Hospitali za REGENCY na TUMAINI zimulikwe!

Hali ni mbaya jamani kwenye Hospitali zetu, nakumbuka nikiwa chuoni like 2 yrs ago tulimpoteza mwenzetu ambaye alikuwa na maleria kali wakampiga kwinini bila kushusha homa na kumcheki presha. alikuwa kichwa sana drsni.

.
Wabongo hufa na tai shingoni, kuna dhana kwamba mtu akipelekwa kwenye hosp za kulipia inaonyesha eti yuko juu. Ni sawa tu na ulimbukeni wa dhana ya zuzu fulani kwamba kifo cha kugongwa na gari aina ya mercedizi benz kina hadhi kuliko cha kugongwa na toyota corolla. Tunatakiwa kwa kupitia organisation zinazoshughulika na masuala ya uraia na haki za watu kuibana serikali kutoa maelezo ya kwanini pamoja na kukusanya kodi za watanzania mil 40 inashindwa ku-maintain matibabu ya asilimia moja tu ya hao watu. Na badala yake inategemea mteremko kwenye hosp za mission kana kwamba kuna kodi zinazokusanywa na hazi taasisi za kidini au za kibinafsi.Shame on you ccm government!!
 
Pole sana wafiwa. Ni masikitiko makubwa sana kumpoteza kijana mdogo kama huyo, ambaye angekuwa msaada mkubwa kwa taifa.

Kuna kitu inaitwa ''informed consent'' na mtu yeyote huwa anasaini kabla ya kufanyiwa operation..bahati mbaya watu huwa wanamwaga wino tu hata bila kusoma kilichoandikwa. Hayo mambo yote huwa yanakuwa yameorodheshwa i.e risks and unexpected outcomes za operation..death being one of them. Sitetei uzembe unaoweza kufanyika during the procedure, lakini vilevile inabidi kuelewa kuwa such cases huwa zinatokea... mtu mzima kabisa, anapewa anaesthetic drug then anapata cardiac arrest, hata ulaya inatokea. Sina statistics za Hospitali ya Regency, kama kuna case nyingi za aina hiyo, then kuna tatizo ktk utendaji, but all in all inabidi mjue kuwa operation yoyote haina garantii ya kufanikiwa 100%.

Pole sana wafiwa. Ombeni postmortem report ili ukweli ujulikane nini lilimsibu marehemu.
 
Mimi nilidhani kwa hospitali za private maarufu kama Regency haya mambo hakuna! Tutakimbilia wapi?
 
.
Wabongo hufa na tai shingoni, kuna dhana kwamba mtu akipelekwa kwenye hosp za kulipia inaonyesha eti yuko juu. Ni sawa tu na ulimbukeni wa dhana ya zuzu fulani kwamba kifo cha kugongwa na gari aina ya mercedizi benz kina hadhi kuliko cha kugongwa na toyota corolla. Tunatakiwa kwa kupitia organisation zinazoshughulika na masuala ya uraia na haki za watu kuibana serikali kutoa maelezo ya kwanini pamoja na kukusanya kodi za watanzania mil 40 inashindwa ku-maintain matibabu ya asilimia moja tu ya hao watu. Na badala yake inategemea mteremko kwenye hosp za mission kana kwamba kuna kodi zinazokusanywa na hazi taasisi za kidini au za kibinafsi.Shame on you ccm government!!

Serikali inapeleka Kodi huko ktk Hospitali za Mission...Uliza wahusika.

mambo ya Benzi na Corolla ndio kwanza kukusikia...!!!
 
Regency Hospital (pamoja na Tumaini Hospital jirani hawa) ni hospitali zinazoendeshwa kienyeji sana.
Rgency ilikuwa nafuu lakini sasa inaanza kudorora kwa kasi.
Siri ya kutoperform hospitali hizi ni kwa sababu karibu mabingwa wote ni wa kuazimwa toka muhimbili na hospitali zingine.
Mabingwa hawa hawana seriousness katika kazi zao hapo mahospitalini.
Sasa hivi wagonjwa kupoteza maisha imekuwa kama mchezo, mimi nilipoteza shemeji yangu pale Tumaini miezi minne iliyopita(wakati wa Easter).
Daktari alikataa kuja kumwona mgonjwa mpaka akafa, kisa yuko shamba!
Sheria lazima ziangaliwe ili hospitali na daktari mhusika washitakiwe kwa makosa ya kitaaluma.
 
Mimi
mwezi April,nilipoteza Dada yangu ambaye tulimpeleka hapo hospitali anatembea mwenyewe ilikua Alhamisi na usiku wa kuamkia Jumapili nilipigiwa simu kuwa moyo ulisimama ghafla akifanyiwa operation ya dialysis. Hii hospitali inamatatizo makubwa hatujajua kuna nini hapa.

EEEHHH!!???
hapana bana, hakuna OP ya aina hiyo...
hebu kaulizie tena ilikuwa operation ya nini.
Figo?
 
Nakubali Regency kuna uzembe fulani hapo. Namfahamu mgonjwa fulani wa figo (RIP), alifanyiwa dialisis hapo kwa muda wa mwezi tuu, akajikuta ameambukizwa magonjwa ya ajabu, akapelekwa India kufanyiwa transplant, kufika kule, akaambiwa it was too late, dialisis waliokuwa wakimfanyia ilikuwa na contermination, there was no way back, alirudishwa kwenye sanduku!.

Nikatamani ningekuwa na uwezo, kufanya utafiti, ni wagonjwa wangapi wa dialisis ya Regency huwa wanasurvive.

Dialysis ni kubadilisha damu yote kwenye mwili wa binadamu kwa kutumia mashine maalum ili kuisafisha na kuirudisha mwilini.

Hata baada ya kutokea vifo vinavyosababishwa na uzembe, madaktari, wanalindana. Hii issue ya kijana, inaenekana walizidisha dose ya anaesthesia. Postmortem wataandika, mortar brain failure, iliyopunguza heart pulse iliyopunguza blood supply kwenye brain iliyosababisha brain demage na hivyo kusimamisha figo na kusababisha kifo. Ukichunguza zaidi, unaweza ukakuta hata hiyo appendix haikuwa chanzo!.

Absolutely!

hapo kimbembe ni kwa Anethesiologist na nurse wake waliokuwa theatre siku hiyo.
Kila ishara inaonekana walimzidishia kipimo cha nusu kaputi, matokeo yake dawa ikawa sumu.

Wanandugu hapo hakuna kazi ya mungu, ni uzembe tu huo ambao mkiwakalia kidedea mnaweza kulipwa fidia nzuri sana iwe fundisho kwa kina Dr Patel.
Charges za Regency kubwa mno, na ukiangalia makampuni mengi yanatumia AAR kwa treatments hapo.
Lazima wawajibishwe hawa, vifo vingi vinatokana na uzembe kama huu, wao wanafichiana siri.
 
Tunakosa REGULATORY BOARDS kwenye huduma muhimu sana za AFYA na ELIMU. Badala yake tumeunda haraka boards hizi kwenye simu( TCRA), daladala(SUMATRA) na dizeli( EWURA). Nilimsikia JK akiahidi kuunda ile ya elimu wakati tayari kuna TEA ambayo ingepewa nguvu za kisheria tu.
Chagua Slaa upozwe machungu!!
 
depends na pesa zako

Kama unazo zakutosha bora uende Muhimbili uhonge upate huduma bora...lakini wale mbu ndio watakufaidi
Unichekesha kweli.. sikuhizi madactari wa muhimbili ni kama Trafic police !! hospitali hii madactari inabidi waanze kuwajibishwa
 
Huo ni zembe mkubwa sana wala sio siri.
Lakini ukifatilia kwa ukaribu kuna makosa mengi tu yanayoweza kusababisah hicho kifo cha kijana
1.amekuja kama emergency na inaonekana hawa madakitari hawakuwa hata na mda wa kufanya pre-operative preparations,yaani kuchukukua baadhi ya vipimo amabavyo nivya mhimu kama vya moyo,figo,ini etc. ili hata kama likitokea lolote basi wanakuwa katika safe position ,lakini je walifanya?
watajiteteaje kuwa moyo ulisimama kwa matatizo mengine kama sio overdosage of anaesthesia?
kama walifanya preoperative check up basi wanaweza kuwa na back-up ,but which kind of back up? maana kama vipimo vilionyesha kuwa anamatatizo kama ya moyo basi ilikuwa ni lazima watoe taarifa kwa ndugu ili hata wanapo sign watambue kwa lolote lile.
2.Ni wazi kuwa huu ni uzembe mkubwa ni ni aibu sana kwa uzembe kama huu kufanyika katika hospital kama hii ambayo tunasikia ni hospital bora tz..mmh kumbe ni ubabaishaji tu.
3.Wizara lazima ifikie wakati wawe na sheria kali za kuwa bama wauguzi kwenye medical tangle or malpractice, kama sivyo basi tutaendelea kuona vifo kila siku ambavyo vinaepukika kabisa.
Kwa nini wizara iko kimya tu? wanafanya nini?
4.Hawa ni mmoja au wawili waliotoa tarifa au walio na uelewa kutoa taarifa kwenye media ,je ni wangapi ndugu kama mimi waliofanayiwa vitendo kama hoivyo na hawakutoa taarifa? au hawakujua kama ni makosa ya madaktari? au walisema basi ni kazi ya Mungu?
Kuna kazi ya Mungu lakini pia kuna vifo vingine ni uzembe kabisa wa mwanadamu.
5.Mwisho wizara lazima ianziwe Insurance coverage for doctors/nurses etc so that they will be accountable for compensation.
 
Kuna madaktari wenye asili ya kiasia katika hospitali ile vyeti vyao na weledi kwa ujumla una walakini.Wahusika wafuatiliei,kuna wadanganyika wengi wapoteza uhai kwa uzembe huu.Idara inayoshughulikia kina mama wajawazito yupo mmoja.Ni hatari sana kwa wiki ambayo mgonjwa wangu alikaa pale kina mama wajawazito saba waliharibu mimba zao kwa sababu za kizembe kabisa.Mimi sio professional gyna,lakini niliyajua yote hayo baada mgonjwa wetu kuzidiwa.Huyo muasia gynaceologist wa pale akasema muhamisheni mgonjwa wenu mimi siwezi kumshughulikia tena.Thank god,Tumaini walitupokea,ingawa tulimkosa mtoto lakini mama aliponea tundu ya sindano.
Nilipomuuliza yule gyna wa Tumaini kulikoni?akaniambia kulikuwa na kasoro nyingi za kiutendaji katika kumshughulikia mgonjwa wa hali ile pale Regency.
 
Pole sana sio wewe peke yako unayetaabika na ile hospitali, wananchi wengi hivi karibuni wamekuwa wakiilalamikia!
 
Hata baadhi ya waswahili wanaofanya pale ni vihiyo, ni wale jamaa wenye diploma za pale Tumbi Kibaha lakini wanajiita 'dr', mambo yakikaribia kubumburuka ndipo wanaita daktari kutoka Muhimbili.
 
Nakumbuka mama watoto wakati ni mjamzito nilimpeleka hapo kwa ajili ya clinic akaja kupata tatizo ambalo nusura nimkose mwanangu kama sio daktari mmoja kunipa namba za simu za daktari bingwa wa gyn. nilipompigia akaniambia nimhamishie mgonjwa wangu muhimbimbili fast track kwa kweli huduma aliyoipata kutoka kwa yule daktari na jinsi ambavyo alivyomsimamia yule daktari alikuwa tayari wakati wowote nikiwa na tatizo nikimpigia simu kama kunatatizo lolote kama ni usiku basi atakuwambia nimpeleke mke wangu muhimbili nikifika nimjulishe na nikifika utakuta kashapigasimu na atatoa maelezo vipimo gani vichukuliwa na matokeo ya vipimo na nini kifanyike. kwa kweli namshukuru kwani pamoja na matatizo aliyokuwa nayo mke wangu lkn alikuja kujifungua salama na mtoto sasa ana miaka mitano siku alipojifungua mke wangu nilimpa hella kama ahsante kwa moyo wake kwa sababu ya furaha niliyokuwa nayo kwani nilikwisha kata tamaa. Na ndio maana alipofariki huyu daktari siku hiyo sikujizuia kwa machozi kwani alikuwa zaidi ya daktari kwangu alishakuwa kama daktari wa familia yangu kwa ushauri mbalimbali aliokuwa akinipa taifa lilipoteza daktari mzuri sana na Mungu amlaze pema peponi Amina Ni daktari ambaye sitamsahau kwa utu na uzalendo wake na hasa uwezo wake wakugundua mimba ya mke wangu ina matatizo kwenye wiki ya 30 kwa kushika tu tumbo ijapokuwa aliomba tupige Ultrasound na matokeo yakawa kama alivyofikiria na kuchukua hatua za haraka za kumfanyia Operation(CS)
Mungu akurehemu na akujaalie pepo na akufutie madhambi yako , kila jema ulilofanya akulipe mara 70 na akujaalie pepo hakika sintokusahau ulikuwa zaidi ya Daktari kwenye familia yangu ijapokuwa nilikufahamia kazini kwako Leo una mwaka wa tatu tangu ututoke

kufurahisha huyu Dr. wa pili aliyekuwa rafiki yako hapa muhimbili naona naye anafuata nyendo zako na mungu amuongoze kwani naye ni mwema sana kwangu na anaijui kazi yake

Nakumbuka siku ile ulivyoniambia madaktari wazuri wako Muhimbili ambako wamesoma kwa kodi zenu hivyo watumieni
 
Roho inaniuma sana aisee. Two months ago, Baba angu alijiskia vibaya, tukampeleka Hindu Mandal hospitali akiwa anatembea mweyewe, tukaingia kumuona daktari, akamfanyia vipimo mbalimabli na kubaini ni malaria tu hivo akashauri apewe mapumziko kidogo ili baada ya muda aanze dozi ya malaria. Akapewa dozi ya malaria na wakaamua kumlaza.
Asubuhi tukaenda kumuangalia Baba, tukamkuta yupo kitandani hawezi kuongea wala kunyanyuka ikabidi tumuite daktari mmoja wa kihindi pale ili atupe maelezo kamili, wakatuambia tutoke nje wamfanyie vipimo tena, baada ya muda wakatueleza kuwa baba amepata stroke na hivo ameparalize, roho iliniuma sana kumona baba anapata matatizo sababu ya uzembe wa madaktari kutofanya vipimo mapema kubaini matatizo. Na mpaka sasa hivi baba angu hawezi ku-move, nashkuru mungu kwamba anaweza kuongea japo kwa tabu
 
Uchunguzi unahitajika kufanyika, maana it seems sheria zipo loose sana, na wanatumia upenyo huo kufanya wanavyotaka.
 
WAO wanapima malaria na mafua INDIA na Marekani,kazi kwa mdanganyika,ZINDUKENIIIIIIIIIIIIIII
 

Mnamo saa moja jioni ndugu zake ikiwamo mama yake na kijana waliitwa na kuelezwa kuwa kijana anashindwa kuaamka kutoka kwenye usingizi mzito baada ya upasuaji na kwamba wanahaingaika kumuamsha.

hali iliendelea hivyo mpka siku ya pili na kuendelea. Cha kusikitisha hakukuwa na jitihada madhubuti za kumsaidia mtoto aamke. baada ya ndugu kuja juu ndipo walipoelezwa kuwa moyo wa mtoto ulisimama wakati wa upasuaji hivyo kuathiri ubongo wake na hatimaye figo zake kushindwa kufanya kazi bila kutoa sababu za moyo kusimama
.

source :MICHUZI

Poleni sana kwa wafiwa,
Ajali za Nusu Kaputi (General anaesthesia) huweza kumtokea mgonjwa yoyote hata kama kuna vifaa vya kisasa na madakitari waliobobea. kwa nchi zilizoendelea vifo vinavyotokana na nusukaputi ni wastani wa kesi 1 kati ya operesheni 10,000, kwa nchi kama yetu (health resource restricted countries) ajali hizo ni nyingi zaidi. Ajali kama za aina ya anaphylaxis/allergy (mzio) ya dawa ya usingizi inaweza kumtoa roho mgonjwa hata kabla hajafanyiwa upasuaji, au mtu anapoteza maisha kwa ka-operesheni kadogo kama kutairiwa au kupasuliwa jipu, ktk hali kama hiyo jamii hutuhumu wahudumu kuwa wameua kwa uzembe (negligent conduct au deliberate misconduct).
Wahudumu wa afya ni binadamu kama wengine, ambao kila kukicha wanaombea siku ipite bila mgonjwa kumfia katika himaya yake.
 
Poleni wahanga wote wa huduma mbovu za afya hapa nchini. Binafsi ninaelekeza lawama zote kwa serikali kwa kuacha suala la afya za wananchi wake kuwa la kibiashara kama njugu. Watanzania, tunahitaji mabadiliko hapa nchini vinginevyo wananchi wengi watapotea kwa uzembe tu wa serikali wa kuruhusu huduma za afya kuendeshwa kiholela.
 
Back
Top Bottom