Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
Afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema kuwa pamoja na barua waliyoipokea toka kwa madaktari bingwa kwamba na wao wamesitisha utoaji huduma, Hospitali hiyo bado haijafungwa kama baadhi ya wananchi wanavyoposha na kueneza taarifa ambazo si sahihi.
Alisema kuwa huduma zinaendelea kutolewa na madaktari wachache waliopo na kusisitiza kuwa kamwe Hospitali hiyo haitafungwa katika kipindi hiki cha mgomo wa madaktari.
Binafsi nilipita katika Hospitali hiyo jana majira ya saa 9 alasiri na kushuhudia uchache wa watu katika barabara na korido za Hospitalini hapo tofauti na tulivyozoea.
Source: Radio One asubuhi hii.
My take: Chonde chonde madaktari wakati kamati ya bunge ya huduma za jamii ikisikiliza madai yenu, rudini kazini mkaokoe maisha ya watanzania wenzetu.