Hostel mpya UDSM zina hadhi ya chini sana! Huwezi linganisha na 'white' houses za UDOM

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Jana nilifanikiwa kupata aerial view ya zile hostel mpya zilizogharimu bilioni kumi, kweli nilisikitika sana kwa tule tujengo tolivyokaa kama nyumba za Tembe maarufu sana mikoa ya kanda ya kati kama Singida.

Nikasema pengine ni wivu wangu binafsi juu ya jitihadi hii, nikaona ngoja nijaribu kuzilinganisha na majengo ya hostel za UDOM! Kwa kweli hazikuweza kufua dafu hata kwa asilimia hamsini...

Ninachowashukuru mkandarasi wa TBA ni kuwa anakupa kulingana na kadri ulivyonunua.

Ninapongeza jitihadi za Mheshimiwa Rais katika kutatua changamoto za malazi UDSM ila ninamuomba tena mheshimwa, next time wakiingia awamu ya pili, angalau apande dau ili UDSM wapate vitu vya maana zaidi...

MABWENI-UDSM-20.jpg
dom1.jpg
 
Huwa nakasirika sana nikisikia mtu anasema hizo hostel za udsm gharama yake ni bil. 10, hakuna mtu yeyote anayeweza kujenga hizo hostel kwa hiyo hela, kinachonisikitisha zaidi nikuona mtu tunayemwamini na anayesema siku zote msema kweli ni mpenzi wa Mungu naye anashiriki kutudanganya hadharani bila haya usoni, wangetuambia tu ukweli wa kiasi cha pesa kilichotumika hapo, hakuna mtu ambaye haoni umuhimu wa hizo hostel na wote tunawapongeza kwa hilo ila wawe wakweli kwenye kiasi kilichotumika, wasijichukulie credibility kisiasa kwa mambo ya uongo, wanaweza kupata credibility hata kwa kusema ukweli tu.
 
Hostel za UDOM ni habari nyingine...
mpaka serikali imekwenda kuomba hifadhi ya muda katika safari yao ya kuhamia Dodoma...
we jiulize kwanini wasiende pale CBE MIPANGO St.John HOMBOLO...
pale wachina walifanya kazi...
Twende Mbele Turudi nyuma UDOM wana hostel nzuri pasina mfano..
Na hazita tokea pengine
 
Back
Top Bottom