Hospitali ya Aga Khan kitengo cha wazazi sasa mnakera

Rifleman

New Member
Jan 4, 2018
4
32
Kichwa cha habari chahusika.

Aga Khan Hospital upande wa wazazi imekuwa na sifa njema kwa kipindi kirefu kwa huduma zake ambazo miaka yote zilitolewa bila usumbufu kwa wateja wake kama ilivyokuwa kwenye hospitali za uma.

Mke wangu amejifungua watoto wetu wawili kwenye hospitali hii, hata mara moja hakuwahi kuagizwa kufika hospitali na furushi kama msafiri. Sasa anaelekea kujifungua mtoto wetu wa tatu lakini masharti yanayotolewa utafikiri tuko Temeke au Mwananyamala.

Mama anaagizwa abebe furushi kila anapokwenda clinic na anapokwenda kujifungua ndo anatakiwa abebe mabegi mawili....!!

Najiuliza huku Aga Khan kumekuwaje...? Au mkuu wa kitengo hiki ameajiriwa kutoka kwenye zile hospitali zetu tunazozikimbia??

Hili limekuwa ni kero kubwa hasa kwetu sisi tunaopenda kuwasindikiza wake zetu clinic. Tukianza kujiandaa kwa safari ya clinic utadhani tunasafiri kwenda Marangu kwa bibi..!!

Nilitamani tuendelee kuzaa lakini sasa nimeghairi sitaki tena hii kero.

Hebu liangalieni hili Agha Kahan hospital.

Naomba kuwasilisha.
 
Leo nimefura.

Imagine kwenye moja ya polyclinics zao

Kupata chanjo ya surua wametuambia tutafutane tuwe sita ndio tuchome.....

Heri wangesema imeisha twende ya mjini kuliko kutuambia mpaka tuwe sita.

Au hata wangesema hawatoi huduma hii kutokana na idadi ya watu kuwa ndogo... bali waende ya mjini
 
Huku hospital za serikali wanasema bure sasa yule daktari alietaka laki moja yangu sijui katokea Rwanda?


Lunatic
 
Hamia Hindu mandal ipo hapo jirani tu. Hawana Mambo mengi clinic Wala kujifungua pochi yako Inaongea
 
Back
Top Bottom