Hospitali ya Mwananyamala yakumbwa na kashfa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali ya Mwananyamala yakumbwa na kashfa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quinine, Feb 1, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,922
  Likes Received: 12,118
  Trophy Points: 280
  MAITI za watoto 10 zimekutwa zikiwa zimefukiwa kwenye shimo moja huku zikiwa zimefunikwa kanga na mashuka ya Hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.

  Maiti hizo zimekutwa katika eneo la Mwananyamala Msisiri, jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa makaburi ya kwa Kopa mita chache kutoka katika hospitali hiyo.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Amour Mbaga, anayeishi kwenye eneo hilo, alisema alibaini hali isiyokuwa ya kawaida wakati akifanya usafi jana saa 3.00 asubuhi.

  “Wakati nafanya usafi niliona shimo la takataka likiwa limefukiwa mchanga, nikashangaa shimo halikuwa limejaa taka, lakini limefukiwa, nikajiuliza ni nani kafukia, wakati naangalia nikauona mkono wa mtoto,”alisema.

  Alisema aliwaita majirani na kuwajulisha polisi wa kituo kidogo Mwananyamala kwa Kopa na baadaye Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

  “Ndipo polisi walipokuja, wakafukua na kukuta watoto wachanga 10, huku watoto wengine wakiwa wameharibika vibaya na kukatika viungo vyao,”alisema. Maiti hizo zilikuwa ndani ya shimo fupi ambalo halizidi mita moja.

  Aliongeza, “wakati miili ya watoto hao ikiondolewa kwenye shimo hilo, harufu iliwafanya watu wengine washindwe kusaidia kufanikisha zoezi hilo hali iliyothibitisha kuharibika vibaya kwa miili hiyo.”

  Mbaga alisema kuwa watoto hao walikutwa wakiwa na alama za plaster zikionyesha kwamba walitokea kwenye wodi namba moja ya Hospitali ya Mwananyamala.

  Mbaga alisema walikuwa wamefunikwa kanga na mashuka yenye jina la hospitali ya Mwananyamala

  “Polisi walipofika hapa kufukua, waliwaita madaktari wa hospitali hiyo ambao walishuhudia miili ikiondolewa kwenye shimo hilo na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo,” alisema.

  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi umeshaanza kufanyika ili kuwabaini waliohusika katika tukio hilo.

  “Maofisa wa upelelezi walikuwepo hapa tangu mchanga na hivi sasa wanaendelea na uchunguzi na tutaendelea kuwafahamisha lolote litakalojitokeza kwenye uchunguzi huu,” alisema.

  Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alikutana na viongozi wenzake wa wilaya hiyo wakiwemo madaktari kwenye ukumbi wa hospitali hiyo.

  Mara baada ya mkutano huo ambao uliochukua saa mbili, viongozi hao walikwenda kwenye eneo la tukio ili kujionea shimo hilo.

  Akizungumza, Rugimbana aliwapa pole wakazi hao na kuahidi kwamba uchunguzi utafanyika ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

  Rugimbana alisema viongozi wa hospitali hiyo wanaandaa ripoti kuhusu tukio anatarajia kutoa taarifa leo atakapokutana na waandishi wa habari, ofisini kwake.
   
 2. L

  LUMBAKALA Senior Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 147
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Aaaagh inatia uchungu sana.Daktari aliyesomea usalama wa uhai wa mtu kufanya DHAMBI ya mauaji inauma sana. Uchunguzi ukikamilika wote waliohusika wawajibishwe, khaaa!!! Unyama gani huu
   
 3. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Great thinkers dunia imekaribia ukingoni...nahisi kiama ndio kinabisha hodi, unyama gani huu? ukatili usioweza kuelezeka...vilikosa nn hivi vichanga? wakati dunian kuna maelfu ya watu wanatumia gharama kubwa kutafuta watoto wengine wanapata halaf wanavifanyia ukatili huu....very sad news i have read this morning...my day is ruined completely..:sad::sad::sad:

  chanzo cha habari...JIACHIE
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Very sad story how can a person be cruel to this extent? Najiuliza je waliozaa hao watoto ilikuwaje au ni kitu gani kilitokea? Inauma sana
   
 5. S

  Shuza New Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haiwezekani watoto 10 wakazikwa kwenye shimo moja , na kuwa karibu na Hospitali na wakiwa wamwfunikwa mashuka ya Hospitali Bila Hospiali kuwa imehusika ichunguzwe kwa kina nini chanzo cha unyama huu
   
 6. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Eti mganga mkuu amesema watoto hao ni wale waliozaliwa wakiwa wamekufa na wengine kabla ya wakati, this is very cheap, kwani ndio mara ya kwanza watoto kuzaliwa wakiwa wamekufa, huyu aliyetoa hiyo statement achubguzwe kwa kina
   
 7. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  likuwa anaongea matope matupu, kwanini wazikwe kama mizoga kwa pamoja? Wanao husika lazima itakuwa Management ya Hospitali. Haiwezekani maiti itoke huko bila management kujuwa!

  Hapo Mwananyamala Hospitali hakuna BINADAMU kuna WATU tu walimaliza madarasa!

  A
   
Loading...