Hospitali ya Dk Khan yashindwa kulipa Sh 127 milioni

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
215,413
2,000
Hospitali ya Dk Khan yashindwa kulipa Sh 127 milioni
Thursday, 16 December 2010 20:46

Hassan Mohamed
UONGOZI wa hospitali ya Dk Khan jijini Dar es Salaam umeshindwa kulipa deni la Sh127 milioni baada ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuudai uongozi wa hospitali hiyo kama pango.

Akizungumza na Mwananchi Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Ruth Alice Lembuya alisema wameamua kuondoka katika jengo hilo na kwamba wanatafuta wafadhili ili wawasaidie kulipa deni hilo.
“Tumejitahidi kuwasiliana na wafadhili ili watusaidie kulipa deni tunalodaiwa,” alisema Lembuya.

Alisema hospitali yake bado haijapata sehemu nyingine ya kuendelea na huduma na kwamba mafaili ya wagonjwa wa hospitali hiyo, yamehamishiwa katika hospitali ya Hindu Mandal ili wagonjwa waendelee na huduma za matibabu.

Naye Meneja Madeni wa NHC, Japhet Mwanasenga alisema awali hospitali hiyo iliomba kulipa deni hilo kwa awamu,
lakini ilishindwa kufanya hivyo.

“Dk Khan ni miongoni mwa wadaiwa sugu, tumekuwa tukiwasiliana nao mara kwa mara kabla ya uamuzi huu wa kuawatoa katika jengo letu.

“Tumeamua kuchukua hatua hii ili kufidia deni tunalowadai na, ni onyo kwa yeyote anayedaiwa alipe kabla hajapata usumbufu,”alisema Mwanasenga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya Mzizima iliyopewa kazi ya kuhamisha vifaa vya hospitali hiyo, Merick Sagwa alisema wanaendelea na shughuli ya kutoa vifaa hivyo na kuvipeleka katika bohari yao.

“Vifaa vyote tunavyovitoa hapa tunavipeleka katika bohari yetu, wadaiwa wanatakiwa kuja kuvikomboa ndani ya siku 21, baada ya muda huo kwisha tutatangaza mnada wa hadhara magazetini ili kupata fidia ya kodi inayodaiwa na NHC,” alifafanua Sagwa.

Wakionyesha hisia zao katika tukio hilo, wafanyakazi wa hospitali hiyo wameutaka uongozi kuwalipa haraka mishahara yao na gharama za kusitisha ajira zao.

“Tuliomba mkopo benki, uongozi wa hospitali unatukata mshahara kwa ajili ya kulipa mkopo huo, lakini sasa naona kama wanataka kutufunga,” alisema Asira Rashidi mmoja wa wafanyakazi wa hospitali ya Dk Khan.
Pamoja na kuulaumu uongozi wa hospitali hiyo baadhi ya wafanyakazi wameilaumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua mbadala kuokoa ajira na huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
215,413
2,000
Naye Meneja Madeni wa NHC, Japhet Mwanasenga alisema awali hospitali hiyo iliomba kulipa deni hilo kwa awamu,
lakini ilishindwa kufanya hivyo.

"Dk Khan ni miongoni mwa wadaiwa sugu, tumekuwa tukiwasiliana nao mara kwa mara kabla ya uamuzi huu wa kuawatoa katika jengo letu.

"Tumeamua kuchukua hatua hii ili kufidia deni tunalowadai na, ni onyo kwa yeyote anayedaiwa alipe kabla hajapata usumbufu,"alisema Mwanasenga.

Kinachojitokeza hapa ni kuwa hospitali ya Dr. Khan yaendeshwa kwa hasara na ninaamini kuwa hospitali nyingi biashara hizo hazilipi..............hivyo kazi wafanyayo ni ya huduma tu...............kinachofaa kufanyika ni kuangalia namna ya kuwapunguzia mzigo wa kodi ili ziweze kujiendesha zenyewe..................................ikumbukwe huduma ya afya haipaswi kuwa ni ya kibiashara..............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom