza thamani ya fedha za mikopo, kujenga uhimilivu wa mfuko wa mikopo ya wanafunzi na kuzingatia mwenendo wa viwango vya mfumuko wa bei vya sasa; na

imefanya maboresho ya mfumo wa kusimamia mikopo (Intergrated Loan Management System - iLMS) kwa kufanya yafuatayo:
kuanzisha mfumo rahisi wa kidigitali wa urejeshaji mikopo (Loanee Individual Permanent Account – LIPA) ambao unamuwezesha mnufaika au mwajiri kupata taarifa za deni na utaratibu wa kulipa kutoka popote alipo kupitia tovuti (www.heslb.go.tz);
kuimarisha uhakiki wa maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi waliodhaminiwa katika masomo ya sekondari au stashahada ili kuepuka udanganyifu; na
kuimarisha mfumo wa kidigitali wa haraka wa malipo ya fedha kwa wanafunzi (Digital Disbursement System - DiDis) kwa kufikisha huduma hiyo kwa asilimia 91 ya wanufaika wote 148,012. Kupitia mfumo huu, mwanafunzi aliyesajiliwa anaweza kupokea fedha ndani ya dakika tano (5) baada ya kusaini kwa njia ya biometriki.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, imeendelea kuendesha programu za elimu kwa waajiri, wanufaika na wanafunzi kuhusu uombaji sahihi wa mikopo na umuhimu wa urejeshaji wa mikopo kwa wakati kama ifuatavyo:
imeendesha programu 15 kuhusu wajibu wa wanafunzi wanufaika kwa jumla ya wanafunzi 5,250 na viongozi wao waliopo katika taasisi za UDSM, UDOM, SAUT - Mwanza, DUCE, SUA, MU, MUST, CUCoM, TIA -MBEYA, CBE - MBEYA, TEKU, ISW, KCMC, MWUCE, na DMI;
imeendesha programu za elimu ya uombaji sahihi wa mikopo kwa wahitimu wa kidato cha sita katika mikoa 14 ya Tanzania Bara na Zanzibar ambapo wanafunzi 9,898 walifikiwa;
imeendesha programu za elimu ya uombaji sahihi wa mikopo kwa wanafunzi 22,681 waliokuwa wakipewa mafunzo katika kambi 18 za

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT);

imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika ujazaji fomu za maombi ya mikopo watoa huduma za intaneti 33 katika vituo mkakati vya huduma za intaneti katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza;
imeendesha programu za elimu zilizolenga waajiri na wanufaika kupitia redio na televisheni ambapo jumla ya programu 24 ziliendeshwa na matangazo 336 yalitolewa; na
imeendelea na kampeni ya #WeweNdioFuture kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Kampeni hii inalenga kuhamasisha wateja wa Bodi ya Mikopo kuomba mkopo kwa usahihi ili kutimiza ndoto zao na pia kurejesha mikopo kwa wakati ili kuepuka adhabu.

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (BOHUMATA)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania imetekeleza kazi zifuatazo:
imeongeza vitabu 432,449 (432,144 kutoka Book Aid International,
305 kutoka Legal Deposite Law), magazeti 3,246 na majarida 13 katika vituo 43 vya Mikoa 22 kwa ajili ya watu wazima na watoto;
imetoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uanzishaji, upangaji na uendeshaji wa maktaba za Shule za Msingi na Sekondari 33 zilizopo katika Wilaya tano (5) za Ilala, Ubungo, Kinondoni, Temeke na Kigamboni; na
imetoa mafunzo ya ukutubi na uhifadhi nyaraka kwa washiriki 648 (NTA Level 4: 318; NTA Level 5: 150 na NTA Level 6: 180) kwa lengo la kuongeza ujuzi.

Uendelezaji wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imetekeleza kazi zifuatazo:
imekamilisha Mfumo wa Usimamizi wa Utafiti na Ubunifu (Research and Innovation Management System - RIMS) kwa lengo la kuhamasisha na kuongeza matumizi ya bunifu katika mifumo rasmi ya uchumi;
imetoa fursa kwa watafiti 13 wakiwemo wanafunzi wa Shahada ya Uzamili na Uzamivu kutoka katika Taasisi za Utafiti na Maendeleo wanne (4) na kutoka katika Vyuo Vikuu tisa (9) kushiriki kufanya utafiti katika kazi za kongano 15 zinazotekeleza mradi wa kongano bunifu. Aidha, Kongano tano (5) kati ya 15 zilizopo zimepata fursa ya kushiriki kufanya majaribio ya utekelezaji wa miongozo mitano (5) ya usimamizi wa kongano bunifu;

imewezesha taasisi nne (4) za kisekta (TALIRI, TARI, TAFIRI na TAFORI) kuandaa taratibu za uendeshaji (Standard Operating Prosedures – SOPs) kwa ajili ya uanzishwaji na uendeshaji wa kamati za maadili ya utafiti (Research Ethical Committee - REC). Uanzishwaji wa kamati za kusimamia maadili ya utafiti utasaidia nchi kukuza ubora wa tafiti ambazo zinazingatia viwango na maadili ya utafiti nchini; na
inaendelea na utekelezaji wa miradi 173 (ubunifu 106, utafiti 56 na miundombinu 11) inayotekelezwa kupitia taasisi mbalimbali za utafiti na maendeleo, Elimu ya Juu, Vyuo vya Kati na Ufundi Stadi ambapo miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume imewezesha upatikanaji wa maandiko 42 kutoka katika taasisi 19 vikiwemo Vyuo Vikuu. Maandiko hayo yalikuwa katika maeneo manne (4) na yalilenga kuendeleza na kuboresha:

Ng’ombe na nyama kwa ajili ya usindikaji; Teknolojia za kuchakata mazao ya kilimo; Teknolojia ya kuchakata ngozi; na Teknolojia za kuchakata nishati na madini hususan kwa wachimbaji wadogo. Kati ya maandiko hayo, maandiko 13 yaliibua miradi minne (4) iliyopata ufadhili wa fedha kutoka International Development Research Cooperation (IDRC). Miradi mingine iliyofadhiliwa ni mradi wa kimkakati kutoka Zanzibar kuhusu masuala ya miti shamba (tiba asilia) na miradi miwili (2) ya utafiti kwa lengo la kukuza matokeo ya awali ya utafiti katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na Taasisi ya NYUMBU.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imeendelea kutoa elimu kuhusu ufumbuzi wa matatizo mbalimbali ya kijamii kwa umma kwa kusambaza machapisho 83 yanayohusu sayansi, teknolojia na ubunifu katika magazeti na majarida mbalimbali, kurusha jumla ya vipindi 103 katika redio, runinga na mitandao ya kijamii.

Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa tafiti na bunifu zinazofanyika nchini zinakidhi vigezo vya ushindani, zinaendelezwa na wabunifu/watafiti wanajengewa uwezo wa kusimamia kazi zao, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imetekeleza kazi zifuatazo:
imetathmini bunifu 73 za wabunifu 70 walioshiriki katika mashindano ya MAKISATU kutoka mikoa 22 ya Tanzania Bara kwa lengo la kubaini mahitaji ya kila mbunifu ambapo wabunifu hao walipatiwa mafunzo ya utaratibu wa kusimamia na kuendesha miradi yao kabla ya kupatiwa ruzuku;
imetathmini miradi 120 ya utafiti kwa lengo la kusimamia na kubaini hali ya utekelezaji ambapo tathmini ilibaini kuwa takribani miradi yote ilikuwa katika hali nzuri ya utekelezaji; na
imepitia maombi 101 ya wabunifu waliotembelewa na Tume ambapo

maombi 61 yalikidhi vigezo vya kuendelezwa kwa kupatiwa fedha, mafunzo, kutambulishwa na kuunganishwa katika taasisi mbalimbali kulingana na ubunifu wao.


Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imewezesha wabunifu 10 wa Tanzania wenye Kampuni changa (Startups) wanaotumia teknolojia katika kutatua changamoto za kijamii kushiriki mafunzo ya awali. Mafunzo hayo yalilenga kujenga uwezo wa uanzishaji wa biashara au kampuni zinazojitegemea na kuboresha ujasiriamali kwa kutetea na kunadi ubunifu kwa wawekezaji (Pitching for investors). Baada ya mafunzo hayo, bunifu 18 kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Zambia, Namibia na Botswana zilichaguliwa kushiriki mashindano ya kiulimwengu ambapo kati ya hizo bunifu tatu (3) (Huduma smart, Medikea na Novfeed) zilikuwa za Tanzania. Bunifu moja (1) ya Tanzania (Huduma smart) ilishinda tuzo tatu (3) za Think Africa Prize ya USD 5000; Amazon Web Server; na Node by SLUSH (International Investment Matchmaking Platform) katika mashindano hayo.

Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) imetekeleza kazi zifuatazo:
imepima viwango vya mionzi kwa wafanyakazi 1,920 wanaofanya kazi katika vyanzo vya mionzi ambapo ilibainika kuwa viwango vya mionzi vilivyopo vinakubalika kisheria. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 41.3 ikilinganishwa na wafanyakazi 1,359 waliopimwa katika mwaka wa fedha 2019/20;
imepima viwango vya mionzi katika sampuli 11,378 ambapo kati ya hizo vyakula kutoka nje 3,266, vyakula vilivyosafirishwa nje ya nchi 7,055, mbolea 164 na tumbaku na bidhaa nyingine 893 kwa lengo la kudhibiti na kusimamia matumizi salama ya mionzi. Kiwango hicho ni

sawa na ongezeko la asilimia 44.5 ikilinganishwa na sampuli 7,873 zilizopimwa katika mwaka wa fedha 2019/20;
imekusanya mabaki ya vyanzo vya mionzi 16 na kuhifadhiwa katika kituo maalumu cha kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi ili kulinda wananchi na mazingira yasichafuliwe; na
imekagua vituo 364 ambavyo vinamiliki na kutumia vyanzo vya mionzi ili kudhibiti hali ya usalama kwa wagonjwa, wafanyakazi na umma ambapo vituo vilivyokaguliwa vimeongezeka kwa asilimia 74.2 ikilinganishwa vituo 209 vilivyokaguliwa katika mwaka wa fedha 2019/20.


Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha huduma za teknolojia ya nyuklia zinazotolewa na TAEC, Serikali imeendelea kutekeleza yafuatayo:
kusimamia kituo cha kupima uchafuzi wa hewa katika anga unaotokana na majaribio ya silaha za nyuklia chini ya mkataba wa kimataifa wa Comprehensive Nuclear Test-Ban Treaty (CTBT) for Non-Proliferation Test (NPT) of Nuclear Weapons;
kufanya tafiti 18 za matumizi ya teknolojia ya nyuklia na tayari machapisho matano (5) yameshatoka katika majarida mbalimbali ya kisayansi; na
kutengeneza na kuhakiki vifaa/mitambo 92 inayotumia teknolojia ya nyukilia katika kuimarisha ubora wa vifaa, usalama wa wafanyakazi na jamii inayowazunguka. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia
76.9 ikilinganishwa na vifaa 52 vilivyofanyiwa matengenezo na uhakiki katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20.


Mheshimiwa Spika, ili kuboresha na kusogeza huduma za teknolojia ya nyuklia karibu na jamii, Serikali kupitia TAEC imetekeleza kazi zifuatazo:
imepokea na kutathmini maombi 630 ya vibali vya umiliki, utumiaji

na usafirishaji wa vyanzo vya miozi ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 26 la lengo la maombi 500;
imetoa leseni 336 za kumiliki na kutumia vyanzo vya mionzi ambapo kati ya hizo leseni za kumiliki na utumiaji wa vyanzo vya mionzi 285, uingizaji wa vyanzo vya mionzi nchini 28, kusafirisha vyanzo vya mionzi nje ya nchi 7, na usafirishaji wa vyanzo vya mionzi ndani ya nchi 16. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 24.9 ikilinganishwa na leseni 269 zilizotolewa katika mwaka wa fedha 2019/20;
imesajili wataalam wa mionzi 278 ambapo kati yao wataalam wa kutoa huduma za mionzi kwa wagonjwa ni 262 na 16 wa usimikaji, uendeshaji, utengenezaji wa vifaa/mitambo inayotoa mionzi; na
imeendelea na ujenzi wa maabara changamano awamu ya pili itakayogharimu Shilingi bilioni 10.4 ambapo ujenzi umefikia asilimia
73. Kukamilika kwa ujenzi kutaongeza uwezo wa kulinda wananchi dhidi ya madhara ya mionzi ambayo yanaweza kujitokeza pamoja na kuiwezesha TAEC kuwa Kituo cha Umahiri cha Kikanda katika Nyanja ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia.

TUME YA TAIFA YA UNESCO (FUNGU 18)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu na kusimamia utekelezaji wa Mikataba na kazi za UNESCO nchini kama ifuatavyo:
imesimamia utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali iliyopitishwa katika mpango wa UNESCO wa Mwaka 2020 - 2022;
imeshirikisha wadau katika fursa mbalimbali zinazotokana na uanachama wa Serikali katika shirika la UNESCO;
imefanya tathmini juu ya usimamizi na uelewa wa wadau na ushiriki wao katika uhifadhi wa maeneo ya Urithi wa Dunia, Binadamu na Hifadhi Hai, na Urithi wa Kijiolojia;
imeratibu vikao vya Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti Matumizi ya Dawa na Mbinu za Kuongeza Nguvu Michezoni kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;
imeratibu na kutathmini utekelezaji wa maamuzi ya Kamati ya Urithi wa Dunia ndani ya maeneo yaliyo katika Orodha ya Urithi wa Dunia ambayo ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Eneo la Hifadhi la Ngorongoro, Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar, Michoro ya Miambani ya Kondoa na Magofu ya Kilwa Kisiwani na Magofu ya Songo Mnara;
imefanya tathmini ya utekelezaji wa programme za kimataifa za maji (International Hydrological Programme) na pia kusimamia utekelezaji wa programme ya kamisheni ya kimataifa ya mazingira ya bahari kwenye kuelekea uchumi wa blue na tahadhari kwenye majanga yanayotokana na bahari (International Oceanography Committee); na
imeratibu utekelezaji wa Programme za UNESCO nchini zinazohusuana na Elimu kwa wote (EFA) na Elimu ya Mafunzo ya Elimu ya Ufundi (TVET).

MPANGO NA BAJETI YA FUNGU 46 KWA MWAKA WA FEDHA 2021/22​

Mheshimiwa Spika, Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2021/22 yamezingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa (2025), Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 -2025/26), Ilani ya Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) (2020 - 2025) na Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliyoitoa tarehe 22 Aprili 2021 mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, maandalizi yamezingatia michango ya Waheshimiwa Wabunge katika Hotuba ya Waziri Mkuu, Hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI. Hivyo, Wizara itatoa kipaumbele katika kuimarisha elimu na kufanyia kazi maoni na ushauri ambao umekuwa ukitolewa na wadau wa elimu. Vilevile, Wizara itaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi kama yalivyoanishwa katika Hati Idhini ya waka 2016.

Maeneo ya Kipaumbele​

Mheshimiwa Spika, Serikali itafanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa lengo la kuhakikisha kuwa inakidhi mahitaji ya sasa. Aidha, Serikali itafanya mapitio ya Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 ili kuhakikisha inaendana na mazingira ya sasa ya utoaji wa elimu nchini.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaweka msisitizo zaidi katika ufundishaji wa Masomo ya Ufundi kwa kuimarisha Mafunzo kwa Vitendo katika shule za Sekondari za Ufundi zilizopo ambazo ni: Iyunga, Ifunda, Tanga, Bwiru Wavulana, Musoma, Mwadui, Moshi na Mtwara. Vilevile, Serikali itaimarisha ufundishaji wa masomo yanayowajengea wanafunzi ujuzi katika shule za msingi na sekondari. Masomo hayo ni pamoja na Kilimo, Ufundi, Stadi za Kazi, Michezo, na Biashara.
Mheshimiwa Spika, Serikali itafanya ufuatiliaji na tathmini ya kina ya mitaala inayotumika kwa sasa ili kuhakikisha kuwa ufundishaji na ujifunzaji

unafanyika kwa kuzingatia viwango na vigezo vilivyowekwa. Vigezo hivyo ni pamoja na uwepo wa walimu kulingana na idadi ya wanafunzi, vitabu na mazingira ya kujifunzia. Pia Serikali itaanza kufanya mapitio ya mitaala katika ngazi zote za elimu ili kuhakikisha kuwa elimu na mafunzo yanayotolewa yanajikita katika kujenga ujuzi na kuzingatia mahitaji ya sasa.

Mheshimiwa Spika, Katika utekelezaji wa Maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza tarehe 01 Mei, 2021, Serikali itaondoa tozo ya asilimia 6 ya kulinda thamani ya fedha katika urejeshaji wa mkopo kuanzia tarehe 1 Julai, 2021 iliyokuwa inatozwa kwa wanufaika wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Aidha, Serikali inaiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuondoa pia tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo hiyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali itafanyia kazi maoni na ushauri wa Wadau wa Elimu kuhusu utekelezaji wa Sheria ya mwaka 2018 iliyounda Bodi ya Kitaalamu ya Walimu. Aidha, Serikali itazingatia pia maoni na ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo walioutoa katika majadiliano kuhusu Kanuni za Bodi ya Kitaalamu ya Walimu yaliyofanyika tarehe 28 Aprili 2021 kati ya Wizara ya Elimu na Kamati hiyo. Vilevile, Wizara itazingatia kikamilifu maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu Bodi ya Kitaalamu ya Walimu aliyoyatoa katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza tarehe 01 Mei, 2021.
Majukumu ya Msingi ya Wizara
Mheshimiwa Spika,
maeneo mengine ya Mpango na Bajeti katika mwaka wa fedha 2021/22, yatatekelezwa kupitia Idara, Vitengo na Taasisi kama

ilivyofafanuliwa katika majukumu ya Wizara. Malengo yatakayotekelezwa ni kama ifuatavyo:

Uendelezaji wa Elimumsingi na Sekondari​

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha Elimumsingi na Sekondari, Serikali itatekeleza kazi zifuatazo:
itafanya ufuatiliaji na tathmini ya uendeshaji na usimamizi wa shule Shikizi katika mikoa 15 ili kupima matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji na kuweka afua stahiki;
itaratibu mashindano ya insha ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa lengo la kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri, kuandika na kujieleza;
itatoa mafunzo ya malezi, unasihi na ulinzi wa mtoto shuleni kwa walimu 200 wa shule za sekondari kutoka katika Kanda mbili (2) za Uthibiti Ubora wa Shule za Mashariki na Kusini ili kuwajengea uwezo na kuimarisha stadi za utoaji wa huduma za malezi shuleni; na
itaandaa mwongozo wa kuwabaini na kuwaendeleza wanafunzi wenye vipawa na vipaji katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya Ualimu. Mwongozo huo utawezesha kuwatambua wanafunzi hao na kuweka mikakati ya kuwaendeleza.


Ithibati na Usajili wa Shule na Vyuo vya Ualimu​

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu la kusimamia Sera na kuongeza fursa za Elimu na Mafunzo, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/22, itatekeleza yafuatayo:
itasajili shule 450 kwa lengo la kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu nchini;
itaendesha mafunzo kwa maafisa wa Wizara na Wathibiti Ubora wa Shule katika halmashauri kuhusu Mwongozo wa Usajili na Uendeshaji

wa Shule uliohuishwa pamoja na mfumo mpya wa usajili wa shule wa kieletroniki; na
itafanya ufuatiliaji katika shule 100 kati ya 450 zilizopata usajili wa masharti ya kukamilisha miundombinu iliyopungua ili kuhakiki kama wamezingatia masharti.


Usimamizi wa Elimu ya Ualimu​

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha mafunzo ya Elimu ya Ualimu, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/22 itatekeleza yafuatayo:
itaratibu mashindano ya michezo na sanaa (UMISAVUTA) katika Vyuo vya Ualimu;
itadahili wanachuo 8,000 wa mwaka wa kwanza katika Vyuo vya Ualimu; na
itaratibu mafunzo ya ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na Visivyo vya Serikali.


Usimamizi na Uendelezaji wa Elimu Maalum​


Mheshimiwa Spika,
katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa Elimu maalum, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/22 imepanga kutekeleza yafuatayo:
itanunua na kusambaza vifaa maalum vya kielimu na saidizi katika shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya Ufundi na vyuo vikuu ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, vifaa hivyo ni pamoja na viti mwendo, vifaa vya michezo, mafuta na kofia kwa ajili ya wenye ualbino na vifaa vya utengamao na uchechemuzi (bembea);
itaendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakufunzi 400 wa vyuo vya ualimu, VETA na Wathibiti Ubora wa Shule kuhusu Elimu Maalumu na Elimu Jumuishi ili kuweza kuwahudumia wanafunzi

wenye mahitaji maalumu;

itawawezesha wanafunzi wenye ulemavu wanaotoka katika familia zenye kipato duni kupata mahitaji muhimu ikiwemo ada na vifaa vya kujifunzia kwa lengo la kupunguza changamoto zinazokabili upatikanaji wa elimu katika ngazi mbalimbali;
itafanya utafiti kuhusu ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi wenye ulemavu wa akili, usonji na viziwi ili kubaini changamoto na kuweka mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi hao; na
itaendesha mafunzo kwa walimu 400 kuhusu ubainishaji na utoaji wa huduma stahiki kwa wanafunzi wenye ulemavu wa akili na wenye usonji ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wanafunzi hao.


Kusimamia Ubora wa Elimu katika Shule na Vyuo vya Ualimu​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule na Vyuo vya Ualimu itatekeleza yafuatayo:
itafanya tathmini ya jumla katika asasi 7,263 zikiwemo shule za Msingi 5,598, Sekondari 1,607 na Vyuo vya Ualimu 58;
itafanya tathmini ya ufuatiliaji katika asasi 1,453 zikiwemo shule za Msingi 1,120, Sekondari 321 na Vyuo vya Ualimu 12; na
itasimamia ujenzi wa ofisi tano (5) za Uthibiti Ubora wa Shule katika wilaya za Ubungo, Njombe Mji, Bunda DC, Pangani na Tarime.


Baraza la Mitihani la Tanzania - NECTA​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania itatekeleza kazi zifuatazo:
itaendesha Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) 2021 kwa wanafunzi 1,705,650;

itaendesha Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2021 kwa watahiniwa 1,140,571;
itaendesha Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) 2021 kwa watahiniwa 822,509;
itaendesha Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2021 kwa watahiniwa 583,898 na Mtihani wa Maarifa (QT) 2021 kwa watahiniwa 9,904;

iwa Spika, Tume ya Taifa ya UNESCO (Fungu 18) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,679,073,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida (Mishahara ni Shilingi 1,146,780,000 na Matumizi Mengineyo ni Shilingi 1,532,293,000.00). 215. Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa naomba sasa Bunge lako tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Mafungu yote mawili (Fungu 46 na Fungu 18) yenye jumla ya Shilingi 1,387,093,874,000.00. 216.

Mheshimiwa Spika, napenda kuhitimisha kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwako wewe na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. 217. Mheshimiwa Spika, Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizara ambayo ni Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. 218. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja itaendesha Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2022 kwa watahiniwa 100,492;
itaendesha Mitihani ya Ualimu katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa watahiniwa 7,324 mwaka 2022; na
itaendesha Upimaji wa Kitaifa wa Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu - KKK kwa sampuli ya watahiniwa wa Darasa la Pili 2022.

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)​

Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha ubora wa elimu nchini katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania itatekeleza kazi zifuatazo:
itapitia na kuboresha mtaala wa Elimu ya Sekondari Kidato cha I - VI ili kukidhi mahitaji ya sasa na kuweka mkazo zaidi katika elimu inayojenga ujuzi;
itachapa na kusambaza vitabu vya kiada ngazi za sekondari, moduli za Elimu ya Ualimu na vitabu vya hadithi kwa darasa la I na II;
itatoa mafunzo kazini kwa Walimu, Wakufunzi, Wathibiti Ubora wa Shule na Maafisa Elimu kuhusu mtaala ulioboreshwa;
itafanya tathmini ya vitabu vya ziada na rejea kutoka kwa waandishi binafsi ili viweze kupatiwa ithibati; na
itaboresha mtaala na mihtasari ya wanafunzi viziwi na wasioona katika ngazi ya Elimu ya Msingi.

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji, Serikali itatekeleza yafuatayo:
itaandika vitabu vya kiada na Kiongozi cha Mwalimu kwa masomo ya Sekondari Kidato cha I - VI ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa vitabu katika ngazi hiyo;
itaandaa vitabu vya kiada katika mfumo wa maandishi makubwa kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu na maandishi ya Breli kwa ajili wanafunzi wasioona kwa masomo ya Sekondari; na
itaandaa maudhui ya kielekroniki kwa ngazi ya Elimu ya Msingi Darasa la I na II ili kukuza stadi za kusoma na kuandika.


Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu, itatekeleza kazi zifuatazo:
itadahili walimu 2,515 watakaosoma kozi za Stashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu na Uthibiti Ubora wa Shule ili kuwapa ujuzi na maarifa katika Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathmini katika Elimu;
itaandaa Mtaala wa Shahada ya Menejimenti na Uthibiti Ubora wa Elimu (Bachelor of Education Management and Quality Assurance) ili kuimarisha usimamizi na utoaji wa elimu bora katika ngazi zote za elimu;
itatoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu Uthibiti Ubora wa Shule wa Ndani, Uongozi na Usimamizi wa Elimu kwa Wakuu wa shule za msingi na sekondari 14,627 ili kuwajengea uwezo wa kusimamia ufundishaji na ujifunzaji wenye kuleta tija katika elimu;
itafanya tafiti nne (4) kuhusu Uongozi na Usimamizi wa Elimu ili kubaini upungufu na kuandaa mafunzo wezeshi kwa wahusika;
itajenga jengo la ghorofa moja (1) katika Kampasi ya Mbeya na

ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 katika Kampasi ya Bagamoyo ili kuimarisha ufanisi katika shughuli za utoaji wa Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu; na
itawezesha watumishi 66 kushiriki mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.


Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima itatekeleza kazi zifuatazo:
itaendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo na Elimu kwa Umma yaani National Adult Literacy and Mass Education Rolling Strategy (NALMERS) unaolenga kupunguza kiwango cha watu wasiojua kusoma na kuandika; kwa kuwajengea uwezo maafisa na wataalamu wa kisomo na kutekeleza miradi ya kisomo inayotumia mtaala wa IPOSA;
itaongeza fursa za utoaji wa Elimu ya Sekondari Nje ya Mfumo Rasmi kwa kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 14,930 hadi 15,130;
itafanya utafiti wa kitaifa kuhusu hali ya kisomo na elimu kwa umma utakaoboresha utekelezaji wa mkakati wa kisomo na elimu kwa umma;
itawezesha wasichana takribani 4,000 walioacha shule kupata elimu ya sekondari kwa njia mbadala kupitia utekelezaji wa Miradi ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, ikiwemo Mradi wa Elimu ya Sekondari kwa Wasichana Walio Nje ya Mfumo Rasmi (SEOSAG), Mpango wa Elimu Changamani Baada ya Elimu ya Msingi (IPPE) na Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP);
itaongeza udahili wa wanafunzi wa Astashahada, Stashahada na Shahada kutoka 4,766 hadi 5,200;

itajenga na kukarabati miundombinu ya ufundishaji na ujifunzaji katika vituo vya taasisi vya mikoa minne (4) ambayo ni; Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro na Mwanza; na
itafanya utafiti wa hali ya kisomo (kujua kusoma na kutojua kusoma) katika mikoa 10 ya Tanzania Bara kwa lengo la kupata takwimu sahihi zitakazosaidia kuweka mikakati na mipango nje ya mfumo rasmi.


Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (BOHUMATA)​

Mheshimiwa Spika, katika kutoa nafasi kwa umma wa watanzania kutumia maktaba zote za umma kwa ajili ya kupata taarifa sahihi na maarifa ili kujikwamua katika ujinga, umaskini na maradhi; Serikali kupitia Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania katika mwaka wa fedha 2021/22, itatekeleza yafuatayo:
itaimarisha na kuinua ubora wa huduma za Maktaba katika Mikoa 22 ili kuongeza fursa za kupata taarifa na maarifa yatakayo wasaidia kujikwamua katika changamoto za kimaendeleo;
itaendelea kuhifadhi nyaraka muhimu za serikali kwa kizazi cha sasa na kijacho;
itatoa mafunzo ya ukutubi na uhifadhi nyaraka kwa wanafunzi takribani 1,000;
itatoa ushauri wa kitaalamu katika vituo 350 juu ya uanzishaji, upangaji na uendeshaji wa Maktaba za shule, Vyuo, Taasisi na Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji na Wilaya;
itaendelea kutoa elimu kwa watumishi jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kutoa huduma kwa watumishi wanaoishi na virusi vya Ukimwi; na
itaendelea wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwa kujenga Maktaba katika Chuo cha Ukutubi (SLADS); na kufanya ukarabati katika Maktaba za Tanga, Arusha, Mara na Mwanza.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu itatekeleza kazi zifuatazo:
itawezesha ujenzi wa madarasa 210 katika shule 70 za msingi na sekondari;
itawezesha ujenzi wa ofisi za walimu mbili (2) katika shule mbili (2) za sekondari na ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi katika 03 shule za sekondari;
itawezesha ujenzi wa matundu ya vyoo 1,920 katika shule 80 za msingi na sekondari;
itawezesha ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule 10 za msingi na sekondari;
itaanza ujenzi wa jengo la ofisi za Mamlaka ya Elimu Tanzania Dodoma katika awamu ya kwanza; na
itatoa mkopo nafuu kwa taasisi ya Umma ya Elimu ya Juu moja (1) kwa ajili ya uendelezaji wa miundombinu ya elimu.


Kituo cha Maendeleo Dakawa​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Kituo cha Maendeleo Dakawa, itatekeleza kazi zifuatazo:
itaendelea kusimamia uhifadhi wa kumbukumbu za majengo, makaburi na nyaraka za makumbusho ya wapigania uhuru wa ANC ili kutunza historia;
itaendelea kukarabati nyumba za makazi ya watumishi ili kuboresha mazingira ya kazi na kuwafanya watumishi wavutiwe kuishi katika eneo hilo; na

itaendelea kupanda miti kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira.


Uimarishaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Idara ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi itatekeleza kazi zifuatazo:
itawezesha utoaji wa mafunzo ya muda mrefu ya Ufundi Stadi na Elimu ya Wananchi (Folk Education) kwa washiriki 15,000 katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 54 ili kuwawezesha washiriki kupata ujuzi na maarifa yatakayowawezesha kujiajiri au kuajiriwa na pia kuweza kuongeza thamani katika shughuli za uzalishaji wanazozifanya;
itatoa mafunzo ya muda mfupi na mafunzo nje ya Chuo kwa washiriki 24,000 kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi ili kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa;
itaratibu mafunzo kwa Wakufunzi 150 kwenye Taasisi za Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa lengo la kuwaongezea uwezo wa ufundishaji wa mitaala inayoendana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya soko la ajira;
itawezesha usimamizi na ukaguzi wa shughuli za mafunzo katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 54 ili kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanakidhi viwango vinavyohitajika;
itawezesha upatikanaji wa vifaa vya kiufundi vya kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 54 ili kuhakikisha mafunzo yanaendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia;
itawezesha mkutano wa kimkakati wa wadau wanne (4) katika Mafunzo ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuwajengea uwezo wa kusimamia na kuratibu mafunzo na uandaaji wa Mitaala ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi;

itafanya ufuatiliaji na tathimini ya utoaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuhakikisha ubora unazingatiwa katika Taasisi za Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kulingana na soko la ajira na mabadiliko ya sayansi na teknolojia;
itaendelea kuratibu utekelezaji wa mradi wa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP) katika vituo vya umahiri vinne (4) kwenye nyanja za TEHAMA - Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Usafiri wa anga - Chuo cha Usafirishaji cha Taifa, Nishati jadidifu - Chuo cha Ufundi Arusha na Mazao ya ngozi - Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Kampasi ya Mwanza;
itaratibu mafunzo ya muda mfupi kwenye taaluma ya ufundishaji kwa masafa kwa wakufunzi 240 wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na VETA; na
itaendelea kuratibu ujenzi wa vyuo vipya vya ufundi stadi kwenye Wilaya ambazo hakuna vyuo ikiwemo Chuo cha Ufundi cha Dodoma (DTC) kinachojengwa kwenye eneo la Nala.


Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Mamlaka itaendelea kuimarisha ubora wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kutekeleza yafuatayo:
itaendelea kutoa fursa sawa katika elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini kwa kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 357,850 hadi takribani 500,000 ambapo wanafunzi wenye ulemavu 1,000 na wanaotoka katika mazingira magumu 2,400 watadahiliwa;
itarasimisha ujuzi wa wanagenzi takribani 10,000 ambao wataongeza nguvukazi yenye ujuzi wa kiwango cha kati;
itaandaa na kuhuisha mitaala 10 kulingana na mahitaji ya soko la ajira na kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za soko la ajira;

itaanza ujenzi wa vyuo vipya vya VETA vya mikoa mitatu (3) ya Dar es Salaam (Kampasi mpya ya Kigamboni), Simiyu na Songwe;
itaendelea na ujenzi wa vyuo vya VETA vya mikoa minne (4) ya Geita, Njombe, Rukwa na Kagera;
itaendelea na ujenzi na ukarabati wa karakana tano (5), madarasa nane (8), mabweni sita (6), nyumba za watumishi 13, bwalo la chakula na jiko katika Vyuo vya VETA 30 vya Wilaya pamoja na kujenga jengo la Ofisi za Makao Makuu ya VETA jijini Dodoma;
itakarabati vyuo vikongwe vya mikoa mitano (5) ya Mwanza, Dar es salaam, Dodoma, Mtwara na Tanga pamoja na kununua na kusimika mitambo na zana za mafunzo;
itakarabati Jengo la Chuo cha Mafunzo ya TEHAMA Kipawa na majengo manne (4) ya ghorofa yaliyoko Tabata – Dar es Salaam ambayo ni makazi ya watumishi;
itaimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma na mafunzo kwa kuunganisha vyuo 11 katika mtandao wa LAN na WAN pamoja na kuandaa mfumo wa ukusanyaji taarifa za mafunzo;
itawajengea uwezo wa kitaaluma na umahiri watumishi 110 wa Mamlaka kwa lengo la kuongeza ujuzi na ufanisi katika utendaji wa kazi; na
itanunua magari 30 kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya VETA nchini.


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Baraza itatekeleza kazi zifuatazo:
itasajili vyuo 50 ili viweze kuendesha elimu ya ufundi na mafunzo nchini kwa lengo la kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya ufundi nchini;

itatoa ithibati kwa vyuo 60 vinavyotoa elimu ya ufundi na mafunzo nchini kwa lengo la kuhakikisha vyuo vinakidhi viwango vya utoaji wa Elimu ya Ufundi;
itafanya ufuatiliaji na tathmini ya ubora wa elimu katika vyuo 200 vya Elimu ya Ufundi kwa lengo la kuangalia uzingatiaji wa sheria, kanuni na miongozo ya utoaji wa elimu ya ufundi nchini na kutoa ushauri wa namna ya kuboresha utoaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo;
itaratibu na kuhakiki udahili wa Wanafunzi 159,500 katika fani mbalimbali za ngazi ya Astashahada na Stashahada;
itatoa namba ya uhakiki wa tuzo (AVN) 20,000 ambayo itasaidia kuondoa udanganyifu wa wahitimu wanaoendelea na masomo ngazi ya Elimu ya Juu. Aidha, namba hii itavirahisishia vyuo kufanya uhakiki wa wanafunzi wa Stashahada wanaoomba kujiunga na Elimu ya Juu;
itafanya ulinganifu wa tuzo 1,050 ili kudhibiti viwango vya Elimu ya Ufundi nchini;
itahakiki mitaala 150 itakayokuzwa na Vyuo vya Ufundi kwa lengo la kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa yanakidhi soko la ajira nchini na kimataifa;
itaendelea kutoa mafunzo ya namna ya upimaji na ufundishaji wa mitaala inayozingatia umahiri (CBET) kwa wakufunzi zaidi ya 1,000 wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi. Mafunzo hayo yatasaidia wahitimu kuwa mahiri katika ujuzi uliokusudiwa; na
itaendelea na ujenzi wa ofisi za kanda katika mikoa ya Arusha, Mtwara, Dodoma, Mwanza, Tabora na Mbeya.


Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Chuo cha Ufundi Arusha itatekeleza kazi zifuatazo:
itaongeza fursa za upatikanaji wa elimu kwa kujenga bweni la

wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 252;

itadahili jumla ya wanafunzi 3,172 ambapo ngazi ya Stashahada (NTA Level 4) 1,327, Shahada (NTA Level 7) 400 na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET) 1,445;
itarahisisha ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya TEHAMA kwa kusimika mtandao wa ndani (LAN) katika majengo ya Chuo;
itaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kukamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa tatu (3) lenye madarasa, maabara na ofisi za walimu ambapo ujenzi upo katika hatua ya upauaji. Kukamilika kwa mradi huu kutaongeza udahili wa wanafunzi;
itaboresha utoaji wa mafunzo, uzalishaji na ushauri wa kitaalamu kwa kununua mashine mbili (2) za kisasa katika maabara mbili (2) kwa ajili ya kupima ubora wa maji na vifaa vya ujenzi;
itaongeza udahili na kuboresha utoaji wa elimu kwa kutekeleza mradi wa EASTRIP katika Kituo cha Mafunzo cha Kikuletwa. Mradi huo unahusisha ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia nguvu za maji (turbine) kwa ajili ya kutolea mafunzo, madarasa, ukumbi wa mihadhara, hosteli mbili (2), karakana tatu (3), maabara moja (1), jengo la nyumba za watumishi 10, jengo la utawala, maktaba, chumba cha usanifu, ukumbi wa mikutano, canteen na sehemu za mapumziko;
itajenga kliniki (Medical Clinic) itakayohudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa maeneo ya jirani kwa lengo la kuboresha huduma za afya zao; na
itaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu kwa walengwa mbalimbali kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu uimara wa udongo, kokoto na lami zinazotumika katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali, kupima ubora wa maji, usanifu wa miradi ya maji na ujenzi wa aina mbalimbali.

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere itatekeleza yafuatayo:
itaongeza udahili wa wanafunzi kutoka 11,790 katika mwaka wa masomo 2020/21 hadi wanafunzi 14,564 mwaka 2021/22. Ongezeko hilo litatokana na kuimarishwa kwa mazingira ya ufundishaji pamoja na uanzishwaji wa Tawi la Pemba na uanzishwaji wa Programu za Uzamili katika idara mbalimbali;
itapitia na kuboresha mitaala ya Chuo ili iweze kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri;
itakarabati miundombinu chakavu ya maji, umeme, barabara na majengo ya Chuo (madarasa na nyumba 8 za watumishi), mifumo ya TEHAMA na mitambo;
itawezesha tafiti 14 na ushauri wa kitalaam katika maeneo ya Uongozi na Maadili, Sayansi za Jamii, Jinsia na Ujasiriamali.

Tafiti hizo na ushauri wa kitaalam zitalenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii;
itagharamia jumla ya watumishi 24 katika mafunzo ya muda mrefu na watumishi 55 katika mafunzo ya muda mfupi ili kupunguza uhaba wa wataalam na kuongeza ufanisi wa utendaji wa kazi kwa watumishi wa Chuo; na
itaongeza miundombinu kwa kutekeleza miradi sita (6) ya ujenzi ambayo ni:
kuendelea na awamu ya kwanza ya ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi katika Kampasi ya Karume yenye uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 1,536 (Wanawake: 768 Wanaume: 768);
kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa Maktaba yenye uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 2,500 katika Kampasi ya Kivukoni;

kujenga ukumbi wa mihadhara (Lecture Theater) wenye uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 1,000 katika Kampasi ya Kivukoni;
kujenga jengo la utawala na ofisi za watumishi katika Kampasi ya Kivukoni;
kujenga nyumba tatu (3) za ghorofa za wafanyakazi zenye uwezo wa kukaliwa na watumishi 30 katika Kampasi ya Karume; na
kujenga madarasa na bweni la wanafunzi katika Tawi la Pemba.


Usimamizi na Uendelezaji wa Elimu ya Juu​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Idara ya Elimu ya Juu itatekeleza kazi zifuatazo:
itaendelea kuratibu upatikanaji wa fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka nchi rafiki na mashirika mbalimbali nje ya nchi;
itaendelea na ufadhili wa wanafunzi 10 raia wa China waliokubalika kimkataba kusoma Lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;
itaendelea kufadhili wanataaluma 68 katika Shahada ya Umahiri na Uzamivu kutoka Vyuo Vikuu vya Umma kusoma katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati;
itaendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum waliopo katika Taasisi za Elimu ya Juu ili kuwawezesha kusoma kwa ufanisi;
itaandaa na kuhuisha daftari la kumbukumbu la wanafunzi wanaopata ufadhili wa masomo ndani na nje ya nchi;
itafuatilia wahitimu waliotoka kwenye taasisi za hapa nchini kama wanaajirika kulingana na ujuzi walioupata na kushauri vyombo vya uthibiti ubora na vya kitaalam ipasavyo; na
itaratibu na kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa ajili

ya kuleta Mageuzi ya Kiuchumi Higher Education for Economic Transformation (HEET).

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu itatekeleza kazi zifuatazo:
itakagua na kufanya tathmini ya Vyuo Vikuu 25 kwa lengo la kuhakiki ubora;
itafanya tathmini ya programu 200 za masomo mbalimbali katika Vyuo Vikuu nchini na kuzipa ithibati kwa zitakazokidhi vigezo;
itafanya tathmini ya tuzo 5,000 zilizotolewa katika Vyuo Vikuu vya nje ya nchi na kuzitambua zitakazokidhi vigezo;
itaratibu udahili na kuhakiki maombi ya wanafunzi 120,000 wa mwaka wa kwanza wanaotarajiwa kuomba udahili katika vyuo vya Elimu ya Juu ili kujiunga na programu mbalimbali za masomo kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada, Shahada ya Awali na Shahada ya Umahiri;
itavijengea uwezo Vyuo Vikuu katika masuala mbalimbali ya ithibati na uthibiti ubora ili kuimarisha ubora wa Elimu ya Juu;
itafanya utafiti kuhusu masuala mbalimbali yenye lengo la kufanya maboresho katika mfumo wa utoaji Elimu ya Juu nchini ili kuweza kuchukua hatua stahiki;
itaboresha mfumo wa utoaji na ukusanyaji taarifa za Elimu ya Juu kwa kutumia TEHAMA ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wakati na matumizi yake katika kupanga mipango na kufanya maamuzi;
itakagua Asasi/Kampuni nne (4) zinazojishughulisha na uratibu wa wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi kwa lengo la

kuzitambua na kuzisajili zile zitakazokidhi vigezo;​

itashiriki katika makongamano na mikutano inayohusu uimarishaji na Uthibiti wa Ubora wa Elimu ya Juu katika ukanda wa Afrika Mashariki na kimataifa kwa lengo la kuongeza ujuzi na weledi katika kuthibiti ubora wa Elimu ya Juu nchini; na
itaratibu maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu nchini ili kutoa elimu kwa umma kuhusu vyuo na programu mbalimbali zitolewazo.


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu itatekeleza kazi zifuatazo:
itaimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuwa na mifumo rafiki itakayowezesha ukusanyaji wa Shilingi bilioni 200;
itaanzisha Kituo Mahsusi cha Wateja (Dedicated Customer Relations Centre) jijini Dar es Salaam ili kuboresha huduma za Bodi ya Mikopo kwa wateja hususan katika urejeshaji wa mikopo;
itasimamia uombaji, uchambuzi na utoaji wa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 500 kwa wanafunzi wahitaji wapatao 148,581. Kati yao, wanafunzi 50,250 watakua wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo 98,331;
itakamilisha mifumo ya TEHAMA kupitia Mradi wa Maboresho ya TEHAMA wa Bodi ya Mikopo (HESLB-GASi++) itakayowezesha uunganishwaji wa mifumo ya Bodi na ya wadau ili kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa na hivyo kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wanafunzi, waajiri na wanufaika wa mikopo;
itakamilisha tathmini ya namna bora ya kugharimia wahitimu wenye ufaulu wa juu na wale wanaopata skolashipu za kusoma katika vyuo maalum nje ya nchi (Presitigous Overseas’ Universities) kusomea fani

mahsusi (High – Impact - Degree) zinazoweza kuchochea ufanisi na kuchangia ukuaji uchumi;

itafanya mapitio ya viashiria na ving’amuzi vya uhitaji (Means - Testing) vinavyotumika kupima uhitaji wa mikopo (neediness) kwa kuzingatia hali za kimaisha (socio - economic status) kwa lengo la kuboresha utoaji wa mikopo kwa wanufaika;

itaandaa Mpango Mkakati wa Bodi wa Awamu ya Tano (2022/23 – 2026/27) utakaolenga kujenga uwezo wa Bodi ya Mikopo kuwa himilivu na kujiendesha kama mfuko wa mikopo (Student Revolving Loans Fund); na

itaendeleza na kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimkakati ili kuwafikia waajiri na wanufaika katika mikoa na wilaya mbalimbali kwa kuendesha programu mahususi za elimu ya uombaji na urejeshaji wa mikopo.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)​

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam itatekeleza kazi zifuatazo:

itaongeza udahili wa wanafunzi kutoka 42,745 hadi 43,600 ambapo wanafunzi wa kike wataongezeka kutoka 19,633 hadi 20,026;

itatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu 60 kwenye masomo ya Sayansi hususani wanafunzi wa kike waliohitimu mitihani ya Kitaifa ya Kidato IV na Shahada za Awali;

itaendelea kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa kigeni wa Shahada ya Umahiri katika Lugha ya Kiswahili;

itaongeza idadi ya miradi ya utafiti kutoka 239 hadi 289 kwa kuwafadhili watafiti 50 ili wafanye tafiti katika maeneo yanayolenga uchumi wa viwanda kwa kuzingatia Ajenda ya Utafiti ya Taifa;

D. SHUKRANI 208. Mheshimiwa Spika, napenda kutambua mchango mkubwa wa viongozi wenzangu katika kutekeleza na kufanikisha majukumu ya Wizara yangu. 123 Kipekee kabisa namshukuru Mheshimiwa Omary Juma Kipanga (Mb), Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ushirikiano mkubwa anaonipa katika kusimamia Wizara hii. Aidha, namshukuru Katibu Mkuu, Dkt. Leonard Douglas Akwilapo, Naibu Katibu Mkuu Profesa James Epiphan Mdoe, Naibu Katibu Mkuu Profesa Carolyne Nombo , Kamishna wa Elimu, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Vitengo, na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa ushirikiano wao wa karibu katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya kila siku ya Wizara. 209.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru viongozi wa vyama vya wafanyakazi, Watumishi wa Wizara na Taasisi zake, Walimu, Wanafunzi na Wadau wote Elimu kwa ushirikiano wao. Aidha, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wamiliki wa Shule, Vyuo na Taasisi Binafsi ambao wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika utoaji wa elimu hapa nchini. 210. Mheshimiwa Spika, Nawashukuru sana wananchi wa Kasulu Mjini kwa kuniamini na kunichagua kwa kura nyingi sana ili niwe mwakilishi wao. Nawaahidi utumishi uliotukuka. 211.

Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru Washirika wa Maendeleo na Wadau wa Elimu wote ambao wamechangia kufanikisha utekelezaji wa Mipango na Miradi ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Naomba kuwatambua baadhi yao kama ifuatavyo: Serikali za: Algeria, Austria, Brazil, Canada, China, Cuba, Finland, Hungary, India, Indonesia, Italia, Israel, Japan, Korea ya Kusini, Malta, Marekani, Malaysia, Misri, Morocco, Netherland, New Zealand, Norway, Palestine, Romania, Saudi Arabia, Sweden, Thailand, Ufaransa, Urusi, Uswisi, Uingereza, Uholanzi, Ujerumani na Venezuela. Aidha, natambua pia mchango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika. 124 212.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuyashukuru mashirika ya kitaifa na kimataifa yaliyochangia kufanikisha miradi na programu za Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo ni pamoja na; Benki ya Dunia, Foreign, Commonwealth and Development Office (FCDO), Swedish International Development Agency (SIDA), Umoja wa Nchi za Ulaya, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Jumuiya ya Madola, Global Partnership in Education (GPE), United Nations International Children’s Emergency Fund (UNICEF), United Nations Development Programme (UNDP), United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO), USAID, Inter University Council for East Africa (IUCEA), Human Development Innovation Fund (HDIF), Deutscher Akademischer Austauschdienst (DAAD), British Council, Campaign for Female Education (CAMFED), Commonwealth Secretariat, Aga Khan Education Services, Japan International Cooperation Agency (JICA), Karibu Tanzania Organization (KTO), Korea International Cooperation Agency (KOICA), WaterAid, Plan International, Tanzania Education Network/Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Christian Social Services Commission (CSSC) na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA). E. MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2021/22 213. Mheshimiwa Spika, ili kuwezesha utekelezaji wa malengo kwa mwaka wa fedha 2021/22, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Fungu 46) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,384,414,801,000.00 kwa mchanganuo ufuatao:

(i) Shilingi 480,474,878,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya kawaida ya Wizara ambapo Shilingi 447,214,694,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara na Shilingi 33,260,184,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo; na

(ii) Shilingi 903,939,923,000.00 zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 706,639,923,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 197,300,000,000.00 fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo. 125 214. Mheshimiwa Spika, Tume ya Taifa ya UNESCO (Fungu 18) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,679,073,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida (Mishahara ni Shilingi 1,146,780,000 na Matumizi Mengineyo ni Shilingi 1,532,293,000.00). 215.

Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa naomba sasa Bunge lako tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Mafungu yote mawili (Fungu 46 na Fungu 18) yenye jumla ya Shilingi 1,387,093,874,000.00. 216. Mheshimiwa Spika, napenda kuhitimisha kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwako wewe na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. 217.

Mheshimiwa Spika, Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizara ambayo ni Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. 218.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
 

Attachments

  • HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA (1).pdf
    3.8 MB · Views: 20
... pia kama ni sheria au kanuni zilikuwa zina-enforce huo ujinga zirekebishwe haraka! Hii ilikuwa miongoni mwa maeneo ambayo akili haikutumika kabisa! Ni aibu kuwafanyia wenye nchi yao ukatili wa ajabu kama ule! Government is for the people and should act for the people's interests and not otherwise!
 
Kwanini wasubiri mpaka Julai Mosi na sio yaanze sasa wakati hayo matozo yanaumiza?
Mama Samia alitangaza kuyafuta May Mosi, sasa kwanini May na June yaendelee tena?
 
Kwanini wasubiri mpaka Julai Mosi na sio yaanze sasa wakati hayo matozo yanaumiza?
Mama Samia alitangaza kuyafuta May Mosi, sasa kwanini May na June yaendelee tena?
... kukamilisha budget cycle i think!
 
Serikali itaondoa tozo ya asilimia sita ya kulinda thamani ya fedha katika urejeshaji wa mkopo kuanzia 1 Julai 2021, iliyokuwa inatozwa kwa wanufaika wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ikiwa ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan

Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichakob ameeleza bungeni kuwa Serikali inaiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuondoa pia tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo hiyo

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), hadi kufikia Machi 2021, imekusanya Sh.139.2 bilioni ya lengo la Sh.194.1 bilioni kwa mwaka 2020/21. Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), imetoa mikopo kwa wanafunzi 149,398. Kati yao 55,337 wa mwaka wa kwanza na 94,061 wanaoendelea na masomo.

Mwaka 2021/22, Serikali itapitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 kwa lengo la kuhakikisha kuwa inakidhi mahitaji ya sasa. Pia, itafanya mapitio ya Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 ili kuhakikisha inaendana na mazingira ya sasa ya utoaji wa elimu nchini
Haya basi na mimi tukutane na bodi hiyo julai kwa sasa waniache..
 
Kweli Mungu mkubwa kuna baadhi ya vitu Watanzania tuliaminishwa na Kayafa kuwa havibadilishiki, mathalani ukandamizaji na ufilisi uliokuwa unafanywa na Bodi ya mikopo!! Aishi maisha marefu Mama Suluhu.
... hakuna kitu hatari kama kutumia state machinery kueneza propaganda za mtawala huku ukizuia wengine kuhoji au kuelezea upande wa pili wa shilingi kama free media; political rallies; kuchomoa yasiyowapendeza kwenye budget mbadala za wapinzani, etc! Checks and balances zinakosekana na, in the long run, ni total failure!
 
Ni kweli asilimia za tozo zilikuwa kubwa. Kama inflation rate ni 3.45% unatozaje 6% za kulinda thamani ya fedha?
... ndio maana hadi mabenki ya kibiashara yalijimwambafy kununua madeni ya mikopo ya elimu ya juu kuvutia wateja na walifanikiwa kweli! Yaani mkopo wa elimu wa serikali ulikuwa ghali kuliko mkopo wa mabenki ya kibiashara. Hiyo ipo Tanzania tu! Halafu legacy! Fvc@#$!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom