Hospitali gani hapa dar inatibu makengeza kwa ufanisi mzuri

emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
682
918
Habari wakuu nina mtoto ana umri wa miezi 8 na wiki 4, wakati anazaliwa kidogo alipata shida kwa sababu mama alishindwa kusukuma, ingawa Mungu alisaidia akazaliwa bila upasuaji.

Kutokana na hayo aliugua nimonia akiwa mchanga sana hvo akapata degedege, alipelekwa KCMC akawekwa kwenye incubator wanapowekwa watoto wachanga wanaozaliwa na matatizo mbalimbali alifanikiwa kupona.

Lakini alitoka akiwa macho hayajakaa vizuri, naweza sema kengeza. tumempeleka hospitali kadhaa kubwa bado hatujapata tiba. sehemu ya kwnza tulioenda alipewa vibandiko awe anaziba jicho moja kwa zamu kwa matarajii kuwa yatatengamaa na kuwa sawa lkn haikuzaa matunda.

KCMC tumerudi mara mbili, ya mwisho docter kasema anahitaji operasheni lakini mpka afikishe miaka 2 au 1. Napata shida kwa sababu kila hospitali na hata tunaporudi hospitali hiyohiyo na kukutana ma docter tofauti kila mmoja anatoa tiba tofauti juu ya tatizo lake. Jicho moja la kulia liko vizuri, limebaki la kushoto tu. Naombeni ni hospitali gani au clinic ipi kwa dar es saalam wako makini na kazi yao nimpeleke dogo.

ahsanteni
 
Pole mkuu!mpeleke Muhimbili ndio kila kitu kaka!one day nlikutana na dada mmoja namfahamu nlikua na mgonjwa pale anakaniambia mwanae alifanyiwa operation wa kurekebisha makengeza!
 
Au kama upo dar umpeleka pale Morocco kwa Dr Massawe then atakuandikia referal ya muhimbili ili iwe rahisi pia kwani kwenda pale direct wanaeza kuanza kukuzingua kaka!pole sana
 
Sidhan kama kuna tatizo hapo,issue ni kwamba tayari mtoto jicho moja lipo vzr na nadhan hilo lingine litakaa vzr tuu mkuu
 
Pole mkuu!mpeleke Muhimbili ndio kila kitu kaka!one day nlikutana na dada mmoja namfahamu nlikua na mgonjwa pale anakaniambia mwanae alifanyiwa operation wa kurekebisha makengeza!
mwanae alikua na umri gani, maana madocter wanasema kwa umri sahihi wa kufanyaiwa surgery ni kuanzia mwak 1 au 2 kwa sababu chini ya hapo mishipa inakuwa haijaonekana vizuri
 
Sidhan kama kuna tatizo hapo,issue ni kwamba tayari mtoto jicho moja lipo vzr na nadhan hilo lingine litakaa vzr tuu mkuu
doct anasema akibaki ivo badaye linaweza likafunga kabisa kwa sababu ubongo hauwezi tafsiri taswira mbili kwa pamoja. moja ndo litabaki.
 
Pole mkuu!mpeleke Muhimbili ndio kila kitu kaka!one day nlikutana na dada mmoja namfahamu nlikua na mgonjwa pale anakaniambia mwanae alifanyiwa operation wa kurekebisha makengeza!
Alikuwa na umri gani mwanae, nafikiria kumpeleka na wa kwangu pia.
 
Back
Top Bottom