TECHMAN
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 2,651
- 1,125
Mnamjumbuka yule ally sahaf..comic ally..chemical ally wa Iraq?
Ndio tunamjumbuka, kwahiyo? au nayeye alikuwa Doctor? nayeye aligoma? nayeye posho yake ilikuwa ndogo? nayeye alikuwa mbongo?
Mnamjumbuka yule ally sahaf..comic ally..chemical ally wa Iraq?
Hoja yako ni nzuri, tatizo
Wanajamvi!
Mimi si daktari au mbunge ila ni mwananchi wa kawaida tu katika maisha ya kawaida sana!
Ninashindwa kuwaelewa wale wanaosema "MUUOGOPENI MUNGU" huku wakielekeza kauli hii kwa madaktari tu! Kwani anyepaswa kumuogopa Mungu ni daktari pekee na sio mafisadi wanaoimaliza nchi yetu kwa kula fedha za umma kiasi cha kusababisa watu kufanya kazi katika mazingira HATARISHI! Ninapata uchungu kwa kuona watu wanapoteza maisha, lakini hali hii haisababishwi na madaktari ila MAFISADI!
Kwa mtazamo wangu ieleweke kwa sasa taasisi yoyote pindi ikatokea wanafanyakazi katika mazingira hatarishi lazima mgomo utatokea. Siombei bali ikifikia nchi jirani inataka kuishambulia Tanzania kwa kipindi hiki, basi hata WANAJESHI nao watagoma kupigana kwani mazingira yao yatakuwa HATARISHI!
Sijui nani ana haki ya kutomuogopa Mungu katika nchi yetu hii ambayo watu wanajineemesha kwa rasilimali za umma?
Ndugu yangu KENGEMUMAJI! Sijapinga ulilosema ila nimeona nami nitoe yaliyomo moyoni mwangu.............................
PIGANGOMA
Nasikitishwa na mwenendo wa viongozi wa serikali....
Itapendeza kama watarudi kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya maslahi ya nchi.