Madaraka Amani
Member
- Mar 9, 2011
- 89
- 17
Ndugu zangu wana JF, juzi nilipatwa na tatizo la kuuguliwa na mtoto wangu mchanga wa miezi sita. Ugonjwa unaomsumbua hadi saa ni kuharisha na kutapika. Siku hiyo mtoto alikumbwa na tatizo kuanzia saa sita usiku alitapika na kuharisha mfululizo hadi ilipofika saa kumi usiku tulilazimika kumpeleka katika Hospitali iliyojirani (hospitali ya rufaa) kwa matibabu kwa sababu daliili zilikuwa mbaya. Tulipofika mapokezi tulimkuta dada mmoja aliyekuwa amelala usingizi tukamuamsha kwa kujivuta sana alituandikia cheti kazi ikaanza wapi alipo daktari tukamuomba huyu dada utueleze wapi alipo daktari akatuelekeza tuende chumba cha sindano huko tutamkuta nesi ambaye ataenda kumtafuta daktari mtoto alikuwa anaendelea kutapika na kuharisha. tulipofika huko dada wa chumba cha sindano akasema huyo dada wa Reception ndio anapaswa kuwaitia daktari tukarudi mapokezi dada wa reception akatuambia mimi ninaumwa rudini chumba cha sindano nurse akawasidie daktari sijui alikuwa wapi.tukarudi chumba cha sindano Yule nurse nafikiri kwa utu uzima wake na kuliona tatizo tulilokuwa nalo akaamua kuingia kusikojulikana kumsaka dakatari.hadi akampata yaliyofuata unaweza kulia naomba niishie hapa. swali langu mi kwamba tufanyeje watanzania kuondoa aina hii ya uzembe hivi ni wagonjwa wangapi wanafia mapokezi kutolkana na mazingira haya ya uzembe, hivi Mitaala ya vyuo vyetu vya ma nurse na madaktari hawana somo la namna ya kuhandle emergency, mbona nchi za wenzetu wana ethics za namna ya kushughuikia dharura. hali hii hadi lini? Watamzania tumelogwa na nani tukamuombe msamaha na kama amekufa tukatambikie. haya sio mazingira ya kawaida kwani hata mtu asiye na dakatari huwa n ahuruma tufanyeje watanzania.