Hospitali ya rufaa Iringa yaanzisha huduma ya kujifungua na mwenza, ndugu au mwenza atashuhudia namna tukio la mama akijifungua

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
364
713
Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa imeanzisha rasmi huduma mpya ya kujifungua, huku ndugu au mweza wako akishuhudia namna tukio hilo linavyotea.

Akizungumza na mwananchi ofisini kwake December 10, 2024 Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk Alfred Mwakalebela amesema huduma hiyo ni mpya katika mkoa huo, hivyo mjamzito atapaswa kwenda na mwenza au ndugu wa karibu wakati yupo katika hatua za uchungu.

“Mtu anayetaka kuja naye, mjamzito ndiyo atachagua kati ya mweza au ndugu yake wa karibu na wataweza kuingia wote katika chumba cha kujifungulia,” amesema Dk Mwakalebela.

1733924550473.png
 
Taratibu tu watafika na kuja kuanza kushuhudia mimba inavyoingia!, dunia imevaa sketi la hudhurungi!
 
Wizara ya Afya waboreshe na kadi za kliniki waongeze kipengele wawe wanarekodi mtoto amezaliwa saa ngapi na dakika ya ngapi. Kujua mtoto amezaliwa dakika ya ngapi ina umuhimu astrologically katika kujua potential ya mtoto aliyopewa na Mungu kuja nayo duniani .
 
Hayo ni mambo ya faraga kwa upande mwngne itawaathiri saikolojia.hayo mambo tuwaachia waaguzi au wenye fanh yao
 
Hii nzuri sanaaaaa

Itaokoa ndoa nyingi na kuimairisha wana ndoa mume akiyaona hayo.
 
Back
Top Bottom