Hoteli ya kitalii aliyozindua Rais Kikwete yabomolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoteli ya kitalii aliyozindua Rais Kikwete yabomolewa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by asha ngedere, Dec 22, 2009.

 1. a

  asha ngedere Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Ina thamani ya Shilingi bilioni 10
  [​IMG] Tanroads: Ilijengwa barabarani

  [​IMG]
  Baadhi ya wanakijiji wakisafisha mabaki ya sehemu ya mbele ya Hoteli ya Snow baada ya Wakala wa ujenzi wa Barabara Nchini (Tanroads), kuvunja sehemu hiyo mkoani Arusha jana.

  [​IMG]
  Hoteli hiyo ilivyokuwa kabla ya kuvunjwa.

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]  Hoteli ya kimataifa ya Snow Crest iliyojengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 10 imevunjwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Arusha, kwa maelezo kuwa imejengwa ndani ya eneo la barabara.
  Tukio hilo limetokea siku mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua hoteli hiyo na kutoa wito kwa wafanyabiashara wazawa kuwekeza katika sekta ya utalii.
  Tanroads ilishikilia msimamo kuwa ingeibomoa hoteli hiyo iliyopo eneo la Ngulelo, kandokando ya Barabara Kuu ya Arusha-Moshi, ikidai kuwa imeingilia eneo la barabara kinyume na sheria.
  Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli hiyo, Wilfred Tarimo, akizungumzia tukio hilo, alisema wafanyakazi wa Tanroads walifika juzi usiku wa manane wakiwa na askari sita wenye silaha na tingatinga na kubomoa eneo la mbele na maegesho ya hoteli hiyo.
  “Nilipigiwa simu usiku na wasaidizi wangu kuwa hoteli inavunjwa, nilifika na sikuamini nilichokuwa nakiona kwa macho yangu, hoteli imevunjwa na kutokea kwa uharibifu mkubwa,” alisema Tarimo.
  Aliongeza kuwa tukio hilo lilisababisha wageni zaidi ya arobaini waliokuwa wamefikia hotelini hapo kupatwa na hofu ya kupoteza maisha au mali zao.
  “Mimi kama mwekezaji mzawa nilikuwa najitahidi kuwekeza katika utalii, nimeumizwa na kufedheheshwa sana na tukio hili, kila mwenye uwezo wa kufikiri anaweza kuwauliza Tanroads walikuwa wapi mpaka Rais azindue hoteli ndio waje wavunje?”alihoji Tarimo.
  Aidha,Tarimo alihoji ni kwanini hoteli hiyo tu ndiyo ivunjwe wakati kuna majengo mengine katika eneo hilo.
  Akizungumzia tukio hilo aliyewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Arusha na Diwani wa Kata ya Baraa eneo ilipo hoteli hiyo, Paul Laizer, alihoji uhalali wa Tanroads kufanya zoezi la uvunjaji usiku alihoji: “Kama kweli walikuwa wakifanya jambo la haki ni kwa nini walifanye zoezi hilo wakati wa giza kwanini wasifanye mchana kweupe,” alihoji.
  Chama cha Mawakala wa utalii kimepokea tukio hilo kwa masikitiko makubwa na kusema kuwa halikuwa la haki.
  Katibu Mtendaji wa chama hicho, Mustafa Akuunay, alilisitiza kuwa Tanroads haikuwajibika ipasavyo na kwa wakati unaofaa na picha inayojitokeza inaacha maswali mengi yasiyo na majibu.
  Akuunay alihoji ni kwanini hoteli hiyo ikalengwa na majengo mengine kuachwa.
  “Ni kwanini tingatinga limeacha majengo mengine na kuvunja hoteli pekee kuna nini hapa kinachofichwa,” alisema.
  Aidha alisema kuwa hatua hiyo itapunguza idadi ya watalii wanaozuru kaskazini mwa nchi na kuleta fedha za kigeni na ajira kwa Watanzania huku ikikatisha waazawa tamaa ya kuwekeza katika sekta hiyo.
  Mgogoro wa hoteli hiyo na Tanroads umekuja baada ya wakala huo kudai kuwa imeingiliwa katika eneo lake ambalo linatajiwa kutumika katika upanuzi wa njia nne za barabara kati ya Arusha-Moshi katika siku zijazo.
  Hali hiyo ndio iliyoifanya Tanroads kutaka uongozi wa hoteli hiyo kuibomoa kabla ya Novemba 10, mwaka huu.
  Meneja wa Tanroads Mkoa wa Arusha, Desdatus Kakoko, alisema jana kuwa ataitisha mkutano na wanahabari kuelezea kuhusu sakata hilo.
  Hoteli ya Snow Crest yenye hadhi ya juu, ina vyumba 83 na imeasisiwa na kumilikiwa na wafanyabiashara watatu wazawa.
  Hata hivyo, haikuweza kufahamika ilikuwaje uongozi wa Mkoa wa Arusha kumruhusu Rais kufungua hoteli hiyo Ijumaa iliyopita bila kujua kuwa hoteli hiyo ilikuwa katika mgogoro na Tanroads.
  CHANZO: NIPASHE


  Niliuliza hivi karibuni kwamba Muungwana alikuwa anakwenda kuzindua hoteli moja arusha na kuhoji uhalali wa hoteli hiyo, au kama inahusiana na wale wanaotajwa kwa ufisadi. bahati mbaya thread ile sikuiona na sielewi kama ilihamishiwa kwingine. Sasa mambo ndiyo hayo tena, siku mbili tu baadaya sherehe za uzinduzi inabomolewa.
  Hivi mamlaka zinazohusika zikuwa wapi mpaka hoteli hii inajengwa kwenye eneo la barabara, halafu wakasubiri imezinduliwa ndipo wakaibomoa? au ilikuwa inajengwa usiku na kuhamishwa asubuhi kiasi kwamba watu walikuwa hawaioni hadi ilipozinduliwa ndipo wakaiona?
  Nadhani kuna walakini mahali fulani. Mwenye dondoo naomba atusaidie jamani. tunakwenda wapi tanzania.
   
 2. a

  asha ngedere Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli tunahitaji kujiangalia upya, vinginevyo tunaweza kushangaa mambo makubwa yanaibuka tukiwa hatujui kinachotokea.
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hapa kuna kitu kilichojificha siyo bure
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hakuna lolote jamani, mwenye hotel kajenga uzio ndani ya hifadhi ya barabara,
  na alishapewa taarifa na tanroads kwamba avunje, akaomba izinduliwe kwanza ndio atavunja.
  hivyo ilivunjwa sawa kabisa kutokana na makubaliano waliyofikia kati ya tanroads na mmiliki.
  period.
   
 5. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hii inaonesha wasaidizi wa Muungwana hawafanyi homework yao ipasavyo!! Ilikuweje wamruhusu mheshimiwa azindue hotel ambayo iko kwenye mgogoro na mamlaka za serikali???

  Hivi kabla ya viongozi wetu wakuu hawajatembelea sehemu mbalimbali kwa ajiri ya shughuli fulani due diligence huwa inafanywa?

  Huku ni kumfanya Muungwana kutumika kama rubber stamp na watu wasio waaminifu kwa masilahi binafsi.

  Ningelikuwa mimi ndo Rais basi wahusika wote cha moto wangekiona, hii Xmas ingekuwa chungu balaa kwao!!
   
 6. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huo ndio ukweli wenyewe. Japo kuwa nchi inahiatji wawekezaji wazalendo kama hawa waliojenga hotel nzuri kama hiyo, lakini vile vile tunataka wawekezaji hawa wawe wanaheshimu sheria mbali mbali zilizowekwa na mamlaka za nchi yetu. Kwakuwa hawa walivunja sheria basi hapa sheria imechukua mkondo wake. Hata hivyo nawapa pole kwa hasara walioipata
   
 7. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hivi itifaki ilizingatiwa kwa Mkulu kwenda sehemu yenye tatizo? dah hii inazidi kumharibia
  Afu kwanini anapenda kufungua fungua Hotel,ningempa pole kama angezindua Shule
  Ila kwa hilo nadhani ilipangwa apelekwe sokoni..
   
 8. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mod unganisha thread ziko nyingi
   
 9. Shukuru

  Shukuru JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa mi simulewi elewi nakumbuka alishasaini cheque feki.. sa sijui ni kimchezo au..... dah usijekuta bunge liko barabarabi....
   
 10. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  What was so special for him (Presida) to inaugurate the hotel considering that there is Mwangunga as a minister who dealing with tourist matters, the team what they did is to cheat teh man.

  I know nothing about system security but always his caravan accompanied by a number of personels (vijana wa kazi) waht do they always do? Is it their duty is only to seat somewhere and drink. We have to work seriously on the department like this one because failure to work properly on this department is going to cost us as a nation.
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwani tatizo ni rais kufungua hoteli? Huyu mwekezaji inaelekea alikuwa tayari na demolition order na ndiyo akataka kufanya usanii wa kujificha nyuma ya wigo wa "Hoteli imefunguliwa na Rais." Suala si rais kafungua hoteli, suala si mbona jirani hawajabolewa. Suala ni je amejenga ndani ya road reserve? Suala ni je alishapewa demolition order? Kuwa mwekezaji MZAWA hakumpi blank cheque ya kufanya atakalo. Kajenga parking kwenye sehemu isiyoruhusiwa na sheria imefuatwa. Asitake kutubabaisha.

  Amandla.......
   
 12. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ni kwa mwendo huo huo taifa linaonekana halieleweki linakokwenda na ni nani analipeka huko na kwa makusidi gani. Kwa uzembe kabila hii, kuna siku mkuu atapelekwa kuzindua soko la wauza mihadarati
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jayfour.

  Sio lazima uandike kimombo. Naona kiswahili kingeeleweka zaidi. JF =GT
   
 14. a

  asha ngedere Member

  #14
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndiyo maana nikauliza kitambo, ni hoteli ya nani hasa. yawezekana huyu jamaa ni geresha tu, kwa sababu angekuwa mwenzangu na miye mla ugali kwa kipande cha papa angekuwa amebomoa siku nyingi, asingeingia gharama ya kuizindua. lakini yaonekana pamoja na kuwa na demolition order, bado alikuwa na jeuri fulani, possibly kutoka mahali fulani, kwa watu fulani, kwa maslahi fulani.
  Mwenye nyeti za wamiliki wa hoteli hii hebu atumwagie. Mkuu GT, upo???
   
 15. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160

  Jambo hili nilishalisema awali. Hoteli hii nzuri kweli, lakini ina hadhi hiyo ya kwenda kufunguliwa na Rais? Mbona anachoshwa na vitu ambavyo havina uzito jamani?
  Pili, washauri wake wanamshauri nini katika maamuzi ya kufanya hiki au kile? Vitu petty petty anafanya Rais badala ya vitu vya maana, aah!
   
 16. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuna tetesi kwamba hiyo fence inajengwa upya, kama kuna ukweli hii imekaaje? nitapata proof baadaye kidogo maana nitakuwa napita maeneo hayo.
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwanza kuna upotoshaji katika habari hii. Kilichobomolewa inaelekea ni uzio na si jengo la hoteli yenyewe. Hoteli haijabomolewa.

  Amandla.......
   
 18. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #18
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Haya, basi na ninyi mliojenga barabarani, kule Michungwani, Kwedikwazu, Dumila, Kibaigwa, Chalinze, na kwingineko, nanyi mjiandae kwa nyungo kuu ya TANROADS, kwani nanyi mmejenga barabarani.

  TANROADS mnasubiri nini kuwabomolea watu hao? Kila tunaposafiri barabarani, kwenye mabasi au magari yetu binafsi, tunawaona... hata Korogwe mjini, nyumba kadhaa za kudumu zipo kwenye eneo la hifadhi ya barabara, mbona hazibomolewi?

  Kilichopelekea mpaka uzio wa Snow Crest Hotel kubomolewa USIKU ni nini? Kwani hawakuweza kusubiri kufanya kazi hiyo MCHANA kweupe, kama kweli sheria ilikuwa upande wao? Wakati hoteli ilipokuwa ikijengwa, TANROADS walishindwa nini kuweka "injunction" au "stop order" ili uzio huo usijengwe kwenye eneo la hifadhi ya barabara?

  Hakuna kingine! Chuki binafsi!

  Walikubaliana, ati mnasema? Haha! Walikubaliana UZIO UBOMOLEWE USIKU? Serikali gani inayofanya kazi USIKU? DAIMA NITASEMA UKWELI, mwenye kuchukia na achukie!

  TUACHE UNAFIKI!

  ./Mwana wa Haki
   
 19. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Suala tunataka sheria za ujenzi na barabara zizingatiwe. Hakuna cha Rais kufungua wala nini?? Kwanza wataalam wa Ras hawakuona tatizo hilo?? Na Je mwana usalama wa mkoa hakuwa na taarifa za uvunjaji huo wa sheria?? Tuache masihara. Bomoa kabisa Tanroad. Keepit up. Bomoa na nyinginezo ambazo hazitii sheria.

  Kuna sheria za umbali unatakiwa kujengwa kwa barabara kuu na zile za mitaa/vitongoji na ni lazima uzingatiwe. Tunakosa kuwa na mipango miji na ya miundo mbinu bora kwa sababu ya watu wachache. Tutii sheria na taratibu kwa maendeleo.
   
 20. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Inaonekana kuna kutunishiana misuli kati ya tanroad na mmiliki wa hotel hiyo. baada ya kubomolewa sasa anaujenga upya. may be kiburi cha fedha, may be ni agizo la wakubwa kwamba ujengwe tena, lakini meneja wa Tanroad mkoa wa arusha anasema lazima atauvunja tena. (lets wait and see)
   
Loading...