Hospitali ya Apollo inaweza kusitisha kupokea wagonjwa kutoka Tanzania kutokana na deni

Phd Hewa

JF-Expert Member
Oct 3, 2016
572
500
Hospitali ya Apollo India huenda ikasitisha kupokea wagonjwa kutoka nchini Tanzania kutokana na deni kubwa inayodai.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hayo leo wakati alipokuwa akizindua bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Waziri Ummy amesema Apollo inadai Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 30 na kwamba wameshaanza kulipa deni hilo.
Apollo-660-300x200.jpg

"Tulikuwa tunapeleka wagonjwa wengi kufuata matibabu nje ya nchi, tumeanza kulipa deni hilo na tunashukuru idadi imepungua hadi wagonjwa 304 mwaka 2016 kutoka wagonjwa 533 2015 sawa na asilimia 45.
 
shiu yang

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
3,293
2,000
Watuvumilie tu maana wakisitisha masikini wenzangu ndio watakufa.

Hawa viongozi walio wahi sema Tz haihitaji kukopa wao
hata wakiugua wanatibiwa kwingine.
 
MABAKULI

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
1,383
2,000
sasa wapi kasema apollo wamesema watasitisha
Nikisikia jina la bashite mnanikumbusha mwalimu mmoja wa chekechea watoto.walikuwa wanamwita kibagia kumbe alikuwa anawambia watoto waende na Bagia shule mkifika nazo anakusanya halafu anaanza kufundisha kuhesabia na anachukua bagia moja anauliza hii ngapi mkisema moja anashika halafu anakula anaendelea hivyo hivyo mpaka sufuria linakwisha. Tujihadhali haya ni maccm tutazubaa tunangoja cheti tutakuta kodi yalitunyanganya yamekula yote
 
mhuri25

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
1,829

Mkuu unahangover nn Wapi katajwa Bashite... Au Ww Ndio Mwl Kibagia
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,718
2,000
Kuna haja kuendelea kuwekeza katika vifaa tiba na wataalamu wetu wenyewe
 
nuruyamnyonge

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
4,234
2,000
Uzuri ni kwamba, Apollo na Tanzania ni marafiki sana, hawawezi kufanya hivyo. Pia niwaondolee watanzania hofu , juzi tu team yetu ya wataalam kutoka Tanzania , wamekwenda kusoma hapo Apollo maswala ya moyo ili wakirudi waje kuwahudumia watanzania hapa hapa nchini kwetu.

Kwa hiyo, swala la kwenda kutibiwa Apollo siku za usoni itakuwa historia. Tanzania wataalamu wapo tatizo ni vifaa tu, kuna timu nyingine iko nchini Israel wanacheza na moyo tu kwa ajili yako, mimi na wewe.
 
Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
6,021
2,000
Viongozi wakiugua mafua tu breki ni Apollo, walalahoi ikitokea umefikishwa Apollo unaambiwa too late, hakuna jinsi ya kusaidika maana tatizo limeshafika pabaya.
 
WAZIWAZI

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
1,797
2,000
Nikisikia jina la bashite mnanikumbusha mwalimu mmoja wa chekechea watoto.walikuwa wanamwita kibagia kumbe alikuwa anawambia watoto waende na Bagia shule mkifika nazo anakusanya halafu anaanza kufundisha kuhesabia na anachukua bagia moja anauliza hii ngapi mkisema moja anashika halafu anakula anaendelea hivyo hivyo mpaka sufuria linakwisha. Tujihadhali haya ni maccm tutazubaa tunangoja cheti tutakuta kodi yalitunyanganya yamekula yote
wewe ni hoho nene ndani tundu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom