Hospitali ya Musoma, Hongera Rais Magufuli kwa kutoa hela. Haikujengwa tangu Nyerere

Watery

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
2,720
3,456
Hongera

IMG_20201022_122803.jpg

View attachment 1626805View attachment 1626806View attachment 1626807View attachment 1626808View attachment 1626809View attachment 1626810View attachment 1626812View attachment 1626811View attachment 1626813
View attachment 1627099View attachment 1627100
 
Tunaomba Baba, asante baba. Watanzania wote tumekua omba omba na tukitupiwa visenti tunakumbuka kutoa shukran ya kuoewa haki yetu.
Ujue nini mkuu?

Hao wanaoshukuru wacha washukuru tu wala tusiwalaumu.

Ni kodi zetu na ni haki yetu kufanyiwa yote hayo kweli.

Lakini je, wenye mamlaka wasipokuwa na ari ya kutekeleza hayo wakawa wanabwia tu hela, kuna cha kuwafanya, zipo sheria za kuwawajibisha katika nchi zetu hizi za Afrika?

Embo nitolee mfano kama hautojali.
 
Tunaomba Baba, asante baba. Watanzania wote tumekua omba omba na tukitupiwa visenti tunakumbuka kutoa shukran ya kuoewa haki yetu.
Ujenzi wa hospilai hii uliasisiwa miaka ya sabini kabla ya vita; ukakwama kuendelea kwa sababu ya vita laiki baada ya Nyerere kutoka madarakani, imepita miaka 30 bila mtu kukumbuka mradi huo tena. Je wale marais watatu waliopita walikuwa hawakusanyi kodi au ni swala la priority katika matumizi ya kodi?
 
Ujue nini mkuu?

Hao wanaoshukuru wacha washukuru tu wala tusiwalaumu.

Ni kodi zetu na ni haki yetu kufanyiwa yote hayo kweli.

Lakini je, wenye mamlaka wasipokuwa na ari ya kutekeleza hayo wakawa wanabwia tu hela, kuna cha kuwafanya, zipo sheria za kuwawajibisha katika nchi zetu hizi za Afrika?

Embo nitolee mfano kama hautojali.
Wawe huoni kama katiba yetu inakasoro?
 
Jipongeze wewe kwanza kwa kodi yako kufanya kazi hiyo.
Haikufanya kazi miaka yote imefanya kazi enzi hizi, kuna kutoa kodi na jinsi serikali inavyotumia kodi, si kila mtu akipewa serikali anaweza kuitumia kodi vizuri
 
Ujenzi wa hospilai hii uliasisiwa miaka ya sabini kabla ya vita; ukakwama kuendelea kwa sababu ya vita laiki baada ya Nyerere kutoka madarakani, imepita miaka 30 bila mtu kukumbuka mradi huo tena. Je wale marais watatu waliopita walikuwa hawakusanyi kodi au ni swala la priority katika matumizi ya kodi?
Mkuu watakaokuelewa ni wachache...wengi huku mitandaoni ni wapinzani, kupinga kila kitu.
 
Wawe huoni kama katiba yetu inakasoro?
Kwa hilo tupo mrengo mmoja.

Ninasema bila kumumunya maneno kuwa, ina kasoro kubwa!

Na kwamba, yote atayofanya Magufuli kwa kipindi chake na kisha akasahau kulisimamia suala zima la katiba mpya tena ile pendekezwa ya Warioba, kazi zake zote, juhudi zake zote hizo zitanajisiwa kwa kasi ya upepo kwa muda mfupi sana baada ya kutoka madarakani.

Tunamuombea abadili msimamo wake wa: ....'katiba mpya siyo kipaumbele cha serikali yangu'...Asimamie katiba mpya ya Warioba na siyo ile pendekezwa ya Bunge la katiba iliyoandaliwa kupigiwa kura.
 
Back
Top Bottom