Hospitali ya mbunge Godbless Lema Arusha utata, mmiliki wake hajulikani kisheria

Unaruhusiwa kuhamia nchi ambayo rais anagawa hela bure na maisha siyo magumu. Kwani umelazimishwa kuishi Tanzania?
Uchumi umesimama, hakuna viwanda, mabenki hayakopeshi, watumishi wanapunguzwa, biashara zinafungwa, nguvu ninayo naitumia wapi ili niweze kupata tonge au unataka niwe mbunifu kama scorpion au panya road? Tumia ubongo kutafakari
 
Kada usiyependa Mama na Mtoto wapate afya njema nenda kasome kuhusu Bugando Hospital na Weill Cornell walipotoa ufadhili na wakaomba hiyo Program iitwe Weill Cornell Bugando Medical Centre tena hiyo program Rais wa awamu ya nne alipongeza unatokwa na ufahamu kwenye mambo yamanufaa.
 
Hospitali inayodaiwa kuwa itakuwa kwa ajili ya mama na mtoto ambayo Godbless Lema anasema kuna wazungu wanaijenga Arusha imedhihirika kuwa mmiliki wa hospitali hiyo hajulikani kisheria ni nani.

Tatizo hilo la kisheria ni kama ifuatavyo.

1.Kisheria unaposema mtu katoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali maana yake unakabidhi hati zako zote zibadilishwe kwa jina la huyo uliyemkabidhi ili majina ya kiwanja hicho yasomeke jina la huyo mjenzi.HILO HALIJAFANYIKA kiwanja kinasomeka majina ya watu binafsi.Kwa hiyo ni hospitali inayojengwa kwa title deed ya watu binafsi.

2.Wazungu wanasema wanajenga hilo jengo la hospitali wao.Kisheria hilo jengo halitakuwa la kwao kwa kuwa liko katika kiwanja cha watu binafsi ina maana wanawajengea akina Godbless Lema?

3.Hao wazungu wanajenga hospitali yao au wanaijengea halmashasuri au serikali? Je ikimalizika kujengwa itakuwa chini ya nani? maana yake kelele zinazopigwa ni kuwa inajengwa nani ataendesha hiyo hospitali baada ya ujenzi kukamilika haijulikani.Kwa hiyo haieleweki hiyo hospitali itakuwa ya binafsi au ya serikali.Kama ni binafsi ,binafsi ya nani ya hao wazungu,ya hao wenye kiwanja wenye title deed ya kiwanja au ya nani.Kama ikijengwa ikakamilika kama wazungu wataikabidhi kwa serikali au manispaa ya arusha wataikabidhije wakati hati ya kiwanja sio yake? Pia hospitali hiyo haijaingizwa kwenye mipango ya jiji au serikali ili serikali iandae mpango wa uendeshaji wake ikikamilika ikiwemo kujiandaa kuajiri watumishi wa hospitali ,bajeti za madawa nk

Swali liko pale pale mmiliki halali wa hiyo hospitali kuanzia kiwanja hadi majengo atakuwa ni nani?
Godbless Lema amekuwa akifumba fumba haweki wazi mambo ya hiyo hospitali .Inaonyesha kuna utapeli unataka kufanywa kuwafanyia hao wazungu.

Kwani CCBRT inamilikiwa na Serikali ? Kwani Serikali kwa maana ya wananchi hawafaidiki?

Kinachogombewa kuhusu umiliki ni ukweli kwamba huduma zitakazotolewa zitakuwa sifa kwa Upinzani na siyo CCM ndiyo maana kuna ugomvi....!

Ujinga huu wa propaganda dhaifu peleka kuliko na elimu ya duni huku hatuhitaji ujinga wa wasiojua uongozi ni dhamana tu! MUNGU anaruhusu uwe na mamlaka kwaajili ya watu wote siyo eti ndio uwe mateso kwa unaowatawala

MUNGU hachoki kusimamia ukweli hata uwe na mamlaka gani hatakuheshimu ukiwanyanyasa watu wake

Tuone watafika wapi!!!!!
 
1476933698285.png
hii kitu kwanini imekuwa mvinyo mchungu kwa jirani?
 
Lema ndiye raisi wa Arusha, uyo RC wenu anajitia ndolemwa na atajinusa mwenyewe

Lema ni mbunge wa Arusha mjini tu wewe ACHA VIROBA.Arusha ni zaidi ya Arusha mjini.Mkoa wa ARusha una wabunge kibao.Kwanza huyo Lema sio mtu wa Arusha kwao kilimanjaro ndio maana kutwa anaivuruga Arusha mjini kwani sio kwao .Hata pakiharibika yeye hana uchungu napo sababu sio mzawa wa hapo Arusha ni mtu wa kuja
 
hapa ndipo ile kauli ya kazi tu mliotuaminisha inakosa maana na inatuchanganya kabisa...mmeshavua ngozi ya kondoo tayari tunawaona sura zenu halisi
 
sisi hatujali hospitali ni yanani coz hio haitusaidii chochote, tunachojali hospitali iwepo iwasaidie watu basi..nyie kama mnaona hio hospitali ni ya lema wambien hao wabunge wenu walio weng bungen kila mbunge ajenge hospitali kwakufanya hvyo mtakua mmetusaidia watanzania na chama chenu kitajijenga vyema
 
Hospitali inayodaiwa kuwa itakuwa kwa ajili ya mama na mtoto ambayo Godbless Lema anasema kuna wazungu wanaijenga Arusha imedhihirika kuwa mmiliki wa hospitali hiyo hajulikani kisheria ni nani.

Tatizo hilo la kisheria ni kama ifuatavyo.

1.Kisheria unaposema mtu katoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali maana yake unakabidhi hati zako zote zibadilishwe kwa jina la huyo uliyemkabidhi ili majina ya kiwanja hicho yasomeke jina la huyo mjenzi.HILO HALIJAFANYIKA kiwanja kinasomeka majina ya watu binafsi.Kwa hiyo ni hospitali inayojengwa kwa title deed ya watu binafsi.

2.Wazungu wanasema wanajenga hilo jengo la hospitali wao.Kisheria hilo jengo halitakuwa la kwao kwa kuwa liko katika kiwanja cha watu binafsi ina maana wanawajengea akina Godbless Lema?

3.Hao wazungu wanajenga hospitali yao au wanaijengea halmashasuri au serikali? Je ikimalizika kujengwa itakuwa chini ya nani? maana yake kelele zinazopigwa ni kuwa inajengwa nani ataendesha hiyo hospitali baada ya ujenzi kukamilika haijulikani.Kwa hiyo haieleweki hiyo hospitali itakuwa ya binafsi au ya serikali.Kama ni binafsi ,binafsi ya nani ya hao wazungu,ya hao wenye kiwanja wenye title deed ya kiwanja au ya nani.Kama ikijengwa ikakamilika kama wazungu wataikabidhi kwa serikali au manispaa ya arusha wataikabidhije wakati hati ya kiwanja sio yake? Pia hospitali hiyo haijaingizwa kwenye mipango ya jiji au serikali ili serikali iandae mpango wa uendeshaji wake ikikamilika ikiwemo kujiandaa kuajiri watumishi wa hospitali ,bajeti za madawa nk

Swali liko pale pale mmiliki halali wa hiyo hospitali kuanzia kiwanja hadi majengo atakuwa ni nani?
Godbless Lema amekuwa akifumba fumba haweki wazi mambo ya hiyo hospitali .Inaonyesha kuna utapeli unataka kufanywa kuwafanyia hao wazungu.

Hivi ni kweli kuna wakati unakuwa na uelewa angalau wa ABCD......??????
Uwanja alipewa ArDF na Adv Mawala, na ArDF wakaukabidhi Maternity Africa kisheria kwa masharti ya kujenga kituo cha Afya (siyo Hospitali) kwa ajili ya akina mama. Hata unayemtetea Gambo naye alisema hivyo. Sasa wewe hayo maswali ya Kalulu na PAKA Jimmy yanatoka wapi??? Mpigie Gambo simu akwambie labda ndo utaamini hayo maneno
Ebu tulifanye hili jukwaa liwe la weledi na siyo blaa blaa
 
Pongezi kwa mleta Mada umeweza kujiuliza Maswali magumu ambayo wengine hawajiulizi...
JF yote ingekuwa inawatu Kama wewe Tanzania Ya viwanda tungeipata mapema Sana kabla Ya 2020...!!
Haiwezekani mtu povu limtoke namna ile...!!
 
Umenena sawa kabisa, na hakuna kitu wasichokipenda wazungu kama alivyofanya Lema, nadhani wataukosa msaada.

wazungu wakisusa tutajenga wenyewe. wewe unajua thamani ya kiwanja Burka. Hongera Lema, Hongera Mawalla Advocates kwa uzalendo uliotukuka.
 
kweli bana hilo la umiliki liwekwe wazi. isije ikawa wamiliki ni lema mwenyewe huku lema anajidai mawalla katoa ardhi katoa kumpa nani. lema aliwahi kudaiwa kunywa ambulance alizopewa kama msaada sasa lazima tuwe makini. katika clip moja akigombana na mkuu wa mkoa amesikika akisema yeye atakua kwenye bodi ya udhamini wa hospitali hiyo milele. mimi nimeelewa hivyo nadhani wengi pia wameelewa hivyo. huenda lema anahofia lengo lake kwenye mradi huo kutibuka ndio maana anamuhofia mkuu wa mkoa kushirikishwa na wafadhili kwenye mradi huo.
 
Kuondoa utata wa umiliki serikali iitishe kikao cha mwenye hati miliki ya hicho kiwanja ambaye ni Mawalla na wafadhili wanaojenga hiyo hospital ili kuweka mambo sawa kuhusiana na hati miliki ya hilo eneo kabla ya wafadhili kumwaga pesa za ujenzi MAwalla ahamishe umiliki wake isibaki kwa jina lake na serikali na wafadhili waelewe wazi umiliki wa hiyo hospital uko na nani kisheria wasiende kichwa kichwa.huo mkutano ni muhimu kufanywa kati ya mwenye ardhi ambaye ni mawalla,mtoa hati ya ardhi ambaye ni serikali na mjenzi ambao ni hao wazungu.huyo lema hatakiwi kukanyaga wala sura yake kuonekana kwenye hicho kikao
 
Back
Top Bottom