Bandugu,
siku chache zilizopita - nilikwenda hospitali ya mikocheni kwa ajili ya matibabu. Kutokana na dalili nilizokuwa nazo daktari alishauri nipime vipimo mbalimbali ikiwemo kipimo cha sukari. Kipimo cha sukari kilionyesha nina sukari 16.5, yule lab technician akashtuka kweli akaniuliza kama nina tatizo la sukari, nikamwambia hapana sijawahi kuwa na hilo tatizo. Pia akaniuliza umeshakula? ni kamwambia of course nimeshakunywa chai maana muda huo ulikuwa ni kama saa sita hivi mchana, akasema hebu ngoja tupime tena ambapo majibu ya mara ya pili yakaonyesha ni 14.2 basi akaniambia ndio hivyo kisukari kina kunyemelea hivyo nenda kwa daktari akakupe ushauri.
Kufika kwa daktari akaniambia hii sukari sio nzuri lakini kwa kuwa nimeshakula, niende kesho yake asubuhi kabla sijala kitu chochote tupime tena tuone ikoje ndio tuamue ufanye nini. Nikaandikiwa madawa mengine kwa ajili ya vilivyoonekana kutokana na vipimo vingine nilivyopima nikaondoka zangu.
Kesho yake asubuhi niliamkia mjini kwa shughuli zangu zingine na nikaamua kwenda Burhani kupima, kwa kuwa nilishaambiwa nisile kitu, ni kawa kweli mtiifu sikula kitu chochote. Majibu yakaonesha sukari ni 5.4, na daktari akanieleza kuwa hii ni sawa haina tatizo. Lakini out of curiosity nikasema ngoja nirudi pale pale mikocheni nikapime tena bila kula kitu chochote. Kufika wakanipokea vizuri wakanipima na majibu yakaonyesha sukari ni 15.0. Yule mpimaji akaniambia majibu ni hayo una kisukari. Duu nikamwambia hii inawezekanaje? Nikamweleza scenario yote kuanzia ya jana yake (mpimaji hakuwa yule aliye nipima jana yake) na nikamuonyesha majibu ya burhani. Nikamwambia mi nafikiri hii mashine yenu ni mbovu, akasema haiwezekani hizi mashine hazitoagi majibu ya uongo, unless labda kama kuna mtu alikosea strips sijui etc (aliniambia maneno ya kitaalam kidogo). Lakini akasema ngoja ajipime na yeye aone majibu yatakuaje. Alipofanya hivyo majibu yake yakasoma 11.5 akasema kweli kuna kitu sio sawa hapa ikabidi amuite in charge ambapo wakawa wanajiongelesha hapo, wakijaribu kufikiria what could be the issue, pia wakagusia kwamba wakati mwingine mashine za kupimia huwa hazifanani. To cut a long story short, tulikubaliana kuwa niende tena nikapime hapo tuone majibu yatakuaje. Bado sijaenda tena (mambo yaliingilia but nitafuatilia)
My take;
- kwa madaktari/lab technician - je inawezekana majibu yakatofautiana kutokana na aina ya kipimo kinachotumika?
- mimi nafikiri mashine yao ni mbovu - wataalamu nisaidieni kama kuna any explanation to this variation if we rule out ubovu wa mashine.
NB; Nasisitiza kuwa vipimo vya siku ya pili nilivifanya nikiwa sijala kitu chochote.