masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,880
- 13,164
Hili sakata la kutaka kufunga Hoteli ya Sugu huko Mbeya limeleta hisia nyingi.
Lakini baya zaidi ni lile la the dark side ya watu fulani ndani ya Serikali.
Serikali inaendeshwa na watu.
Na watu hao maafisa ndiyo waliotaka watumie mgongo wa Serikali kubomoa Hoteli hiyo.
Kwa wafanyabiashara tunajua kuna watu-maafisa, wenye mamlaka na wana wivu, au kinyongo na maendeleo ya wananchi, hasa wafanya biashara.
Nimeambiwa huko Mbeya kuna viongozi wa ajabu sana. Pengine Magufuli atembelee Mbeya kujionea vioja cha maafisa au viongozi wake.
Miaka ya 2017 uwekezaji wa maparachichi ulitiwa misukosuko. Mwekezaji mzalendo wa ufugaji samaki kule Tukuyu-Kiwira badala ya Serikali kumtia moyo, kupitia DED wakamfungia mradi karibia miaka miwili bila sababu za msingi. Waliposikia Magufuli anatembelea Mkoa wa Mbeya, wakamfungulia mradi.
Hili ni kielelezo cha watu ndani ya Serikali wenye roho mbaya, na ni mbaya kwa wawekezaji.
Watu wa aina hii wako wengi na idara tofauti kuanzia ma DED, TRA, NEMC, hata baadhi wakuu wa Wilaya.
Hili sakata la Hoteli ya Sugu ni kielelezo tosha cha Watu wasioitakia mema serikali ya Awamu ya Tano.
Maafisa hawa wana msimamo wa kukomoa wafanyabiashara au wawekezaji.
Serikali kupitia Rais anasema hili, wakati baadhi ya maafisa wa Serikali wanatekeleza matakwa yao.
Rais Magufuli kwa kweli inabidi aelezwe tu kwamba kuna wafanyakazi/maofisa ndani ya Serikali yake wanamhujumu.