Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
HOSPITALI ya Tengeru (Patandi) Wilaya ya Arumeru inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa vitanda hali inayosababisha wagonjwa kulala zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja.
Hayo yamebainika wakati wa kukabidhi vyandarua vilivyotolewa na wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) tawi la Arusha kutokana na michango yao ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
Wakizungumza na FikraPevu mara baada ya kupokea msaada huo, wagonjwa hao wamesema wamekuwa wakipata tabu mara wanapoandikiwa kulazwa, kwani wanabanana na mara nyingi wanakosa vitanda, hivyo kulazimika kulala chini.
Habari zaidi => Hosptali ya Tengeru yakabiliwa na uhaba wa vitanda | Fikra Pevu