Hospitali ya mkoa Kilimanjaro: Serikali na wizara ya afya wanasemaje kuhusu chumba cha upasuaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali ya mkoa Kilimanjaro: Serikali na wizara ya afya wanasemaje kuhusu chumba cha upasuaji?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by measkron, Dec 31, 2011.

 1. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Chumba cha upasuaji katika hospitali ya Mawenzi kilifungwa 27/12/2010 na wakaguzi wa wizara kwani kilikuwa kibovu na kwa taarifa nilizopata kwa mhudumu chumba hicho kilikuwa jiko wakati hospitali hiyo ikiwa kituo cha Afya ikiwa inamilikiwa na wajerumani zama hizo. Serikali waliichukua na kuwa hospitali mwaka 1946, hata hivyo hadi mwaka jana chumba hicho kidogo kilifungwa na sasa wagonjwa kwa mwaka mzima wanateseka sana kupata huduma ya upasuaji. Tulishuhudia Mh Grace Kiwelu katika kikao cha bajeti mwezi wa saba akieleza watoto waliopoteza maisha kwa mama zao kukosa huduma ya dharura ya upasuaji na kutaka maelezo, wakaahidi kushughulikia. Jana nimepeleka mgonjwa aliyeumia nikaambiwa hawana hata chumba kidogo cha upasuaji, minor theatre kwa ajili ya kushona majeraha. Serikali na wizara, nini mpango wa jengo la upasuaji katika hospitali hii ya mkoa?
   
Loading...