Hospitali ya Kigamboni haina hadhi ya kuwa hospitali ya Wilaya, Serikali itazame kwa jicho la tatu

be unique

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
2,374
2,273
Habari za muda huu wakuu,

Naandika kwa masikitiko makubwa sana, nikiwa na ushahidi wanachosema kwakuwa mimi ni mmoja kati ya wahanga wa huduma mbovu za hospitali hiyo.

Sitaki kuanza kulaumu watumishi wa hospitali, maana sina hakika kama ni wao au serikali ndio haifikishi vifaa vya sisi wananchi kuhudumiwa.

Inawezekana vipi kwa huduma ndogo kama ya kusafisha kidonda uambiwe vifaa hakuna, tena isitoshe unatumia bima, tuachane na bima wengi watasema kwakuwa wanachelewa kulipwa, unalipia kuosha kidonda elfu tano then unaambiwa ununue gloves serious kweli?

Unaenda duka la dawa la watu wa bima, unatakiwa upewe gloves ulafanyiwe huduma wanasema hakuna kanunue nje, ni kawaida sana kwenda kupata huduma tena hata sio huduma hizo kubwa ndogo tu na bado ukaambiwa vifaa hakuna.

Kuna faida gani kuipa hadhi na kuita hospitali ya wilaya wakati hata huduma ndogo tu wanashindwa kutoa kwa uhakika, nadhani liangaliwe vizuri hili swala la kuipa hadhi kubwa kisa majengo mapya wakati huduma zake bado mbovu.

Nawasilisha.
 
Kwan kipimo cha uwepo wa gloves hospital ndicho kinafanya iitwe hospitali ya wilaya? Ingekuwa vyema ukapitie taratibu na miongozo ya kuipa hadhi hoapitali ya wilaya ili uweze leta hoja hapa kwenye jukwaa hili la Great thinkers.
 
Waziri wa Afya anapaswa kujitathmini, muda anaotumia kuwaita watu wezi na kupambania kujifukiza angeugawa kidogo akafanyia kazi changamoto za muhimu zilizopo.

Kwa Hospitali iliyopo mjini kama hiyo ninaamini haina changamoto ya mapato, itakua inakusanya pesa ya kutosha kujiendesha kwenye kununua dawa, vifaa tiba na vifaa vya hospitali.

Tatizo lililopo ni wapi watapata vifaa hivyo, Bohari kuu (Msd) katika kanda zao nyingi hawana bidhaa nyingi muhimu, ikiwemo hiyo mipira ya kukinga mikono inayofaa kwa shughuli zinazohitaji usafi zaidi (surgical gloves).

Utaratibu wa manunuzi unamlazimisha mteja (hospitali) kuagiza bidhaa hiyo Msd, akikosa aagize kwa Mzabuni alieidhinishwa ambae nae anaweza asiwe nayo (zimekua adimu na kupanda bei hivyo hawataki kuuza kwa bei ya mkataba). Maana yake ni kwamba Hospitali ikikosa isubiri hadi watu hao wawili watakapopata hiyo bidhaa.
 
Kwan kipimo cha uwepo wa gloves hospital ndicho kinafanya iitwe hospitali ya wilaya? Ingekuwa vyema ukapitie taratibu na miongozo ya kuipa hadhi hoapitali ya wilaya ili uweze leta hoja hapa kwenye jukwaa hili la Great thinkers.

Nadhani hata hiyo miongozo iangaliwe vizuri pia,kama hospitali inachangamoto yakutoa hata huduma ndogo kwa uhakika na bado ina hadhi ya kuwa ya wilaya hapo inabidi tujitafakari.

Tusiishie kuona kisa ina majengo yenye nafasi na eneo kubwa basi ipewe hadhi wakati hakuna huduma ya uhakika.
 
Unaipa vipi hospitali hadhi kubwa wakati inachangamoto ya kutoa kwa uhakika hata hizo huduma ndogo.
Ndio nina kuambia umekosea sana kuhoji hadhi ya hospitali bila kujua hadhi hiyo inapatikanaje, pili ungekuwa una shida ungeuona uongozi wa hospitali ukupe majibu kabla kuja kubwabwaja humu, sie hayatuhusu. mambo ya kigamboni yanahojiwa huko huko ukileta humu huo ni umbea
 
Jaribu kutazama namna yako ya kufikiria,nimekujibu post yako ya kwanza kwa sababu umeandika kitu cha muhimu na mimi pia nikajifunza kitu(umeongelea muongozo) ila hapa kwa majibu haya nimejua bado kuna tatizo katika namna yako yakufikiria.
 
Sasa wafikiri nani atakujibu hapa ishu ya gloves? Tumia tu akili za kawaida utamlaumu nesi aliekwambia hana gloves je ulitaka akufunge na mikono yake mitupu (bare hand)? La hasha isingewezekana je ulitaka anunue kwa pesa yake binafsi? Nafikiri hata hilo haliwezekani, huko huko kigamboni kuna mtu amekosea au alikuwa na majibu sahihi kujibu shida uliyopata, kuna uongozi sio kila mtu hospital anafahamu manunuzi au anahusika na manunuzi ila uongozi unajua, sasa hapa JF kuna kiongozi wa idara ya afya kigamboni?
 
Kufikisha naweza kuwa nimebeba malalamiko ya wengi na wahusika wakisoma wanaweza kutazama kwa jicho ambalo walikuwa hawatazimii mwanzo.

Kwani yule aliyepost video shule iliyokuwepo ubungo wanafunzi wanasomea nje je kila mtu mtandaoni ni mkazi wa ubungo? Na je kwani hakuna viongozi ambao wanahusika ambao angeweza kufikisha maoni yake na malalamiko nje ya kupost mtandaoni?
 
Back
Top Bottom