TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI KWAMBA WAGONJWA WENGI WANAPOTEZA MAISHA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MLOGANZILA.
Dar es Salaam. 06 Januari, 2020
Kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Jamii Forum ambazo bila kuchanganua zinatuhumu kwamba Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inasababisha vifo kwa wagonjwa. Uongozi wa hospitali unapenda kuwahakikishia Umma wa Watanzania kwamba habari hizi si za kweli na hazitoi picha halisi ya huduma ambazo zinazotolewa hospitalini hapa. Takwimu tulizonazo zinaonyesha kwamba wagonjwa wanaotibiwa MNH-Mloganzila wameongezeka katika makundi yote.
Wagonjwa wa nje wameongezeka kutoka 17,115 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba, 2018 kufikia wagonjwa 25,493 katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2019 ambalo ni ongezeko la asilimia 48.8. Aidha, wagonjwa wanaotibiwa na kulazwa wameongezeka kutoka 1,459 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba, 2018 na kufikia wagonjwa 2,795 katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2019 ambalo ni ongezeko la asilimia 91.6.
Wakati huo huo idadi ya vifo (mortality rate) ikipungua kutoka asilimia 14.9 iliyokuwepo katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba, 2018 na kufikia asilimia 10.4 katika kipindi cha Julai-Septemba 2019. Aidha, takwimu za MNH-Upanga zinaonyesha kwamba katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba 2018 wagonjwa waliolazwa walikua ni 12,375 ambapo kulitokea vifo 1,000 (mortality rate) ambayo ni asilimia 8.1. Vilevile katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019 MNH Upanga ililaza wagonjwa 17,230 na kati ya hao vifo vilikua 1,673 ambayo ni asilimia 9.7(mortality rate).
Hivyo basi takwimu kati ya MNI-1-Mloganzila na MNI-1-Upanga za asilimia ya wagonjwa waliofariki hazitofautiani sana ambapo MNH-Upanga ni asilimia 9.7 wakati ni asilimia 10.4 katika robo ya Julai — Scptcmba, 2019. Hatua hii inaonyesha juhudi ambazo zinafanyika za kuboresha utoaji wa huduma katika Mloganzila zinazaa matunda. Moja ya sababu ambazo imeelezwa na mtoa taarifa kwamba Madaktari wanaotoa huduma MNH-Mloganzila ni wanafunzi waliopo katika majaribio si za kweli, hivyo tungependa kufafanua kwamba Hospitali ya MNH-Mloganzila ina Madaktari Bingwa 52, Madaktari wa kawaida 50 na kwa sasa ina Madaktari tarajali 53.
Licha ya Madaktari Bingwa hawa walioajiriwa 1VINH-Mloganzila kutoa huduma lakini pia wanashirikiana na Madaktari Bingwa kutoka MNH-Upanga katika kutoa huduma hapa MNH-Mloganzila. Vilevile hospitali hii ina madaktari wawili waliobobea wenye hadhi ya Profesa kutoka Korea nao wapo wanatoa huduma. Hivyo sio kweli kwamba madaktari ambao wapo mafunzoni wanafanyakazi bila usimamizi kwani hospitali imeweka utaratibu wa kila mgonjwa anayefika kupata huduma anaonwa na Daktari Bingwa kwa ajili ya maamuzi.
Wakati uongozi wa hospitali ukifanyia kazi tuhuma na malalamiko yaliyotolewa juu ya utoaji huduma katika taarifa hii, tunapenda kuutarifu Umma kwamba tangu MNH ipewe dhamana ya kusirnamia hospitali hii, turnejielekeza katika kutatua changamoto zilizokuwepo katika utaaji huduma na kwa kiasi kikubwa imeonyesha mafanikio ambayo yanaonyesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa na pia kuna ushuhuda wa wagonjwa ambao wametibiwa na kuridhika na utoaji wa huduma zetu.
Tunawahakikishia Watanzania kwamba huduma zinazotolewa katika Hospitali ya MNH-Mloganzila zimeboreshwa na tunawakaribisha Watanzania wenye jukumu la kuelimisha jamii waje kuzungumza na wataalam na waone jinsi huduma zinavyotolewa ili waweze kutoa taarifa sahihi kwa jamii.
Imetolewa na
Prof. Lawrence Museru
Mkurugenzi Mtendaji,
Pia soma
1) Rais Magufuli, ukiwa unatoka Chato pitia Hospitali ya Mlonganzila iliyobatizwa Vingunguti
2) Mloganzila yakanusha juu ya taarifa za vifo vya wagonjwa
3) Haya yanayosemwa kuhusu Hospitali ya Mloganzila ni kweli?
MAONI YA WADAU NJE YA JF (Social Media):.

Nilianza kuisikia zaidi Mloganzila mwakajana, wakati ndugu yangu akiwa amelazwa hapo. Naye hakuishi tena.
Kwa sasa kuna ndugu yangu anatibiwa hapo. Amefanyiwa upasuaji mara 3, hakuna mabadiliko makubwa. Siamini kuwa inatokana na ukubwa wa tatizo, uwezekano mkubwa ni huduma ya kiwango cha chini.
Majengo tulijengewa na Wakorea Kusini, ni mazuri, yanapendeza. Vifaa tiba navyo ni msaada, na vimejaa sana.
Baada ya kufuatilia kwa wataalam wa pale Muhimbili, taarifa nilizopewa na maprof. watatu tofaiti, ni kuwa hatuna wataalam wenye uwezo wa kuvitumia vifaa tiba vya kisasa vilivyopo pale.
Hata huyu prof. aliyeitoa hii taarifa, kama utakutana naye kama mtu binafsi, hatakosa kukuambia ukweli wa tatizo la Hospitali ya Mloganzila.
Bahati mbaya serikali yetu inaamini tuna uwezo wa kila kitu. Hatuna mipango ya kuwapeleka watu kwenda kujifunza nje ya nchi.
Jitihada kubwa zilizofanywa na Rais Kikwete mpaka kupata msaada huu mkubwa toka South Korea, zimeshindwa kufikia matarajio yake.
Ukweli ni kuwa:
HOSPITALI YA MLOGANZILA INA VIFAA TIBA VINGI VYA KISASA AMBAVYO MADAKTARI WETU HAWANA UWEZO WA KUVITUMIA.
Kama serikali itaendelea na huu utaratibu wa kuzuia watu kwenda kusoma nje, yaliyopo Mloganzila, msitarajie yatabadilika.
Hizi takuwimu wamezipika, simshauri mtu yoyote kupeleka mgonjwa wake muhimbili unless imeshindikana kabisa kupata huduma sehemu nyengine, chance ya ku-survive nasubutu kusema ni less than 1%, si hospital ni execution chamber.
Yamenitokea kwa wagojwa wangu 3, mmoja ameenda kwa maradhi mengine amekufa kwa maradhi mengine yaliosababishwa na either wauguzi au madoctor, mwengine alifariki emergency department after awaiting more than 30 hours bila kupata huduma, mwengine alifariki njiani kuelekea nyumbani after just one hour after being discharged from the hospital eti amepona, hao wote are closed related to me.
nukija kwa marafiki na majirani case ni nyingi JF hapatoshi.
Never ever again, pale nitawachia viongozi waende kupiga picha tu.