Hospitali ya Musoma, Hongera Rais Magufuli kwa kutoa hela. Haikujengwa tangu Nyerere

Huwa ninashangaa sana pale mTanzania anapo ona haki yake ya msingi ni msaada...
Kupitia kodi yako, huoni wajibu wa serikali mkuu, wala sio hisa
Hospital ilipangwa kujengwa tangu miaka ya sabini bali haikujengwa mpaka awamu ya Magufuli, hizo awamu nyingine wananchi walikuwa hawalipi kodi!?? Je, kushukuru ni tabia njema au mbaya!? Unapokula chakula nyumbani ukasema asante kwani sio haki yako kula!? Kushukuru ni tendo jema na la kutia moyo..
 
Hospital ilipangwa kujengwa tangu miaka ya sabini bali haikujengwa mpaka awamu ya Magufuli, hizo awamu nyingine wananchi walikuwa hawalipi kodi!?? Je, kushukuru ni tabia njema au mbaya!? Unapokula chakula nyumbani ukasema asante kwani sio haki yako kula!? Kushukuru ni tendo jema na la kutia moyo..
Hahaha kwa hiyo aliyeijenga ni Magufuli?!

Mnamagonjwa ya kujipendekeza.
 
Hela wanatoa walipa kodi na wala siyo Magufuli.CCM kila mahali ni vilaza wa lufikiri kuanzia balozi wa nyumba kumi hadi Rais wa nchi!
 
Acha upuizi mkuu hivi hii hospitali imeanza kujengwa miaka ya 80 ina maana watu walikuwa hawalipi kodi ndo maana haikujengwa miaka yote hiyo. Inamaana kozi zimelipwa tu muda wa magufuli. Heko buldozer wewe ni jembe Mungu akupe afya na akili kubwa kuliko mfalme suleiman utuongoze katika kweli. Nakupenda sana JPM
Kutofautiana kwa mawazo ndiyo kujenga nchi kwenyewe au siyo.

Mimi nimeajiriwa katika utawala wa Nyerere nikiwa mtu mzima hivi hivi kama nilivyo leo.

Ninachokuwa ninakiongelea hasa kuhusu hawa watawala marais, sibahatishi wala sipendelei mtu, ninakuwa ninakijua ninachokiongelea.

Kodi zilikuwa zinalipwa, lakini mfumo wa kutafuna na ukwepaji kodi ulitamalaki.

Jiulize kwanini miradi mingi ilikwama kusonga wakati kulikuwa na option ya kukopa kopa kwa wafadhili?

Any way, mimi na wewe hatujatofautiana sana kimawazo kiviiile!
 
Hiyo Katiba ya Warioba haitekelezeki ! Hata ningekuwa mimi ningeuchuna tu.
Kwa hilo tupo mrengo mmoja.

Ninasema bila kumumunya maneno kuwa, ina kasoro kubwa!

Na kwamba, yote atayofanya Magufuli kwa kipindi chake na kisha akasahau kulisimamia suala zima la katiba mpya tena ile pendekezwa ya Warioba, kazi zake zote, juhudi zake zote hizo zitanajisiwa kwa kasi ya upepo kwa muda mfupi sana baada ya kutoka madarakani.

Tunamuombea abadili msimamo wake wa: ....'katiba mpya siyo kipaumbele cha serikali yangu'...Asimamie katiba mpya ya Warioba na siyo ile pendekezwa ya Bunge la katiba iliyoandaliwa kupigiwa kura.
 
Ujenzi wa hospilai hii uliasisiwa miaka ya sabini kabla ya vita; ukakwama kuendelea kwa sababu ya vita laiki baada ya Nyerere kutoka madarakani, imepita miaka 30 bila mtu kukumbuka mradi huo tena. Je wale marais watatu waliopita walikuwa hawakusanyi kodi au ni swala la priority katika matumizi ya kodi?
Kwa hiyo hakuna hospital nyengine zilizojengwa zaidi ya hizo
 
Kwa hiyo hakuna hospital nyengine zilizojengwa zaidi ya hizo
Deflection; mada inahusu hospitali ya Musoma. Na kama zipo zilizojengwa kiwangoo hicho zitaje basi kwani ninajua kuwa hazipo isipokuwa zile za mashirika ya dini na makampuni binafsi. Hakuna hospitali ya mkoa au ya rufaa nyingine kubwa iliyowahi kujengwa kwa kipindi chote cha miaka 30, ndiyo maana kulikuwa na desk maalum kwenye wizara ya afya la kupeleka watu India kwenda kutibiwa.
 
Sawa, nashukuru kodi yangu inafanya vizuri kwenye bajeti ya serikali but hapo hapo musoma nasikia tu kwenye media kuwa zile bilioni za uwanja zilitoka kitambo ila hakuna kinachofanyika.

Issue kama hizi ndizo zinasababisha miradi iliyotangulia ionekane imepelekwa ili kuziba kombe mwanaharamu apite.
 
Hiyo Katiba ya Warioba haitekelezeki ! Hata ningekuwa mimi ningeuchuna tu.
Ni kipengele gani kisichotekekezeka mkuu?

Maana haiwezi kuwa katiba nzima haitekelezeki.

Tunachohofia sisi pasipokuwepo katiba ya kuwabana watawala, haya yote mema afanyayo Jpm sasa, hayataheshimiwa wala kuendelezwa atapomaliza muda wake.
 
Back
Top Bottom