Hospitali ya Mkapa kuanza upasuaji unene wa tumbo

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1133723


WATU wenye unene uliozidi nchini sasa wana fursa ya kuwa na furaha baada ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kuanza kufanya upasuaji wa kupunguza unene. Upasuaji wa aina hii ni wa kupunguza unene wa tumbo au kwa kuondoa sehemu ya tumbo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonse Chandika, alibainisha hayo jana hapa kuwa hospitali hiyo ya umma kuwa tayari imeshafanya kwa mafanikio ya upasuaji huo kwa mtu mmoja aliyekuwa na unene uliozidi kiasi.

“Tumefanikiwa kufanya upasuaji wa kupunguza unene kwa kijana mmoja aliyekuwa na unene uliopitiliza na upasuaji huu tumeufanya jana kwa mafanikio makubwa,” alisema Dk Chandika wakati wa kuelezea kambi ya upasuaji wa matundu madogo.

Hospitali ya Benjamin Mkapa yenye vitanda takribani 400, iliendesha kambi ya upasuaji wa matundu madogo kwa watu wenye matatizo ya uzazi inayoisha leo. Katika kambi hiyo, takribani watu 500 kutoka Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Dodoma wamehudumiwa katika kambi hiyo ambayo ilianza Juni 7, mwaka huu.

Akifafanua zaidi, Dk Chandika alisema kuwa hospitali yake inaendesha upasuaji wa kupunguza unene kwa watu ambao wana mrudikano mkubwa wa mafuta mwilini ambayo yanatishia afya yao na ambao wameshindwa kudhibiti kwa njia za kawadia ya kupunguza unene na uzito uliozidi. “Kwa hiyo upasuaji wa Bariatric huwasaidia watu wenye unene kupunguza uzito, mafuta yaliyozidi mwilini hivyo kuwanusuru na hatari za kiafya zinazotokana na mtu kuwa na unene uliozidi.

” Tati za kitiba za muda mrefu zinaonesha kuwa upasuaji wa aina hiyo unasaidia mwenye matatizo hayo kupunguza unene hivyo kumuepusha na magonjwa yatokanayo kama vile kisukari, hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kupunguza vifo vya ghaa kwa asilimia 40 hadi asilimia 23.

Dk Chandika alisema upasuaji wa bariatric unatumika katika kupunguza kiasi cha chakula mwilini ambacho tumbo kinaweza kuhifadhi, na kupunguza idadi ya kalori ambayo mtu anaweza kula na kupungua sehemu ya utumbo mdogo, ambao hupunguza kiasi cha kalori na virutubisho vinavyofonzwa mwilini. Uzito na unene uliopitiliza umekuwa ukichangiwa na ulaji wa chakula kupita kiasi na kutofanya mazoezi ya mwili.
 
Ni hatua nzuri...

Mwisho na sisi tufikie ujuzi wa kufanyia watu plastic surgery za aina zote...


Cc: mahondaw
 
Ubonge nao ushatengewa kitengo kwenye afya..?!
Dawa kubwa ya matatizo ya obesity ni mazoezi na kula kwa heshima, tena mlo uliokamilika..

Kuondekeza na kujilemaza kwa kula hovyo kamwe magonjwa hayatokuacha. Tujilinde, tusisubirie hospitali
 
Plastic surgery ni moja ya matawi katika sekta ya utabibu...

Mazoezi na ulaji nayo ni moja ya matawi katika sekta ya utabibu...

Ubonge nao ushatengewa kitengo kwenye afya..?!
Dawa kubwa ya matatizo ya obesity ni mazoezi na kula kwa heshima, tena mlo uliokamilika..

Kuondekeza na kujilemaza kwa kula hovyo kamwe magonjwa hayatokuacha. Tujilinde, tusisubirie hospitali
 
Back
Top Bottom