Hospitali ya Mwananyamala hakuna daktari

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,298
9,524
Nimeongea na ndugu yangu ambae amepeleka mgonjwa Mwananyamala leo. Amefika saa kumi na moja asubuhi hadi saivi hajamuona daktari yeyote. Nimemshauri amutoe hapo mjongwa asije akafa. Sasa anaelekea private.

Hii ni hospital yenye wateja wengi cha kushangaza hakuna daktari kuanzia saa kumi na moja kamili hadi saa kumi na mbili na nusu wakati anaondoka pale. Hii ni leo 16/04/2019.

Viongozi angalieni hili tutamaliza watu.
 
Kuzimu ipo,na malango ya kuzimu yapo hapahapa Duniani.

Sehemu nyingne ni malango ya kuzimu,kulielewa hili inahitaji
akili kubwa.
Vifo vingi vinavyotokea ni mikakati ya kuzimu.
Ogopa kuingia kwny malango hayo,lazma uachwe na majeraha,ukipona ni kama ajali,hurudi tena.
 
Kituo cha afya cha Themi/Kambini/ nanenane arusha saa saba na nusu usiku,nilipeleka mgonjwa,Nurse akagoma kabisa kufungua milango akitutaka tuondoke na kurudi asubuhi maana Doctor AMELALA na hawezi kumwamsha!!
 
Kituo cha afya cha Themi/Kambini/ nanenane arusha saa saba na nusu usiku,nilipeleka mgonjwa,Nurse akagoma kabisa kufungua milango akitutaka tuondoke na kurudi asubuhi maana Doctor AMELALA na hawezi kumwamsha!!
Sema siku gani, na terehe ngapi tuwabaini hao Nurse na Daktari wake, kwamba walikuwa wanafanya nini wakati huo.
Maelezo yako inabidi yakamilike isionekane ni majungu ya kuichafua huduma yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri: Ukipata shida kama hiyo ambayo inaonyesha kabisa kuna uzembe, fanya mawasiliano na viongozi wa hospital, kama huna mawasiliano yao chukua hatua zaidi kwa kulifikisha kwa viongozi wa serikali katika eneo ulilopo. Maana tatizo lisipotatuliwa ina maana litaendelea. Magonjwa hayana hodi, inaweza kutokea shida ambayo huwezi kuchagua hospitali, sasa je wakinipeleka kule ambako bado shida ipo si ndio itakuwa tiketi.....wananchi tushughulike na haya matatizo kwa kutoa taarifa mahala stahiki, watoa huduma wakiona tupo serious nao watabadilika.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom