Hoteli ya ‘kigogo’ aliyekuwa MWENYEKITI wa CCM KILIMANJARO yapigwa mnada Moshi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Daniel Mjema

Posted Jumatatu,Juni3 2013 saa 21:46 PM

KWA UFUPI



  • Kabla ya kufanyika kwa mnada huo, madalali hao walitoa matangazo katika magazeti ya Daily News na Uhuru ya Mei 17,2013, wakiujulisha umma kuwa baada ya siku 14 wangeiuza hoteli hiyo.


Moshi. Mambo yamezidi kumwendea vibaya Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Vicky Swai kutokana na hoteli yake yenye ghorofa moja kuuzwa kwa mnada kwa Sh600 milioni.





Hoteli hiyo iliyopo kiwanja namba 89 eneo la Shanty Town mjini Moshi inayofahamika kama Kibo Executive Lodge, iliuzwa mwishoni mwa wiki ili kufidia deni la Sh350 milioni anazodaiwa na Benki ya CRDB.

Mnada wa kuuza hoteli yake hiyo ulifanyika Jumamosi iliyopita, ukiendeshwa na Kampuni ya Madalali ya Comrade Auction Mart Co Ltd ya jijini Dar es Salaam iliyopewa idhini hiyo na Benki ya CRDB.

Kabla ya kufanyika kwa mnada huo, madalali hao walitoa matangazo katika magazeti ya Daily News na Uhuru ya Mei 17,2013, wakiujulisha umma kuwa baada ya siku 14 wangeiuza hoteli hiyo.

Kampuni ya Charan Singh and Sons Ltd kupitia kwa mwakilishi wake, Agustino Rafael Mrema ndiyo iliyotoa ofa ya juu zaidi ya Sh600 milioni ambayo haikuweza kufikiwa na mnunuzi mwingine yeyote.

Swai amekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa Kilimanjaro kwa vipindi viwili mfululizo (2004-2008 na 2008-2012) na kabla ya hapo,alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Jumuiya ya Wanawake (UWT).

Mwaka jana hakutetea wadhifa wake huo lakini akagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) kupitia Wilaya ya Hai Mkoa Kilimanjaro, lakini kamati kuu haikurudisha jina lake.

Mumewe, marehemu Nsilo Swai alikuwa ni miongoni mwa mawaziri sita Waafrika waliounda baraza la mawaziri wakati Tanganyika inapata uhuru wake mwaka 1961 na yeye kuteuliwa Waziri wa Biashara.

 
Na Daniel Mjema Posted Jumatatu,Juni3 2013 saa 21:46 PMKWA UFUPI
  • Kabla ya kufanyika kwa mnada huo, madalali hao walitoa matangazo katika magazeti ya Daily News na Uhuru ya Mei 17,2013, wakiujulisha umma kuwa baada ya siku 14 wangeiuza hoteli hiyo.
Moshi. Mambo yamezidi kumwendea vibaya Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Vicky Swai kutokana na hoteli yake yenye ghorofa moja kuuzwa kwa mnada kwa Sh600 milioni.Hoteli hiyo iliyopo kiwanja namba 89 eneo la Shanty Town mjini Moshi inayofahamika kama Kibo Executive Lodge, iliuzwa mwishoni mwa wiki ili kufidia deni la Sh350 milioni anazodaiwa na Benki ya CRDB.Mnada wa kuuza hoteli yake hiyo ulifanyika Jumamosi iliyopita, ukiendeshwa na Kampuni ya Madalali ya Comrade Auction Mart Co Ltd ya jijini Dar es Salaam iliyopewa idhini hiyo na Benki ya CRDB.Kabla ya kufanyika kwa mnada huo, madalali hao walitoa matangazo katika magazeti ya Daily News na Uhuru ya Mei 17,2013, wakiujulisha umma kuwa baada ya siku 14 wangeiuza hoteli hiyo.Kampuni ya Charan Singh and Sons Ltd kupitia kwa mwakilishi wake, Agustino Rafael Mrema ndiyo iliyotoa ofa ya juu zaidi ya Sh600 milioni ambayo haikuweza kufikiwa na mnunuzi mwingine yeyote.Swai amekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa Kilimanjaro kwa vipindi viwili mfululizo (2004-2008 na 2008-2012) na kabla ya hapo,alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Jumuiya ya Wanawake (UWT).Mwaka jana hakutetea wadhifa wake huo lakini akagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) kupitia Wilaya ya Hai Mkoa Kilimanjaro, lakini kamati kuu haikurudisha jina lake.Mumewe, marehemu Nsilo Swai alikuwa ni miongoni mwa mawaziri sita Waafrika waliounda baraza la mawaziri wakati Tanganyika inapata uhuru wake mwaka 1961 na yeye kuteuliwa Waziri wa Biashara.
Watu wapate somo hapo sasa, yani hapo nikwamba tuko pamoja ila tukishaachana utajijua mwenyewe, nawengine wapate funzo hapo.
 
Huyu mama amekaa Marekani muda mrefu sana na watoto wake wako Marekani wameshindwa nini kulipa deni la mama yao? Ukisikia mwanzo wa kuugua kwa pressure ndio huo sasa.
 
Pole yake

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Sioni hasara kubwa ila naona mahesabu makali yankuuzwa hotel milioni 600 kwa deni la milioni 350 inayobakia anarudishiwa mama swai anaenda kufungua kitu kipya kwingine.

Au mawazo yangu ndio finyu kwenye hili?
 
Safiii safi sanaaaa!!!
Waache magamba waendelee kufilisiana tu.

Mama alikubali kutumiwa na CCM kama Condo.. na sasa wamemtupa kama takataka.
Hana mwelekeo wowote, sio ubunge wa viti maalum wala udiwani wa viti maalum.
Huyu mama ni kama Janeth Kahama alivyotupwa kama kinyesi na CCM.
Haya ndio matunda ya kina mama kuitumia CCM.

Chezea CRDB wewe!!!!
 
Huyu mama amekaa Marekani muda mrefu sana na watoto wake wako Marekani wameshindwa nini kulipa deni la mama yao? Ukisikia mwanzo wa kuugua kwa pressure ndio huo sasa.
Mkuu haijalishi kama watoto wapo marekani tu inawezekana wanabeba mabox kama lile gamba kris lukosi ili wapate kwenda choo tu......
Safi sana crdb mmelikomesha hilo gamba!!!!
 
kibo-executive-lodge.jpg
 
Huyu mama amekaa Marekani muda mrefu sana na watoto wake wako Marekani wameshindwa nini kulipa deni la mama yao? Ukisikia mwanzo wa kuugua kwa pressure ndio huo sasa.

Kuishi Marekani siyo kigezo cha kuwa na pesa! Siyo kila mtu anayeishi kwa Obama ako na pesa!
 
Mtafika mahala mtakubali tu kuwa riba ni haram, inayotesa hvo ni riba tu hyo.

Lakini kuna wengine ndani ya CULT ya CCM hawajalipa hiyo MIKOPO na ni ya CRDB Chama kimewakinga...
 
Back
Top Bottom