Hospitali ya Benjamin Mkapa wamekithiri kwa huduma mbovu

Babake mwanaidi

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
641
693
Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya utendaji kazi mbovu wa hospitali hii ya Benjamin Mkapa iliyoko hapa jijini Dodoma.

Nimeshuhudia zaidi ya matukio matatu ya watu kupoteza maisha kwa uzembe wa madaktari,wauguzi na wahudumu wa hospitali hii. Ninaomba serikali itupie jicho lake katika hospitali hii ili tusiendelee kupoteza roho za Watanzania kwa uzembe na sababu zinazoweza kuzuilika.

Nawasilisha.
 
Duu umenikumbusha tukivyokuwa Udom tulikuwa tunataniana “ukiumwa kula panado tu ila ukienda pale kwenye ule mjengo tunakuaga”
Wanafunzi wengi wameaga dunia waliopelekwa benja ayo mambo ya kufa kwaajiri ya uzembe sijui.
 
Poleni sana.hiyo hospitali kuna jamaa yangu alikua anafanya hapo anakwambia madaktari hapo wanawaachia wanafunzi kufanya operations za kuuwa watu
 
Hiyo hispitali ni tatizo nimeshasikia baadhi ya watu wakiilalamikia serikali fuatilieni.
 
Duu umenikumbusha tukivyokuwa Udom tulikuwa tunataniana “ukiumwa kula panado tu ila ukienda pale kwenye ule mjengo tunakuaga”
Wanafunzi wengi wameaga dunia waliopelekwa benja ayo mambo ya kufa kwaajiri ya uzembe sijui.
tatizo sio madaktari..tatizo linaanzia kwa walioijenga.hahaaaahaaa...hii statement ni kwa ajili ya watu wazima tu.
 
Babake mwanaidi,
Wewe umejuaje Kama Ni uzembe? Ile Ni hospital ya rufaa Kuna sababu nyingi wagonjwa kufariki. Au unataka kufungua hospital mshindane? Hakuna hoja ulioandika naona Ni majungu tu
 
Ni sawa lakini wanatibiwa pia watu wakawaida,
Wajerekebishe palipo na tatizo!
Baadhi pia ya nurses pale sijui ni utoto au bado wanaushule shule wajitahidi kubadilika
Wewe umejuaje Kama Ni uzembe? Ile Ni hospital ya rufaa Kuna sababu nyingi wagonjwa kufariki. Au unataka kufungua hospital mshindane? Hakuna hoja ulioandika naona Ni majungu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ipo kwa karibu hospital zote za serikali,nenda pale buguruni kwa mnyamani hatari ,zakhem na mbagala ndo utachoka na siku hizi wana tabia ya kupiga watu opareshen hasa wajawazito hata kama hakuna sababu ya msingi...Wiki iliyopita dada wa rafiki yangu(kwa maelezo yake) alilazwa pale buguruni ni mjamzito wakataka kumfanyia oparesheni ila ikashindikana kwa sababu ya hela jioni pesa ikapatikana wakapeleka kwa bahati mbaya kukawa na dharura muda wa kufanya hilo zoezi ukasogezwa.

Masaa mawili kabla akaja ndugu yao ambaye nae ni muhudumu wa afya baada kuuliza sababu hakupewa jibu la kueleweka wakadai pesa yao kwa nguvu wakapewa wakamuhamishia pale Gongo la mboto (kardinal lugambwa) kufika pale akafanyiwa uchunguzi ikaonekana siku yake haijafika bado mpaka tarehe 22 december.

Hata dada yangu alifanyiwa oparesheni pale temeke kwa stahili kama hii japo hakukuwa na sababu za msingi wanachojali hela tu,hiyo laki 2+ waipate bila kujali.

Na kama hiko kituo cha buguruni madaktari wana dharau sana na kuna muda hukimbia wagonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duu umenikumbusha tukivyokuwa Udom tulikuwa tunataniana “ukiumwa kula panado tu ila ukienda pale kwenye ule mjengo tunakuaga”
Wanafunzi wengi wameaga dunia waliopelekwa benja ayo mambo ya kufa kwaajiri ya uzembe sijui.

Labda wabadili jina la hospital, nakumbuka janga la MV Bukoba, ajali mbaya ya treni Dodoma na wale wapemba waliopotelea majini walihusishwa na jina hilo
 
Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya utendaji kazi mbovu wa hospitali hii ya Benjamin Mkapa iliyoko hapa jijini Dodoma.

Nimeshuhudia zaidi ya matukio matatu ya watu kupoteza maisha kwa uzembe wa madaktari,wauguzi na wahudumu wa hospitali hii. Ninaomba serikali itupie jicho lake katika hospitali hii ili tusiendelee kupoteza roho za Watanzania kwa uzembe na sababu zinazoweza kuzuilika.

Nawasilisha.
"Hili ni jungu"
 
nenda hospital ya rufaa wako vizur hasa kitengo cha bima kama ulaya vile unaweza opoa hata mke kuna visu yaan
 
Poleni sana.hiyo hospitali kuna jamaa yangu alikua anafanya hapo anakwambia madaktari hapo wanawaachia wanafunzi kufanya operations za kuuwa watu
Nimeisikia hiyo, anampasua mgonjwa huku ana Google nini aendelee nacho, Mimi ninaipenda maana walimsadia bint yangu, wakati wanaisema Mimi nikatetea, wote wakanibishia na kuniambia kama nahitaji matibabu mazuri ni hospital X

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhimbili kiwango sana wanajitahidi huwezi linganisha na hiyo benjamini mkapa kwa hospitali za umma
Nimeisikia hiyo, anampasua mgonjwa huku ana Google nini aendelee nacho, Mimi ninaipenda maana walimsadia bint yangu, wakati wanaisema Mimi nikatetea, wote wakanibishia na kuniambia kama nahitaji matibabu mazuri ni hospital X

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Babake mwanaidi,
Wewe umejuaje Kama Ni uzembe? Ile Ni hospital ya rufaa Kuna sababu nyingi wagonjwa kufariki. Au unataka kufungua hospital mshindane? Hakuna hoja ulioandika naona Ni majungu tu
Majungu kivipi.mtoa hoja kasema sababu ni uzembe wa madaktari kwani wewe hujui vifo vinavyotokana na uzembe.badilikeni bana mbona muhimbili hakuna hiyoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi bado Nina Imani nayo Sana tu ndugu zangu wanne wamefanyiwa operation pale na madaktari bingwa na wapo salama, Kwa hili nashukuru haya.mapungufu madogo madogo watajirekebisha, Ila ukweli hii limevuma Sana hapa mjini wengi wanalalamika. Bado ni hospital yetu na tunaihitaji sana, Kwa manesi wapo ambao ni pasua kichwa kama hospitali zingine zilivyo na uongozi unawajua washughulike nao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie ndio madaktari wenyewe mnaoua wagonjwa kwa uzembe hapo benjamini mkapa

Sent using Jamii Forums mobile app
"Ugonjwa huwa na matokeo matatu. Kupona, kudhurika au kupoteza maisha. So kuwasingizia wahudumu wa afya kwamba wamesababisha mgonjwa kufa ni ulimbukeni mkubwa.
Mgonjwa anapaswa kujilaumu mwenyewe kwa kushinda kujikinga na maradhi kwani elimu ya kinga ipo yakutosha. Kifupi ni kwamba matatizo mengi ya kiafya husababishwa na wagonjwa wenyewe. Mfano Ajali, Kipindupindu, AIDS nk"
 
Kama wewe ni daktari basi utakua dokta wa hovyo kuliko wote na kama siyo dokta nakusamehe kwa ujinga uliouandika hapa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom