Hospitali za taasisi za dini zatajwa kugushi madai ya Bima ya Afya

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,464
2,000
HOSPITALI za Taasisi za kidini, zimedaiwa kuwa mstari wa mbele katika kudai malipo hewa ya Mfuko wa Bima ya Afya, jambo linalosababisha kuwepo kwa changamoto katika utekelezaji wa huduma zinazotolewa na mfuko huo (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoani Kilimanjaro.


Meneja wa Bima ya Afya mkoa wa Kilimanjaro, Fidelis Shauritanga, ameiambia FikraPevu leo Mei 21, 2014 kuwa mfuko huo upo katika mchakato wa utoaji elimu kwa wadau walio katika Kata za Manispaa ya Moshi mkoani humo ili kutatua tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu.


Soma zaidi - Hospitali za taasisi za dini zatajwa kugushi madai ya Bima ya Afya | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 

Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,133
2,000
Hilo swala ni kweli nami nimeliona sehemu kadhaa, wengine hutumia mbinu ya kuwapa wagonjwa dawa za bei nafuu ilihali wamewaandikia dawa au huduma za bei ghali kwenye fomu za bima kwa kuwa wanajua zinafanya kazi ileile. Ila ni mchongo wa hospitali nzima, kuanzia uongozi hadi wafanyakazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom