Hospitali ya Taifa Muhimbili yajibu hoja za Wana JamiiForums kuhusu vifo Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila

Usitake kuharibu mada ,jiekeze huko hizi tuhuma zipo humu muda tuache siasa chafu ,tuungane na jpm kufichua maovu


State agent
Yaani michango ya rambirambi ya marehemu umeila Sasa unataka na fidia ya kifo Cha marehemu uwe na huruma na marehemu jamani.Marehemu angejua hili angejigomea kufa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ni hospital za rufaa, majibu mepesi ya asilimia kwa vifo ni kuficha ukweli,

Wale Wahanga wa ajali ya moto Morogoro wote waliisha, na majibu yakawa : Wale waliungua 100%, je, wakati wa kuwapakia kwenye helicopter haikujulikana?

Je, upasuaji aliofanyiwa Tundu Lisu ungefanyika hapo, angeendelea kuwa hai leo (Angepona) ?
 
Nilisikia wagonjwa walioungua moto Morogoro na kuhamishiwa Muhimbili walikufa wote.

Lakini kuna siku rais alikuwa kanagawa miburungutu ya pesa kwa maiti zile.

Hao nao wamo kwenye hizo asilimia?!

Hizi takwimu zimeruhusiwana NBS au Mzee Museru kaaamua kujilipua?!

Na je Ummy atazikubali hizi takwimu au yatakuwa yake ya Mwale Malechela?!

Niliwahi kusikia Rais aikisema mwenye mamlaka ya kutoa takwimu ni waziri pekee sasa huyu senior Museru ataachwa kweliau ndio muda wake umeisha hivyo?!
 
Ukiwa wafikiria kama great thinker watakiwa uanze kwa kufikiria aina ya wagonjwa wanaoenda Mloganzila. Watanzania wengi wakienda hospitali ujue wako terminally ill, na hospitali huwa kama sehemu ya wao kufia.
Mloganzila ukihamishiwa wameshaona wewe si wa kupona unapelekwa pale ukamsubirie Israel.
 
Mbona mie naona takwimu ni za mwaka 2018?
Hamna takwimu recently za mwaka 2019?
Naimani Mloganzila wanatumia electronic medical records inayoweza hata kutoa taarifa ya robo ya Oktoba - Desemba 2019.
Wapi tunakwama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
weye propesa wacha bujanjabujanja! nani atakubali hayo majibu ya kuandikiwa, Waziri Ummy tafadhali unda tume huru ichunguze swala hili, ni nyeti sana kwa maisha ya watu! Ni muhimu kurejesha heshima ya hiyo nembo ya taifa kwenye tasnia ya huduma za afya nchini, hospitali kubwa kama hiyo kuitwa "Vingunguti" ni aibu kubwa sana kwa taifa!
 
Idadi ya wagonjwa wanaopelewa imeongezeka maradufu ila idadi ya vifo inapungua!!
 
asitudanganye watu wanakufa sana, sasa hao madaktar 52 ukiwagawa kwa shift tatu unakuta kwa shift ni madaktar 20 hv, alafu namba ya wagonjwa ipo pale pale (wao wamepungua kutoka 52 hadi 10 na kitu) sasa hapo vifo lazima viwepo tu
 
cha kufanya serikali itoe ajira na isomeshe wanafunzi wengi wanaotoka form 6 haya mambo ya kubania wasome watu wachache mwisho wa siku tunapoteza ndugu zetu
 
Absolutely true! na sasa hiyo form six ya PCB "kila" mtu anapata AAA! , BBB, AAB etc in this range. This was unthinkable in the 70s and 80s! Sasa uchafu mtupu unakwenda Muhimbili and other rubbish medical schools!
Angalia mtihani wa mwaka jana wa Biology eti ni form six!
View attachment 1313942View attachment 1313943View attachment 1313944View attachment 1313945
Mkuu acha kutudharau tuliofanya hii paper, mimi niliambulia D hapa. Ingawa kuna paper 2 na 3 hujaziweka hivo hatuwezi kulinganisha uwiano na ugumu wa mtihani mzima.
 
Back
Top Bottom