Hostel za bei nafuu jirani na Nairobi Hospital

watown

Platinum Member
Sep 25, 2016
45
27
Habari zenu wana JF, poleni na majukumu,

Naombeni kwa yeyote anayefahamu hosteli iliyoko jirani na Nairobi hospital aniambie, nauguza mtoto sasa gharama za hoteli ziko juu na hostel.

Ninayoifahamu hapa ni Flora hostel ya masister na yenyewe naona gharama ziko juu sababu wanacharge ksh 3300 per day.

Msaada wenu wa haraka wakuu unahitajika.
 
Wakuu msaada jamani pesa zenyewe za matibabu zamchango naona kama zitaishia kwenye malazi sasa
 
Nairobi city center maisha ni ghali mnoooo . Yaani hotel za beI rahisi zinaanzia 3500 kwenda juuu . Na ukitaka kukaa sehemu za maaana ndio balaa kabisa . Bila 15000 kwenda juu hulalii. Unless otherwise uende kulala Isilii kwa wasomali
 
Mkuu sogea maeneo ya River Road - unaweza kupata Hoteli za 1500-2500 hivi. Zitakupunguzia hayo makali kidogo.
 
River road ni umbali gani kutoka hospital,naweza kwenda hata kwa mguu maana hawa watu wa boda na tax wakishajua wewe ni mtz na gharama wanaongeza.
 
Kuna matatu ya kwenda eastleigh kutoka hapo city Centre yanapaki hapo karibu na makumbusho ya kenya tena huko Kuna wasomari vyakula vya kitanzania vipo na usafiri hata usiku saa tano upo na alfajiri saa 11
 
Ulizia matatu halafu sio mbali kutoka city Centre unaweza tembea kutoka maeneo ya Hilton hotel mpaka huko 20 to 30 minutes tu ukafika
 
Sasa wenger matatuu za huku naona zinaenda kinamba zinazoelekea huko ni namba ngapi?
 
Sorry mimi pia sio mkenya nilikaa huko mwaka jana baada ya kuona hostel za Nairobi university garama halafu tuvyumba tudogo. Niliamua kwenda mtaani .Fika hapo maeneo ya Ghana Avenue ulizia magari ya kwenda Eastleigh kumetulia huko .Kuna hospital inaitwa kimweni maternity hospital maeneo hayo utapata sehemu nzuri kabisa
 
Asante sana kaka
 
River road ni umbali gani kutoka hospital,naweza kwenda hata kwa mguu maana hawa watu wa boda na tax wakishajua wewe ni mtz na gharama wanaongeza.

Unaweza kwenda na Matatu tu - ndio stendi za matatu zilipo - na zinapital hapo Nairobi Hospital.
 
Makonda wa Daladala zao waungwana sana utafika sio mbali toka mjini ni sawa na kutoka Magomeni kwenda Posta mpya tu
 
Habari zenu wana JF, poleni na majukumu,

Naombeni kwa yeyote anayefahamu hosteli iliyoko jirani na Nairobi hospital aniambie, nauguza mtoto sasa gharama za hoteli ziko juu na hostel.

Ninayoifahamu hapa ni Flora hostel ya masister na yenyewe naona gharama ziko juu sababu wanacharge ksh 3300 per day.

Msaada wenu wa haraka wakuu unahitajika.
budget yako ni kiasi gani mkuu?
 
Back
Top Bottom