hotuba kali kutoka kwa mkurugenzi mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hotuba kali kutoka kwa mkurugenzi mkuu

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by mpalu, Aug 26, 2011.

 1. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Jamaa mmoja ambaye ni mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya mawasiliano alikaribishwa kutoa speech katika tamasha moja la vijana lililokuwa limeandaliwa kuhusu kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha maradhi ya kisasa..Speech ya mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo;

  "Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa ugonjwa huu ni mkubwa,mimi nashauri muwe makini.
  Jitahidini sana kukaa bila kupiga.

  Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si kupiga piga kwani hii gharama yake ni kubwa.Kama shida ya kupiga itakuwa kubwa, basi hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, na hivi vinapatikana kwa wingi na gharama yake si kubwa.

  Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata madhara yanayoweza kupatikana
  kutokana na mionzi iliyoko katika simu hizi za kisasa.

  Ni mwiko kabisa kupiga Voda kwa Voda kwani hii ina hatari kubwa mno. Pia unashauriwa kutopiga tigo kabisa kwani hii inaweza kuharibu kabisa mfumo wa mawasiliano ya simu yako.

  Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna hamu angalau ya kupibu, lakini hii nayo ni hatari, kwani mwenzako akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi sana kwako kuamua kupiga kabisa.

  Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu zitamaliza chaji, hii si kweli.Hakikisha tu kwamba simcard iko katika hali nzuri,hii ndio ina kumbukumbu zote na ndio inaongoza mawasiliano yote.

  Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana. Usidanganyike na simu kuwa eti ina Kamera au double skrini. Hizo ni mbwembwe tu.Kuna simu nyingi sana feki siku hizi zinauzwa zimevishwa cover mpya,usidanganyike.

  Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, tafuta sehemu inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia sana kwani simu ukitumia peke yako inadumu zaidi kuliko ile yenye subscribers wengi."

  AHNSATENI KWA KUNISIKILIZA!
   
 2. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  M.s.h.e.z.i. wewe ni noma kwani jinsi ulivyoitunga hiyo mistari utazani kweli, any way nitafanyia kazi ushauli wako ingawa sitoacha kupiga voda kwa voda, ingawa tigo naipenda zaidi
   
 3. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 3,951
  Likes Received: 1,650
  Trophy Points: 280
  ''Asante mkurugenzi''
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 36,361
  Likes Received: 14,638
  Trophy Points: 280
  haya bhana............
   
 5. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Aisee..ishamtokea mkuqugenzi kupiga ovyo hovyo nn
   
 6. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 6,906
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mmmmmmmmh! Hapa jamaa aliua kinoma, yaani kama wewe ni mbumbumbu unatoka kapa
   
 7. S

  SWASHBONGE New Member

  #7
  Aug 26, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Sawa mheshimiwa kwa speech nzuri, and da reporter kazi nzuri sana ya caught
   
 8. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inabidi akili ya ziada kuelewa.
   
 9. C

  Cognitivist JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 80
  This is what Great Thinkers need to do. Big up! Imekaa poa.
   
 10. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,506
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  mi naendelea kupiga tu, tena ntakuwa napiga tiGO zaidi, na simu yangu siweki kwenye kipochi.....
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,914
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ni ubunifu swafi kabisa.
   
 12. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,527
  Likes Received: 2,451
  Trophy Points: 280
  Watakuwa walitoka kapa.
   
 13. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,527
  Likes Received: 2,451
  Trophy Points: 280
  Mionzi haikuathiri????????????
   
 14. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  Vijana wengine wanatamba eti simu zao zimejaa chaji na zina uwezo wakupandisha mkungu wa ndizi mlima wa Kitonga huku akina mama wengine ukisikia milio ya simu zao inahita mpyampyamya kumbe ni screpa au used
   
Loading...