Hospitali ya KCMC yakumbwa na tuhuma nzito za ufisadi wa mabilioni ya fedha

Mkumbuke kuwa hiyo hospitali sio ya serikali

17 PHD these are results
 
Uandishi mzima una kasoro nyingi sana. Lakini sio haba, ujumbe umefika.
Nitajaribu kuchambua baadhi ya hoja kwa uchache.

1/Ni makosa makubwa sana kuilinganisha KCMC na Muhimbili kwa sababu...
-Muhimbili ni shirika kuu la serikali(umma) lina fungu kubwa rasmi la bajeti yake kutoka serikalini kila mwaka kwa ajili ya kuendesha kila kitu. Idadi ya watumishi wa Afya walioajiriwa Muhimbili ni wengi kuliko taasisi yoyote ya Afya hapa tanzania(interms of Patient to medical personnel ratio), na wote wanalipwa na serikali, tena mishahara mikubwa zaidi kuliko watumishi wengine wote wa Afya hapa Tanzania wa serikali.(Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi ya watumishi wa Sekta ya Afya serikalini)

-KCMC ni taasisi ya kanisa, inaendeshwa kwa pesa za kanisa, misaada ya marafiki, malipo ya wagonjwa wanapotibiwa na ruzuku ya serikali. Wanajiendesha kwa wakati mgumu sana. Kuajiri watumishi wao itakuwa ni mbinde kweli kweli.

2/Japokuwa sijafanikiwa kufika KCMC kwa miaka mingi sana, lakini mara kadhaa siku za hivi karibuni nimeona kupitia kwenye vyombo vya habari kuwa ndani ya miaka mitatu wameweza kuanzisha vitengo vipya maalum vya Dharula(Emergency), Moto(Burn), Figo bandia, Kansa, Ulemavu wa mifupa, kitengo cha kihasibu cha malipo kutumia mtandao/benki nk.
Sasa sijui kama hao wakuu wao wapya waliyakuta hayo tayari au wao ndio waliwezesha hayo?

3/Ukweli ni kwamba mpaka sasa KCMC ndio hospitali tegemeo sana kwa ukanda mzima wa Kaskazini, ikihudumia mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga, lakini pia mikoa ya Singida, Dodoma na baadhi ya maeneo ya Kenya nk. Kuna vitengo viko pale(kama macho, ngozi nk) ambavyo ni tegemeo kubwa kwa Afrika na dunia. Lakini KCMC imekuwa ikipewa ruzuku kidogo mno kutoka serikalini. Katika mazingira hayo usitegemee mambo makubwa sana zaidi ya watu kutibiwa na kwenda zao. To sustain that thing sio jambo la mchezo mchezo.

4/Tuhuma nyingi zimelenga watu fulani badala ya kulenga hoja. Na nyingi ni hisia zenye aina fulani ya chuki au wivu. Kwa mfano, mleta mada anahoji kwanini viongozi wa hospitali hiyo ambao ni madaktari wanafanikisha huduma bora katika hospitali zao binafsi lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa KCMC? Jibu ni moja tu, kule kunakomlipa mtu vizuri kutakuwa bora tu.

5/Nadhani KCMC ni mali ya kanisa la Lutherani Tanzania kwa 100%. Serikali ni mdau tu mwenye dhamana ya kuhakikisha malengo makuu ya KCMC ya kutoa huduma za Afya yanatekezwa. Sasa malalamiko yake dhidi ya Kanisa hilo katika ufujaji wa fedha zake zenyewe yanakosa nguvu ya kufanyiwa kazi hata kama ni malalamiko yana ukweli kabisa. Ni nani wa kufuatilia hayo kwa kina? Ni nani wakuchukua hatua dhidi ya Kanisa hilo?
Huo ni ushabiki usio kuwa na tija kwani dini inaruhusu kufanya ubadhilifu? acha kutetea ujinga

Kkkt pamoja na serikali wanazua balaa KCMC, wakati Roman catholic pamoja na serikali wanazua balaa BMC(Bugando).Hizi taasisi za dini maslai kwanza utu baadae
 
Huo ni ushabiki usio kuwa na tija kwani dini inaruhusu kufanya ubadhilifu? acha kutetea ujinga
Siwezi kushabikia kitu, mimi nimechambua hoja katika mada husika.
Kama mwizi ameamua kujiibia yeye mwenyewe, nani atamshtaki na nani atamkamata?

Mleta mada amejenga hoja kuwa, wamiliki na waendeshaji wa hospitali ya KCMC wanaiba fedha zao wanazozipata. Sasa tunafanyeje hapo?
 
mambo mengine sina uhakika nayo, lakini hilo la wamama kulala chini na kulala wawili wawili si la kweli hata kidogo...umeongeza chumvi...wodi hiyo tunaifahamu vizuri
 
Hata huduma za KCMC kwa sasa sio bora.
Mkuu ni lini huduma zao zilikuwa bora?
Kikubwa hospitali ziko nyingi sana, na gharama zina unafuu kuliko KCMC, basi suluhisho ni kwenda kwingine tu kutibiwa kuliko kulazimisha kutibiwa mahali ambapo hauridhiki nako.
Na kama huna option nyungine, basi kubali kutibiwa hapo hapo ambako ni pabovu.
 
Da we jamaa siwezi pinga baadhi ya hoja zako kwasababu sina ushahidi wa kupinha hizo hoja Hasa zile ambazo umesema umepata nafasi ya kuona vielelezo.
Hata hivyo kwa sababu hujaweka hivyo vielelezo hapa. Ambapo kusingekua na wa kuvipinga basi hata hizo hoja bado siziamini .

Na kama baadhi walivyo judge baadhi. hoja yako kubwa imekaa kimajungu.maana kwa asilimia kubwa imekaa kumsema mkurugenzi.

1. Kwanza umesema hospitali inakumbwa na tuhuma za ubadhilifu wa mabilioni ya fedha.
Kama umeweza kuwataja kwa majina na vyeo ambao hasa ni watuhumiwa wakuu, mbona hujaeleza ni nani anaituhumu au anawatuhumu, ni wewe ama?

2. Miradi uliyo iainisha Mingi kwa asilimia kubwa ilikuwepo kwenye Mipango endelevu ya Muda na, hao uliowataja kabla hata hawajaingia kwenye hizo nafasi wameikuta. Aliye kuwepo kipindi inabuniwa ni mmoja tu, mkurugenzi wa fedha . na hakuibuni yeye, ni kamati ambazo zinashirikisha wadau wengi, naamini wakiwemo wakuu wa idara na baadhi ya miradi ni mapendekezo ya watumishi.

3. Hill jengo la hostel ulisemalo halikua lijengwe bure na mfuko wa hifadhi. Ulikua ni mkopo ambao kcmc ingelipa in time . na ninaamini hata wewe unakubali mkopo sikizote ni gharama zaidi kuliko kutumia fedha zako mwenyewe.

4.kuhusu gharama kubwa za matibabu ya cancer kwa yeyote anaye fuatilia matibabu ya cancer ni wazi yana gharama kubwa. hasa madawa. Dose zake zaweza kuanzia laki saba hadi 1000000+ na sio jambo la kushangaza. Pia inajulikana cancer center yenye vifaa vya kutosheleza angalau, na wataalau so far ni ocean road tu.
Hivyo ni sahihi kwa wagonjwa kuhamia huko, kwanza kwa matibabu zaidi ambapo naamini wengi hupewa rufaa na madaktari wa hapo kcmc kwenda huko, na sio kwamba wanakimbia
Pili gharama za ocean road lazima ziwe nafuu( relatively) maana ni kituo maalum cha matibabu ya cancer cha taifa na kinamilikiwa na serikali.

Labda jambo ambalo naliona sio sahihi ni kama watumishi wanakatwa mishahara kwa sababu ya huo mradi hasa kama sio kwa ridhaa yao( huo ni wizi /uonevu) kwa mtazamo wangu.

Swala la gharama "hasa za bima" ni makubaliano kati ya hospitali na nhif . sidhani kama ni wizi.
Kuhusu mgao pande mbili ni kati ya nani na nani, na una ushahidi? Au hata chanzo cha uhakika ni kipi basi hata ofisi tu taja au taasisi.

Swala la watumishi kumiliki vituo binafsi na kutoa huduma bora zaidi ya zitolewazo hapo. Ni jambo la kushukuru walau wenye uwezo wana sehemu ya karibu ya kupatia Huduma bora zaidi. Tena kwa wao kufanya hivyo wapunguza msongamano hapo kcmc, ambapo wangebaki hapo basi Huduma zingekuwa duni zaidi maana rasilimali isingeongezeka wakati Wateja ( wagonjwa) ni wengi.
Au ulitaka wasafiri hadi Kenya au dar.
B. Ni haki yao na wajibu, hao watumishi kutoa Huduma hizo kwenye vituo vyao binafsi japo inaweza leta "conflict of interest " lakini unaweza thibitisha hilo? Kwamba imeleta conflict of interest. Pili hawawezi, hata wewe usingeweza kuwekeza fedha zako au rasilimali zako kwenye hospitali ambayo siyo mali yako(kcmc) hutoweza Fanya mambo vile upendeleavyo wewe wana haki na nisahihi kuwa na vituo vyao binafsi.

>>> kcmc napafahamu walau vya kuyosha.
Kuna changamoto nyingi wanazo kabili, nyingine umezisema mwenyewe.
Wana watumishi wachache japo kazi ni nyingi. Na kama mtoa maada unaifahamu kcmc vizuri, nadhani ni hospitali inayo hitaji pongezi. Hasa watumishi wake kwa kujitoa, wakiwemo hata ulio wataja. uwiano wa kazi wanazofanya na rasilimali hasa watumishi ni mkubwa. Hata Muhimbili uliyo itaja haifikii kcmc . maana Muhimbili wana watumishi wengi. Na uwiano na kazi inanafuu zaidi.

Serikali ndio inayolipa mishahara na baadhi ya stahiki nyinginezo za watumishi hivyo kcmc haiwezi kuajiri bila kibali cha serikali na hata wakifanya hivyo basi watumishi hao itapaswa walipwe na kcmc wenyewe na sio serikali.

Mtoa maada ilipasa uiombe serikali itoe vibali Ili walau waiongezee watumishi. au basi hao waliokuwa wakijitolea wapate ajira.

Kwa Ufupi kunachanga moto nyingi shirika hilo inazipata hasa kama hizo ruzuku ukiacha mishahara kwa hao ambao tayari serikali inawalipa.

Asilimia kubwa ya ruzuku kutoka serikalini kwa kipindi nilichokua nikifahamu mimi ilikua ikipungua mwaka hadi mwaka.Japo ni wazi mahitaji yalikua yakiongezeka mwaka hadi mwaka.

Hivyo ni wazi ili hospitali iweze kuendelea kutoa Huduma lazima gharama za uchangiaji Huduma zipande maradufu na pengine mwaka hadi mwaka.

Hospitali nyingi zenye kuwa na ubia na serikali zinakuwa na chamgamoto hasa kutokana na kutokua na umiliki wa moja kwa moja toka serikalini hivyo serikali haijisumbui hasa kwasababu, management pia, haiwajibiki moja kwa moja kwa serikali.

Nnalokubaliana na mtoa maada .
Hospitali hizi za namna hii hujinadi hazipo kwa ajili ya kupata faida. Shabaha yao ni kutoa Huduma.

Ni vema kuweka utaratibu ambao mapato na matumizi( mzunguko wa pesa) ukawa wazi kwa watumishi hata pamoja na serikali. Na serikali iwe na mamlaka ya moja kwa moja kufanya ukaguzi (auditing) ikiwezekana na taarifa zao ziwemo kwenye kumbukumbu za serikali.. Maana serikali ni M'bia mkubwa.

Hilo litaleta uwajibikaji na uwazi( transparency) kwa management na utawala wa hizi taasisi, jambo ambalo litaondoa au kupunguza mamalalamiko ya watumishi na majungu dhidi ya utawala na wamiliki. Pia litaleta uaminifu kwa watumishi, na chachu ya kuwajibika na utendaji.

Sisemi kwamba hakuna upigaji kwenye hizi taasisi .upigaji upo kila sehemu na kwa kila mtu kulingana na nafasi aliyonayo. Ndio Tanzania yetu na binadamu wengi tulivyo.

Ila mtoa maada ulizidisha kuipaka matope hii taasisi. Hata kama Kuna baadhi ya hoja ni kweli na ni kutokana na mapungufu ya viongozi wake, utoaji wako wa hoja umeziharibu maana umekaa kimajungu hadi umeondoa kuziamini.
Hasa ipo wazi kwa mkurugenzi. Kama wewe ni mfanyakazi wa hapo kumbuka walau( kwa nijuavyo Mimi) tangu kipindi cha Mkurugenzi Shao, mkiwachoka wakurugenzi wenu mnawaundia Majungu watoke, wakija wampya mnaishia kujilaumu, na kusema afadhali aliyepita. Nyie watumishi ndio wenye shida!!

Sasa next Mkurugenzi ni Temba.JM

Siungi mkono baadhi ya hoja.
 
i.mbona hujamtaja mfanyakazi Wa hapo ambaye ndio bingwa Wa kupewa tender za mabilion na kuikopesha Hosp hiyo.Na vp kuhusu hiyo machine ya ct scan ni nani aliagiza na pesa zililipwaje,na je machine ilifika kwa wakati?je Hosp ilitoa wataalam wangapi kwenda kujifunza kuhusiana na hiyo machine.na je wataalamu hao wanasemaje kuhusiana na machine hiyo kuwa mbovu kila wakati?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasema hawaajiri vipi raisi naye anaajiri ???
Hivyo naye fisadi.???
Acha umbea maana inaonekana ulikuwa mfanyakazi pale ila ULIFUKUZWA KWA VYETI FEKI.
Shame on you.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadi sasa naona watuhumiwa wanazidi kupangua tuhuma hizi bila mafanikio..kigwangala na boss waziri ummy wameshazipata.

Just wait.
 
Kasome ujiendeleze uwe na wewe mkurugenzi achana na majungu si mtaji ndugu.Wakati wenzio wanasoma we ulikuwa wapi?Shida hawa wa vyeti Feki wakishasombwa na mafuriko ya bashite ndio kuchafulia wengine.Kweeendraaaa kule pumbavuuuu
 
Acha kuwashwa
Subiri muda usome
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom