Hospitali Ya Muhibili na Aibu ya Kudhibiti Mbu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali Ya Muhibili na Aibu ya Kudhibiti Mbu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by payuka, Jul 23, 2010.

 1. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Juzi nimesikia habari ambayo inasikitisha na ni aibu kwa taifa letu, Yaani hospitali kubwa ya taifa ambayo inaonekana ndo mkombozi wa afya zetu endapo hizi hospitali ndogo ndogo zitashindwa "inashindwa kudhibiti mbu"

  ....au mpaka hii wanataka wafadhili wa marekani ili warushe kwenye redio one " Mpango huu wa kudhibiti Mbu Hospitali ya Muhimbili umefadhiliwa na Msaada wa watu wa Marekani kwa Kushirikiana na madaktari bingwa wa Muhimbili"
   
 2. M

  MJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Sijui unaposema Muhimbili wameshindwa kudhibiti mbu unamaanisha nini maana sikusikia habari yenyewe. Upande wangu nimeshuhudia ongezeko la mbu liko ukanda mzima wa mto hadi maeneo ya selander hivyo mbu hao hawawezi kudhibitiwa kwa Muhimbili pekee bali eneo zima. Ukiwalaumu Muhimbili kwa kushindwa kudhibiti mbu kwani lini Tanzania tumefanikiwa kwa hilo? Malaria inavyoongezeka si ni kutokana na kushindwa kudhibiti mbu kwani watu wanaipata Muhimbili tu? Wanaosema "kwa hisani ya watu wa marekani" si hao hao Clouds waliokula fedha ya tamasha la malaria hawakujua hilo kipindi wanakula?
   
 3. Kamtori

  Kamtori Member

  #3
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  :bowl: HAPO CHACHA wajameni MBU tangu nineteen kweusi ni issue hapo "daraja la salender bridge" leo hiii MUHIMBILI mh kazi tunayo
   
 4. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,960
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Kuna mfereji unaotoa maji taka kutoka ndani ya kiwanda cha Tanzania Breweries. Mfereji huu unapita nyuma ya uwanja wa michezo wa Yanga kisha unavuka barabara ya morogoro na kupita karibu na shule ya wasichana ya Jangwani, Azania sekondari na nyuma ya hospitali ya Muhimbili.

  TBL inaelekea hawausafishi huu mtaro tena, kama zamani, umejaa mchanga, chupa za plastic na kila aina ya uchafu, ambao umezuia maji yatuame eneo lote kuanzia shule ya jangwani hadi nyuma ya hospital, siku za nyuma eneo la bondeni ya hospital kulikuwepo na kiwanja cha mpira lakini sasa hivi pamegeuka bwawa kubwa la maji, ambalo ndilo sasa limegeuka shamba la kuzalishia mbu wanaotishia uhai wa wagonjwa na wanafunzi wa Jangwani, Azania, Chuo kikuu cha tiba, watumishi wa hospital na wakazi wa maeneo hayo.

  Lawama zote ni lazima wabebe TBL kwa uzembe wa kutiririsha maji taka bila udhibiti wa kutosha. Ombi langu kwa serikali, iwalazimishe wajenge bomba la kupitisha maji taka toka ndani ya kiwanda chao hadi baharini, badala ya kupitisha maji taka kwenye mtaro wa wazi. TBL watoe gharama zote za kupuliza dawa za kuangamiza mbu eneo liloadhiriwa na mfereji wao. Kisha wagharamie uchunguzi wa vipimo vya afya kwa wanafunzi wa Jangwani, Azania na Muhimbili.
   
Loading...