Hospitali binafsi zitakazoshirikiana na serikali kuziba pengo la madaktari hizi hapa

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
TMJ,Regency,Aga khan,CCBRT,Hindu mandal na lugalo ya jeshi.

pia serikali imeweka mkazo na kuongeza nguvu katika hospitali za mwananyamala,temeke na Amana.

Pia madaktari wastaafu na wale waliopo wizara ya afya wataenda katika hospitali zenye upungufu wa madaktari.

My take;tunaomba sana roho za watanzania zisipotee kutokana na mgomo.
 
Siku moja baada ya Serikali kutangaza kutumia hospitali za Jeshi na madaktari wastaafu kunusuru afya za wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini, juhudi zaidi zimechukuliwa na sasa itatumia pia hospitali binafsi.

Hospitali zilizotajwa kukubali kushirikiana na Serikali kutoa huduma za afya kwa watakaohitaji tiba ya haraka na walio katika tiba isiyoweza kusitishwa ni pamoja na TMJ, Regency, Aga Khan, Hindu Mandal, CCBRT na Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Aidha, nguvu zimeongezwa katika hospitali za Mwananyamala, Amana na Temeke za Dar es Salaam kunakodaiwa hakuna mgomo, ili kutotoa rufaa nyingi kwa wagonjwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kunakodaiwa kuwa na mgomo.
 
Hapa naona matatizo mengi ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na rushwa kutokea na hizo hospitali binafsi kutolipwa pesa. Vilevile sijui kwamba hizo hospitali zitaweza kumudu wagonjwa wake wa kila siku pamoja na wagomjwa wengine wanaoletwa na serikali. Haya ngoja tuone na tusikie!
 
hospital binafsi zitapoteza wateja wake wanaozilipa na nina wasi wasi watajali pesa zaidi
 
Hizi zote zilizotajwa ni za Dar tu. Vipi sisi wa huku mikoani? Au sisi hatuna haki ya kuishi?
 
Back
Top Bottom