Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099


Rais Mzalendo na anayejali wawekezaji leo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa tamko au salamu kuwa SUGU au Mbunge mstaafu wa Mbeya Joseph Mbilinyi ni muwekezaji hivyo atalindwa na hotel yake haitabomolewa na mtu yeyote.

Kulikuwa na uzushi mitandaoni kuwa hotel imejengwa kwenye uoto wa asili yaani pembezoni mwa mto hivyo kulikuwa na mpango wa kuibomoa.

Kwa ufupi Rais amesisitiza hilo eneo limepimwa na linafahamika,Watu wa mazingira yaani NEMC wanalifahamu vizuri.

Mkuu wa mkoa ameonyesha jinsi Sugu anavyolinda mazingira ya mto huo huku maji yakitiririka na kumiminika.

Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.

Maendeleo hayana chama

 
Akizungumza hotelini hapo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amedai kwamba amepata maelekezo kutoka kwa Rais wa Tanzania kwamba Hoteli hiyo isivunjwe kwa vile inavyo vibali vyote vilivyotakiwa kabla ya ujenzi wake na kwamba vyanzo vya maji vilivyopo karibu na hoteli hiyo havijaathirika , hivyo hakuna sababu yoyote ya kuhujumu hoteli hiyo .

Hotel ya Kisasa ya Desderia inamilikiwa na Joseph Mbilinyi aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini

Niliwahi kuweka uzi humu kuhusu jambo hili lakini ulifutwa kibabe bila hata kuupa nafasi ya kuomba maji ya kunywa , bali nilichojifunza ni kwamba UKWELI HAUFICHIKI , leo kiko wapi ?

sugu.jpg

 
Daniel mgogo ktk moja ya hotuba yake mbele ya John Joseph alipata kumwambiwa kuwa Serikali inatoa kubali eneo fulani kujengwe jengo fulani.

Serikali hiyohiyo inakuja kustuka kuwa alaah kumbe hapa tulipaswa kupitisha nyaya za umeme wanakuja kubomoa.

Akatoa ushauri kuwa ni vyema kuhakikisha unapotoa vibali ujue kabisa miaka 40 ama 50 mbele eneo hilo litakuwaje. Isije kuwa serikali ya kujenga na kubomoa na kulipana fidia.
 
Lipo wazi hilo visasi vyake huwa haviishi.

Hao hao nemc ndio waliotoa vibali vya ujenzi na ndio hao hao watakao jengo livunjwe. Wanaweza wakawa wanamkoa Sugu sawa atakaa kimya serikali nyingine ikingia anashtaki na anashinda analipwa fidia ya jengo plus faida ya KILA siku kwa miaka yote hio. Tuoneeni huruma Kodi zetu kwani ndizo zitakazotumika kuwalipa fidia wengi awamu ijayo sababu ya mkurupuko wa mtu mmoja tu asiye na uchungu na kodi zetu.

Maana serikali ipo awamu ndizo upita. Hata wa kimara watashinda kesi usione wamekaa kimya tu wanasubiria mwingine akiingia tu kesi zinafufuka Hawa watawala wanapita lakini haki za watu hazitopita asipolipa anaye atalipa mwingine.
 
Nemc hivi wanajielewa kweli ifike hatua mambo ya kipumbavu wasiwe wanatueleza.

Yaan mtu anunue eneo wanamuangalia tu aanze kujenga wanamtazama tu amalize ujenzi wapo tu then wanakuja kutueleza mtu yupo ndani ya hifadhi ya maji. Siku zote walikua wapi?

Na je, in afaida gani kuita vyombo vya habari na kutueleza hayo?

Sisi Watanzania wengine hatutaki ujinga huo wamalizane wenyewe huko.
 
Back
Top Bottom