Kwani tatizo ni rais kufungua hoteli? Huyu mwekezaji inaelekea alikuwa tayari na demolition order na ndiyo akataka kufanya usanii wa kujificha nyuma ya wigo wa "Hoteli imefunguliwa na Rais." Suala si rais kafungua hoteli, suala si mbona jirani hawajabolewa. Suala ni je amejenga ndani ya road reserve? Suala ni je alishapewa demolition order? Kuwa mwekezaji MZAWA hakumpi blank cheque ya kufanya atakalo. Kajenga parking kwenye sehemu isiyoruhusiwa na sheria imefuatwa. Asitake kutubabaisha.
Amandla.......
Ina thamani ya Shilingi bilioni 10
Tanroads: Ilijengwa barabarani
Baadhi ya wanakijiji wakisafisha mabaki ya sehemu ya mbele ya Hoteli ya Snow baada ya Wakala wa ujenzi wa Barabara Nchini (Tanroads), kuvunja sehemu hiyo mkoani Arusha jana.
Hoteli hiyo ilivyokuwa kabla ya kuvunjwa.
Hoteli ya kimataifa ya Snow Crest iliyojengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 10 imevunjwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Arusha, kwa maelezo kuwa imejengwa ndani ya eneo la barabara.
Tukio hilo limetokea siku mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua hoteli hiyo na kutoa wito kwa wafanyabiashara wazawa kuwekeza katika sekta ya utalii.
Tanroads ilishikilia msimamo kuwa ingeibomoa hoteli hiyo iliyopo eneo la Ngulelo, kandokando ya Barabara Kuu ya Arusha-Moshi, ikidai kuwa imeingilia eneo la barabara kinyume na sheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli hiyo, Wilfred Tarimo, akizungumzia tukio hilo, alisema wafanyakazi wa Tanroads walifika juzi usiku wa manane wakiwa na askari sita wenye silaha na tingatinga na kubomoa eneo la mbele na maegesho ya hoteli hiyo.
Nilipigiwa simu usiku na wasaidizi wangu kuwa hoteli inavunjwa, nilifika na sikuamini nilichokuwa nakiona kwa macho yangu, hoteli imevunjwa na kutokea kwa uharibifu mkubwa, alisema Tarimo.
Aliongeza kuwa tukio hilo lilisababisha wageni zaidi ya arobaini waliokuwa wamefikia hotelini hapo kupatwa na hofu ya kupoteza maisha au mali zao.
Mimi kama mwekezaji mzawa nilikuwa najitahidi kuwekeza katika utalii, nimeumizwa na kufedheheshwa sana na tukio hili, kila mwenye uwezo wa kufikiri anaweza kuwauliza Tanroads walikuwa wapi mpaka Rais azindue hoteli ndio waje wavunje?alihoji Tarimo.
Aidha,Tarimo alihoji ni kwanini hoteli hiyo tu ndiyo ivunjwe wakati kuna majengo mengine katika eneo hilo.
Akizungumzia tukio hilo aliyewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Arusha na Diwani wa Kata ya Baraa eneo ilipo hoteli hiyo, Paul Laizer, alihoji uhalali wa Tanroads kufanya zoezi la uvunjaji usiku alihoji: Kama kweli walikuwa wakifanya jambo la haki ni kwa nini walifanye zoezi hilo wakati wa giza kwanini wasifanye mchana kweupe, alihoji.
Chama cha Mawakala wa utalii kimepokea tukio hilo kwa masikitiko makubwa na kusema kuwa halikuwa la haki.
Katibu Mtendaji wa chama hicho, Mustafa Akuunay, alilisitiza kuwa Tanroads haikuwajibika ipasavyo na kwa wakati unaofaa na picha inayojitokeza inaacha maswali mengi yasiyo na majibu.
Akuunay alihoji ni kwanini hoteli hiyo ikalengwa na majengo mengine kuachwa.
Ni kwanini tingatinga limeacha majengo mengine na kuvunja hoteli pekee kuna nini hapa kinachofichwa, alisema.
Aidha alisema kuwa hatua hiyo itapunguza idadi ya watalii wanaozuru kaskazini mwa nchi na kuleta fedha za kigeni na ajira kwa Watanzania huku ikikatisha waazawa tamaa ya kuwekeza katika sekta hiyo.
Mgogoro wa hoteli hiyo na Tanroads umekuja baada ya wakala huo kudai kuwa imeingiliwa katika eneo lake ambalo linatajiwa kutumika katika upanuzi wa njia nne za barabara kati ya Arusha-Moshi katika siku zijazo.
Hali hiyo ndio iliyoifanya Tanroads kutaka uongozi wa hoteli hiyo kuibomoa kabla ya Novemba 10, mwaka huu.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Arusha, Desdatus Kakoko, alisema jana kuwa ataitisha mkutano na wanahabari kuelezea kuhusu sakata hilo.
Hoteli ya Snow Crest yenye hadhi ya juu, ina vyumba 83 na imeasisiwa na kumilikiwa na wafanyabiashara watatu wazawa.
Hata hivyo, haikuweza kufahamika ilikuwaje uongozi wa Mkoa wa Arusha kumruhusu Rais kufungua hoteli hiyo Ijumaa iliyopita bila kujua kuwa hoteli hiyo ilikuwa katika mgogoro na Tanroads.
CHANZO: NIPASHE
Niliuliza hivi karibuni kwamba Muungwana alikuwa anakwenda kuzindua hoteli moja arusha na kuhoji uhalali wa hoteli hiyo, au kama inahusiana na wale wanaotajwa kwa ufisadi. bahati mbaya thread ile sikuiona na sielewi kama ilihamishiwa kwingine. Sasa mambo ndiyo hayo tena, siku mbili tu baadaya sherehe za uzinduzi inabomolewa.
Hivi mamlaka zinazohusika zikuwa wapi mpaka hoteli hii inajengwa kwenye eneo la barabara, halafu wakasubiri imezinduliwa ndipo wakaibomoa? au ilikuwa inajengwa usiku na kuhamishwa asubuhi kiasi kwamba watu walikuwa hawaioni hadi ilipozinduliwa ndipo wakaiona?
Nadhani kuna walakini mahali fulani. Mwenye dondoo naomba atusaidie jamani. tunakwenda wapi tanzania.
Mkuu Jayfour.
Sio lazima uandike kimombo. Naona kiswahili kingeeleweka zaidi. JF =GT
Huo ndio ukweli wenyewe. Japo kuwa nchi inahiatji wawekezaji wazalendo kama hawa waliojenga hotel nzuri kama hiyo, lakini vile vile tunataka wawekezaji hawa wawe wanaheshimu sheria mbali mbali zilizowekwa na mamlaka za nchi yetu. Kwakuwa hawa walivunja sheria basi hapa sheria imechukua mkondo wake. Hata hivyo nawapa pole kwa hasara walioipata