Hospitali ya Muhimbili yafanikiwa kupandikiza figo kwa mara ya kwanza

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imefanikiwa kufanya upandikizaji wa figo kwa mara ya kwanza

Hii itakua imeondoa gharama ya Sh900,000 kwa wiki kwa ajili ya kusafisha figo kwa wenye matatizo hayo (dialysis).

============

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUANZISHWA KWA HUDUMA ZA UPASUAJI WA UPANDIKIZAJI WA FIGO (RENAL TRANSPLANT) KWA MARA YA KWANZA NCHINI TANZANIA TAREHE 24/11/2017

Ndugu wananchi, ninayo furaha kuwafahamisha Watanzania kwamba, kwa mara ya kwanza hapa nchini, Hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na wataalam kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi, India, 2017 wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kihistoria wa upandikizaji wa figo (Renal Transplant) siku ya Jumanne, tarehe 21 Novemba 2017

Ndugu wananchi, upasuaji huu wa kihistoria ni kielelezo cha juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, za kuboresha huduma za afya nchini zikiwemo zile za ubingwa wa daraja la juu (Super Specialized Services). Aidha, upasuaji huu ni juhudi zinazofanywa na Serikali za kupunguza rufaa za wagonjwa wanaohitaji huduma hizo nje ya nchi na hivyo kuokoa fedha ambazo zingelipwa nje ya nchi kugharamia matibabu hayo na badala yake fedha hizo zitumike kuleta maendeleo kwenye maeneo mengine yenye uhitaji hapa nchini.

Ndugu wananchi, kwa zaidi ya mwaka mmoja Hospitali ya Taifa Muhimbili ilijikita kuwekeza katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa aina mbalimbali wakiwemo wataalamu wa upasuaji wa kupandikiza figo ambapo Wataalam 19 walipelekwa nchini India kwa mafunzo ya vitendo, na Wataalam 2 walipelekwa nchini Norway. Vilevile, hospitali ilijikita katika kuboresha miundombinu yake ikiwemo uimarishwaji wa sehemu za kutolea huduma za afya na ununuzi wa vifaa tiba. Juhudi zote hizi zililenga kuwezesha huduma za kibingwa za daraja la juu ziweze kutolewa hapa nchini na ambazo leo wote tunashuhudia matunda yake.

Ndugu wananchi, utoaji wa huduma hii ya upasuaji wa kupandikiza figo hapa nchini, utawezesha kwa kiwango kikubwa kupunguza gharama ambazo Serikali imekuwa inatumia pale inapopeleka wagonjwa nje ya nchi. Inakadiriwa kwamba, utayarishaji wa mgonjwa kwa ajili ya matibabu ya upandikizaji figo ikiwemo vipimo mbalimbali vinavyohitajika kwa mpokeaji na mtoaji figo (donor and recipient) pamoja na upasuaji unagharimu wastani wa Shilingi za Kitanzania 21 milioni. Hii ni nafuu sana ukilinganisha na gharama ya Shilingi milioni 80 hadi 100 iliyokuwa ikitumiwa na Serikali kupeleka mgonjwa mmoja nje ya nchi ili kupata huduma hii ikiwemo gharama za matibabu, usafiri na malazi. Kwa mwaka Serikali imekuwa ikipeleka nje ya nchi wastani wa wagonjwa thelathini na tano (35) kwa ajili ya kupandikiza figo.

Ndugu wananchi, kuanzishwa kwa huduma hizi hapa nchini kutaleta nafuu katika gharama na hivyo kuwezesha wagonjwa wengi zaidi kutibiwa. Hii inatokana na ukweli kwamba, kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo huku wengi wao wakihitaji huduma ya utakasishaji damu (Renal Dialysis). Takribani wagonjwa 400 wanakadiriwa kuwa katika huduma ya dialysis katika vituo mbalimbali hapa nchini ambapo kwa hospitali ya Muhimbili wanaopata huduma hii sasa ni wagonjwa 200 na waliobakia wako katika vituo mbalimbali vya Serikali na vya binafsi.

Ndugu wananchi, Aidha, kutokana na ongezeko hili la wagonjwa wanaohitaji huduma za dialysis, Serikali imeanzisha vituo vya utakasishaji damu katika hospitali za Mbeya Rufaa, Chuo Kikuu cha Dodoma, KCMC na Bugando. Vile vile, huduma hii inapatikana katika hospitali za binafsi hapa Dar es Salaam zikiwemo za Kairuki, TMJ, Regency, Aga Khan, Access na Hindu Mandal. Aidha, usajili wa hospitali zinazotoa huduma hizi unaendelea kwa kadri zinavyotimiza vigezo. Wataalamu wanakadiria kuwa, 60% ya wagonjwa wanaopata huduma ya utakasishaji damu wanaweza wakahitaji huduma ya upandikizaji figo. Kutokana na uhitaji huu, ndiyo maana Serikali imeweka juhudi eneo hili na hatimaye leo tunashuhudia kuanzishwa kwa huduma hizi ambazo tayari mgonjwa mmoja ameshapandikizwa figo na anaendelea vizuri. Kupatikana kwa huduma hii nchini kutawezesha kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi tofauti na kama wangehitaji kupelekwa nje ya nchi.

Ndugu wananchi, Mafanikio ya upasuaji huu pia yatasaidia kuweka msingi wa kuanzisha programu nyingine za upandikizaji viungo (organ transplant) hapa nchini kama vile upandikizaji wa ini (liver transplant) na viungo vingine.

Ndugu Wananchi, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na Sekta ya Afya katika kuhakikisha kwamba, huduma za afya za ubingwa wa daraja la juu zinapatikana hapa nchini. Tunamshukuru sana !

Nawashukuru sana wataalamu kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi, India ambao wameshirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa zaidi ya mwaka mmoja katika mipango na maandalizi ya utoaji wa huduma ya upandikizaji figo hapa nchini. Kwa kipekee natambua juhudi kubwa za wataalamu 11 ambao tupo nao hapa wakiongozwa na Prof. H.S. Batyal, Dr. Sunil Prakash, Dr. Rajesh Kumar Pande na Dr. Anil Handoo. Wataalamu hawa ndiyo ambao kwa kushirikiana na wataalamu wetu wamefanikisha upasuaji huu.

Aidha, napenda kuwashukuru Wakurugenzi, Wataalamu pamoja na Wafanyakazi wote wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiongozwa na Prof. Lawrence Museru, kwa juhudi ambazo zimefanikisha upasuaji huu wa kihistoria wa upandikizaji figo hapa nchini. Prof. Museru amenihakikishia kwamba, kufuatia mafanikio ya upasuaji huu wanatarajia kufanya upasuaji mwingine kwa wagonjwa wengi zaidi ifikapo mwezi Januari, 2018 na baadae kuendeleza zaidi.

Napenda kuwashukuru viongozi na wataalamu wote wa Wizara yangu ambao kwa kushirikiana na Hospitali yetu ya Taifa Muhimbili wamechangia kuanzishwa kwa huduma hizi.

Imetolewa na:

Ummy A. Mwalimu (Mb)
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dar es Salaam,
24 Novemba, 2017
 
Watazitoa wapi hizo figo?
Isiwe wengine wanatekwa mitaani na kung'olewa ili wenye pesa wapandikiziwe.

Ila hongera zao ni hatua nzuri na kubwa kwenye tiba na afya.
 
Back
Top Bottom