Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Dawa nI Katiba mpya ili tupunguze nguvu za mtu mmoja laa sivyo atakuja mtu aseme achimbiwe Ziwa kijijini kwake
Katiba mpya haiwezi kuwa dawa kama hakuna watu wa kuilinda i.e. wananchi. Pamoja na ubovu wa katiba hii hii tuliyonayo bado kuna mambo au vifungu vizuri sana, lakini bado ameweza kuvikiuka na kufanya apendavyo kwa sababu hakuna wa kumuuliza. Hivyo hata ikiwepo katiba mpya nzuri sana ataikunjia mfukoni na atende atakavyo kwani anajua hakuna kizuizi.
 
Mkuu si uhamie Chato kama miradi inaenda huko sana hili ukanufaike pia maana yote ni Tanzania na una uhuru wa kwenda popote pale ndani ya mipaka ya nchi yetu.
 
Ndugu yangu vijana wa CCM huwa wanajenga hoja kama wamekatwa vichwa vimehifadhiwa kwenye masanduku Lumumba.
Ukisikiliza vilio vya wabunge pale Bungeni kuhusu shida zao majimboni, kisha tazama Rais anavyotumia nafasi yake kuelekeza miradi Chato kwake! Huyu mtu ni MBAGUZI na mwenye roho mbaya sana.
Nimetokwa na machozi !
 
Katiba mpya haiwezi kuwa dawa kama hakuna watu wa kuilinda i.e. wananchi. Pamoja na ubovu wa katiba hii hii tuliyonayo bado kuna mambo au vifungu vizuri sana, lakini bado ameweza kuvikiuka na kufanya apendavyo kwa sababu hakuna wa kumuuliza. Hivyo hata ikiwepo katiba mpya nzuri sana ataikunjia mfukoni na atende atakavyo kwani anajua hakuna kizuizi.

Ndio maana makamu wa Rais wa Zanzibar aliyeapishwa juzi ameweka wazi umuhimu wa kuwa na taasisi za umma zenye nguvu ili kulinda utawala wa sheria!!
 
Hayo mahotel yatageuka kuwa magofu mara tu atakapotoka madarakani.

Mtalii gani ataenda CHATO? Kwa lipi?
Tena kwa lipi? Maana duniani kote watalii wana kwenda kuona Kilimanjaro, Ngorongoro, Meru, Serengeti na Zanzibar tu! Wakienda Rwanda wanafuata hivyo, wakienda Malawi ni kuona Kilimanjaro tu! Chato wanafuata nini?
Hiyo hoteli ingejengwa Kilimanjaro au Arusha, kwa nini Chato?
 
Nilifikiri biashara ya hoteli wangewaachia watu binafsi wawekezaji badala ya TANAPA kujiingiza ktk shughuli ambazo siyo dhumuni kuu (core) la TANAPA.

Hii sasa imezidi, kila shirika au mamlaka za umma kushindana kutumia fedha za walipa kodi kupeleka kila kitu Chato.

Tujikumbushe shughuli zilizopelekea kuanzishwa kwa TANAPA na majukumu-msingi (core activities) za kuanzishwa TANAPA

Mission and Vision​


MISSION​

To sustainably conserve National Parks through innovative approaches for maximization of ecosystem services and optimizing tourism development for human benefits

VISION​

Sustainable Conservation of National Parks Resources and values for the benefits of mankind

Source: Mission and Vision |TANZANIA NATIONAL PARKS
 
Back
Top Bottom