Hotel ya Ngurdoto yafafanua kuwatimua wafanyakazi wake 50

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Uongozi wa hotel ya kitalii ya Ngurdoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha wilayani Arumeru, umewatimua kazi wafanyakazi wake 50 kwa madai ya kushindwa kujiendesha , licha ya kwamba wafanyakazi hao wanaidai kampuni hiyo malimbikizo ya mishahara yanayofikia kiasi cha sh milioni 129.

Uamuzi huo umefikiwa Mei 3 mwaka huu kwa kuwakabidhi barua za kuwaachisha kazi, baada ya kampuni hiyo kukumbwa na changamoto za kibiashara ,hata hivyo wafanyakazi hao waligoma kupokea na kuzua taharuki wakishinikiza kulipwa kwanza Madai yao.

Hatua hiyo ilimlazimu mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro kukutana na wafanyakazi hao ,hotelini hapo akiwa ameambatana na maofisa kadhaa kutoka idara ya kazi, Takukuru na Mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF kwa ajili ya kusikiliza madai ya wafanyakazi hao.

Akiongea na wafanyakazi hao Muro alimtaka mwanasheria wa hotel ya Ngurdoto, Edmund Ngemela kusitisha barua hizo ili waangalie namna nyingine Sahihi ya usuluhishi juu ya mgogoro huo baina ya wafanyakazi hao na mwajiri wao.

Akiongea suala la kuachishwa kazi kwa wafanyakazi 50 wa hotel hiyo mwanasheria Ngemela alisema kwamba taratibu zote zilifuatwa baada ya mteja wake( mwajiri) kuona ipo haja ya kufanya hivyo kutokana na mwenendo mbaya wa kibiashara.

Wakili Ngemela aliongeza kwamba mteja wake amefikia uamuzi huo baada yakuwepo kwa changamoto za kibiashara na hivyo kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.

"Wafanyakazi walioachishwa kazi kutokana na changamoto za kibiashara watalipwa stahiki zao Ila walioacha wenyewe kwa kutofika kazini kwa mujibu wa sheria hawatalipwa" alisema Ngemela

Hata hivyo wakili Ngemela aliwasihi wafanyakazi hao kuacha kulalamika bali ambaye anaona kwamba hakutendewa haki katika maamuzi hayo afuate taratibu za kisheria kwa kupeleka malalamiko yake katika tume ya Taifa ya usuluhishi CMA.

Kuhusu Kauli ya mkuu huyo wa wilaya kufuta barua za kuwaachisha kazi wafanyakazi 50 alisema mkuu huyo hana mamlaka ya kisheria kushinikiza mwajiri asipunguze wafanyakazi wake na kuhoji kwamba nani atawalipa au yeye ndo atawalipa alihoji Ngemela.

Kwa upande wake meneja wa hotel hiyo ,Beatrice Dala's alisema kuwa kampuni hiyo imefikia uamuzi wa kupunguza wafanyakazi wake kutokana na changamoto za kibiashara zinazotokana na ugonjwa wa korona na migogoro ya wafanyakazi .

Alifafanua kwamba walioachishwa kazi ni 50 na wengine 13 wamejifukuza kazi wenyewe kwa kutofika kazini kwa muda wa zaidi ya siku tano Kama Sheria inavyosema.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Joan Mrema alisema mgogoro wa wafanyakazi pamoja na mahakama kuamuru baadhi ya Mali za mwajiri kukamatwa ni sehemu ya Changamoto zinazopelekea kushindwa kuendesha biashara kwa ufanisi .

Hata hivyo Joan alisisitiza kwamba wafanyakazi wote wenye haki ya kulipwa stahiki zao watalipwa bila shida yoyote na kuwataka wawe na uvumilivu kwa kuwa kampuni hiyo ipo kwenye mipango mizuri ya haraka itakayofanikisha malipo yao kuliko kutumia njia nyingine ya kudai haki yao.

Akijibu hoja ya mkuu wa wilaya hiyo kwamba kampuni hiyo imeajiri wafanyakazi wapya kumi wakati kuna madai ya wafanyakazi wa zamani ,alifafanua kuwa alilazimika kuongeza idadi ya walinzi kufuatia kuwepo kwa viashirio vya baadhi ya wafanyakazi kuhujumu Mali za hotel hiyo hasa nyakati za usiku

"Fedha kidogo tunazopata kutokana na wanafunzi wa chuo Cha uhasibu Arusha waliopanga katika hotel yetu tunatumia kulipa umeme,maji na mahitaji mengine muhimu hivyo hazitoshelezi kulipa madai ya wafanyakazi hapo"alisema

Mmoja ya wafanyakazi hao Christopher Mbote alimweleza mkuu huyo wa wilaya kwamba hawakubaliani na uamuzi wa mwajiri wao kuwaachisha kazi wakati bado wanadai malimbikizo ya mishahara.

Alisema kwa Sasa hawaruhusiwi kuingia ndani ya lango la hotel hiyo na hata kama mkuu huyo wa wilaya ataamuru warejee kazini huduma za usafiri na chakula zimesitishwa na hivyo kuwaweka katika mazingira magumu.

Hivi karibuni mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliamuru baadhi ya Mali za hotel hiyo kukamatwa na kupigwa mnada ili kufikia madai ya wafanyakazi 93 wanaodai malimbikizo ya mishahara kiasi Cha sh milioni 129.

Ends.......

IMG_20210507_155810_513.jpg
 
Hii ndio maana halisi ya "Asiyekuwepo na lake halipo"......sijui kama Marehemu Mrema anaona yanayoendelea huku alipopaacha.
 
Kimsingi Wakuu wa Wilaya hawana kazi za kufanya zaidi ya kufuja fedha za walipa kodi.
 
Huyu anatafuta naniliii
Kipato kimepungua mwendazake aliwawezesha kiaina
Kuna wakuu wa wilaya sijui mikoa ni shida elimu uelewa basi vurugu tu
Uchumi mgumu nini asichoelewa!
 
Muro ni janga la Taifa unafutaje umeambiwa hawezi kuwalipa? Baadhi mali zinauzwa ? Mpuuzi yeye anfekomaa walipwe stahiki zao zote kabla sign barua zao .....CMA sio option nzuri sababu watasota miaka 5 bila mia heri wambane sasa awalipe huko CMA watajuta...
 
Serikali ndio inetengeneza hili tatizo.

Mikodi kibao na kusumbua hoteli kipindi cha korona
Mwisho wa siku watafunga sasa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom