Hospitali ya Mzena inamilikiwa na nani? Kwanini iitwe Mzena?

Mbona humu ndani hamuombolezii. ????? wIii mna mapepo??? Aouth africa wana lia sana mqana mapinduzi kaondoka. angalia hii...
 
Ndo mkurugenzi wa usalama wa Taifa wa kwanza Tanzania
Huyu Emilio Mzena kwa uhalisia, nasikia ndiye yule mtu aliyejulikana kama "Chief" kwenye riwaya za mzee Elvis Musiba miaka hiyo, alikuwa bosi wake na Willy Gamba. Mcheki kwenye Njama, Kikomo, Kikosi cha Kisasi, Uchu etc. Kama ndivyo basi watakuwa wanamuenzi maana huyu mzee alikuwa ni lulu sana kwenye medani (ushushu)
 
Mzena gani huyu?au ndio yule mhehe aliyewatesa akina Mapalala,Fundikira hadi home boy wake Tuntemeke Sanga?kama ni yeye kwangu ni no aliyeijenga Tiss ya heshima ni Kitine na Kombe .
 
Mzena Memorial Hospital ni hospitali ya kisasa sana naweza kusema hata Muhimbili haifikii viwango vya Mzena ndio maana inaogopeka sana, kesho ntafanya ziara ya kushtukiza ntawapa mrejesho, waTanzania mniombee nirudi salama
 
Poleni wana JF kwa msiba mzito wa kumpoteza kiongozi shupavu na mpenda maendeleo!

Pengine wapo watanzania wengi kama mimi ambao jina hili la Hospitali hii nyeti ya Mzena limekua geni kwao na wamekuja kulisikia siku za hivi karibuni, ni kawaida kwa taasisi kubwa kama hospitali kupewa majina ya watu mashuhuri au viongozi mbali mbali, na pengine Mzena ni mmoja wao. Kama kuna mwana JF mwenye kufahamu asili ya hili jina basi atiririke kwa faida ya wengi.
Nani kakwambia wana JF wote wamesikitishwa na kifo cha Jiwe, , , ,
 
Huwezi amini hata Google haina taarifa za ndani kuhusu hii Hospitali aisee, nimesearch wanasema "Be the first to add the photo" nikajiuliza mimi ni nani hata niwe wa kwanza kuweka picha?
IMG_20210319_175121_979.JPG
 
Kwanini hospitali ya Usalama wa Taifa inaitwa Mzena?

Emilio Mzena, alikuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Idara ya Usalama wa Taifa, na aliongoza idara hii kuanzia mwaka 1961 hadi 1975, akiwa ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14).

Emilio Mzena, aliaminiwa sana na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, baada ya Idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua. Na hiyo ikapelekea Mwl. Nyerere, kumpa heshima ya kuiita hospitali hiyo kwa jina lake.
 
Emilio Mzena, alikuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Idara ya Usalama wa Taifa, na aliongoza idara hii kuanzia mwaka 1961 hadi 1975, akiwa ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14).

Emilio Mzena, aliaminiwa sana na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, baada ya idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua. Na hiyo ikapelekea Mwl. Nyerere, kumpa heshima ya kuiita hospitali hiyo kwa jina lake.

Kama Ulikuwa Hujui Ndio Ujue
 
Back
Top Bottom