tweenty4seven
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 15,672
- 19,186
Hii tutafugia nyuki hakuna namnaSalaam Wakuu,
Jumamosi ya tarehe 11 Sept 2021, nilienda Chato kuangalia Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita ambayo iliwekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na aliyekuwa Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita tarehe 11 Januari 2021 haifai kuwa ya rufaa.
Dk Gwajima alidai hospitali hiyo ikikamilika itakuwa nauwezo wa kuhudumia wananchi milioni 14 kutoka Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora, Rukwa, Geita, na wilaya za Mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Gwajima alidanganya. Mtu hawezi kutoka Tabora aende Chato badala ya Dodoma. Au atoke Geita, Mwanza Shinyanga aende Chato badala ya Bugando Mwanza.
Ukweli hii Hospitali ya Chato Ni bajeti ya Wati wa Kagera Walinyang'anywa. Kagera ina Wilaya Nyingi, Walitakiwa wawe na Hospitali yao ya Rufaa. Sema Chuki za Awamu ya tano dhidi ya Wanakagera ndo ilisabiaha ijengwe Chato
Kulingana na Sensa ya 2012,Chato ilikuwa na watu Laki tatu(365,127) Wanajengewa Hospitali ya kuhudumia watu Milioni 14. Aibu.
Kagera yenye Wilaya za Bukoba, Biharamulo, Muleba, Karagwe, Ngara, Kyerwa, na Missenyi, kwa Sensa ya 2012 ilikuwa na watu 2.458 millioni hawana Hospitali ya Rufaa.
Mgawanyo wa Cake ya Taifa haupo sawa. Geita, Shinyanga na Mwanza wana Hospitali yao ya Rufaa Bugando, lakini ile ambayo ingejengwa Kagera, wameijenga chato.
Eti Hospitali ya Rufaa Bugando inapokea Wagonjwa 10 kwa siku. Wakati ukienda Pale Bukoba Government wagonjwa wanalala wawili wawili kitanda kimoja wengine chini.
Kwani kosa la Kagera ni nini?
Kagera Walipata tetemeko Serikali ikasema sio wao walileta tetemeko, hata misaada iliyotolewa na Wasamalia haikupelekwa.
Rais Samia arekebishe hii.
View attachment 1941878View attachment 1941879
Muonekano wa Hospitali ya rufaa Chato
Huu ni Wizi kwa Walipa kodi wa Kagera na Kanda ya Ziwa
Chato ni kwao na rais wa awamu ya tano Hayati Magufuli mwenda zake ambaye Mgombea urais wa Chadema 2020 alimuita Dikteta Uchwara.
Super woman Samia Suruhi hii imfikie. Naamini ataongea neno ili cake ya taifa kila mtu aifaidi.
View attachment 1941952
Magufuli: Serikali haitawajengea nyumba wahanga wa tetemeko Kagera