Hotel ya LIVERPOOL pale Mombo mnauza viporo??

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
3,246
5,756
Habari wana JF.
Natumaini hawa wahusika wa hii hotel watapata ujumbe huu....
Siku chache zilizopita nilisafiri kusherehekea pasaka kutoka dar kwenda moshi. Kutoka Ubungo tulifika Mombo saa nane kwa ajili ya chakula cha mchana, nikachukua chips na nyama choma kwa gharama ya shilingi 7000.
Kurudi kweye basi nilishtukia kile ni kiporo na sikula tena maana najua madhara yake na wengi ndani ya basi walilalamika sana.

Shida ilikuwa siku ya kurudi dar basi lilifika pale saa sita kasoro na kweli nilikuwa na njaa, nikaamua kuagiza aina nyingine ya chakula, nikala lakini nilipata taabu sana maana tumbo liliuma sana na nikagundua kilikuwa kiporo.
Pia abiria wenzangu walilalamika sana na kumuuliza dereva kwani lazima kupita hotel ile? NAWASHAURI KAMA MNAUZA VIPORO ACHENI MARA MOJA MAANA MTAUA WATU.

Na madereva muwe makini ipo siku nitapiga dereva nimvunje taya maana mtu nimezidiwa nataka huduma unanijibu mbovu, nakuvunja meno. Nilitaka kushuka mahali fulani ninunue dawa dereva akanizuia wakati yeye ndiye kanipitisha hotel ya kishenzi.
 
Nilidhani Mo sala katua Mombo... jamaa misosi wanauza bei za down town...
 
Hotelini hawamwagi chakula hata siku moja,

Usiulize jibu.


Unaposafiri beba chakula chako. Kaanga hata NYAMA uikaushe NUNUA soda take away ,maji Basi safiri.


Vyakula vya Hotellni BEI KUBWA HALAFU NI VIPORO HALAFU NI KIDOOGO.BEI HUWA 6/000= KUENDELEA.


Kupanga NI kuchagua.
 
Back
Top Bottom