Hotel aliyofikia Lema jijini Dar es Salaam yazingirwa na Polisi, alikuwa aongee na Wanahabari

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,628
218,059
Askari wa Polisi wamezingira Hotel aliyofikia Mikocheni, Dar es Salaam, wakimtafuta Waziri Kivuli wa Wizara ya mambo ya ndani na Mbunge wa Arusha mjini kwa sababu ambazo hazijajulikana. Mhe. Lema alikuwa azungumze na vyombo vya habari leo jijini D'Salaam kumjibu DPP

Polisi hao wenye silaha, wasiokuwa na sare za Polisi, wako ndani ya gari na wengine mapokezi ya Hotel ya Regency Park. Wamelazimisha uongozi wa hotel ufungue chumba cha Godbless walivyojibiwa ni kinyume cha taratibu, wamewaonya wafanyakazi iwapo hawatampata Mbunge huyo.

======

Habari za asubuhi? Mkutano wa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema (Mb) na waandishi wa habari, umeahirishwa, hivyo hautafanyika leo, kwa sababu amelazimika kuanza safari kuelekea Singida kwa kupitia Arusha kwa dharura. Tutawataarifu waandishi wa habari siku ambayo Lema atafanya press conference, kuhusu suala hilo. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote. Asante.

Makene
 
Inabidi CHADEMA wabadilishe utaratibu kuhusu kuzungumza na Vyombo vya Habari.

Waanzishe Kitengo Maalumu kitakachokuwa na kazi ya kurekodi SAUTI na VIDEO za Mikutano yote ya Chama na wapakie YouTube huko.

Media house zikafuate information huko.

Ila kwa mwendo huu, watahengwa sana na Serikali hii ambayo haipendi free-speech za kisiasa.
 
CCM wanashida aisee...Huku wanadili na Corona Kule wanadili na CHADEMA..?

Ndio maana Rais anachoka aisee!
Corona hakuna bongo.we jiulize mtu hajui kama anaumwa alafu anajiweka chumbani mwenyewe ajue kama ana corona. Ingekuwepo kweli hata magu asingefanya mkusanyiko barabarani jana. Na hawa polisi wasingekuwa wanafanya ujinga wa kiwango hicho. We ngoja iingie kweli utaona kama kutakuwa na UPUMBAVU wa namna hii.
 
Back
Top Bottom