MAGALEMWA
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 6,415
- 4,881
Maswali ya kijingaHospitali inayodaiwa kuwa itakuwa kwa ajili ya mama na mtoto ambayo Godbless Lema anasema kuna wazungu wanaijenga Arusha imedhihirika kuwa mmiliki wa hospitali hiyo hajulikani kisheria ni nani.
Tatizo hilo la kisheria ni kama ifuatavyo.
1.Kisheria unaposema mtu katoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali maana yake unakabidhi hati zako zote zibadilishwe kwa jina la huyo uliyemkabidhi ili majina ya kiwanja hicho yasomeke jina la huyo mjenzi.HILO HALIJAFANYIKA kiwanja kinasomeka majina ya watu binafsi.Kwa hiyo ni hospitali inayojengwa kwa title deed ya watu binafsi.
2.Wazungu wanasema wanajenga hilo jengo la hospitali wao.Kisheria hilo jengo halitakuwa la kwao kwa kuwa liko katika kiwanja cha watu binafsi ina maana wanawajengea akina Godbless Lema?
3.Hao wazungu wanajenga hospitali yao au wanaijengea halmashasuri au serikali? Je ikimalizika kujengwa itakuwa chini ya nani? maana yake kelele zinazopigwa ni kuwa inajengwa nani ataendesha hiyo hospitali baada ya ujenzi kukamilika haijulikani.Kwa hiyo haieleweki hiyo hospitali itakuwa ya binafsi au ya serikali.Kama ni binafsi ,binafsi ya nani ya hao wazungu,ya hao wenye kiwanja wenye title deed ya kiwanja au ya nani.Kama ikijengwa ikakamilika kama wazungu wataikabidhi kwa serikali au manispaa ya arusha wataikabidhije wakati hati ya kiwanja sio yake? Pia hospitali hiyo haijaingizwa kwenye mipango ya jiji au serikali ili serikali iandae mpango wa uendeshaji wake ikikamilika ikiwemo kujiandaa kuajiri watumishi wa hospitali ,bajeti za madawa nk
Swali liko pale pale mmiliki halali wa hiyo hospitali kuanzia kiwanja hadi majengo atakuwa ni nani?
Godbless Lema amekuwa akifumba fumba haweki wazi mambo ya hiyo hospitali .Inaonyesha kuna utapeli unataka kufanywa kuwafanyia hao wazungu.
Mmiliki hajulikani huyo RC bwege alikuwa anaweka jiwe la msingi hewa?
Msilete wivu kwenye jitihada za watu. Hicho kikamba cha CCM kupitia Gambo mnaendelea kukisugua ili kikatike kabisa.