Hospitali za Tanzania na huduma ya emergency madaktari wetu wamelogwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali za Tanzania na huduma ya emergency madaktari wetu wamelogwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Madaraka Amani, Oct 4, 2011.

 1. M

  Madaraka Amani Member

  #1
  Oct 4, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wana JF, juzi nilipatwa na tatizo la kuuguliwa na mtoto wangu mchanga wa miezi sita. Ugonjwa unaomsumbua hadi saa ni kuharisha na kutapika. Siku hiyo mtoto alikumbwa na tatizo kuanzia saa sita usiku alitapika na kuharisha mfululizo hadi ilipofika saa kumi usiku tulilazimika kumpeleka katika Hospitali iliyojirani (hospitali ya rufaa) kwa matibabu kwa sababu daliili zilikuwa mbaya. Tulipofika mapokezi tulimkuta dada mmoja aliyekuwa amelala usingizi tukamuamsha kwa kujivuta sana alituandikia cheti kazi ikaanza wapi alipo daktari tukamuomba huyu dada utueleze wapi alipo daktari akatuelekeza tuende chumba cha sindano huko tutamkuta nesi ambaye ataenda kumtafuta daktari mtoto alikuwa anaendelea kutapika na kuharisha. tulipofika huko dada wa chumba cha sindano akasema huyo dada wa Reception ndio anapaswa kuwaitia daktari tukarudi mapokezi dada wa reception akatuambia mimi ninaumwa rudini chumba cha sindano nurse akawasidie daktari sijui alikuwa wapi.tukarudi chumba cha sindano Yule nurse nafikiri kwa utu uzima wake na kuliona tatizo tulilokuwa nalo akaamua kuingia kusikojulikana kumsaka dakatari.hadi akampata yaliyofuata unaweza kulia naomba niishie hapa. swali langu mi kwamba tufanyeje watanzania kuondoa aina hii ya uzembe hivi ni wagonjwa wangapi wanafia mapokezi kutolkana na mazingira haya ya uzembe, hivi Mitaala ya vyuo vyetu vya ma nurse na madaktari hawana somo la namna ya kuhandle emergency, mbona nchi za wenzetu wana ethics za namna ya kushughuikia dharura. hali hii hadi lini? Watamzania tumelogwa na nani tukamuombe msamaha na kama amekufa tukatambikie. haya sio mazingira ya kawaida kwani hata mtu asiye na dakatari huwa n ahuruma tufanyeje watanzania.
   
 2. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah...pole sana....magamba on action
   
 3. l

  luckman JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  hili suala litaondoka tukiwa na watu wanaojua maana ya kazi, hawa watu ni wazembe ila wahusika wanashindwa kuchukua hatua ndo maana uzembe unaongezeka, uongozi legelege huwezi kuleta huduma iliyo bora kamwe, mimi mwenyewe rafiki yangu aliugua malaria ikapanda kichwani, tulimpeleka pale chuo udsm, usku saa nane, hali yake mbaya tena sana lakini dk kumpata ilikuwa kwenye saa tisa na wala hakuwa mbali bali chumba cha jirani katoka na mijasho yako hata hatukuelewa alkuwa nanafanya nini,sindano alikuja chomwa saa kama tisa tukaenda legency hospital, kwa hiyo kaka haya mambo yapo ila ndo matunda ya watawala wenu,lazima tuwe na viongozi wanaojua maana ya uongozi nini , wanaoweza kuwajibisha watu wanaposhindwa kutimiza majukum, waliofanikiwa lazima wameyafanya haya!nawasilisha!
   
 4. N

  Ndole JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi nafikiri sasa hivi inabidi kila mtu anunue secret camera ili ikitokea la kutokea atoe ushahidi vizuri. Inasikitisha sana ukimrudia huyo receptionist atakuruka futi mia na kwamba alikuonesha daktari.
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Oct 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Nadhani na maslahi madogo kwa madaktari wetu ndio yanayosababisha yote haya. Mfumo wa utendaji katika serikali yetu unatakiwa kubadilika, tena kuanzia katika ngazi ya familia.
   
 6. l

  lumimwandelile Senior Member

  #6
  Oct 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  pole dada. inabidi 2015 tuwachague CHADEMA labda hali inaweza ikabadilika katika HOSPITALI zetu
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ambao ni hopeless kuliko tulichonacho
   
 8. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Tatizo bongo ni Politicians zaidi ndo serikali inawajali zaidi. Solution = Kipaumbele kifutwe kwa wanasiasa.
   
 9. regam

  regam JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inabidi tuunde tume kuchunguza tatizo hilo!
  Mkiambiwa tubadilike mnakataa. Hili ni tatizo la ststem nzima kuanzia kwa raisi na watendaji wooote.
   
 10. Gajungi

  Gajungi Senior Member

  #10
  Oct 5, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mungu atusaidie tuwe madaktari wawajibikaji.
   
 11. l

  luckman JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mbopo kwetu waropokaji!nadhani jina liko sahihi kwako! Hivi wewe utasemaje chadema hopeless?umewapa jukum gani wakashindwa kudeliver hadi uwahukumu?tunaongea mambo ya maana unaropoka!hopeless ni nani sasa ambao hawajashika madaraka na hatujaona uongozi wao au waliopo kwa zaidi ya miaka 50 alafu hospitali zinaendeshwa kifara kama tunnayoyaona! Hapa hata tuwape miaka 100 hakuna lolote litakalofanyika bila kuleta mawazo mapya kwenye uongozi!wakati mbopo unalopoka huku ushakura pesa za walalahoi kuna watu wanafiwa na wagonjwa mapokezi, njiani, na wengine wodini kwa kukosa huduma stahiki!hii yote ni kutokana na mfumo legelege toka kwa uongozi legelege! Hii iko wazi mifano ni mingi tena sana na hata vichaa wanaelewa sana kuwa huu ni uongozi legelege!
   
 12. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  pole sana,inatakiwa uwasisitize watoto wako na wadogo zako wote wakasomee health sciences,ipo siku uhaba utapungua! Daktari anashida sana kwa sabb anadeal na uhai ndo maana analaumiwa,mbona wengine hawalaumiwi? Kuna wau wanaachaga folen za watu wakiwasubiri yeye anaenda kula bila kujali? Daktari alijua kwamba hiyo emergence itakuja? Ndo maana wanaitwa ON CALL Dr! Waoneeni huruma jamani,working 24hrs mshahara wenyewe duni,mazingira ya kazi duni. These ar pple like u! Kusomea mambo ya afya hawajaondoa ubinadamu wao wa kukosea muda mwingine!
   
 13. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mnaweza kupitia pia thread hii Vyuo vikuu Tanzania: Kwa nini customer care mbovu? Vinatoa Mfano gani? katika Habari na Hoja Mchanganyiko.
   
Loading...