Hosptali ya Palestina Sinza huduma mbovu kwa wagonjwa, Waziri wa Afya shitukiza muda huu ujionee.

ngoshaboy

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
231
193
Wanajamvi,

Kwa haya ninayoyaona ni dhahiri serikali inayo kazi kubwa ya kuboresha huduma, ni masaa manne sasa tangu nikabiziwe kadi ya kumwona Dr lakini sijabahatika kwani Dr mwenyewe hakai muda mrefu chumbani anatoka kila wakati.

Wanajamvi taifa bado linahitaji viongozi wakali zaidi kwa haya ninayoyaona hapa haki ya Mungu wagonjwa wanateseka sana.
 
Masuala kama haya yako chini ya wizara ya tamisemi ama wasiliana na DMO wa wilaya atakusaidia hili haliko chini ya waziri wa afya tupunguze kumpa mzigo waziri wa afya sasa kweli hata hospital za mtaa nazo aje waziri
 
Wanajamvi,

Kwa haya ninayoyaona ni dhahiri serikali inayo kazi kubwa ya kuboresha huduma, ni masaa manne sasa tangu nikabiziwe kadi ya kumwona Dr lakini sijabahatika kwani Dr mwenyewe hakai muda mrefu chumbani anatoka kila wakati.

Wanajamvi taifa bado linahitaji viongozi wakali zaidi kwa haya ninayoyaona hapa haki ya Mungu wagonjwa wanateseka sana.
Wasiliana na uongozi wa wilaya yako kuna migawanyo ya kazi na ndio maana kila wilaya ina DMO na kila mkoa ina RMO sasa ngazi zote hizo zimeshindwa mpaka waziri aje
 
Wanajamvi,

Kwa haya ninayoyaona ni dhahiri serikali inayo kazi kubwa ya kuboresha huduma, ni masaa manne sasa tangu nikabiziwe kadi ya kumwona Dr lakini sijabahatika kwani Dr mwenyewe hakai muda mrefu chumbani anatoka kila wakati.

Wanajamvi taifa bado linahitaji viongozi wakali zaidi kwa haya ninayoyaona hapa haki ya Mungu wagonjwa wanateseka sana.
Ngazi zote mkuu umeshindwa kufuata mpaka unakimbilia kwa waziri hizi hospital ziko chini ya wilaya mzeee unataka waziri atembelee hospital za mitaaa. Acheni kumbebesha mizigo waziri bwana acheni apambane na madawa kwanza hili ongea na mkuu wako wa wilaya ama mtendaji wa kata yako atakusaidia
 
ili kupunguza hayo matatizo kunatakiwa kuwe na namba za simu za DMO au RMO kwenya hayo maeneo
 
ili kupunguza hayo matatizo kunatakiwa kuwe na namba za simu za DMO au RMO kwenya hayo maeneo
Sawa lakini sio suala linalohusu elimu hata kama ni la afisa elimu wa kata lazima waziri wa elimu aje so kwa suala hili tujaribu kuwasiliana ama kupeleka haya matatizo kwa wahusika wetu
 
Hospitali ya Palestina Sinza jamani haipo chini ya Wizara ya Afya.......hapo ni TAMISEMI...kwahiyo Mh. Simba Chawene..au Mkuu wa Mkoa na Wilaya wa eneo husika.....
 
Muda wa mawaziri kushtukiza umepita,wamerudi maofisini Kufanya Kazi.Hadi sasa wamegundua Ngoma ni nzito,On call allowance hazijalipwa Kitambo... Watumishi wanalipwa Vijiweni.
 
Waziri hausiki hapo mkuu wapo wa kuwajibika sinza hapo ummy umemuonea kabisa
 
Back
Top Bottom